Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?

Benittotz

Member
May 24, 2018
68
122
KWANINI TUNAZALIWA MASIKINI NA KUFA MASIKINI/ MAFUKARA NDIO WENYE AKILI NYINGI LAKINI BADO NI MAFUKARA.

"yuleaa ana akili Sana ni vile tu bado hajapata pakutokea". "Aah yule si anatumia tu Mali za baba yake, yani mi ningekua ndi geto yeye ningekua mbali Sana".

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kila siku mitaani,makazini,majumbani kwetu na sehemu zinginezo. Ni kauli ambazo zimesemwa tofauti lakini zote zikiwa na maana inayofanana, zikionyesha ni namna gani mtu mwenye hali duni kimaisha amekua akionekana mwenye akili,kujitambua,maono na mipango mizuri kwa manufaa ya maisha yake.

Lakini bahati mbaya katika jambo hili ni kwamba wengi wa masikini hawa wamekuwa wakiendelea kuishi hivyo hivyo na ndoto zao kichwani mpaka siku ya mwisho wa safari yao hapa duniani. Huku wale wanaoonekana hawana akili ya maisha wakiwa na maisha yao mazur na yakiendelea kuboreka kila kukicha.

Nini hasa tatizo,nini sababu ya watu hawa wenye akili na mawazo mazuri kushindwa kufanikiwa kimaisha? Kukosa kazi? Mshahara mdogo? Kutofahamiana na watu wenye uwezo? Au tatzo ni nini hasa? Mada hii ni pana na imezungumziwa na wahamasishaji na waandishi wengi kwa namna tofauti tofauti,ila Mimi nitajaribu kuelezea sababu chache ambazo zitakusaidia wewe unaeteseka kutaka kutoka katika ufakara huu kwa muda mrefu sasa.

1. NI JAMBO LA KIMAPOKEO

Hapa sababu hii imegawanyika Mara mbili; moja ni kutoka kwa wazazi na pili kiimani.

(i) Kutoka kwa wazazi.

Mara nyingi wazazi ndio huwafundisha na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae. Wakati wazazi matajiri wanawaandaa watoto wao kwa kuwashirikisha katika biashara zao,kuwatambulisha katika ulimwengu wa kibiashara na kuwatengea mtaji au biashara za wao kuja kuongoza baadae. Mzazi masikini ni kipi basi anaweza kumrithisha mwanae zaidi ya elimu? Elimu inayomfanya mtoto huyu kuwa na ndoto nyingi na maono kinadharia pasi kuwa na uzoefu wowote na masuala ya fedha na kiuchumi yanavyokwenda katika dunia ya kweli. Mwandishi na mhamasishaji Robert Kiyosaki katika kitabu chake Cha Rich dady poor dady anasema "tatizo kuhusu fedha ni kwamba haifundishwi mashuleni,tunajifunza kuhusu fedha kutoka kwa wazazi wetu. Je mzazi masikini atamfunza nini mwanae kuhusu fedha?" Ni wazi kuwa mtoto huyu atakuwa akiwa hajui hili wala lile katika kutengeneza,kutunza na kufanya maamuzi ya kifedha.

Namna ya kuepuka hili ni kujaribu kuishi katika maisha ya tofauti na uliyolelewa,jichanganye na watu waliokuzidi kipato, jifunze kutoka kwao namna wanavyofanya mambo yanayohusu fedha,wanawekeza vipi na kwenye kitu gani hasa. Wanaweka vipi akiba na mahitaji yao ya kila siku wanayamudu vipi kuweza kubaki na akiba ya kufanya Mambo ya maendeleo.

(ii) Kiimani

Kutoka katika vitabu vya dini inaandikwa kwamba alienacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa kabisa. Hivyo hali hii ya ufukara na utajiri imekua ikijiendeleza kutoka kizazi hadi kizazi. Namna pekee ya kuepukana hili ni kupambana na kukikuza kidogo ulicho nacho. Ota ndoto Kubwa ila anza taratibu itakusaidia kustahimili matarajio yao. Usikae kusubiri siku upate hela nyingi au dili Kubwa,hapo hapo ulipo ipo ngazi ya kupandia kuelekea juu itumie kabla hajapewa mwingine.

