HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Data haina maana yoyote ile, ifutwe tu.
Iko hivi, sahili inavyoitishwa na kusimamiwa na mwajiri, ni mwajiri ndiye anaye-set minimum standards wa wana ajira wake wapya. Wangu mie ni kituko cha karne, mtu wa database kwa sahili ya katibu msaidizi wa bunge, kupangiwa post ya uhasibu kwa taasisi kisa tu inaonekana alifaulu sahili ya katibu msaidizi na akakosa nafasi, lakini, qualification yake ni muhasibu.

Ukitazama kwa makini, sahili ya katibu msaidizi wa bunge inapima vitu tofauti na majukumu ya uhasibu, hivyo ina apply kwa sahili nyingine.

Pili, kila taasisi hutoa mafunzo kabla ya kuanza majukumu ya kazi rasmi. Kabla ya kufika huko, taasisi husika hupendelea kuona washiriki takita sahili wanafikia viwango wanavyotaka wao, viwango hivyo, hupimwa kwa hiyo mitihani, katika meneo wanayoona wao yanafaa, kumtoa mtu database kumpeleka huko taasisi X kwa kufaulu tu usaili wa taasisi Y, ni kumnyima fursa huyu mwajiri wa taasisi X wa kupima na kujiridhisha juu ya ufaham wa huyu mtu anayeletewa.
Database ifutwe.
Watanzania kinachotu gharimu ni Ubinafsi.....
Nipe utofauti wa Utumishi saili zao na Tamisemi sail zao...
Alafu nani anatakiwa afutiwe Data base
 
Watanzania kinachotu gharimu ni Ubinafsi.....
Nipe utofauti wa Utumishi saili zao na Tamisemi sail zao...
Alafu nani anatakiwa afutiwe Data base
Labda uniambie lini TAMISEMI wamefanya usaili,. Tuanzie hapo.
 
Elewa auditor lazima awe na CPA lakin TMA ni ilikua degree tu ya account
Kuna Kada Wana mitihan ya board hvy mpaka uwe certified
Mfano mawakili na wanasheria wapo wenye degree na wengine wamefanya law school hvy same to accounting
Nikurekebishe hapa kwanza mkuu, kua auditor hakuhitaji ulazima wa kuwa na CPA, kinachohitajika ni kwa muhusika tu kuwa na skill zote muhim kufanikisha utekelezaji majukum kwa ufasaha.

Hii ni kote, kwa auditing firms na huko kwa mkaguzi, na blunder atayofanya auditor katika kipindi cha ukaguzi, office husika huwajibika, maana rahisi ni kuwa mkaguzi huwajibika kwa niaba ya office ambayo ndiyo certified kwa kazi hizo.
 
Achana na io kauli mkuu, kauli ya database ya February inatosha usijiongezee ahadi nyingine.
Ni kweli mkuu, asijiongezee ahadi, twende na hili kwanza la pdf la mama Mhagama, japo hata picha zake, ikiwemo za kikao kile alichotangaza kuhusu pdf, katika tovuti ya psrs wameshazifutilia mbali.
 
Kama unajua hawafanyi usali wanakupa ufahamu wa kufika hapo ulipo wanatoka database...
Leo wenye ufahamu kwnn wafutiwe data base
Hao walichagua mkondo huo, toka awali hakukua na mambo ya kushindanishwa.

Huku upande wa pili, toka awali, ili upate kazi lazima kushindana. Usimamie hapo.
 
Achana na io kauli mkuu, kauli ya database ya February inatosha usijiongezee ahadi nyingine.
Leo Chawene amethibitsha database ipo na ameongeza muda amesema mtu atakaa database kwa muda wa mwaka mmoja, mwaka ukiisha nafasi haijapatikana ndo unatolewa
 
Naomba kuchangia hoja
Kuhusu database ni sawa kabisa wala haina shida interview zimewekwa sababu ya competition haijalishi umefanya usahili wa kazi gani au taasis ipi kwani qualifications za kazi zimewekwa na ipo minimum (entry level) kwa kazi nying za serikali hivyo yeyote yule anaweza fanya sababu training na induction course zipo zinatolewa. Sasa huwez niambia eti kisa nimefanya interview ya TMO kwamba sitaweza kupangiwa taasis nyingine kama account officer hapana usahili lengo lake ni kupunguza watu na kuchuja. Ila kiuhalisia psrs wangejitahid kuwapangia kazi waliopo kanzidata kwa sababu ni Moja ya jukumu lao
Usahili lengo lake ni kupima candidate juu ya uelewa/umahiri wake katika kada husika na ndio maana usahili wa TMO uli-base katika module/course za tax pekee na si vinginevyo, maana yake, muajiri alitaka watu wenye uelewa/umahiri wa kuribdhisha katika field ya Tax.

Vivyo hivyo, usahili wa Auditor II NAOT, ulibase katika modules/course ya auditing tu, kwa kuwa, muajiri alihitaji watu wenye uelewa/umahiri wa kuridhisha katika field ya auditing.

Kwa lugha rahisi, kupitia psrs, muajiri hupima candidate kwa core module/course, hii hutoa base ya kutambua umahiri wa candidate, hizo induction ni kukazia tu kama muendelezo baada ya kupata watu waliofika vigezo husika.

Lazima uelewe kuwa, core module/course kwa kada moja ni tofauti kabisa na core module/course ya kada nyingine japo qualification yawezekana kuwa ile ile.
 
Leo Chawene amethibitsha database ipo na ameongeza muda amesema mtu atakaa database kwa muda wa mwaka mmoja, mwaka ukiisha nafasi haijapatikana ndo unatolewa
Database ipo kitambo sana hata pdf za miaka ya nyuma zilikua na data base, uwo mwaka mmoja ata kabla ya chawene ulishaongezwa,

Vijana wanateseka mtaani, kwakuwa vijana wana vyeti vinavyo onesha wana ubora kutoka kwenye vyuo vyao, na wamefanya written wamefaulu wamefika adi oral, na dhani ningekua mm kila aliefika oral alie fika 50 anapaswa kupangiwa kazi kwanza kwa kada yake kabla hujaitisha inter... zingine, kasoro kwa sectors za edu na zinazoutaji watu wenye experience hizi huwezi kutoa watu database ni kuitisha interv tu.
 
Kasema wanamalizia zile za mwaka jana kabla ya mwaka wa fedha kuisha ndipo waanze zile 45,000 kasema hawataanza kuajiri hivi 45,000 bila kumalizia 21,000
Wimbi la 1700 database niliona lilivo vurugaa akili za jobless humu ndani, bado miezi mitatu mwaka wa fedha uishe jobless akijiandaa tena kisaikologia na zisitoke asee siopoa, afya ya akili ni muhimu sana ni bora watu washtukie wametoa.
 
Back
Top Bottom