Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Kwanini ukimwangalia usoni aliyelala huamka?

Anakuwa hana usingizi!! Usingizi ulivyomtamu m siamki aiseeh utakesha!
Anakuwa hajalala huyo anatega tu!
 
Eti kuna ukweli eti ukibana korodani mbwa akung'ati kama alivyosema Dr shika
Kama Nakumbuka Vema Dr.Shika Alibana Korodani Ili yule Mbwa Asibweke ashikwe na Bumbuazi na Hivyo Asipige Kelele/Asibweke na Kumwamsha yule jamaa alielewa na Kulala Asije kumtesa Tens Dr.Shika!
 
Ni sayansi gani hii? Ni uchawi!? Ni mazingaombwe ama ni jambo la kufikirika tu lisilo na ukweli wowote?

Niliahidi kuleta mada hii, baada ya Dr. Shika kuchagiza kwenye simulizi yake ya kutoroka watesi wake kwamba hakumwangalia yule mtesi mlinzi aliyebaki naye machoni la sivyo jamaa angeamka!

Tujadili kipengele kwa kipengele.

A. Kwenye mada zilizopita za jicho la tatu, majinamizi na jicho la rohoni tuliona jinsi jicho la tatu lilivyo na nguvu pale macho yaonekanayo yakiwa yamefumba, yamelala.. Kumbuka jicho la tatu liko kwenye paji la uso.. Tunapozungumzia mawasiliano ya kiroho kiunganishi ni jicho hilo la tatu kwamba kuna muunganiko usioonekana kati ya jicho la tatu na jicho la tatu lingine...
Kama nilivyosema kwenye mada ya majinamizi na ndoto mbaya hatushauriwi kulala chali kwakuwa juu yetu zinapita roho nyingi na za kila aina, ambazo connection yake ni jicho hilo la tatu

B. Wachawi na wanga hutumia sana jicho la tatu kufanya mawasiliano ya kiroho na ndio maana wanapotaka kuingia ndani ya nyumba kwanza kuingia kinyume nyume kwa rivasi na wakiwa uchi... Hapa ni kuepusha uwezekano wowote wa wewe kuna na direct connection ya jicho la tatu na yeye... Akishafanikiwa kuingia ndani akakukuta umelala chali hapo hataweza kuwanga tena bali yataanza mapambano mengine ya kutaka akugeuze au kukupindua ili afanye yake... Lakini kwakuwa tayari ile connection ishakuwa established basi subconscious mind inakuwa alert na ndio mwanzo wa kukabana..
Jiulize kwanini wanaoingiliwa na popobawa hawana kipingamizi chochote, hujikuta tayari washachafuliwa..

C. Muingiliano mwingine wa jicho la tatu ni ndege kunguru mwewe, huyu ni ndege mwerevu na mwepesi sana huwezi kumpiga akiwa mbali, hivyo wajuzi huenda kinyume nyume mpaka kumkaribia kabisa ndio hugeuka na kumpelekea moto... Ukiweza kurudi rivasi kwa kunyooka, unaweza kumkaribia kunguru mpaka umbali wa mita tano.. Unaweza kufanya majaribio

D. Mwili wetu huu una mashine tatu moja ni conscious mind na nyingine ni subconscious mind na ya tatu ni unconscious mind
-conscious mind- ni hii hali tuliyo nayo ya kuweza kufanya kila kitu kwa utashi na bila utashi, kuandika kuongea kuvaa nguo nk nk, ni katika hali hii subconscious mind (jicho la tatu) nayo hufanya kazi.. Hii hufanya kazi ya ulinzi kuzunguka mwili wote na ndio maana huwa tunahisi kuna mtu anatunyemelea, kuna mtu yuko nyuma yetu ama kuna hatari inatukaribia.. Lakini vilevile hufanya kazi ya machale... Jicho la tatu huona zaidi ya kuona (seeing beyond) huwa tunapewa tahadhari na nafsi zetu, huwa tunasita kufanya jambo . hii ni kazi ya subconscious mind... Halafu kuna hali ile ya kuzirai ama kupoteza fahamu... Hii ndio unconscious mind... Macho yote mawili yamezima, jicho la tatu nalo linakuwa kwenye dormance state.. Lipo lakini utendaji hupungua uwezo mpaka kufikia chini ya asilimia 50 ili kulinda uhai kidogo uliobakia. Ni sawa na kukipunguzia mizigo chombo baharini kinachokaribia kuzama ili kisizame

Sasa tuhitimishe kwa suala la Dr Shika, aliachwa na mlinzi lakini akalala kutokana na uchovu pombe na madawa.. Lakini kwakuwa tayari ana ufahamu (inbuilt intuition) wa kumlinda Dr, hivyo hata alale vipi lile jukumu kiroho hubaki kwenye subconscious mind/jicho la tatu na ikitokea ukamwangalia usoni una establishe connection kati yako na yeye na kumfanya ashtuke na kuamka
ef5089328ced34d6ad19285ea79b58d6.gif


Mojawapo ya mafunzo ya walinzi ni hili.. Na subconscious mbili zinapokutana moja ndio hu trigger nguvu ya kuamsha nyingine.. Hivyo haishauriwi kabisa kukutanisha macho Kwenye situation kama hizi

Naomba radhi kwa kuchanganya lugha
Asante kwa Elimu nzuri nazidi kujifunza kitu ila Mkuu hauna darasa unalofundisha ili tuwe tunakuja unatutoza ada?
 
nwezaje kutumiahilo li jicho uliloweka hapo kama avatar na likaendelea kuchezacheza hivyohivyo?
Mkuu hiyo itakuwa ni animated GIF image file hivyo huitaji chochote kuweza kulifanya jicho licheze cheze ni tayari hiyo picha imetengenezwa hivyo.

Unachohitaji ni web browser au app kama whatsap na nyinginezo kuifungua hiyo picha.

Application zingine za kufungulia hiyo picha huondoa hiyo animation na kuwa normal still picture tu.
 
Mkuu hiyo itakuwa ni animated GIF image file hivyo huitaji chochote kuweza kulifanya jicho licheze cheze ni tayari hiyo picha imetengenezwa hivyo.

Unachohitaji ni web browser au app kama whatsap na nyinginezo kuifungua hiyo picha.

Application zingine za kufungulia hiyo picha huondoa hiyo animation na kuwa normal still picture tu.
niliwah kutaka kutukia avatar inayochezacheza kama hiyo hapa jamiiforums ila ilikuja kama picha ya kawaida ndio maana nikauliza kama kuna namna mtu unaweza fanya
 
niliwah kutaka kutukia avatar inayochezacheza kama hiyo hapa jamiiforums ila ilikuja kama picha ya kawaida ndio maana nikauliza kama kuna namna mtu unaweza fanya
Nimekupata mkuu.
Jaribu hiyo ya Mshana Jr labda itakubali.
Nimeona watu wanazo animated GIF na zinafanya kazi. Hiyo ulitumia sijui ilikuwaje ikagoma.
 
niliwah kutaka kutukia avatar inayochezacheza kama hiyo hapa jamiiforums ila ilikuja kama picha ya kawaida ndio maana nikauliza kama kuna namna mtu unaweza fanya

Nimekupata mkuu.
Jaribu hiyo ya Mshana Jr labda itakubali.
Nimeona watu wanazo animated GIF na zinafanya kazi. Hiyo ulitumia sijui ilikuwaje ikagoma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom