HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
So kwa sasa hivi mpo tu?
Habari,
Inaonekana siku 14 ni siku za kazi za serikali jumatatu hadi ijumaa kwaiyo siku 14 kutoka tarehe 14 February zinatimia tarehe 6 march nadhani tarehe 7 march wiki ijayo watatoa tangazo la kutuita kusajiriwa na TRA.
 
Anataka kuturudisha enzi za
Mkurugenzi- Shayo
Meneja - Mushi
Muhasibu-Tesha
HR- Shirima
Watu wanatangaziwa nafasi za kazi kabla hazijatoka zikitoka inakuwa geresha tu. Mimi namfahamu dogo tulikuwa nae UDSM yeye alipomaliza Form six akaanza kufanya kazi TANAPA kama volunteer lakini analipwa baba yake alikuwa Top layer huko TANAPA. Alipomaliza tu chuo kaajiriwa huko huko. UTUMISHI IDUMU MILELE sasa hivi mtoto wa masikini anaweza kuingia TRA
Kwani huyo dogo aliajiriwa peke yake? si alipita pomoja na wenzie .

Mfano tanapa wanahitaji watu madereva 10, IT 4, wildlife conservation 20, , kwa hiyo uyo kigogo atamuweka mtoto wake bila kuwa na vigezo .
Wakati hayo majina na cv zao zitapitishwa kwenye bodi kwa ajili ya kuhakiki.

Na ndio maana huyo Mzee alimchukua dogo akam somesha apo mweka wildlife Ili akimaliza TU . Zitakapotangazwa nafasi . Amsaidi mwanae apate kazi .

Huyu dogo alipata kazi akiwa na vigezo vyote sio kama alibebwa TU. Na huyu Mzee ni mtu wakuigwa kwa sababu anajali familia yake

Alafu mbona kama unachuki na hili kabila👆😁
 
Kukosa ajira kusikie tu kwa mtu akijisemesha, unaweza ona dunia si sehemu salama ya kuishi. hawa UTUMISHI nafasi wanatangaza sawa,ila kupata bdo kiiza nene ila hatukati tamaa coz hatuna options.

Wengi wetu utasikia ,namfahamu jamaa yangu kapata kazi utumishi bila connection!! mkuu how sure you are?
Njia ipo nayo ni
Rais wetu mpenda haki aruhusu TU taasisi na mashirika, wafanye saili wenyewe.

Utokaa ulalamike Tena kwenye huu uzi
 
mmmmh kwa uelewa wangu japo sio deep sana nafikiri utumishi hawahusiki na suala la kulipa watumishi mishahara kwabhiyo ishu ya ucheleweshwaji wa ajira inawezekana hata mlipaji ambae ni hazina anahusika na kibali cha kupitisha budget ya mishahara nafikiri kinatoka kwa General Secretay wa ikulu hadi rais alidhie pia hapo kwenye hiyo chain

taasisi hazijazuiliwa kutangaza bali zinaajiri lkn in contract terms na wanalipa wao kama taasisi

hata za kudumu ukisema taasisi iajiri kama hamna hela ya kuwalipa mshahara kutoka hazina watu watachelewa tu kupangiwa viruo vya kazi

hitimisho Sekretarieti ya Ajira iendelee tu maana kwenye ma taasisi kuna vituko sana wanaajili kwa kuangaliana ndugu wa watumishi mule mule ndani ya taasisi either inaweza kuwa watu wa dini flan au kabila flan ambayo ni hatari sana hiyo
Sijasema kwamba utumishi ndio wanatoa mishahara,

TATIZO:
Bureaucracy kwenye usaili kupitia utumishi.
Ivi mnajua Kuna watu wanasuburi placement huu mwaka wa pili Yan.

Ila kama usaili ungefanyika kwenye taasisi na mashirika. Wala huu uzi usingekuwepo.
 
Duuuh huwa nasikia tu connection ila duuuh siamini maana huyo mtu akushikilie kuanzia written hadi oral kazi sana.japo kweli kuna watu unaona kabisa huyu alishikiliwa kufika pale sio yy
Watu wameingia oral TRA wana majibu yote
 
Nimeguess tu bt sku hizi si ni wanafanya kikanda
Kwa ninavyo jua kila mamlaka ya maji ina jitegemea na zina jiendesha mapato yao na usahili unafanyika mahala mamlaka ilipo na mshahara hupo tofauti kwa kila mamlaka mtalipwa kulingana na makusanyo kwa jinsi yanavyo patikana
 
Oooh sawa. Nlifkr ikitangazwa utumishi bas utumish ndo wana mamlaka wap interview zifanyike
 
Maombi yanatumwa kwa njia ya posta au barua pepe. Wakikuitaji wanakuita kwa ajili ya maojiano.

Hakuna muda wa kupoteza mara written, practical, oral , alafu hakuna kitu
Hayo mambo ya kuitwa moja kwa moja kwa isaili wa mahojiano unakua umetumia criteria zipi kama sio privelleges opportunity ambazo sisi ndio hatuzitaki ziendelee kuwepo

Ndio mana Sekretarieti ya Ajira ikaamua kuwa transparent kwa kuweka usaili wa mchujo (written interview) kuepusha hayo mambo

Ndio inawezekana connection zipo kupitia utumishi lkn sio kama taasisi zikipewa kibali cha kuajiri ajira za kudumu
 
Sio kweli , kama huna ndugu aliyesoma fani hiyo utaweza kumuweka .

Na ukumbuke taasisi na mashirika zinazo bodi zinazo hakikisha Kila kitu Kiko sawa
Naamin unatambua kuhusu mana ya rushwa mfano mm ninaweza kuwa sina ndugu ila kama nimtumishi wa EWURA na wametangaza kazi watakujabwatu tu lazima kunishawishi kwa sababu nipo EWURA niwataftie tobo kwa gharama tutayokuliana ukizngatia uwezo huo labda ninao wa kuwaconnect.
 
Kwani huyo dogo aliajiriwa peke yake? si alipita pomoja na wenzie .

Mfano tanapa wanahitaji watu madereva 10, IT 4, wildlife conservation 20, , kwa hiyo uyo kigogo atamuweka mtoto wake bila kuwa na vigezo .
Wakati hayo majina na cv zao zitapitishwa kwenye bodi kwa ajili ya kuhakiki.

Na ndio maana huyo Mzee alimchukua dogo akam somesha apo mweka wildlife Ili akimaliza TU . Zitakapotangazwa nafasi . Amsaidi mwanae apate kazi .

Huyu dogo alipata kazi akiwa na vigezo vyote sio kama alibebwa TU. Na huyu Mzee ni mtu wakuigwa kwa sababu anajali familia yake

Alafu mbona kama unachuki na hili kabila👆😁
Yaan kabisa na ww unafurahia aona hiyo ya methodology? kwaio mzee anamuweka mtoto wake.mtoto wake nae atamuweka mtoto wake, bro utumishi wa umma sio kama familia ya malkia elizabeth
 
Sijasema kwamba utumishi ndio wanatoa mishahara,

TATIZO:
Bureaucracy kwenye usaili kupitia utumishi.
Ivi mnajua Kuna watu wanasuburi placement huu mwaka wa pili Yan.

Ila kama usaili ungefanyika kwenye taasisi na mashirika. Wala huu uzi usingekuwepo.
Isje ikawa na sisi wa Nov 28 tutasubiri hadi mwaka[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom