HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kuna placement nmepata sjaridhika nayo, ila kuna zingine, mbili super zaid nilifanya vizuri ila hawajatoa placement na nahisi zitatoka soon. Sa nawaza nikaripoti au ningoje?
Muda wa kuripoti ni siku 14 tu. Zikipita hizo fasta nafasi yako anapewa mwingine,. Wewe ripoti tu mambo mengine mbele kwa mbele!
 
Ama kwa kweli kila hatua ina changamoto zake, japo makali ya hizo changamoto yanaweza kutofautiana!!
1. Changamoto moto kwenye hatua ya application:
*Mtandao kusumbua wakati deadline ya application imekaribia
*Application kugoma kwenda kwa kigezo kuwa huna sifa, wakati sifa zako ni hizo hizo zinazotakiwa
kwa hiyo nafasi. Mfumo unakuletea meseji ifuatayo:

Job Application FAILED​

Sorry! You can not apply for the job post, kindly Check Academic Programmes Qualifications Requirements for the Job Post

Please read and understand carefuly Job post qualification requirements before applying

Thank You.
*Kusubiri kwa muda mrefu ukiwa kwenye "received" status kabla ya kuitwa kwenye written interview wakati waombaji wa nafasi zingine wakitwa mara kwa mara kwenye usaili.

2. Changamoto kwenye hatua ya written interview:
*Kuitwa kwenye written interview lakini huna pesa ya nauli, malazi na chakula za kukuwezesha kuhudhuria usaili huo! Kwa mfano uko mwanza lakini unatakiwa uhudhurie usaili Dodoma au Dar!
  • kusubiria matokeo ya written interview hadi usiku wa manane!
  • Kuitwa kwenye usaili lakini haujui uanzie wapi kujiandaa kwa maana ya eneo husika ambalo maswali yanaweza kutoka, nk

3. Changamoto kwenye hatua ya oral interview:
  • Kusubiria tarehe ya oral interview wakati pesa imekuishia lakini unatakiwa usubiri pengine siku moja zaidi baada ya writtewn interview!
  • Kutokuwa na uzoefu kabisa kwenye oral interview!

4. Changamoto kwenye hatua ya placent!!
* Kusubiri placement wakati hujui hata ulipata marks ngapi kwenye oral exam!!
*Kusubiri placement wakati hujui kama ulifaulu au ulifeli oral interview maana huwa hawatoi matokeo!
  • Kusubiri kwa muda mrefu utokaji wa pdf maana ndio njia pekee ya kujua kama ulifaulu au vinginevyo!
  • Kusubiri placement kutoka kwenye data base japo huna uhakika kama kweli jina lako liko kwenye data base maana data base hiyo haijawahi kuwekwa wazi!!

5. Changamoto baada ya kulamba asali (kuitwa kazini) na jina lako kutokea kwenye pdf
* Kuamua je uifuate barua byako dodoma au usubiri baada ya wiki moja barua itumwe kwenye anwani yako ulioweka kwenye akaunti yako ? Upande mmoja unasema niifuate lakini tatizo ni nauli!! Upande mmoja unasema watanitumia lakini ikiwa misplaced na siku 14 zikapita itakuwaje? Wengi (karibuni wote) huamua kufuata barua zao dodoma hata kama itabidi wakope kwa riba!!

6. Changamoto baada ya kuripoti kituo cha kazi alichopangiwa:
* Kijana anaripoti akiwa na vyeti vyote original vinaangaliwa, anajaza form za taarifa binafsi nk. Kisha anaambiwa rudi nyumbani hadi tutakapokuita kwa simu!! Hapo kijana hata pesa ya kujikimu kwa siku moja tu hana na nauli nyenyewe alikopa!!, hana mwenyeji ambapo anaweza kujibanza wakati anasubiria huo wito kwa simu!! Afisa utumishi hapo keshamalizana na wewe na kukutaka umpishe ofisini ili mtu mwingine anayetaka huduma yake aingie!! Hakuna cha posho wala baba yake na posho! Kwa vijana wa kiume, wengine wanakomaa tu na kulala stendi za mabasi nk. Kwa mabinti sitaki kuwaza wanafanyaje maana kwao ni risk kubwa sana! Kuna baadhi ya waajiriwa wapya wanasubiria hadi mwezi mpaka kuitwa, wengine wiki moja, wengine wiki mbili na hakuna formula! Mimi naona hii ni changamoto kubwa zaidi japo matumaini ya uhakika yanawabeba kiasi fulani!

