Kwanini tunazaliwa masikini na kufa masikini?

Poverty is a vicious cycle, na moja ya sababu Ni maamuzi mabovu yanayofanywa waliokutangulia kiumri Mf wazazi, ndugu nk. Kama maamuzi yao hayakuwa na maono ya mbali ya kuweka misingi bora ya kuondokana na umaskini wa kipato, kizazi kkinachofuata kutoka kimaisha inakuwa ngumu. Sisemi haiwezekani Ila utakutana na vikwazo vingi ambavyo vinaweza kukukatisha tamaa. Decision utakayofanya wewe ujue haitakuathiri wewe tu bali unaweza kuathiri na vizazi vijavyo. mfano Baba alikuwa mlevi.
 
Mimi naamini Umasikini unaondoka ukizingatia mambo matatu kwa asilimia zote
1.Time
2.sucrifice
3.hardworking
Kwa kila shughuli zetu za kilasiku
Umesahau kitu kimoja tuuu ambacho wenzetu wachina wamevuka na kuwa na maendeleo. Mwaka 1978 waliweka sheria ya kuzaaa mtoto mmoja. Na Sera iyo ndio imeijenga China ya Leo, kwa sababu unavyokuwa na mtoto mmoja unakuwa na uwezo wa kufanya mambo mengi. Lakini unakuta MTU ana Mali kidogo sana lakini ana watoto wengi, iyo inapelekea kuwa na bajeti ndogo ya kuhudumu family.
Kumbuka family ni uwekezaji, sasa unazaaa mtoto uwezo wa kumtunza huna, inakuwa family ya kutegemea msaaada kutoka serikali na lawama nyingi kwamba serikali
 
KWANINI TUNAZALIWA MASIKINI NA KUFA MASIKINI/ MAFUKARA NDIO WENYE AKILI NYINGI LAKINI BADO NI MAFUKARA.

"yuleaa ana akili Sana ni vile tu bado hajapata pakutokea". "Aah yule si anatumia tu Mali za baba yake, yani mi ningekua ndi geto yeye ningekua mbali Sana".

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kila siku mitaani,makazini,majumbani kwetu na sehemu zinginezo. Ni kauli ambazo zimesemwa tofauti lakini zote zikiwa na maana inayofanana, zikionyesha ni namna gani mtu mwenye hali duni kimaisha amekua akionekana mwenye akili,kujitambua,maono na mipango mizuri kwa manufaa ya maisha yake.

Lakini bahati mbaya katika jambo hili ni kwamba wengi wa masikini hawa wamekuwa wakiendelea kuishi hivyo hivyo na ndoto zao kichwani mpaka siku ya mwisho wa safari yao hapa duniani. Huku wale wanaoonekana hawana akili ya maisha wakiwa na maisha yao mazur na yakiendelea kuboreka kila kukicha.

Nini hasa tatizo,nini sababu ya watu hawa wenye akili na mawazo mazuri kushindwa kufanikiwa kimaisha? Kukosa kazi? Mshahara mdogo? Kutofahamiana na watu wenye uwezo? Au tatzo ni nini hasa? Mada hii ni pana na imezungumziwa na wahamasishaji na waandishi wengi kwa namna tofauti tofauti,ila Mimi nitajaribu kuelezea sababu chache ambazo zitakusaidia wewe unaeteseka kutaka kutoka katika ufakara huu kwa muda mrefu sasa.

1. NI JAMBO LA KIMAPOKEO

Hapa sababu hii imegawanyika Mara mbili; moja ni kutoka kwa wazazi na pili kiimani.

(i) Kutoka kwa wazazi.

