HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kwanza tufahamu we unaishi wapi??

Na jina lako umeliona lini kwenye placement?

Hizo siku 14 wanazosema ni baada ya kupokea barua kutoka utumishi sio tarehe iliyoandikwa kwenye barua, kwahyo we kama jina lilitoka jana tarehe 10 na leo ndio umeifuata, anzia hapo kuhesabu siku 14 .

Ni hayo tu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Ninaishi kibaha, na je ile tarehe waliyoandika inamaana gani
Kwani nmeipokea Leo, placement zimetoka jana, Ila wao wameonyesha tarehe 30/03/2023
 
Wakuu, ninaomba kuelewa kuhusu hili.
Halmashauri ya Wilaya X ni miongoni mwa Halmashauri za Wilaya zilizopewa vibali vya kuajiri Afisa Y (hili nalifahamu sio story ya kufikirika). Lakini mpaka PDF ya jana ni Halmashauri ya Wilaya X pekee bado haijapangiwa huyo Afisa Y (nasema hivo kwa sababu nafasi za Afisa Y zilizotangazwa imebaki moja tu).
Je, hapa shida inaweza kuwa ni nini/ nani?
Mwifwa Mr Spider na wengineo mtakaokuwa na uelewa wa hili.
Kuwa na subra mkuu ndicho ninachoweza kukushauri kwa sasa kwani utumishi tunawalalamikia kwa swala zima la ucheleweshwaji wa placements. Huenda wakatoa pdf lijalo, si unaona pdf zinatoka kidogo kidogo sanaa.?

Mimi mwenyewe ninasubiria placement niliyoifanya taasisi fulani mwanzoni mwa mwezi wa pili mpaka sasa hawajatoa pdf kwa nafasi zilizotangazwa na hiyo taasisi lakini cha kushangaza kuna mwambwa alipangiwa kazi kwenye halmashauri fulani na hakuwahi kufanya oral before na hata hivyo hakuna nafasi ya kazi iliyokwisha tangazwa na utumishi kwenye kada yetu.

Kwahiyo ni mambo ambayo yanachanganya muda fulani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninaishi kibaha, na je ile tarehe waliyoandika inamaana gani
Kwani nmeipokea Leo, placement zimetoka jana, Ila wao wameonyesha tarehe 30/03/2023
Barua za kuitwa kwenye ajira hutayarishwa mapema na waajiri kutumiwa nakala. Hiyo tarehe haina uhusiano na usalama wa ajira yako. Hata hivyo kwa utaratibu wa sasa hivi hata ukiripoti leo siyo kwamba leo ndiyo utaanza kazi. Kuna wiki kadhaa za kusubiria kwa madai ya kuhakiki vyeti. Wewe mshukuru Mungu kwa kuramba asali na ukawe mtumishi mwema!!!
 
Shukran sana mkuu 🙏🏼
 
Subira inahitajika!! Mwisho wa siku nafasi zote zilizotangazwa zitajazwa! Rasilimali fedha bado ni changamoto sana katika utekelezaji wa mipango mizuri ya sarikali. Serikali hupanga kwa matarajio ya kupata fedha (toka kwenye kodi na mikopo/misaada). Kodi zisipokusanywa kwa wakati na mipango haitatekelezeka kwa wakati!! Serikali huwa haina muujiza wala ujanja mwingine zaidi ya kodi toka kwa raia wake! Natamani sana elimu ya uraia na wajibu wa raia hasa eneo la kodi ingekuwa inafundishwa tangu kwenye elimu ya awali hadi chuo kikuu!! Si ajabu kuna watu wanaomba "mungu" wapate ajira sehemu ambazo zitawawezesha kuiibia serikali na kula rushwa!! Mbaya zaidi kuna watu wako katika nafasi ambazo badala ya kuisaidia serikali kukusanya mapato ya kodi, kinyume chake wanashirikiana na watu kukwepa kulipa kodi kwa kupewa "kitu kidogo". Na bila kuelewa athari wanayoisababisha kwa Taifa, wanaweza kujitokeza tena kuilaumu serikali kwa kutokutoa ajira kwa vijana kwa wakati!!
Asante sana mkuu. I got you.
 
Kuwa na subra mkuu ndicho ninachoweza kukushauri kwa sasa kwani utumishi tunawalalamikia kwa swala zima la ucheleweshwaji wa placements. Huenda wakatoa pdf lijalo, si unaona pdf zinatoka kidogo kidogo sanaa.?

Mimi mwenyewe ninasubiria placement niliyoifanya taasisi fulani mwanzoni mwa mwezi wa pili mpaka sasa hawajatoa pdf kwa nafasi zilizotangazwa na hiyo taasisi lakini cha kushangaza kuna mwambwa alipangiwa kazi kwenye halmashauri fulani na hakuwahi kufanya oral before na hata hivyo hakuna nafasi ya kazi iliyokwisha tangazwa na utumishi kwenye kada yetu.

Kwahiyo ni mambo ambayo yanachanganya muda fulani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, asante sana. Nimekuelewa vema.

Umenikumbusha jambo.
Kuna jamaa tulisoma wote Chuo kimoja, Mwaka mmoja wa masomo lakini Kozi tofauti (Yeye Kozi X, mimi Kozi Y). Huyu jamaa alikuja akapangiwa kituo cha kazi halmashauri flani kama Afisa Y (zingatia alisoma Kozi X na angeitwa kama Afisa X, lakini akaitwa kazini kama Afisa Y). Nafasi ile haikuwahi tangazwa, ingetangazwa tungeiona na ku-apply sababu tupo wengi tulo-graduate na bado ni jobless. Huyu jamaa mara kwa mara tukiwasiliana hua ninamuuliza hivi ulipataje hiyo nafasi na wakati ulisoma Kozi tofauti na hiyo nafasi, hakuwahi nijibu kabisa zaidi ya kucheka na kuleta story za mzaha. Ila nilipokaa na kutafakari nikagundua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara (kipindi jamaa ameenda kazini) inayosimamia taasisi za Kada yangu na yake alikuwa ni mtu wa jimboni kwao (kwa sasa ni Mbunge) na huenda alikuwa ni connection yake. Hizi mambo zinachanganya sana.
 
Wewe utakubali !?mf umeomba kazi serikalini ambayo unaamini ukipata utakuwa nayo kwa miaka kama 35 hv halafu ghafla unapelekwa kwenye kazi ya mkataba mwaka 1 au miwili.Hapana kwakweli huko waende tu hao hao walioomba huku wakijua kuwa ni ya mkataba wa mwaka 1.
Umenena vema!!
 
kwanza tuanzia hapa PMGSS 4 ni shs ngap ? kama ni hela nzuri ntaenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu naomba msaada wenu
Barua yangu imeandikwa nmeipokea tarehe 30 mwezi wa 3 badala ya Leo tarehe 11, inanitaka kureport katika kituo Cha kazi ndani ya siku 14 na sehemu niliyopangiwa ni mbali kidogo wilaya ya mji wa kasulu.
Sasa naona siku 14 zinaisha Leo, hii imekaaje wakuu, itakuwa walikosea kuichapa niwarudishie tena??
Mbona siku hz kasulu sio mbali? Unafika siku hiyo hiyo.Labda wewe nenda utawaelewesha kule kasulu kuwa umeipata lini.
 
Kibaha kongowe
Ok. Wewe jiandae tu vizuri kwenda huko kwenye ajira uliyoitiwa wala usikurupuke!! Unajua Kasulu ni mbali na kwa utaratibu wa sasa wa kuripoti kisha unaambiwa rudi tutakupigia simu taratibu zitakapokamilika za kuhakiki vyeti zina usumbufu sana kama nyumbani ni mbali!! Hivyo jiandae na fedha za kukuwezesha kusubiri huko huko kwa muda usiopungua wiki 2. Kama una jamaa zako huko itasaidia sana!! Tuna habari na watu waliochelewa kuripoti baada ya siku 14 kupita lakini walipokelewa vizuri tu. Pia hatuna taarifa ya mtu aliyepoteza nafasi yake kwa sababu ya kuripoti baada ya siku 14. Ila hakuna sababu ya kuchelewa kama huna changamoto zinazokufanya kuchelewa! Na ukipata changamoto inayokulazimu siku 14 zipite, nenda halmashauri iliyo karibu nawe na uwaombe wakupe mawasiliano ya halmashauri unayokwenda na utoe taarifa ya changamoto zako!! Ukishatoa taarifa you are well covered!!
 
Ahsante Sana kwa ushauri huu mzuri Mkuu 🙏🏼
 
Kwa hiyo ukiichukua barua psrs ndani ya wiki unapasika kuipeleka halmashaur husika ndani ya muda gani?
Na baada ya kupeleka barua halmashaur unaambiwa urudi utapigiwa simu, ni baada ya muda gani ndo wanawapigia simu??
 
Nilikua naahitaji muda wa kufanya maandalizi hasa hela ya kujikimu na Lodge
Usifanye makosa ya kwenda huko mbali bila maandalizi mazuri ya kifedha!!. Kumbuka utalazimika kusubiri si chini ya siku 14 baada ya kuripoti kabla ya kuitwa tena ili upewe barua yako ya ajira!. Ukiona unahitaji muda zaidi ya hizo siku 14 ili ukamilishe maandalizi, nenda hapo halmashauri ya wilaya ya kibaha, ukaombe mawasiliano na halmashauri ya kasulu. Uwaambie utaripoti japo kwa kuchelewa kutokana na changamoto za kifamilia! Very serious, kuna vijana wanalazimika kulala kwenye stendi za bus kwa kuwa hawana pesa za malazi pindi wanaposubiria. Pesa kidogo walizo nazo wanazitumia kula kwa mahesabu makali!! Wanaoga kwenye washroom za kulipia! Kibegi kidogo mgongoni wanazunguka nacho mitaani kila kukicha!! Wengine wanalazimika kutembelea site za ujenzi na kubembeleza kibarua!! Hii hatua ya placement japo ni tamu sana lakini ina changamoto ngumu sana kwa baadhi ambao wanajibeba wao kama wao bila kuwa na msaada wa mtu mwingine!!
 
Back
Top Bottom