Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Ninyi endeleeni tu kutokwenda kanisani kwa amani, hakuna anayewahukumu, japokuwa naamini hapa yenyewe nafsi zenu zinawasuta ndiyo maana mnajifanya kutafuta justification tu ya matendo yenu hamna lolote..!
Ajabu na wewe huwenda hujaenda
 
Ulitaka uhubiriwe nini mtoa mada? Hayo unayotaka kuhubiriwa una uhakika utayafuata? Ukiambiwa mpende jirani yako kama nafsi yako utafanya hivyo? Ukiambiwa uache wivu, masengenyo, uzinzi n.k utaacha?
@Khantwe hili si ndio lengo kuu la kuanzisha kanisa...linapaswa lipewe msisitizo zaidi kuliko mengine. Mambo muhimu hayazungumzwi ila ya sadaka yanazungumzwa tena kwa ukali.
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Kanisa linajengwa na wewe, mimi na yule........

Usichoke kutolea...
 
Msipolijenga kanisa nani atalijenga ? Michango yote hiyo ni kwa ajili ya kuendesha shughuli za kanisa
Kwani zamani waliwezaje kuyamudu yote hayo kwa Zaka na Sadaka pekee..??
 
Huwa kuna sababu mbali mbali ambazo humfanya mtu kutokupenda kuhudhuria ibada siku ya jumamosi au jumapili (kutokana na dhehebu)..😣😔Sababu kubwa iliyo nikera" viongozi wa dini kuktwa na mashtaka pamoja na recodi za kulawiti watoto 😫😫Kama sikosei ili kuwa 2007. Pia nakumbka nilikuw na rafiki yngu ambaye amebatizwa na Kila cku ya ibada alikuwa mbele ya madhabahu akisaidiana na wenzake mbele ya padri kuongoza misa kumbe msela ni mzinifu mkubwa alikuwa na mahusiano ya kimapenz na sister hapo church 😡🚶🚶.

Mimi sababu ilinifanya nisiwe nahudhuria kanisani ni pale mchungaji alipokuwa anahubiri kuhusu sadaka na matoleo tu kwa ibada tatu mfululizo.

Nini sababu yako?
 
Kipindi fulani niliacha karibia mwaka mzima bila kwenda kanisani kisa nilisalitiwa na watu wenye nafasi nzuri kanisani tena niliowaamini ila baadae nkaelewa natakiwa kwenda kanisani kumuambudu Mungu wangu wala sio viongozi wa kanisa.
 
Back
Top Bottom