Mara nyingi wazazi ndio huwafundisha na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae. Wakati wazazi matajiri wanawaandaa watoto wao kwa kuwashirikisha katika biashara zao,kuwatambulisha katika ulimwengu wa kibiashara na kuwatengea mtaji au biashara za wao kuja kuongoza baadae. Mzazi masikini ni kipi basi anaweza kumrithisha mwanae zaidi ya elimu? Elimu inayomfanya mtoto huyu kuwa na ndoto nyingi na maono kinadharia pasi kuwa na uzoefu wowote na masuala ya fedha na kiuchumi yanavyokwenda katika dunia ya kweli. Mwandishi na mhamasishaji Robert Kiyosaki katika kitabu chake Cha Rich dady poor dady anasema "tatizo kuhusu fedha ni kwamba haifundishwi mashuleni,tunajifunza kuhusu fedha kutoka kwa wazazi wetu. Je mzazi masikini atamfunza nini mwanae kuhusu fedha?" Ni wazi kuwa mtoto huyu atakuwa akiwa hajui hili wala lile katika kutengeneza,kutunza na kufanya maamuzi ya kifedha.

Namna ya kuepuka hili ni kujaribu kuishi katika maisha ya tofauti na uliyolelewa,jichanganye na watu waliokuzidi kipato, jifunze kutoka kwao namna wanavyofanya mambo yanayohusu fedha,wanawekeza vipi na kwenye kitu gani hasa. Wanaweka vipi akiba na mahitaji yao ya kila siku wanayamudu vipi kuweza kubaki na akiba ya kufanya Mambo ya maendeleo.

(ii) Kiimani

Kutoka katika vitabu vya dini inaandikwa kwamba alienacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa kabisa. Hivyo hali hii ya ufukara na utajiri imekua ikijiendeleza kutoka kizazi hadi kizazi. Namna pekee ya kuepukana hili ni kupambana na kukikuza kidogo ulicho nacho. Ota ndoto Kubwa ila anza taratibu itakusaidia kustahimili matarajio yao. Usikae kusubiri siku upate hela nyingi au dili Kubwa,hapo hapo ulipo ipo ngazi ya kupandia kuelekea juu itumie kabla hajapewa mwingine.

2.SAIKOLOJIA NA IMANI KUHUSU UTAJIRI.

Kuna misemo mingi sana mitaani kuhusu fedha misemo ambayo tumekuwa tukiisikia au kuiishi wakati mwingine tangu utotoni mpaka sasa. Baadhi ya misemo hii ni Kama vile

(i) matajiri ni walafi

(ii) pesa ni uovu

(iii) huwezi kuwa tajiri kifedha na kiroho kwa pamoja

(iv) huwezi kuwa tajiri na ukawa na furaha

(v) hatuwezi nunua kile au hali yetu hairuhusu hiki.

Maneno huumba na kutufanya tuishi katika kile tunachoamini. Kama umekua ukiamini siku zote kuwa pesa ni uovu hata siku moja huwezi kufanikiwa kuwa na fedha nyingi kama usipoiondoa hiyo imani iliyojijenga ndani yako. Unaweza pata ajira nzuri ukalipwa vizuri lakini kila ukipata mshahara haukai,siku mbili umeisha,madeni yanakuzunguka majanga ni mengi unajiuliza kwanini hupati jibu,tatzo haliko mbali tatizo ni kile unachokiamini. Kwa sababu unaaamini utajiri ni uovu na wewe hutaki kuwa muovu, kila upatapo fedha nyingi ni lazima zipate matumizi ya haraka kusudi zipungue na kukuepusha na uovu Kama unavyoamini.

Hivyo nimeshakufungua macho sasa jaribu kutathimini upya imani yako kuhusu fedha,ifanyie kazi upya badili mfumo wako wa kuamini na kufanya kazi utayaona matokeo.

3.DHAMIRA YA KUYATAKA MADANIKIO NI NINI?

Mwandishi T Harvey anasema watu wengi wanaokuwa katika mazingira ya umasikini hugeuka waasi wa hali hiyo hivyo dhamira yao kuu huwa katika kufanikiwa huchochewa na uasi huu. Hali ya umasikini ni Hali inayokosesha furaha hasa pale umasikini huu unapopelekea kukosekana kwa mahitaji muhimu. Tunapozaliwa katika mazingira ya kimasikini na kubahatika kuwa na akili nyingi hukuwa tukiwa na ahadi za kupambana na kubadilisha maisha yetu na ya nyumbani. Kama ilivyo ada ukitafuta baraka huwa zinakuja siku zote. Lakini hata baada ya kupata mafanikio huwa tunajisihi bado hatuna amani,ile furaha haipo moyoni mwetu kama ambavyo tulitarajia ingekuwa. Mwisho tunayachoka maisha ya huzuni na kuona namna pekee ya kuirudisha furaha ni kujiweka mbali na utajiri. KOSA! Baada ya kuupoteza utajiri huzuni,msongo na kukosa amani huongezeka Maradufu. Kwanini? Kwa sababu tumeondoa kitu ambacho si sahihi. Tulipaswa kutafuta namna ya kuipata furaha bila kurudi kwenye umasikini. Furaha na umasikini havihusiani, Bali Ile Hali yetu ya uasi na majeraha ya umasikini mioyoni mwetu ambayo yalikua bado hayajapona ndio chimbuko la huzuni yetu.

Lakini pia kuna baadhi yetu tuliotoka kwenye maisha haya ya dhiki,tunapopambana na kuanza kuiona njia Mara nyingi huwa tunataka kufanikiwa wenyewe. Tunataka kulipiza. Hivyo Mara nyingi tunajikuta tumebaki wenyewe hakuna my katika mzunguko wetu wa kutushika mkono wakati wa uhitaji sababu tulijitenga tangu mwanzo. Happy ndipo anguko letu wengi hufuata.

Namna Bora na nzuri ya kufanikiwa ni kwa kutokula wenyewe. Hatujui maisha yatatukutanisha wapi kesho. Ni vyema kuwa na mtaji wa wema kwa kusaidia kunyanyua ndoto za wengine pale unapokua na uwezo wa kufanya hivyo. Si tu utapata thawabu kwa Mungu lakini pia unajitengenezea ngome imara hapa duniani ambayo ni ngumu kutetereka achilia mbali kuanguka kabisa.

4.CHAGUZI NA MAAMUZI YA KIFEDHA.

Mfumo wetu wa elimu kwa bahati mbaya hata kwa masomo ya kibiashara bado umefeli kugusia suala hili nyeti,usimamizi na utumiaji wa fedha. Mashuleni na vyuoni tunafundishwa namna ya kusimamia kukagua na kuzalisha fedha za mataasisi na mashirika,ila ni namna gani tunapaswa kukuza na kutumia kipato chetu hilo limesahaulika kabisa. Kama nilivyosema awali nikimnukuu Robert Kiyosaki Mambo ya fedha tunajifunza nyumbani. Kama wazazi walikua wakitumia kipato chote kwenye chakula na malazi kiasi kwamba ikitokea dharura tunaanza kukimbia kwa ndugu kuomba msaada,haitakua ajabu kama mtoto atakua hajui na haoni umuhimu was kuweka akiba.

Tunaweza kuwa tunapata kipato kinachojitosheleza lakini namna tunafanya tunavyofanya maamuzi yetu ndio tatizo. Masikini kununua shati sababu amelipenda kwake si tatizo,ila tajiri atanunua endapo tu lilikua kwenye mipango hiyo. Kwa masikini kununua simu ya toleo jipya ilihali aliyonayo ni nzima na inafanya kazi vizur haoni shida,ila tajiri atanunua simu mpya pale anapokuwa na uhitaji wa simu mpya.

Hivyo tunaweza kuwa na akili nyingi Sana za kutengeneza hela lakini matumizi yasiyo sahihi yakatudumaza na kuturudisha nyuma kila siku. Mada hii ya utunzaji na utumiaji wa fedha ni pana na muhimu Sana,nitaiongelea zaidi katika makala za mbele.

Jambo la msingi ili kudhibiti matumizi yasiyo muhimu ni kuandaa taarifa ya mahitaji yako,yalinganishe na kipato chako. Anza na yale ya muhumu hakikisha huendi nje ya ulichojiwekea hi itakusaidia kudhibiti na upotevu was hella zako katika Mambo yasiyo ya lazima.

5. KUISHI KWA KUJIOMYESHA.
Hili sitalieleza Sana sababu lipo mtaani Sana na tunaishi nalo kila siku. Tunaona namna ambavyo watu wa kipato Cha chini wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi kutaka kuonyesha dunia kuwa Hali zao ni bora. Wakiweka fedha nyingi kwenye mavazi,muonekano,simu na vitu vingne vinavyozidisha umasikini wao badala ya kuwanyanyua. Wenyewe wanasema umaridadi unaficha umasikini, lakini ukweli ni kwamba umaridadi huo huo ndio unaozidi kuwadidimiza katika dimbwi Hilo la umasikini.

Natumaini makala hii fupi imekuwa msaada kwako kwa namna moja au nyingine. Pengine na wewe NI mmoja Kati ya wanaopambana kutaka kujinasua na umasikini huu Kama ilivyo wengi wetu na Leo umejifunza kitu au kuongeza kitu kwa mtazamo mwingine. Karibu kwa ushauri,nyongeza, usahihisho na pongezi pia.

Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
EMAIL ; bensonflexon@gmail.com
FB ; Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.
GREAT ARTICLE, tho my swahili is not good being a kenyan i have not understood much but maybe i have gotten your point,as a person who was born and brought up in kenya, and now living in one of the richest countries in the world, i have came to understand that the enviroment in which you grow up in has a lot of influence on how you turn out in life.here in EU where i am kids start learning very early vital things, the schools are well equiped, teacher higly qualified, well paid, the kids go for holidays abroad, they see riches all over, so their minds get to THINK AND DREAM BIG, hence they get to do wonders.Lets take a case of tz, i know tz very well, in some villages no clean drinking water, no schools nearby, some schools you have teachers teaching 60 kids per teacher, teachers poorly paid, kids grow in poverty, hence tz remainds very very poor.But lets define what poverty is, poverty is not lack of RESOURCES, its lack of CREATIVITY AND INNOVATION.Tz is very blessed with lots of natural resources, but with a lot of UNEDUCATED people, tz remains poor.so in order to create wealthy and make people have wealth, we need to FIX our education system. hii mambo ya magufuli ya viwada ni porojo tu, utajenga aje viwanda when your citzens are ILLITERATE.
 
Well said, we must review our education system and priotise our needs. Rome wasn't built in a day. If we can't plan for the future nothing is going to change.
 
Tutarudi Pale Pale Hizo Machine Ataziendesha Nani? Bakhresa Anaweza Kusimamia Mashine (Lift) Ya Kubebea Makontena?
Wazungu Hujitahidi Kutengeneza Robots Mpaka Za Ngono Lakini Mwishowake Wote Zinahitaji Muendeshaji Kwani Robot Ni Sawa Na Computer Haiwezi Kufanya Kazi Mpaka ipate Binadamu Wa Kumsimamia.

Kabla Ya Kusimamia Machine nani Atazitengeneza Hizo Mashine? Koz Tutahitani Raw Materials Zakutengenezea Mashine Amabazo Ni Chuma! Kama Sote Ni Mabilionea Nani Angelienda Mererani au Geita Kuzama Mgodini Kutafuta Chuma?

MKUU UMASIKINI NI LAZIMA UWEPO ILI DUNIA IENDE, VENGINEVYO MATAJIRI WATUPU HAWAWEZI KUISHI! ASILI YA KILA KITU HAPA DUNIANI NI MASIKINI NDIYO WANAFUATA.

MKUU MAISHA HAYAWEZI KUWA BILA YA KUWEPO NA FOOD CHAIN! In Biological System Producers Ni Plants! Lakini Katika Life System Producers Ni MASKINI.

Mkuu, unachokiandika kinaleta mantiki, kwamba, hiyo ndiyo nidhamu ya "nature" kuwepo matajiri na masikini. Hii fikra yako ni ngumu sana kufikirika. Pengine kama hautojali tafsiri sahihi ya masikini ni ipi? Nauliza hivi kwa sababu nimeona miongoni mwa nukta zako zinaonesha wachini kumtumikia wa juu umetafsiri kama ni umasikini.

Umasikini nini? Nielimishe kama hautojali.
 
Ni kweli kabisa, umasikini au utajiri ni mtazamo wa mtu binafsi.
Mfano, mimi siamini kuwa na ukwasi wa mali kupindukia ndio utajiri!!
 
KWANINI TUNAZALIWA MASIKINI NA KUFA MASIKINI/ MAFUKARA NDIO WENYE AKILI NYINGI LAKINI BADO NI MAFUKARA.

"yuleaa ana akili Sana ni vile tu bado hajapata pakutokea". "Aah yule si anatumia tu Mali za baba yake, yani mi ningekua ndi geto yeye ningekua mbali Sana".

Hizi ni baadhi ya kauli ambazo tumekuwa tukizisikia kila siku mitaani,makazini,majumbani kwetu na sehemu zinginezo. Ni kauli ambazo zimesemwa tofauti lakini zote zikiwa na maana inayofanana, zikionyesha ni namna gani mtu mwenye hali duni kimaisha amekua akionekana mwenye akili,kujitambua,maono na mipango mizuri kwa manufaa ya maisha yake.

Lakini bahati mbaya katika jambo hili ni kwamba wengi wa masikini hawa wamekuwa wakiendelea kuishi hivyo hivyo na ndoto zao kichwani mpaka siku ya mwisho wa safari yao hapa duniani. Huku wale wanaoonekana hawana akili ya maisha wakiwa na maisha yao mazur na yakiendelea kuboreka kila kukicha.

Nini hasa tatizo,nini sababu ya watu hawa wenye akili na mawazo mazuri kushindwa kufanikiwa kimaisha? Kukosa kazi? Mshahara mdogo? Kutofahamiana na watu wenye uwezo? Au tatzo ni nini hasa? Mada hii ni pana na imezungumziwa na wahamasishaji na waandishi wengi kwa namna tofauti tofauti,ila Mimi nitajaribu kuelezea sababu chache ambazo zitakusaidia wewe unaeteseka kutaka kutoka katika ufakara huu kwa muda mrefu sasa.

1. NI JAMBO LA KIMAPOKEO

Hapa sababu hii imegawanyika Mara mbili; moja ni kutoka kwa wazazi na pili kiimani.

(i) Kutoka kwa wazazi.

Mara nyingi wazazi ndio huwafundisha na kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadae. Wakati wazazi matajiri wanawaandaa watoto wao kwa kuwashirikisha katika biashara zao,kuwatambulisha katika ulimwengu wa kibiashara na kuwatengea mtaji au biashara za wao kuja kuongoza baadae. Mzazi masikini ni kipi basi anaweza kumrithisha mwanae zaidi ya elimu? Elimu inayomfanya mtoto huyu kuwa na ndoto nyingi na maono kinadharia pasi kuwa na uzoefu wowote na masuala ya fedha na kiuchumi yanavyokwenda katika dunia ya kweli. Mwandishi na mhamasishaji Robert Kiyosaki katika kitabu chake Cha Rich dady poor dady anasema "tatizo kuhusu fedha ni kwamba haifundishwi mashuleni,tunajifunza kuhusu fedha kutoka kwa wazazi wetu. Je mzazi masikini atamfunza nini mwanae kuhusu fedha?" Ni wazi kuwa mtoto huyu atakuwa akiwa hajui hili wala lile katika kutengeneza,kutunza na kufanya maamuzi ya kifedha.

Namna ya kuepuka hili ni kujaribu kuishi katika maisha ya tofauti na uliyolelewa,jichanganye na watu waliokuzidi kipato, jifunze kutoka kwao namna wanavyofanya mambo yanayohusu fedha,wanawekeza vipi na kwenye kitu gani hasa. Wanaweka vipi akiba na mahitaji yao ya kila siku wanayamudu vipi kuweza kubaki na akiba ya kufanya Mambo ya maendeleo.

(ii) Kiimani

Kutoka katika vitabu vya dini inaandikwa kwamba alienacho ataongezewa na asiye nacho atapokonywa kabisa. Hivyo hali hii ya ufukara na utajiri imekua ikijiendeleza kutoka kizazi hadi kizazi. Namna pekee ya kuepukana hili ni kupambana na kukikuza kidogo ulicho nacho. Ota ndoto Kubwa ila anza taratibu itakusaidia kustahimili matarajio yao. Usikae kusubiri siku upate hela nyingi au dili Kubwa,hapo hapo ulipo ipo ngazi ya kupandia kuelekea juu itumie kabla hajapewa mwingine.

2.SAIKOLOJIA NA IMANI KUHUSU UTAJIRI.

Kuna misemo mingi sana mitaani kuhusu fedha misemo ambayo tumekuwa tukiisikia au kuiishi wakati mwingine tangu utotoni mpaka sasa. Baadhi ya misemo hii ni Kama vile

(i) matajiri ni walafi

(ii) pesa ni uovu

(iii) huwezi kuwa tajiri kifedha na kiroho kwa pamoja

(iv) huwezi kuwa tajiri na ukawa na furaha

(v) hatuwezi nunua kile au hali yetu hairuhusu hiki.

Maneno huumba na kutufanya tuishi katika kile tunachoamini. Kama umekua ukiamini siku zote kuwa pesa ni uovu hata siku moja huwezi kufanikiwa kuwa na fedha nyingi kama usipoiondoa hiyo imani iliyojijenga ndani yako. Unaweza pata ajira nzuri ukalipwa vizuri lakini kila ukipata mshahara haukai,siku mbili umeisha,madeni yanakuzunguka majanga ni mengi unajiuliza kwanini hupati jibu,tatzo haliko mbali tatizo ni kile unachokiamini. Kwa sababu unaaamini utajiri ni uovu na wewe hutaki kuwa muovu, kila upatapo fedha nyingi ni lazima zipate matumizi ya haraka kusudi zipungue na kukuepusha na uovu Kama unavyoamini.

Hivyo nimeshakufungua macho sasa jaribu kutathimini upya imani yako kuhusu fedha,ifanyie kazi upya badili mfumo wako wa kuamini na kufanya kazi utayaona matokeo.

3.DHAMIRA YA KUYATAKA MADANIKIO NI NINI?

Mwandishi T Harvey anasema watu wengi wanaokuwa katika mazingira ya umasikini hugeuka waasi wa hali hiyo hivyo dhamira yao kuu huwa katika kufanikiwa huchochewa na uasi huu. Hali ya umasikini ni Hali inayokosesha furaha hasa pale umasikini huu unapopelekea kukosekana kwa mahitaji muhimu. Tunapozaliwa katika mazingira ya kimasikini na kubahatika kuwa na akili nyingi hukuwa tukiwa na ahadi za kupambana na kubadilisha maisha yetu na ya nyumbani. Kama ilivyo ada ukitafuta baraka huwa zinakuja siku zote. Lakini hata baada ya kupata mafanikio huwa tunajisihi bado hatuna amani,ile furaha haipo moyoni mwetu kama ambavyo tulitarajia ingekuwa. Mwisho tunayachoka maisha ya huzuni na kuona namna pekee ya kuirudisha furaha ni kujiweka mbali na utajiri. KOSA! Baada ya kuupoteza utajiri huzuni,msongo na kukosa amani huongezeka Maradufu. Kwanini? Kwa sababu tumeondoa kitu ambacho si sahihi. Tulipaswa kutafuta namna ya kuipata furaha bila kurudi kwenye umasikini. Furaha na umasikini havihusiani, Bali Ile Hali yetu ya uasi na majeraha ya umasikini mioyoni mwetu ambayo yalikua bado hayajapona ndio chimbuko la huzuni yetu.

Lakini pia kuna baadhi yetu tuliotoka kwenye maisha haya ya dhiki,tunapopambana na kuanza kuiona njia Mara nyingi huwa tunataka kufanikiwa wenyewe. Tunataka kulipiza. Hivyo Mara nyingi tunajikuta tumebaki wenyewe hakuna my katika mzunguko wetu wa kutushika mkono wakati wa uhitaji sababu tulijitenga tangu mwanzo. Happy ndipo anguko letu wengi hufuata.

Namna Bora na nzuri ya kufanikiwa ni kwa kutokula wenyewe. Hatujui maisha yatatukutanisha wapi kesho. Ni vyema kuwa na mtaji wa wema kwa kusaidia kunyanyua ndoto za wengine pale unapokua na uwezo wa kufanya hivyo. Si tu utapata thawabu kwa Mungu lakini pia unajitengenezea ngome imara hapa duniani ambayo ni ngumu kutetereka achilia mbali kuanguka kabisa.

4.CHAGUZI NA MAAMUZI YA KIFEDHA.

Mfumo wetu wa elimu kwa bahati mbaya hata kwa masomo ya kibiashara bado umefeli kugusia suala hili nyeti,usimamizi na utumiaji wa fedha. Mashuleni na vyuoni tunafundishwa namna ya kusimamia kukagua na kuzalisha fedha za mataasisi na mashirika,ila ni namna gani tunapaswa kukuza na kutumia kipato chetu hilo limesahaulika kabisa. Kama nilivyosema awali nikimnukuu Robert Kiyosaki Mambo ya fedha tunajifunza nyumbani. Kama wazazi walikua wakitumia kipato chote kwenye chakula na malazi kiasi kwamba ikitokea dharura tunaanza kukimbia kwa ndugu kuomba msaada,haitakua ajabu kama mtoto atakua hajui na haoni umuhimu was kuweka akiba.

Tunaweza kuwa tunapata kipato kinachojitosheleza lakini namna tunafanya tunavyofanya maamuzi yetu ndio tatizo. Masikini kununua shati sababu amelipenda kwake si tatizo,ila tajiri atanunua endapo tu lilikua kwenye mipango hiyo. Kwa masikini kununua simu ya toleo jipya ilihali aliyonayo ni nzima na inafanya kazi vizur haoni shida,ila tajiri atanunua simu mpya pale anapokuwa na uhitaji wa simu mpya.

Hivyo tunaweza kuwa na akili nyingi Sana za kutengeneza hela lakini matumizi yasiyo sahihi yakatudumaza na kuturudisha nyuma kila siku. Mada hii ya utunzaji na utumiaji wa fedha ni pana na muhimu Sana,nitaiongelea zaidi katika makala za mbele.

Jambo la msingi ili kudhibiti matumizi yasiyo muhimu ni kuandaa taarifa ya mahitaji yako,yalinganishe na kipato chako. Anza na yale ya muhumu hakikisha huendi nje ya ulichojiwekea hi itakusaidia kudhibiti na upotevu was hella zako katika Mambo yasiyo ya lazima.

5. KUISHI KWA KUJIOMYESHA.
Hili sitalieleza Sana sababu lipo mtaani Sana na tunaishi nalo kila siku. Tunaona namna ambavyo watu wa kipato Cha chini wamekuwa wakitumia muda na nguvu nyingi kutaka kuonyesha dunia kuwa Hali zao ni bora. Wakiweka fedha nyingi kwenye mavazi,muonekano,simu na vitu vingne vinavyozidisha umasikini wao badala ya kuwanyanyua. Wenyewe wanasema umaridadi unaficha umasikini, lakini ukweli ni kwamba umaridadi huo huo ndio unaozidi kuwadidimiza katika dimbwi Hilo la umasikini.

Natumaini makala hii fupi imekuwa msaada kwako kwa namna moja au nyingine. Pengine na wewe NI mmoja Kati ya wanaopambana kutaka kujinasua na umasikini huu Kama ilivyo wengi wetu na Leo umejifunza kitu au kuongeza kitu kwa mtazamo mwingine. Karibu kwa ushauri,nyongeza, usahihisho na pongezi pia.

