Kwanini upange sheria nyumbani kwangu?

Kwanini upange sheria nyumbani kwangu?

Hivi ni kweli unachosema kwamba hujui cha kufanya au?!! Watu mna mioyo jamani, unawezaje kuvumilia huo upumbavu home kwako mwenyewe? Kwa nini mtu wa kuja akukoseshe amani nyumbani kwako? Cha kufanya, timua wote yeye pamoja na huyo wifi yako na watoto wake. Kubali lawama za kijinga lakini unusuru ndoa yako, we endelea kuwakumbatia kama familia haijasambaratika kwa uoga wako wa kijinga.
 
Embu mtimue acha uoga kha! Bora angekua housegrl wake . Shogaa chaaa! Au nyumba kajenga wifi? Mtimue oho ipo cku utamkuta kitandan kwako

Wallah simuogopi ila staki waseme nimewafukuza au staki wageni, Leo nasubiri Mzee arudi na huyu bwana Hana subra atawatimua wote ...
 
Hivi ni kweli unachosema kwamba hujui cha kufanya au?!! Watu mna mioyo jamani, unawezaje kuvumilia huo upumbavu home kwako mwenyewe? Kwa nini mtu wa kuja akukoseshe amani nyumbani kwako? Cha kufanya, timua wote yeye pamoja na huyo wifi yako na watoto wake. Kubali lawama za kijinga lakini unusuru ndoa yako, we endelea kuwakumbatia kama familia haijasambaratika kwa uoga wako wa kijinga.

Ni kweli Nnayosema ndio mana nikamwita wifi awe shahidi, sababu nikija kumwambia huyu bwana Hana mswalie mtume patazuka kizaazaa na watasema siwataki sababu wao masikini maneno tele...
 
...
are_you_serious_xlarge.jpeg

We acha tuu Shosti..
 
Usipoziba Ufa utajenga Ukuta, na siku zote usipo kemea ubaya basi Waufurahia weye!. Kabla hujamfukuza mueleze namna ya kuishi hapo kwako then akiendelea na tabia yake, fukuza wala sio dhambi. Au omba ushauri kwa huyo wifi yako "ambae walifika pamoja" kwamba ufanyeje asije akaharibu ndoa.

Usipofanya maamuzi magumu na yaliyo sahihi anaweza Akawaachia maradhi nyumba nzima, siku hizi undugu umebaki kufanan sura tu! mambo mengne changamka mweyewe mama!!!!!

Asante Leo jioni ntamwambia wifi, kieleweke kimoja...
 
Ni kweli Nnayosema ndio mana nikamwita wifi awe shahidi, sababu nikija kumwambia huyu bwana Hana mswalie mtume patazuka kizaazaa na watasema siwataki sababu wao masikini maneno tele...

Ndio maana nikakuuliza hivi ..unakubali familia yako kubomoka kwa kuogopa hayo maneno ya kijinga? Kama sio lawama za kutunga unaogopa nini? Utajakumbuka shuka kumekucha wewe...
 
Mamaye zake....
Timua haraka sana....
Tena fungasha virago tupa nje...

Sikufichi naku admire ulivyo, mie kuongea naweza ila ugomvi ndio sipendi, kama Mdogo Wangu hata makofi nampiga ila upande wa mume hawana kheir wala hawasarifiki ...
 
Shoga wa wifi aje kukaa likizo nyumbani kwako kwa mwezi mzima kwasababu zipi za msingi?!Huna ushoga nae, huna undugu nae wala sio ndugu wa mume wako anakuwaje confortable nyumbani kwenu mpaka kuwatupia condom sebleni kwenu??!

Aondoke. Kama wifi yako anampenda sana waongozane!!!!

Yani Mpaka sasa sija changanyaa, najiuliza zile condom kavaa Nani? Ndani kuna vijana wa3 mlinzi, gardener na driver wa Mzee na Mzee..
 
Kunawatu wanavipaji vya kulea uozo!!!
 
Wifi na shogake, we unaishi mkoa gani na wao wametoka wapi?Njia sahihi ni kumwambia huyo wifi yako kwamba hupendezwi na mwenendo mzima wa rafiki yake kama hawezi kujirekebisha arudi tu alikotoka.

Niko Zanzibar wifi anaishi comoro.. Vibaya kumsema mtu ila tkt yakujia Mzee ndio katoa na shogake amekuja miezi 6 ilopita wakachukuana kutoka Dar wakaja wote....
 
Weeeeee...
Ukute wifi yako kamleta shoga yako kwenye misheni ya kumfanya yeye mama mwenye nyumba. Ndo kashaanza kazi hivyo, atafanya vituko mpaka kieleweke.

Oooooh usinambie hivo ebu Nipe moyoo angalau, moyo unaniuma ivo sijui ile condom katumia naniiii..
 
Pole sana usifumbie macho hayo usiyoyapenda kaeni wote watatu wewe,wifi yako na rafiki yake tafuta pia ndugu mwingine ambaye atakuwa kama shahidi wako,eleza yote usiyoyapenda na unapenda vipi maisha yenu hapo yaweje na wape live kwamba kama siku nyingine watakiuka hutamvumilia mtu tena atafungasha virago vyake.
 
Ndio maana nikakuuliza hivi ..unakubali familia yako kubomoka kwa kuogopa hayo maneno ya kijinga? Kama sio lawama za kutunga unaogopa nini? Utajakumbuka shuka kumekucha wewe...

Leo namwambia Mzee Manake sikufichi roho inaniuma ilibaki basi..
 
Mtimue shenzi sana na huyo wifi ako ndio nini kuja na shoga yake
 
Pole sana usifumbie macho hayo usiyoyapenda kaeni wote watatu wewe,wifi yako na rafiki yake tafuta pia ndugu mwingine ambaye atakuwa kama shahidi wako,eleza yote usiyoyapenda na unapenda vipi maisha yenu hapo yaweje na wape live kwamba kama siku nyingine watakiuka hutamvumilia mtu tena atafungasha virago vyake.

Asante Leo ntamweleza, huwezi kuamini nimemweleza Mdogo Wangu eti kanambia mie nna damu ya zeru zeru ndio mana nimezubaaa... Yani nasikia uchungu , haya nasubiri Mzee aje tuliongelee..
 
Halafu Mbaya zaidi hakusema kama anakuja na shogake...

Undugu wa hivyo mimi siutaki kwakweli khaaa!!! Kwanini asimpeleke huyo shoga yake kwake sio ustaarabu fanya haraka waende kwao kama hawana sehemu ya kuishi wakakae hata stendi pumbafu sana hao
 
Sina kua na tatizo wakae Mpaka likizo ishe lakini Kwa ilipo fikia bora ajipange, maneno ntayakubali japo yataniuma....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom