Ama kwa kweli kila hatua ina changamoto zake, japo makali ya hizo changamoto yanaweza kutofautiana!!
1. Changamoto moto kwenye hatua ya application:
*Mtandao kusumbua wakati deadline ya application imekaribia
*Application kugoma kwenda kwa kigezo kuwa huna sifa, wakati sifa zako ni hizo hizo zinazotakiwa
kwa hiyo nafasi. Mfumo unakuletea meseji ifuatayo:
Job Application FAILED
Sorry! You can not apply for the job post,
kindly Check Academic Programmes Qualifications Requirements for the Job Post
Please read and understand carefuly Job post qualification requirements before applying
Thank You.
*Kusubiri kwa muda mrefu ukiwa kwenye "received" status kabla ya kuitwa kwenye written interview wakati waombaji wa nafasi zingine wakitwa mara kwa mara kwenye usaili.
2. Changamoto kwenye hatua ya written interview:
*Kuitwa kwenye written interview lakini huna pesa ya nauli, malazi na chakula za kukuwezesha kuhudhuria usaili huo! Kwa mfano uko mwanza lakini unatakiwa uhudhurie usaili Dodoma au Dar!
* kusubiria matokeo ya written interview hadi usiku wa manane!
* Kuitwa kwenye usaili lakini haujui uanzie wapi kujiandaa kwa maana ya eneo husika ambalo maswali yanaweza kutoka, nk
3. Changamoto kwenye hatua ya oral interview:
* Kusubiria tarehe ya oral interview wakati pesa imekuishia lakini unatakiwa usubiri pengine siku moja zaidi baada ya writtewn interview!
* Kutokuwa na uzoefu kabisa kwenye oral interview!
4. Changamoto kwenye hatua ya placent!!
* Kusubiri placement wakati hujui hata ulipata marks ngapi kwenye oral exam!!
*Kusubiri placement wakati hujui kama ulifaulu au ulifeli oral interview maana huwa hawatoi matokeo!
* Kusubiri kwa muda mrefu utokaji wa pdf maana ndio njia pekee ya kujua kama ulifaulu au vinginevyo!
* Kusubiri placement kutoka kwenye data base japo huna uhakika kama kweli jina lako liko kwenye data base maana data base hiyo haijawahi kuwekwa wazi!!
5. Changamoto baada ya kulamba asali (kuitwa kazini) na jina lako kutokea kwenye pdf
* Kuamua je uifuate barua byako dodoma au usubiri baada ya wiki moja barua itumwe kwenye anwani yako ulioweka kwenye akaunti yako ? Upande mmoja unasema niifuate lakini tatizo ni nauli!! Upande mmoja unasema watanitumia lakini ikiwa misplaced na siku 14 zikapita itakuwaje? Wengi (karibuni wote) huamua kufuata barua zao dodoma hata kama itabidi wakope kwa riba!!
6. Changamoto baada ya kuripoti kituo cha kazi alichopangiwa:
* Kijana anaripoti akiwa na vyeti vyote original vinaangaliwa, anajaza form za taarifa binafsi nk. Kisha anaambiwa rudi nyumbani hadi tutakapokuita kwa simu!! Hapo kijana hata pesa ya kujikimu kwa siku moja tu hana na nauli nyenyewe alikopa!!, hana mwenyeji ambapo anaweza kujibanza wakati anasubiria huo wito kwa simu!! Afisa utumishi hapo keshamalizana na wewe na kukutaka umpishe ofisini ili mtu mwingine anayetaka huduma yake aingie!! Hakuna cha posho wala baba yake na posho! Kwa vijana wa kiume, wengine wanakomaa tu na kulala stendi za mabasi nk. Kwa mabinti sitaki kuwaza wanafanyaje maana kwao ni risk kubwa sana! Kuna baadhi ya waajiriwa wapya wanasubiria hadi mwezi mpaka kuitwa, wengine wiki moja, wengine wiki mbili na hakuna formula! Mimi naona hii ni changamoto kubwa zaidi japo matumaini ya uhakika yanawabeba kiasi fulani!
7. Changamoto baada ya kupigiwa simu na kutakiwa kuripoti kuanza utumishi wao!
* Wengi hawajui hata haki na stahiki zao!!
* Changamoto ya kupata mahali pa kuishi (kwa baadhi ya sehemu), hapo watalazimika kuingia kwenye 18 za madali. Baadaye kro ya mama mwenye nyumba na kero ya wapangaji wenzao!!
* Mwisho wa siku ni changamoto ya kuona mshahara hautoshi, ni mdogo sana hasa baada ya makato ya bodi ya mikopo kuanza!!
Inabidi watu wajue tu kuwa, changamoto katika maisha huwa haziishi japo makali ya changamoto hutofautiana. Je wewe uko kwenye changamoto ya hatua ipi?
"