7. Changamoto baada ya kupigiwa simu na kutakiwa kuripoti kuanza utumishi wao!
  • Wengi hawajui hata haki na stahiki zao!!
  • Changamoto ya kupata mahali pa kuishi (kwa baadhi ya sehemu), hapo watalazimika kuingia kwenye 18 za madali. Baadaye kro ya mama mwenye nyumba na kero ya wapangaji wenzao!!
  • Mwisho wa siku ni changamoto ya kuona mshahara hautoshi, ni mdogo sana hasa baada ya makato ya bodi ya mikopo kuanza!!

Inabidi watu wajue tu kuwa, changamoto katika maisha huwa haziishi japo makali ya changamoto hutofautiana. Je wewe uko kwenye changamoto ya hatua ipi?

"
Nipo kwenye changamoto ya 7, Kipengele cha pili cha kero za maisha ya upangaji.
 
Kuna placement nmepata sjaridhika nayo, ila kuna zingine, mbili super zaid nilifanya vizuri ila hawajatoa placement na nahisi zitatoka soon. Sa nawaza nikaripoti au ningoje?
Unajuaje kama hizo nyingine ulifanya vzr utumishi hawako hvyo unavyowafkria ...karipoti kzn mzee
 
Ni kweli, kuna pahala wanamapungufu. Mfn, mm nimefanya saili 5, ajabu nilifaulu tangu usaili wa kwanza. Lakini sikujua maana hawatoi matokeo ya oral.

Nimetumia gharama zaidi kufanya saili nyingine 4.

Saivi nmeitwa job kwa ile saili ya kwanza, ambayo naiona sio dili bcoz saili zingine zilikuwa nono na nilifanya poa zaid.

Nifanyaje hapo
Nenda kachukue barua yako psrs alafu angalia mwisho wa kupeleka barua ya kuripoti kwa mwajiri ni lini na huku unakaa na barua unaendelea kusikilizia. Ikifika siku ya deadline ndio unaipeleka sababu unaweza subiria usipate nafasi tena au ukapata pia maana yupo nayemfahamu alipata placement 2 January 2023 na alifaulu zote alipata direct placement bila kusema ni kanzidata
 
Nipo kwenye changamoto ya 7, Kipengele cha pili cha kero za maisha ya upangaji.
Hongera!! Mtu ambaye yuko kwenye kero ya 1-3 anaona ya kwako siyo kero ya msingi lakini na yeye akifika hapo atakuja kuelewa!!
 
Kuna placement nmepata sjaridhika nayo, ila kuna zingine, mbili super zaid nilifanya vizuri ila hawajatoa placement na nahisi zitatoka soon. Sa nawaza nikaripoti au ningoje?
Jamani mbona kila siku mnaambiwa ukipata nafasi nenda ukaripoti, hayo mengine utayaangalia mbele ya safari Mungu akijalia , ila iliyopo mfukoni mwako ndio yako , hiyo iliyopo kwa mtu mwingine hata kama ulimkopesha siyo yako kwa wakati huo, una uhakika gani kuwa utapata nafasi katika hiyo ambayo majibu hayajatoka na je iwapo kama kuna wenzako wamefanya vizuri dhidi yako wakachaguliwa wao, Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa sasa nenda kafanye kazi.
 
Ila = hela
 
Jua katika maisha kila mtu na plan zake usifikiri kila mtu yupo desperate kiasi hicho people have options and their choices. For instance unakuta upo private sector and una biashara yako ipo vizur umeanza kuona matunda alafu ulikua unatafuta kazi gavoo upate job security then unapangwa sehemu ambayo sio rafiki kulingana na mazingira yako hivyo lazima Kuna ugumu unapata
 
Nfikri jamaa katoa ushauri hajamforce jamaa kwamba lazima aende akaripoti
 
Jua katika maisha kila mtu na plan zake usifikiri kila mtu yupo desperate kiasi hicho people have options and their choices. For instance unakuta upo private sector and una biashara yako ipo vizur umeanza kuona matunda alafu ulikua unatafuta kazi gavoo upate job security then unapangwa sehemu ambayo sio rafiki kulingana na mazingira yako hivyo lazima Kuna ugumu unapata
Sasa hiyo ni njema kama una placement mbili mkononi unaweza make decision na siyo placement moja mkononi na nyingine una hakika kama utapata sasa huoni kama utakuwa una make decisions on unlike events.
 
Jamani mbona kila siku mnaambiwa ukipata nafasi nenda ukaripoti, hayo mengine utayaangalia mbele ya safari Mungu akijalia , ila iliyopo mfukoni mwako ndio yako , hiyo iliyopo kwa mtu mwingine hata kama ulimkopesha siyo yako kwa wakati huo, una uhakika gani kuwa utapata nafasi katika hiyo ambayo majibu hayajatoka na je iwapo kama kuna wenzako wamefanya vizuri dhidi yako wakachaguliwa wao, Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa sasa nenda kafanye kazi.
Kuna baadhi ya saili zina namna ya pekee. Ona, nafasi zilikuwa mbili, tuliitwa watatu ila mmoja hakutokea na maswali ya oral yote yalikuwa rahisi kama moja jumlisha moja.

Sasa hapo itakuwaje adi nisiitwe? Kivip niwe na mashaka na hio nafasi mkuu? Nafasi yenyew ni tutorial assistants.

Otherwise Mungu ndie mtoa ridhiki
 
Kuna baadhi ya nafasi zina namna ya pekee. Ona, nafasi zilikuwa mbili, tuliitwa watatu ila mmoja hakutokea na maswali ya oral yote yalikuwa rahisi kama moja jumlisha moja.

Mkuu hujawi kuona re-advertisements? Hua inatokea nafasi ni moja unaenda pekeako na unakosa. Hapa mimi ningekushauri fuata akili yako na si mapenzi ya moyo wako. Nenda ka-report kazini, ya kesho ni fumbo.
 
Hongera!! Mtu ambaye yuko kwenye kero ya 1-3 anaona ya kwako siyo kero ya msingi lakini na yeye akifika hapo atakuja kuelewa!!
Ni kweli kabisa. Kinachokera ni kuwa mtu ulishaachana na hizi kero na kuishi kwa uhuru fulani,
Ila baada ya kupata mrija nd'o unakuja kukumbana nazo.
 
Kuna baadhi ya nafasi zina namna ya pekee. Ona, nafasi zilikuwa mbili, tuliitwa watatu ila mmoja hakutokea na maswali ya oral yote yalikuwa rahisi kama moja jumlisha moja.

Sasa hapo itakuwaje adi nisiitwe? Kivip niwe na mashaka na hio nafasi mkuu? Nafasi yenyew ni tutorial assistants.

Otherwise Mungu ndie mtoa ridhiki
Hiyo sentensi ya mwisho ndio msingi wa kukuongoza, hivyo nenda karipoti kazini.
 
Kuna baadhi ya nafasi zina namna ya pekee. Ona, nafasi zilikuwa mbili, tuliitwa watatu ila mmoja hakutokea na maswali ya oral yote yalikuwa rahisi kama moja jumlisha moja.

Sasa hapo itakuwaje adi nisiitwe? Kivip niwe na mashaka na hio nafasi mkuu? Nafasi yenyew ni tutorial assistants.

Otherwise Mungu ndie mtoa ridhiki
Mkuu, kwani umepangiwa halmashauri gani unayoikimbia kwa nguvu kiasi hicho?

Ila post ya academian ni nzuri kweli kwa wapendao kufundisha elimu ya juu.
 
Kuna baadhi ya saili zina namna ya pekee. Ona, nafasi zilikuwa mbili, tuliitwa watatu ila mmoja hakutokea na maswali ya oral yote yalikuwa rahisi kama moja jumlisha moja.

Sasa hapo itakuwaje adi nisiitwe? Kivip niwe na mashaka na hio nafasi mkuu? Nafasi yenyew ni tutorial assistants.

Otherwise Mungu ndie mtoa ridhiki
Lolote linaweza kutokea Kuna chuo jamaa alipiga oral interview peke yake na kazi hakupata post ikawa re-advirtise tena written aliitwa peke yake. Hivyo kua makini na sijui kama post za tutorial assistant zina database if ukifaulu.
Fanya kama nilivyokushaur chukua barua sikilizia had karibu na deadline if hawajatoa placement peleka barua kwa mwajiri wako
 
Back
Top Bottom