HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kuhusu kuwa na matamanio na malengo, nadhani hapa vijana wengi hatujui tunataka nini na tunataka kufanya kazi wapi ila wengi wetu wanataka wapate kazi tu. Nadhani hii dhana ya kutaka tu kazi inaondoa morali na hata maandalizi ila kama ukiweka nia ya dhati vipi hata ufeli vipi bado utanyanyuka na kuendelea kupambania. Mimi binafsi ndoto yangu imetimia kwa sababu wakati nipo Advance nilikuwa chairperson wa Tax club hivyo nilikuwa naenda sana kwenye ofisi zao na nilikuwa navutiwa sana. Chuo Nimesoma Mzumbe na kwa utaratibu mwaka wa tatu semister ya kwanza tunakuwaga field semister nzima. Nilifanyaga field yangu TRA kulingana na mazingira ya kazi na ushirikiano niliopata kutoka kwa wafanyakazi niliweka nia kuwa nitakuja kufanya kazi TRA haikuwa rahisi. Kwanza toka 2018 sikuwahi kupata nafasi ya kufanya interview za TRA. Nakumbuka 2018 niliomba kazi(zile ambazo zilifanyika uwanja wa taifa 2019). Nikaitwa kwenye nafasi ya account officer. Nakumbuka siku majina yametoka ndo nilikuwa nipo njiani naenda Dodoma kureport kwenye kibarua nilichokuwa nimepata hivyo nikashindwa kuifanya ile interview. 2019 niliomba tena ambapo interview yake ilifanyika 2020 (sikuitwa kwa sababu nilikuwa sijasaini barua). Nikaomba tena zile za 2020 (ambazo interview yake ilifanyika 2021). Hii interview nilikuwa shortlisted na kiukweli nilikuwa nimeipania sana na nilisoma sana (kwa kushirikiana na washikaji zangu ambao walitoka Dar wakaja kuweka kambi Dom). Tulikuwa tunaenda pale CBE kuanzia saa kumi na moja (baada ya mimi kutoka kibaruani na muda huo washikajj wameshapika magetoni) na kurudi saa sita usiku au saa saba. Pepa kwetu lilikuja poa kwa sababu karibia vitu vingi nilikuwa nimesoma (hasa custom). Bahati lile pepa likafutwa baada ya kuvuja. Nafasi zilipotangazwa tena nikaomba ila sikuwa shortlisted kwa sababu sikuwa nime certify vyeti vyangu(niliumia sana), majina ya walioitwa kazini mwaka jana yalivyotoka niliyaangalia nikasema na mimi nilistahili kuwepo humu ila sijachelewa. Walipotangaza tena nafasi nikaenda kucertify vyeti nikaomba. Majina yalivyotoka nipo shortlisted sikupata ugumu kusoma kwa sababu material nilikuwa nayo. Kutoka hapo kila kitu kwangu kimekuwa historia yenye kumshukuru na kumtukuza Mungu wangu mosi, kwa kunipa kazi, pili kwa kunipa kazi nayoipenda na niliyokuwa naitamani maishani mwangu. Kuna kipindi nilikuwa nikikosa marks chache za kunipeleka oral nilikuwaga najifariji kimoyo moyo kuwa labda ningeenda oral ningepata kazi ambayo siyo niliyokuwa naitamani [emoji23][emoji23][emoji23]. Kwa hiyo washikaji zangu wekeni nia wakati mnasubiri nia zenu kutimia endeleeni na majukumu mengine ya kujikimu kimaisha mpaka pale wakati wako utakapofika japo haimaniishi kila utakachokitilia nia ndo utapata unaweza kuwa umetilia nia kitu flani ila Mungu akawa anaona kuwa unatakiwa kupata zaidi ya hicho. Mungu hukupa unachostahiri. Ni vyema pale unachostahiri ndicho ulichokuwa unataka ila ni vyema zaidi pale Mungu wetu anapoamua kukupa zaidi ya kile ulichokuwa unataka.
Hii story yako Fupi inatuambia na kutufundisha Kukata Tamaa mwiko na kila jambo na Wakati wake.Penye Nia Pana Njia.
Kikubwa ni kupambana kwenye Yale malengo yako unayoyaamini.Hakika Mzee umetisha sana.Mungu akubariki na uwe na kazi njema huko TRA.
 
Mkuu unaweza kuamini kuwa mimi kwenye upande wa education nilitaja chuo tu pamoja na experience niliyo nayo. Sababu ya kufanya hivi niliponzwa na You tube. Nilikuwa nafuatilia videos you tube kuhusu hilo swali na kuna video ya mzee mmoja anafuatiliwa sana alisema kuwa kuna tofauti kati ya tell us about your self and introduce your self. Nakumbuka alisema kuna moja (sikumbuki ni ipi kati ya hizo) inakutaka tu ujitambulishe shortly na kuna nyingine ndo inataka uende deep. Kuna sehemu pia pakasema kuwa kama unafanya interview katika private sector yakupasa uende deep kwa sababu wale jamaa ni performance oriented( yaani kabla ya kukuajiri watataka waone kwanza matokeo yako ya o level na jinsi ulivyo score kila somo) ila hiyo ni tofauti na public sector. Basi mimi nilibaki na notion hiyo na hata nilivyoulizwa nilistick tu na elimu ya chuo na experience. Japo huu mjadala wakati unaendelea humu ulikuwa unaniumiza sana maana nilikuwa najiona kama nimefeli japo nilipokuwa nikikumbuka yale maswali mengine nilivyoyajibu nilikuwa nafarijika.
Hongera sana mkuu! Wakati wa Mungu ni sahihi
 
Hii story yako Fupi inatuambia na kutufundisha Kukata Tamaa mwiko na kila jambo na Wakati wake.Penye Nia Pana Njia.
Kikubwa ni kupambana kwenye Yale malengo yako unayoyaamini.Hakika Mzee umetisha sana.Mungu akubariki na uwe na kazi njema huko TRA.
Aminaa mkubwa
 
Naombeni kuuliza kwa wenye ufahamu na hili jambo mnisaidie, hivi barua ya kuitwa kazini inavyoandikwa kuwa uripoti ndani ya siku 14, Lakin barua imeandikwa tokea tarehe 04 mwezi wa pili.. hapa wanamaanisha nn kuwa wanahesabu siku 14 tokea tarehe barua ilipoandikwa au wanahesabu tokea siku waliyotuita kwenda kuchukua barua!!
 
Wakuu habari hongera kwa waliopata nafasi na waliokosa wasife moyo wakati wa Mungu ni wakati sahihi , jaman mi nataka kuuliza mfano post ina comprise kada tofauti tofauti hapo maandalizi unasomaje? Mfano hizi post za WCF.
 
Back
Top Bottom