Michango mingi sanaaaaaaa sanaaaaa, Yesu hakuchangisha watu fedha mabilioni hivi, kanisa limekuwa linafanya biashara ya kukusanya fedha bilions and bilions kupitia michango isiyoisha kwa majina ya kila aina, mara tegemeza jimbo, mara uwaka, mara wawata, mara ukumbi, mara shule, mara hospitali, mara parokia, mara mfuko wa jimbo, mara sijui nini, michango isiyoisha na ni hela nyingi mno, kanisa sio kanisa tena ni kukusanya fedha tu.
Matangazo ya baada ya misa 90% ni michango, nani katoa nani bado, yaani Yesu tunaye muiga na tufuate mfano wake hatufuati kabisa maisha halisi ya Yesu, shetani kaingia makanisani kwa nguvu sana kuzidi Yesu kupitia fedha, bila hela kanisani wewe sio lolote.
Wengi tunasali majumbani na familia zetu, kanisa limegeuka ni center ya kukusanyia fedha kwa kutumia jina la Yesu, mimi moyo unaniuma sana, sbb muekeleo tunaoenda sio kabisa wa kwenda Mbinguni, Yesu hakujali fedha kabisa, tena alisema ya Caesar mpe Caesar, ya Mungu mpe Mungu, ila leo Kanisa imekumbatia ya Caesar kwa 100%
Kanisani siendi nitasali nyumbani tu, na wengi tunasali nyumbani, na Mungu atatusaidia