Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Carleen Ungekuwa muumini wa kanisa la Gwajiboy ungeendelea kwenda kanisani.. kwa sasa akiwa ni mchungaji/mwanasiasa. Ukijumuisha na swala la wazi lililotokea Kawe linalovunja amri ya 'Usiibe' na 'Usiseme uongo'....Kuna msemo unasema 'hauwezi kuwa mwanasiasa bila kusema uongo'
Kiukweli niseme wazi...ningekuwa nasali pale ningeacha kwenda pale ila siyo kuacha kusali hapana...mpumbavu mmoja wa dunia hawezi kunifanya kuacha kusali...
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Zaka ni lazima siyo hiari.

Sadaka ni kwa kadri unavyofanikiwa. Hayo mengine ni michango ya kawaida haitakiwi kuwa lazima...hakuna sheria ya kuyalazimisha hayo ktk biblia
 
Niliacha kwenda kanisani baada ya kuona viongozi wa imani yangu wameacha kukemea dhambi!
Na hata wakijitutumua siku kukemea basi huangalia aliyeitenda ni nani!!

Tofauti kabisa na manabii ninaowasoma habari zao kwenye kitabu ninachokiamini ambao walitetea Haki na kukemea dhambi bila kuogopa imefanywa na nani!

Nimewapitisha viongozi hawa kuwa ni WANAFKI sana na hawapaswi kuniongoza ibada!
Nasali hom!
Yapo makanisa yanayokemea dhambi...usiache kumwabudu Mungu kwa sababu ya watu...hao wanahukumu yao
 
To be true baada ya kusoma course flan inaitwa world religions mwaka wa mwsho chuon kwakwel ukisoma namna ukiristo uislam na kuenea kwa dini hz za mapokeo kutoka USA na how zna operate nliachaa kwenda church...lkn kingne n jz biblia inavojipinga yenyew....etc. BUT I BLV THERE IS GOD
Biblia inajipinga wapi?
 
Dini ni kwa ajili ya watoto wadogo, ukiona mzazi 'timamu' kanisani ujue ni mnufaika au anapeleka watoto ili watiwe hofu iwe rahisi kuwalea.

Niliacha kwenda kanisani baada ya kuwa na uelewa mpana wa maandiko kuliko wanaonifundisha, nikaona napoteza muda... kama nitaenda tena basi ni kijamii zaidi ili tu nisionekane mharifu machoni pa wengi.
Hakuna aliyeweza kuyaelewa yote ktk biblia ndiyo maana kila siku tunajifunza...
Hujayaelewa yote ndiyo maana ukaacha kwa sababu ya walimu unawaona kuwa vipofu..tafuta walimu
 
Unakuta Msanii ambae Ni KIOO Cha jamii,

Mlevi wa sigara na pombe wa kupindukia, anaimba matusi kibao kwenye nyimbo zake, anachezesha wanawake uchi kwny video zake.

anatuharibia VIJANA wetu.

Akishapata pesa kutoka kwenye iyo kazi yake haramu, Anaituma mkoani kujengea nyumba ya ibada.

Siku moja kabla uzinduzi,
Anapanda usafiri wa Umma, anawalipia nauli watu wote na pombe za bure.

Alfajiri,
Watu wanafika wamelewa mpk wamejinyea.

Saa 3 asbuhi,
anaenda kuzindua nyumba ya ibada.
Viongoz wa dini wanampokea na kumlaki Kama shujaa.

Saa 8 mchana,
Anapiga show kwenye uwanja wa mpira, wamama,wababa, VIJANA, na watoto wanalewa pombe,wanacheza nyimbo za ngono.

Viongozi wa dini wako kimya
Kuna shida mahali lakini haifanyi mtu kuacha kumcha Mungu kwa sababu hii
 
Viongozi wa kanisa langu kubaki kimya kipindi serikali inatesa, kuua na kubambikia kesi wapinzani.

Siendi church labda nje ya nchi au nijiridhishe nyendo za anayeongoza kanisa kuhusu itikadi zake.
Kuna shida kwa viongozi wa dini...hata wale wanaosema kuna taabu nyingi wanapitia hata hivyo wapo wanaoikosoa serikali ktk hayo mambo...kikubwa usimuache Mungu wako unayemuamini kwa hiyo excuse.
 
Uliwezaje kufahamu kuwa ni Mwafrika mweusi
Ni somo refu, na oia ujazwe na Roho mtakatifu! Akufumbue macho! ... alisema kwa kauri yake namnukuu ''niite nami nitakuitikia nitakuonyesha mambo Magumu usiyo yajua''
 
Huwa kuna sababu mbalimbali ambazo humfanya mtu kutokupenda kuhudhuria ibada siku ya Jumamosi au Jumapili (kutokana na dhehebu).

Mimi sababu ilinifanya nisiwe nahudhuria kanisani ni pale mchungaji alipokuwa anahubiri kuhusu sadaka na matoleo tu kwa ibada tatu mfululizo.

Nini sababu yako?
Ushindi wa Gwajima
 
Ninyi endeleeni tu kutokwenda kanisani kwa amani, hakuna anayewahukumu, japokuwa naamini hapa yenyewe nafsi zenu zinawasuta ndiyo maana mnajifanya kutafuta justification tu ya matendo yenu hamna lolote..!
Let then speak out.

Kuna tofauti ya kutokwenda kanisani na kusali. Maybe wanasali wakiwa majumbani.

God is Everywhere let us not judge them but remind them Mungu yupo na wanatakiwa kusali.

Say Amen
 
Let then speak out.

Kuna tofauti ya kutokwenda kanisani na kusali. Maybe wanasali wakiwa majumbani.

God is Everywhere let us not judge them but remind them Mungu yupo na wanatakiwa kusali.

Say Amen
Kwamba umeshajitosheleza kiroho kiasi kwamba huhitaji tena kwenda ibadani..?? Au unaamini kwenda kanisani ni kwenda tu kulitazama lile jengo, kuvaa smart kutoa sadaka na kurudi nyumbani.??
 
Msiache kukutanika, Ebr10:25.Ni agizo la Mungu kukusanyika ndio maana aliagiza mahekalu na masinagogi kujengwa,kwaajili ya kumwabudu,kwa wanaoelewa kutoa sadaka hakujawahi kumfilisi mwanadamu hasa sadaka hizo zikitolewa kwa maelekezo ya Mungu, sasa wewe acha kwenda kanisani uone kama hujafa kiroho na ndio mwanzo wa kuharibikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba umeshajitosheleza kiroho kiasi kwamba huhitaji tena kwenda ibadani..?? Au unaamini kwenda kanisani ni kwenda tu kulitazama lile jengo, kuvaa smart kutoa sadaka na kurudi nyumbani.??
Thank you

Kwanza ulitakiwa kujibu Amen

Naona kama tunaongea lugha moja now.

Kwenda kanisani kunatakiwa kuwe na maandalizi ya kimwili na kiroho. Watu hao wanaona wakienda kanisani watamiss maandalizi ya kiroho na mwisho wa siku wanakua wamefanya kazi bure.

Ndo maana wanaona watumie muda huo kusali nyumbani au kwenye jumuiya.

Asante
 
Back
Top Bottom