2.SAIKOLOJIA NA IMANI KUHUSU UTAJIRI.

Kuna misemo mingi sana mitaani kuhusu fedha misemo ambayo tumekuwa tukiisikia au kuiishi wakati mwingine tangu utotoni mpaka sasa. Baadhi ya misemo hii ni Kama vile

(i) matajiri ni walafi

(ii) pesa ni uovu

(iii) huwezi kuwa tajiri kifedha na kiroho kwa pamoja

(iv) huwezi kuwa tajiri na ukawa na furaha

(v) hatuwezi nunua kile au hali yetu hairuhusu hiki.

Maneno huumba na kutufanya tuishi katika kile tunachoamini. Kama umekua ukiamini siku zote kuwa pesa ni uovu hata siku moja huwezi kufanikiwa kuwa na fedha nyingi kama usipoiondoa hiyo imani iliyojijenga ndani yako. Unaweza pata ajira nzuri ukalipwa vizuri lakini kila ukipata mshahara haukai,siku mbili umeisha,madeni yanakuzunguka majanga ni mengi unajiuliza kwanini hupati jibu,tatzo haliko mbali tatizo ni kile unachokiamini. Kwa sababu unaaamini utajiri ni uovu na wewe hutaki kuwa muovu, kila upatapo fedha nyingi ni lazima zipate matumizi ya haraka kusudi zipungue na kukuepusha na uovu Kama unavyoamini.

Hivyo nimeshakufungua macho sasa jaribu kutathimini upya imani yako kuhusu fedha,ifanyie kazi upya badili mfumo wako wa kuamini na kufanya kazi utayaona matokeo.

3.DHAMIRA YA KUYATAKA MADANIKIO NI NINI?

Mwandishi T Harvey anasema watu wengi wanaokuwa katika mazingira ya umasikini hugeuka waasi wa hali hiyo hivyo dhamira yao kuu huwa katika kufanikiwa huchochewa na uasi huu. Hali ya umasikini ni Hali inayokosesha furaha hasa pale umasikini huu unapopelekea kukosekana kwa mahitaji muhimu. Tunapozaliwa katika mazingira ya kimasikini na kubahatika kuwa na akili nyingi hukuwa tukiwa na ahadi za kupambana na kubadilisha maisha yetu na ya nyumbani. Kama ilivyo ada ukitafuta baraka huwa zinakuja siku zote. Lakini hata baada ya kupata mafanikio huwa tunajisihi bado hatuna amani,ile furaha haipo moyoni mwetu kama ambavyo tulitarajia ingekuwa. Mwisho tunayachoka maisha ya huzuni na kuona namna pekee ya kuirudisha furaha ni kujiweka mbali na utajiri. KOSA! Baada ya kuupoteza utajiri huzuni,msongo na kukosa amani huongezeka Maradufu. Kwanini? Kwa sababu tumeondoa kitu ambacho si sahihi. Tulipaswa kutafuta namna ya kuipata furaha bila kurudi kwenye umasikini. Furaha na umasikini havihusiani, Bali Ile Hali yetu ya uasi na majeraha ya umasikini mioyoni mwetu ambayo yalikua bado hayajapona ndio chimbuko la huzuni yetu.

Lakini pia kuna baadhi yetu tuliotoka kwenye maisha haya ya dhiki,tunapopambana na kuanza kuiona njia Mara nyingi huwa tunataka kufanikiwa wenyewe. Tunataka kulipiza. Hivyo Mara nyingi tunajikuta tumebaki wenyewe hakuna my katika mzunguko wetu wa kutushika mkono wakati wa uhitaji sababu tulijitenga tangu mwanzo. Happy ndipo anguko letu wengi hufuata.

Namna Bora na nzuri ya kufanikiwa ni kwa kutokula wenyewe. Hatujui maisha yatatukutanisha wapi kesho. Ni vyema kuwa na mtaji wa wema kwa kusaidia kunyanyua ndoto za wengine pale unapokua na uwezo wa kufanya hivyo. Si tu utapata thawabu kwa Mungu lakini pia unajitengenezea ngome imara hapa duniani ambayo ni ngumu kutetereka achilia mbali kuanguka kabisa.

4.CHAGUZI NA MAAMUZI YA KIFEDHA.

Mfumo wetu wa elimu kwa bahati mbaya hata kwa masomo ya kibiashara bado umefeli kugusia suala hili nyeti,usimamizi na utumiaji wa fedha. Mashuleni na vyuoni tunafundishwa namna ya kusimamia kukagua na kuzalisha fedha za mataasisi na mashirika,ila ni namna gani tunapaswa kukuza na kutumia kipato chetu hilo limesahaulika kabisa. Kama nilivyosema awali nikimnukuu Robert Kiyosaki Mambo ya fedha tunajifunza nyumbani. Kama wazazi walikua wakitumia kipato chote kwenye chakula na malazi kiasi kwamba ikitokea dharura tunaanza kukimbia kwa ndugu kuomba msaada,haitakua ajabu kama mtoto atakua hajui na haoni umuhimu was kuweka akiba.

Tunaweza kuwa tunapata kipato kinachojitosheleza lakini namna tunafanya tunavyofanya maamuzi yetu ndio tatizo. Masikini kununua shati sababu amelipenda kwake si tatizo,ila tajiri atanunua endapo tu lilikua kwenye mipango hiyo. Kwa masikini kununua simu ya toleo jipya ilihali aliyonayo ni nzima na inafanya kazi vizur haoni shida,ila tajiri atanunua simu mpya pale anapokuwa na uhitaji wa simu mpya.

Hivyo tunaweza kuwa na akili nyingi Sana za kutengeneza hela lakini matumizi yasiyo sahihi yakatudumaza na kuturudisha nyuma kila siku. Mada hii ya utunzaji na utumiaji wa fedha ni pana na muhimu Sana,nitaiongelea zaidi katika makala za mbele.

Jambo la msingi ili kudhibiti matumizi yasiyo muhimu ni kuandaa taarifa ya mahitaji yako,yalinganishe na kipato chako. Anza na yale ya muhumu hakikisha huendi nje ya ulichojiwekea hi itakusaidia kudhibiti na upotevu was hella zako katika Mambo yasiyo ya lazima.

5. KUISHI KWA KUJIOMYESHA.
Hili sitalieleza Sana sababu lipo mtaani Sana na tunaishi nalo kila siku. Tunaona namna ambavyo watu wa kipato Cha chini wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi kutaka kuonyesha dunia kuwa Hali zao ni bora. Wakiweka fedha nyingi kwenye mavazi,muonekano,simu na vitu vingne vinavyozidisha umasikini wao badala ya kuwanyanyua. Wenyewe wanasema umaridadi unaficha umasikini, lakini ukweli ni kwamba umaridadi huo huo ndio unaozidi kuwadidimiza katika dimbwi Hilo la umasikini.

Natumaini makala hii fupi imekuwa msaada kwako kwa namna moja au nyingine. Pengine na wewe NI mmoja Kati ya wanaopambana kutaka kujinasua na umasikini huu Kama ilivyo wengi wetu na Leo umejifunza kitu au kuongeza kitu kwa mtazamo mwingine. Karibu kwa ushauri,nyongeza, usahihisho na pongezi pia.

Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
EMAIL ; bensonflexon@gmail.com
FB ; Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.
 
Yote Uliyoyaandika Ni Miongoni Mwa Dhana Tu Na Si Reason Zinazoexist Kiuhalisia! Kiufupi Tunaita Ni Mawazo Ya Kusadikika.

Headline Ya Ulichokipost Jibu lake Ni Moja tu Whether You Want or Not.

Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .

Nature ikikuchagua uwe wewe basi Hata Ufight Vipi Unakuwa Huna Ujanja (Zari) Wa Kutoboa Lengo likiwa Ni Kubalance Maisha ili Tutengeze Ecosystem.

Dunia Nzima Tungelikuwa Kama Zuckerberg Nani Angelilima Viazi, Maharage, Mpunga, Nyanya, Mahindi, Salad?
Nani Angechunga Ng'ombe, Pigs, Kuku, Mbuzi, Camel Na Kondoo?
Nani Angelivua Samaki and other Marine Creatures?
Nani Angelikesha Baharini Kuendesha Cargo Ships ili Kuleta Bidhaa Hapa Kwetu?

JE TUNGELIKULA NINI?

Nani Angebeba Zege?
Nani Angelikula Unga Wa Saruji Kwa Kutengeneza Matofali?

JE TUNGELIISHI WAPI?

Kwahiyo Mkuu ili SYSTEMS IBALANCE Ni Lazima NATURAL SELECTION ituchague Sisi Wengine Tuwe Maskini ili dunia iendeshwe.
 
Najaribu kukuelewa nashindwa ufafanuzi zaidi unahitajika hapa.

nature ni nini?

inachaguaje nani awe maskini na nani awe tajiri?

kwa vigezo gani?

kama shida ni kulima, kuvua, kukesha baharini mashine haziwezi kufanya hizo kazi?
 
Yote Uliyoyaandika Ni Miongoni Mwa Dhana Tu Na Si Reason Zinazoexist Kiuhalisia! Kiufupi Tunaita Ni Mawazo Ya Kusadikika.

Headline Ya Ulichokipost Jibu lake Ni Moja tu Whether You Want or Not.

Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .

Nature ikikuchagua uwe wewe basi Hata Ufight Vipi Unakuwa Huna Ujanja (Zari) Wa Kutoboa Lengo likiwa Ni Kubalance Maisha ili Tutengeze Ecosystem.

Dunia Nzima Tungelikuwa Kama Zuckerberg Nani Angelilima Viazi, Maharage, Mpunga, Nyanya, Mahindi, Salad?
Nani Angechunga Ng'ombe, Pigs, Kuku, Mbuzi, Camel Na Kondoo?
Nani Angelivua Samaki and other Marine Creatures?
Nani Angelikesha Baharini Kuendesha Cargo Ships ili Kuleta Bidhaa Hapa Kwetu?

JE TUNGELIKULA NINI?

Nani Angebeba Zege?
Nani Angelikula Unga Wa Saruji Kwa Kutengeneza Matofali?

JE TUNGELIISHI WAPI?

Kwahiyo Mkuu ili SYSTEMS IBALANCE Ni Lazima NATURAL SELECTION ituchague Sisi Wengine Tuwe Maskini ili dunia iendeshwe.
Yapo Mambo ya kiasili yanayosababisha mtu kuwa katika Hali fulani ya kimaisha kwa wakati fulani,ila Hali hi sio ya kudumu,lakini pia kila changamoto in njia zake za kuitatua. mf kwa hali ya hewa ya urusi ile barafu Kali ni kikwazo kikubwa Cha utendaji kazi lakini bado uzalishaji upo na watu wanatoboa. Ni namna gani unayachagua maisha yako ya kesho kwa kuvikabili vikwazo vya leo ndio Jambo la msingi zaidi. Asante kwa feedback pia.
 
Yote Uliyoyaandika Ni Miongoni Mwa Dhana Tu Na Si Reason Zinazoexist Kiuhalisia! Kiufupi Tunaita Ni Mawazo Ya Kusadikika.

Headline Ya Ulichokipost Jibu lake Ni Moja tu Whether You Want or Not.

Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .

Nature ikikuchagua uwe wewe basi Hata Ufight Vipi Unakuwa Huna Ujanja (Zari) Wa Kutoboa Lengo likiwa Ni Kubalance Maisha ili Tutengeze Ecosystem.

Dunia Nzima Tungelikuwa Kama Zuckerberg Nani Angelilima Viazi, Maharage, Mpunga, Nyanya, Mahindi, Salad?
Nani Angechunga Ng'ombe, Pigs, Kuku, Mbuzi, Camel Na Kondoo?
Nani Angelivua Samaki and other Marine Creatures?
Nani Angelikesha Baharini Kuendesha Cargo Ships ili Kuleta Bidhaa Hapa Kwetu?

JE TUNGELIKULA NINI?

Nani Angebeba Zege?
Nani Angelikula Unga Wa Saruji Kwa Kutengeneza Matofali?

JE TUNGELIISHI WAPI?

Kwahiyo Mkuu ili SYSTEMS IBALANCE Ni Lazima NATURAL SELECTION ituchague Sisi Wengine Tuwe Maskini ili dunia iendeshwe.

hata weew hapo hakuna ulicho andika zaid ya dhana za kufikirika tu,
na hakuna ukweli wa hata kimoja ulicho kisema
 
Kama wote wangekuwa matajiri, Dunia hiyo ingekuwaje?
Nani amtume nani?
Nani amsikilize nani?
Utegemeano ktk mazingira ungekuwepo?
Utajiri una level zake.. ishu ya msingi ni kuukata ufukara, kutegemea kupo na kutaendelea kuwepo bila kuathiriwa na mafanikio ya watu
 
Umasikini ni nini?
ni hali ya kushindwa kuyapata mahitaji muhimu
1.Chakula
2.Malazi na
3.Mavazi

Naamini kile ulichokijia hapa duniani ndicho utakachofanikiwa nacho (ni ngumu kukijua), lakini mara nyingi hiki ni kile unachokipenda sana kukifanya kutoka moyoni mara nyingi hujulikana kama kipaji.Bahati mbaya nchi yetu haina ujira kwa wingi kupitia vipaji mbali mbali.

Kuna watu (wapo mitaani) wanafanya kazi zenye kipato cha wastani lakini wameondokana na umasikini.Mf.(uliohai) dereva boda boda amejenga nyumba za kisasa (maarufu self container).Wakati huo huo kuna mtumishi wa ofisini (umma au binafsi) mshahara mzuri ila maendeleo yake hayaendani na anachokiingiza.

kuna aliyetangulia amesema
1.time.
2.kujitoa (surcrifice).
3.hard working.
4.Ibada (kwa imani yako).
 
Well said mkuu
 
Loverness umeelezea vizuri
Ila tafsiri ya umasikini haipo tu kwenye vipengele ulivyobainisha,tafsiri ya umasikini inatokana na mazingira,jinsi na pengine hata umri.

1.Tafsiri ya kimazingira:mfano umasaini ukiwa na ng'ombe wawili au watatu wanaweza kukuona ni masikini lakini uchagani suala la ng'ombe hawapimi kwa umasikini,pia jamii nyingi za kiafrika wanaona umasikini ni ile dhana ya kukosa milo mitatu kwa siku ila kwa jamii za magharibi umasikini sio kukosa basic needs maana serikali zinawapa mfano scandnavian countries.
2.Tafsiri ya Jinsi:mfano mwanamke anaweza kuona umasikini ni kushindwa kuwa na mavazi au maua mazuri nyumbani kwake ila mwanaume anaweza kuona umasikini ni kushindwa kuheshimika katika familia
3.Tafsiri ya Umri:mfano mtoto wa miaka kumi anaweza kujiona yeye ni masikini endapo hajanunuliwa vifaa vya michezo ila mtu mwenye umri wa miaka 26 anaweza jiona masikini kwa kukosa ajira tu.
Umasikini hauna tafsiri moja maana tafsiri yake imekaa kimtazamo zaidi
Kuna wakati nilishiriki zoezi la kutoa huduma mahali fulani kwa jamii za vijijini,tulikuwa tunasomewa orodha ya kaya masikini wakati mchakato unaendelea kuna mzee aliandikwa yeye ni kaya masikini,Alikasirika sana akasema mimi sio masikini nina mikono nina miguu ninaongea vizuri tu Tuligundua neno MASIKINI ndilo limemkera.
Hivyo ninakubaliana na aliesema tutumie neno "DUNI"
 
Back
Top Bottom