HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Waidhinishe nn mkuu, ni ukiritimba tu unafanyika pale ndo maana Rais na Waziri wake wamewachana live.
Waziri kasema hizi Ajira zote ni za Mwaka wa fedha huu unaoishia na naweza kusema hata nusu ya kazi hawajafikia, je mwaka huu Rais akija kutoa kibali cha Ajira 30,000 kupitia utumishi wataweza kweli..?
ila si bado bajeti nyengine haijapitishwa na bunge. hadi bunge la bajeti lije likae tena watakua wametoa pdf zote zilizosalia.

ni kweli wanapaswa waongezi speed maana tayari hizo taasisi zilishawasilisha vibali vya ajira sekretariet ya ajira.


kama taasisi ilishawasilisha kibali na wao wakasimamia michakato yote ya ajira hadi oral, basi wanapaswa watoe hizo placement za november and december maana inaonekana tayari selection zilishafanyika bado ku apload tu hizo mikeka.
 
kumbe matokeo yote kuanzia written hadi oral yanaunganishwa kupata average moja
Screenshot_20230217-210829~2.jpg
 
kifungu cha 2. mfano kada moja imesailiwa na jopo zaidi ya moja..

let say iyo kada imefanya written , prac na oral... hapo si imesailiwa na majopo matatu
Hapo wanaanisha majopo ya oral, unakuta mfano TRA oral watu 500+ lazima kunakua na majopo mengi.

Hapo ndo ukusanya matokeo ya majopo yote na kuyapanga
 
navofahamu written ina jopo lake la kusaili, oral ina jopo lake la kusaili , na wale wa practical wana jopo lao. mm ndo nlivoelewa.


ngoja ntume
Mkuu, jopo kwa lugha ya malkia ni panel, kuna saili zile za watu wachache, mfano wanaitwa 6 kwa post moja, ni wazi hapa watasailiwa na jopo moja tu, lakini kuna saili zinaita watu 600+ kwa post 150 kwa mfano, hapa lazma wasailwa wagawanye katika ma-group ya watu mfano 20, kwa mgawanyo huo, utapata grup 30, kila grup litasailiwa katika jopo lake, hivyo utakua na majopo 30 katika usaili huo. Baada ya usaili, kila jopo hukusanya matokeo yake kwa huyo katibu kwa majuisho katika ili kutoa mkeka mmoja.
 
Kaka mzigo huu hapa tutetee wanyonge.
Hivyo vipengele vinaongelea uwasilishwaji wa matokeo.

Kuna written zinafanywa kwenye majopo tofauti mfano kikanda...hivyo matokeo ya kila jopo yatakusanywa kupanga wa kwanza hadi wa mwisho.

The same na kwenye practical na Oral ikiwa kuna majopo tofauti.

Kujua kwamba matokeo ya written na Oral hayajumlishwi, soma kifungu cha 16 kipengele cha 3, hapo wanaeleza kabisa ikiwa usaili unahusisha practical na oral basi matokeo yatajumlishwa kupata alama za jumla.

Hakuna sehemu inaonesha matokeo ya mchujo kujumlishwa na matokeo mengineyo.
 
Back
Top Bottom