Kwanini tunapenda kutuma pesa (kwa njia ya simu) kuliko benki ambazo huwa na gharama nafuu?

Kiongozi, weka Time, kwa ulimwengu wa sasa kuna ATMs ambazo unaweza kutoa fedha, pia hata kwenye simu kuna wakati unaweza kusimama tu kusubria muamala urudishe meseji ya kuthibitisha

Convinience ni ipi ambayo haipo kwenye huduma za kibenk
Kijana sio lazima sisi tufanye kama wanavyofanya....uchumi wa Afrika mashariki umesimama kwe mitandao ya simu..na ndo dunia inapohamia...refer to QR code payment,google money what's app money ipay...mabank mengi yapo rigid na mabadiliko na ndo tatizo linaanzia hapo
 
Kumbe wewe unaongelea maisha ya watu wa dar,sisi wa vijijini tunatumia masaa 2 kuifikia benki,sasa hayo masaa 2 nauli kiasi gani?fikiria kabla ya kuposti ,Tanzania ni kubwa mzee,siyo kwamba sisi tunapebda tukatwe pesa nyingi ni matatizo tj
 
Hii sio hypothesis, imeshakuwa proven kwa tafiti zilizofanywa na wengine wanaotafiti kuhusu poor economics.

Iko hivi ni rahisi kujua kuwa gharama za kutuma na kutoa fedha kwa kutumia simu, iwe M-pesa, Tigo pesa nk ni gharama zaidi kuliko kutumia benki i.e ATM ambazo zimetapakaa nchini.

Kwa maeneo kama Dar, ATM zimetapakaa maeneo mbalimbali na zaidi benki nyingi zinatumia mitandao mikubwa kama VISA, MASTARCARD, MAESTRO nk ambayo haikupi ulazima wa wewe kutafuta benki yako ili kutoa fehda.

Mbali na hayo bado watu wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya simu ambayo ina gharama kubwa za huduma zao kuliko benki, Je shida iko wapi.

Wewe kama mdau unayetumia simu kufanya miamala, Je unadhani ni kipi kinakufanya ukae humo ukizingatia gharama ni kubwa?

Nadhani watu wa benki wanaotengeneza mifumo ya masoko wanaweza kuwa na njia nzuri ya kuweza kujua namna gani ya kuwanasa watu ambao wanatumia simu badala ya benki ambazo zina gharama nafuu.

Hypothesis: Watu hawatumii benki kwa kuwa benki zinaonekana kama ni za watu fulani wenye hadhi na fedha nyingi (It can be tested)

Au ni kuwa watu huwa hawana muda wa kujua kuhusu gharama za masuala ya kifedha.

Signed

Oedipus
Kwa kweli, mwezi huu nimefanya Uamuzi rasmi kuachana kabisa na miamala ya Sim Banking...mafedhuli wakubwa
 
Kiongozi, Chukulia mazingira ya Dar, Jinsi ambavyo ATM ziko maeneo mengi tofauti tofauti, plus unaweza kutoa hela kwa mawakala wa huduma za kifedha kama fahari Huduma na Nmb wakala
Mbona akili yako Iko confined in one area kiongozi.
Ivi hiyo ATM IPO huko kijijini kwenu.
Mfano mie namtumia Hela ndugu huko kijijini Ngorongopa atapata ATM ya kutoa Hela.
Mfano mie nipo ubungo maziwa ATM mpaka pale shell sijui moil pale ila hao mawakala kila duka wametapakaa.
Ila umetumwa sio bure mkuu
 
na ukilipia unapewa namba au kadi? na sis huku bicha mbona abc haipo nafanyaje? nmb wanayo hio online?

Sent using Jamii Forums mobile app
na ukilipia unapewa namba au kadi? na sis huku bicha mbona abc haipo nafanyaje? nmb wanayo hio online?

Sent using Jamii Forums mobile app
NMB wanayo pia wamezindua mwezi wa 9 na ni mastercard. BANCABC ni VISA na ni kadi kabisa unapewa, sio namba pekee. Uzuri wa hizi card hazina makato ya mwezi.
 
Mi sipendi kabisa kutuma pesa kwa simu
Wakati mwingine siyo suala la kupenda ni conveniency... Say nipo shambani, some 60km from town. Nina Cash yangu niliyokuja nayo from town but nahitaji kuongezea vi laki 2 ili kazi za shamba ziendelee sasa badala ya kuvuta hiyo cash kwa CRDB au NMB app iingie kwenye simu yangu au anayenidai huko shamba, nifunge safari tena 60km kufuata Bank services??
 
Sio wote tunaishi Dar es Salaam
Kabisa, mfano mtu anayeishi Kihonda, Morogoro, akitaka ATM lazima apande daladala aende Msamvu, na ukikuta bahati mbaya haina pesa, na banks pale Bus terminal zimefungwa, basi lazima upande tena Bus mpaka town, tayari umetumia 1200 na zaidi ya 3 hrs huku lengo lako lilikuwa ni kumrushia mtu elfu 20 au 30.
 
Yaani mara mtandao uko chini,
Mara hakuna salio,
Mara kadi imemezwa shida zote hizi za nn??
Mara foleni ukifika teller kafunga dirisha anaenda lunch...

Everyday is Saturday...............................
Mfano mzuri ATM ya pale Msamvu sheli, aisee yaani to every 10 trips hesabu trip 4 aidha mashine mbovu au haina pesa...
 
Niwe mkweli tu kwa sasa nimeacha kabisa kutuma pesa kutoka bank kwenda mpesa na kutoka mpesa kwenda bank hebu fikiria kutuma 1million kutoka bank kwenda mpesa ni 12k. na hapo mpesa hujaitoa. Wakati kutoa cash kwenye atm 400k max ni 1200 +vat jumla 1800, for 1m ni sh 5.2k,
Jumlisha nauli ya boda boda au bajaj au teksi kwenda atm na kurudi na masaa utakayokuwa umefunga biashara yako ili uende huko ATM...
 
Mimi mtu akiwa na akaunti ya benk namtumia hiyo pesa benk maana atakapoenda kutoa mawakala wa bank wapo hapo hapo labda vijijini ila mjini ni mwendo wa bank tuu...maana haya makampuni Kama unatuma hela Mara kwa mara ni changamoto kidogo sema wengi hela zinakua kama emergency ndio maana anaona ukihuisha mambo ya bank tena hiyo pesa haitoipata tena...
 
NMB wanayo pia wamezindua mwezi wa 9 na ni mastercard. BANCABC ni VISA na ni kadi kabisa unapewa, sio namba pekee. Uzuri wa hizi card hazina makato ya mwezi.
Ni kama hizi za CRDB walizotoa recently?
 
Siyo wote wana akaunti bank, na pia wengine mahali walipo mpaka wakute bank ni hadi apande gari.
 
Kumbe wewe unaongelea maisha ya watu wa dar,sisi wa vijijini tunatumia masaa 2 kuifikia benki,sasa hayo masaa 2 nauli kiasi gani?fikiria kabla ya kuposti ,Tanzania ni kubwa mzee,siyo kwamba sisi tunapebda tukatwe pesa nyingi ni matatizo tj
Mfano pale Turiani, Madizini, CRDB wana only mobile van yenye ATM, ambayo ikifika saa 12 wanafunga na gari linaondoka. Kwa hiyo maisha si hapo Dar tuu.
 
Ni kama hizi za CRDB walizotoa recently?
Za CRDB sijaziona bado. Mi ninazo za BANCABC na EXIM bank kwa ajili ya kulipia mtandaoni, lakini pia nimegeuza kama akaunti ya bank kwa sababu hazina makato ya mwezi.
Mimi binafsi siwezi kuacha kutumia huduma za kibenk kwa sababu kutoka ninapoishi ni dakika 2 tu hadi ATM.
 
NMB TO Mobile Transfer

From: 1,000 - 5,000 makato800

From: 5,001 - 30,000makato 2,800

From: 30,001 - 100,000makato 3,400

From: 100,001 - 600,000makato 4,920

From: 600,001 - 1,000,000makato 5,500

From: 1,000,001 - 2,000,000 makato 6,500

Hapo bado huyu mpokeaji ajakatwa pesa ya kutole.

Kwa gharama hizi,mimi nitaendelea kutumia simu tu.
 
Back
Top Bottom