Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Kwanini uliacha kwenda kanisani?

Hivi hatuwezi kuwa na makanisa ambayo baada ya kufanikiwa kuchangia ujenzi wa kanisa tu basi kuwe na michango kidogo ya posho ya mchungaji kwa huduma yake, kisha michango ya hiyari ya kuhudumia watu wasiojiweza, na baada ya hapo yawe ni mahubiri tu ya kuhimizana kuacha dhambi ili watu waione pepo. programu za makanisani zimekuwa ni kero kwa waumini walio wengi maana zinaambatana na michango isiyokauka na kupelekea watu wengi kuamua kukacha makanisa. badala ya makanisa kuleta amani ya nafsi baada ya shurba za wiki nzima badala yake sasa yamegeuka kuwa chanzo cha kuzidisha stress kwa waumini.
 
Mm niliacha pale niposhuhudia kuna bibi mmoja mchawi huyo usipime lkn kanisan anaingia tena anakaa siti ya mbele kabisa anaimba na kusifu dah ivumilivu ulinishinda

Ule wimbo Ney wa mitego -Mungu upo wapi namuelewa kiaina japo kuna baadh ya mistar hakuwa sawa
 
Niliacha kwenda kanisani baada ya kuona viongozi wa imani yangu wameacha kukemea dhambi!
Na hata wakijitutumua siku kukemea basi huangalia aliyeitenda ni nani!!

Tofauti kabisa na manabii ninaowasoma habari zao kwenye kitabu ninachokiamini ambao walitetea Haki na kukemea dhambi bila kuogopa imefanywa na nani!

Nimewapitisha viongozi hawa kuwa ni WANAFKI sana na hawapaswi kuniongoza ibada!
Nasali hom!
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Aiseee
 
Kila nikiwawaza Alshaabab na Bokoharam Uislamu unazidi kunisukuma mbaali sana.
Hao sio Waislamu
Islam ni Aman.. Uislam unamtaka Muislamu kumpa haki asie na Muislamu..
Uislamu unamkataza Muislamu kuto mlazimisha yeyote katika dini isipokuwa kumlingania akipenda..
 
Huwa kuna sababu mbali mbali ambazo humfanya mtu kutokupenda kuhudhuria ibada siku ya jumamosi au jumapili (kutokana na dhehebu)

Mimi sababu ilinifanya nisiwe nahudhuria kanisani ni pale mchungaji alipokuwa anahubiri kuhusu sadaka na matoleo tu kwa ibada tatu mfululizo.

Nini sababu yako?
Hakuna ibaada isiyokua na sadaka hata kwa Shetani wanatoa , nikushauri toa kwa kiwango chako unacho weza kumudu pia usitoe kama unampa mchungaji toa kama agano lako na Mungu kwa kila kitu ametenda kwako mwisho sadaka ina fungua mahusiano yako na Mungu, kama unalamika tu buku 2 je ungeambiwa utoe mwanao wa pekee kama Ibrahim ungeweza?
 
To be true baada ya kusoma course flan inaitwa world religions mwaka wa mwsho chuon kwakwel ukisoma namna ukiristo uislam na kuenea kwa dini hz za mapokeo kutoka USA na how zna operate nliachaa kwenda church...lkn kingne n jz biblia inavojipinga yenyew....etc. BUT I BLV THERE IS GOD
 
Dini ni kwa ajili ya watoto wadogo, ukiona mzazi 'timamu' kanisani ujue ni mnufaika au anapeleka watoto ili watiwe hofu iwe rahisi kuwalea.

Niliacha kwenda kanisani baada ya kuwa na uelewa mpana wa maandiko kuliko wanaonifundisha, nikaona napoteza muda... kama nitaenda tena basi ni kijamii zaidi ili tu nisionekane mharifu machoni pa wengi.
 
Dahhhh.....
Ila kwetu michango imezidi mnoooo.....
1. Zaka
2.Sadaka
3. Mavuno
4. Utoto mtakatifu
5. Ujenzi wa nyumba ya Paroko
6. Ukarabati wa kanisa
7. Mfuko wa parokia
8. Wageni wa kanisa
9. Viti vya jumuiya
Mkuu haya ndio yaliliosababisha yote haya yashuhudiwayo.

Kwenda kanisani ni ibada mojawapo, na ibada yoyote ile lazima iwe na sadaka.

Miaka ya hivi karibuni yametokea mabadiliko makubwa sana katika imani, viongozi wa imani ndio waliobadilika na kusababisha haya yote.

Hii imepelekea sadaka kanisa kuwa Kama fashion fulani hivi.

Huku kwetu nisingependa kukutaja, tunaujenzi wa kanisa.
Mimi Ni muamiaji wa eneo hilo kwa Sasa Ni miaka mitano, nilipokuja hapa nilikuta harakati za ujenzi zikiendela na kupamba moto kiasi Cha kusema mwakani tu kanisa tayari.

Lakini huwezi amini mpaka leo hii Ni msingi peke yake ndio umekamilika.

Kipindikile 2016 taarifa za mapato ya ujenzi zilikua zinasoma milioni 800.

Kila siku kila mwezi kila nyakati Ni mchango wa ujenzi wa kanisa.

Jumuiyani huko kila ukipumua Ni ujenzi wa kanisa.

Nimesali makanisa kadhaa mikoa mbali mbali lakini sijawahiona kanisa lenye waumini wanaojitoa Kama hili, sadaka za ibada kwa wiki Ni milion 7.

Michango ya ujenzi milioni 60 kwa mwezi, lakini mwaka karibu wa kumi Ni msingi pekee ulio kamilika katika ujenzi wa kanisa.

Sasa kwa hapa unadhani Ni wangapi waliokatishwa tamaa na hali hii na kupelekea kutokuhudhuria kanisani?
 
Back
Top Bottom