Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Umejibu vema sana naweza kusema kuliko wote hapo juu. Umejibu swali hivyo kufuata itifaki. Mmoja ameuliza swali badala ya kujibu swali. Kumbe Kiranga ulikulia katika Ukristo na ulikuwa muhudhuriaji mzuri wa kanisani eeh?! Nimefurahi kufahamu, nime add kitu kichwani.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
"Ulikuwa umejiandalia majibu haya??!"
"Umemwogopa jamaa??! Mbona kwenye jibu lake maswali kibao?!...."
 
Hii hoja iko nje ya mada.

Hivyo, haifai hata kuendelezwa kwa kujibiwa.

Anzisha uzi wako wa mazuri ya kanisa, nitachangia mengi.

Mimi babu yangu alikuwa mchungaji, nyumbani kwetu ni pembeni ya kanisa.
inawezekana kwa alikuwa mchungaji ,hio haimaanishi kuwa aliijua Kweli.Halafu sijagusia chochote kuhusu mazuri ya Kanisa mkuu,
 
Na kwenye makongamano ndio balaa zaidi. Mchungaji wa kutoa neno anaanza saa kumi na Moja, ujumbe mkuu ni matoleo mpaka mwisho. Akafu unaambiwa Kwa upole muda wa kutoa, jitahidi utoe zaidi ili ubarikiwe zaidi. Yaani ni hatari kabisaaaaa siku hizi. Na makanisa yanajazana kila Kona.
Kutoa sio kosa ila sio focus ya imani ya ukristo.Na ikiwa ni focus tunapaswa kujua kwamba tunatoa kwa upendo sio kwa kulazimishwa kwani yeye [Kristo] alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu.
Focus ni kukua kiimani kwa kumjua Kristo aliyeandikwa kwenye maandiko tangu mwanzo-ufunuo kwa kujifunza maandiko matakatifu kwa usahihi kwa msaada wa Roho mtakatifu.
Hatupaswi kutoa kwa mlengo wa kupokea zaidi bali kwa upendo ambao tumejifunza kutoka kwa Kristo.
 
"Ulikuwa umejiandalia majibu haya??!"
"Umemwogopa jamaa??! Mbona kwenye jibu lake maswali kibao?!...."
Big No! Kiranga hakuweka complications. Si mara ya kwanza kukutana naye kwenye hoja. Ukiuliza swali anajibu swali badala ya kuuliza swali, nimempongeza kwa hilo. Kuhusu mtazamo wake, nauheshimu.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa muumini mzuri sana, basi mwaka 2014 nikiwa pale UDOM maeneo ya Ng’ong’ona baada ya kutoka zangu misa ya kwanza, nikapewa taarifa kuna Lecture anafungua Bar & Gest huko ujasi.

Mwamba nilikuwa nahudhiria sana ishu za sturi ndefu so nami nikawa mmoja wa waalikwa katika uzinduzi huo. Mungu si Athumani kumbe pia wapo jamaa zetu wa mbuzi katoriki nao wamealikwa!!

Kinywaji kikakolea, nyama choma zikaliwa story nazo zikanoga ci ndo mafather wakaanza kufunguka…..” tunagonga sadaka zenu za leo ni pombe na nyama tu” daah naikumbuka siku ile wakanipa na mishe ya kutafuta “totoz” za chuo!! Mambo yakawa sawa, wakaniacha na 50.

Ki ukweli toka siku hiyo sikuwahi sali tena…japo kwa sasa nshakuwa mtu mzima nawaza KURUDI CHURCH MAANA KUNA FAIDA NYINGI SANA ZA KIJAMII HASA KULIKO KUTOKWENDA.
 
Huwezi kumkuta Muislamu hata akiwa haendi msikitini ,haswali na mfanya maasi akijianika na kujisifia kuwa haendi msikitini ,labda huyo awe ameachana na imani ya mara nyingi huwa ujasiri huo hana kwani nafsi yake itakuwa inamsuta.

Misingi ya Uislamu ni haitakiwi mtu kutangaza uovu wake ikiwa Mwenyezi Mungu amemsitiri kwani ni uovu mkubwa mtu kufanya kibri katika maasi na kujisifia kuliko hata uovu wa kosa lenyewe.Na kuna uwezekano mkubwa asitubie kwa kuona ni kitu kizuri ila yule mwenye hofu na akaficha aibu zake kuna uwezekano mkubwa wa kupata rehma akatubu au kusamehewa.