Na
BENSON FLEXON SHIRIMA
MHITIMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SHULE YA BIASHARA.
EMAIL ; bensonflexon@gmail.com
FB ; Benson Flexon Shirima
Instagram @benitto_tz
Twitter Benittotz.
we were born rich,
kuwa Tajiri au maskini ni chaguzi za mtu
 
Jiibu la Mtu Kuzaliwa Maskini Na Akafa Maskini Ni Kwa Sababu Ya NATURAL SELECTION .
Ha ha ha ha mkuu nimecheka sana. Umeandika point kwa kiasi fulani lakini. Ukweli ni kwamba maisha ndiyo yanatuchagua na siyo sisi tunaochagua maisha.
 
Loverness umeelezea vizuri
Ila tafsiri ya umasikini haipo tu kwenye vipengele ulivyobainisha,tafsiri ya umasikini inatokana na mazingira,jinsi na pengine hata umri.

1.Tafsiri ya kimazingira:mfano umasaini ukiwa na ng'ombe wawili au watatu wanaweza kukuona ni masikini lakini uchagani suala la ng'ombe hawapimi kwa umasikini,pia jamii nyingi za kiafrika wanaona umasikini ni ile dhana ya kukosa milo mitatu kwa siku ila kwa jamii za magharibi umasikini sio kukosa basic needs maana serikali zinawapa mfano scandnavian countries.
2.Tafsiri ya Jinsi:mfano mwanamke anaweza kuona umasikini ni kushindwa kuwa na mavazi au maua mazuri nyumbani kwake ila mwanaume anaweza kuona umasikini ni kushindwa kuheshimika katika familia
3.Tafsiri ya Umri:mfano mtoto wa miaka kumi anaweza kujiona yeye ni masikini endapo hajanunuliwa vifaa vya michezo ila mtu mwenye umri wa miaka 26 anaweza jiona masikini kwa kukosa ajira tu.
Umasikini hauna tafsiri moja maana tafsiri yake imekaa kimtazamo zaidi
Kuna wakati nilishiriki zoezi la kutoa huduma mahali fulani kwa jamii za vijijini,tulikuwa tunasomewa orodha ya kaya masikini wakati mchakato unaendelea kuna mzee aliandikwa yeye ni kaya masikini,Alikasirika sana akasema mimi sio masikini nina mikono nina miguu ninaongea vizuri tu Tuligundua neno MASIKINI ndilo limemkera.
Hivyo ninakubaliana na aliesema tutumie neno "DUNI"
Hizi ni porojo tu, umaskini ni kukosa "chakula, mavazi na malazi"; zaidi ya hapo ni porojo tu na mbwembwe zisizokuwa na msingi wowote. Tatizo lenu mnaleta siasa na porojo kwenye kila kitu.
 
Hakuna ambae angetaka kutumwa kila mtu anajitosheleza na mambo mengi yangefeli.

MUNGU kaweka hivi ili kuweka uzani hapa duniani.

Unaweza kuondoa umaskini na mambo yakaenda vizuri tu. Watu watafanya kazi kwa sababu tofauti, wanazipenda hizo kazi, wanaona wanachangia kwenye jamii, wengine wanafanya kazi ili kukutana na marafiki.

Nchi nyingi zilizoendelea mbona kama hufanyi kazi unalipwa pesa za matumizi pamoja na kulipiwa nyumba, umeme, maji, gas na kodi, Lakini watu wengi wanachagua kufanya kazi hata zile za chini kabisa.

Finland wanafanya utafiti wa kuchunguza ukimlipa kila mtu pesa kwenye nchi za kujikimu (Universal Basic Income) itakuwaje? Watu watatumiaje muda wao.

Mungu hajaweka umaskini, Mungu ametupa kila kitu, (akili, rasilimali) ni uwezo wetu mdogo wa kufikiri ndio unatufanya tuwe taifa maskini.
 
Back
Top Bottom