Loh! Jamani pole sana Mungu akutie nguvu hata nami nimejiskia vibaya,kama nilivyokuambia utayaona na utasikia mengi kikubwa kuwa na moyo wa chuma.Mwenyezi Mungu awalinde maana naona huyu wifi anaweza fanya mambo siyo mazuri hana wema tena nawe. Kama nyumba ina ulinzi tafadhali imarisha ulinzi na siku nyingine asiruhusiwe kuingia ndani kabisa.
Pia haina haja ya kuficha waambie tu ukweli kuhusu shangazi yao ila wafundishe wasimchukie wapende na wamuombee yamkini ajitambue naamini umenielewa nachomaanisha,inshort waambie ukweli ila usipande mbegu ya chuki, usipowaambia shangazi ataendelea kuwaharibu sana kisaikolojia.