Ila nashangaa upande wenu kila mtu anafunguka bila wasiwasi kama amefanya jambo ambalo zuri , huu sio uzi wa kwanza upo uzi mwingine watu wakijisifia masiku ambayo wasiyoenda Kanisani wakijiona watabe . Unakuta na mtu humu anahubiri neno la biblia lakini u amkuta kesho anapost uzi jinsi anavyogegeda watoto wa watu tena wakati mwingine akijisifu bila aibu.
Uko sahihi mkuu Uislam una misingi imara sana sio rahisi mtu kuyumba kiimani

Kingine kwenye ukristo wamepeana uhuru sana .Angalia wanaovaa tu nguo za ajabu mitaani asilimia kubwa ni wanaojiita wakristo angalia walevi wengi na wanaoona kuzaa nje ya ndoa ni ujanja ni upande huo huo

Huwezi kuta kijana wa kiislam akajisifia kuhusu uzinzi au ulevi

Sent from my SM-A145F using JamiiForums mobile app
 
Kwamba jua linazunguka kumbe dunia ndiyo inazunguka. Galileo aliwasanua wengi mno.

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
Of course kujua sayansi ni muhimu lakini ni muhimu zaidi kujua kwamba unapata uzima wa milele kwa kumuamini mwana wa Mungu peke yake (yohana 3:16,yohana 6:40)na sio kwa kutegemea matendo yako ya wema (good deeds).
Maisha ya hapa duniani yapo lakini baada ya kufa inakuwaje pia ni muhimu kujua.
 
Ni kumuamini pekee au na kufuata amri zake? Na amri zake unajua ni zipi?

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: apk
Mimi siwezi kuacha kwenda Kanisani. Mambo ya Imani yanaendana na ufahamu wa mambo ya kiroho, ambayo ni ngumu sana kuyaelezea kwa ufahamu wa kawaida. Pia mambo ya Imani na uhusiano na Mungu no mambo binafsi. Kujua uwepo wa Mungu kunatokana na uzoefu binafsi wa mtu anavyomfahamu na kuhusiana na Mungu. Hayo mambo hayatambulikani kwa reasoning za kimwili, ukiyaendea kimwili lazima utakwama na kuishia kusema hakuna Mungu. Mungu yupo, ila ukiwa na ufahamu finyu wa mambo ya kiroho, utaishia kusema hakuna Mungu.
 
Umejibu vema pia! Umeeleza vizuri.!

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Michango imezidi sana, michango yenyewe hainufaishi waumini moja kwa moja, mara mchango wa ujenzi, mara kiwanja, mara gari wakati we huna nyumba huna baiskeli huna biashara, hela inatakiwa tu. Usipotoa utatengwa au kupakaziwa una dhambi ufukuzwe
Huu uongo jmn
Wapi huko usipotoa unatengwa?
Maana kutoa ni hiari
 
Heri ya Jumapili kwa nyote.

Niende madani sasa.

Kwa nini uliacha kwenda kanisani mpaka leo hii? Ni nani au nini kilikufanya usiende tena kanisani? Mbona ulikuwa muumini mzuri tu na ulikuwa kiongozi wa vijana? Mbona ulikuwa kiongozi wa kwaya nk?

Unaweza ku share hapa sababu hasa iliyokupelekea ukaacha kwenda kanisani? Je, uliona ni usanii tu?

Karibu!

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
Siwezi acha kwenda kanisani sbb,kwanza simfuati mtu,ukishalijua hili hupati shida..

Shida ni kuwa watu wengi hata hawajui kanisani wanaenda kufanya nn,hawajui wanaenuabudu ,wanaenda Kwa mazoea tu,...
Kajikuta mkristo basi anaenda kanisani km desturi
Hawa wanaweza kuacha ..
 
Nilikuwa muumini mzuri sana, basi mwaka 2014 nikiwa pale UDOM maeneo ya Ng’ong’ona baada ya kutoka zangu misa ya kwanza, nikapewa taarifa kuna Lecture anafungua Bar & Gest huko ujasi.

Mwamba nilikuwa nahudhiria sana ishu za sturi ndefu so nami nikawa mmoja wa waalikwa katika uzinduzi huo. Mungu si Athumani kumbe pia wapo jamaa zetu wa mbuzi katoriki nao wamealikwa!!

Kinywaji kikakolea, nyama choma zikaliwa story nazo zikanoga ci ndo mafather wakaanza kufunguka…..” tunagonga sadaka zenu za leo ni pombe na nyama tu” daah naikumbuka siku ile wakanipa na mishe ya kutafuta “totoz” za chuo!! Mambo yakawa sawa, wakaniacha na 50.

Ki ukweli toka siku hiyo sikuwahi sali tena…japo kwa sasa nshakuwa mtu mzima nawaza KURUDI CHURCH MAANA KUNA FAIDA NYINGI SANA ZA KIJAMII HASA KULIKO KUTOKWENDA.
Haya
Tuma salamu kwa watu watatu
 
Back
Top Bottom