Kwanini tunapenda kutuma pesa (kwa njia ya simu) kuliko benki ambazo huwa na gharama nafuu?

elimu hii ndio mim naitaka.mkuu em nijulishe ni benk gan hio kutuma wanakata. hivyo.mana mabenk meng wameficha kweli makato yao.yan unakua una guess tu sijui hapa wanakata kias gan kutoa,kuweka,kuhamisha.
ushauri.watuwekee viwango vyao vyote makato,kuweka kutoa.sio kuyatafutaaa weee kwa toch yawe hadharan tu kwenye user interface rahisi tu like ukifika Atm unakuta kabisa wamebandika unajua unajihukum vip

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutuma pesa toka NMB kwenda m-pesa nk ni gharama kubwa Sana ukilinganisha na m-pesa kwenda m-pesa au mitandao mingine.Huyo mleta mada hajafanya ulinganishi.
 
Kutuma pesa toka NMB kwenda m-pesa nk ni gharama kubwa Sana ukilinganisha na m-pesa kwenda m-pesa au mitandao mingine.Huyo mleta mada hajafanya ulinganishi.
Hapa umejichanganya nimezungumzia benk, lakini naona bado mnataka kutoka benki kuja kwenye simu

Swai linakuja kwa nini utumie simu wakati kutoa hela benki ni gharama nafuu.

Badala ya kutoa mpesa toa kwenye ATM
 
NMB TO Mobile Transfer

From: 1,000 - 5,000 makato800

From: 5,001 - 30,000makato 2,800

From: 30,001 - 100,000makato 3,400

From: 100,001 - 600,000makato 4,920

From: 600,001 - 1,000,000makato 5,500

From: 1,000,001 - 2,000,000 makato 6,500

Hapo bado huyu mpokeaji ajakatwa pesa ya kutole.

Kwa gharama hizi,mimi nitaendelea kutumia simu tu.
Rer kwenye jibu langu kwenye hiyo comment ya juu
 
Hii sio hypothesis, imeshakuwa proven kwa tafiti zilizofanywa na wengine wanaotafiti kuhusu poor economics.

Iko hivi ni rahisi kujua kuwa gharama za kutuma na kutoa fedha kwa kutumia simu, iwe M-pesa, Tigo pesa nk ni gharama zaidi kuliko kutumia benki i.e ATM ambazo zimetapakaa nchini.

Kwa maeneo kama Dar, ATM zimetapakaa maeneo mbalimbali na zaidi benki nyingi zinatumia mitandao mikubwa kama VISA, MASTARCARD, MAESTRO nk ambayo haikupi ulazima wa wewe kutafuta benki yako ili kutoa fehda.

Mbali na hayo bado watu wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya simu ambayo ina gharama kubwa za huduma zao kuliko benki, Je shida iko wapi.

Wewe kama mdau unayetumia simu kufanya miamala, Je unadhani ni kipi kinakufanya ukae humo ukizingatia gharama ni kubwa?

Nadhani watu wa benki wanaotengeneza mifumo ya masoko wanaweza kuwa na njia nzuri ya kuweza kujua namna gani ya kuwanasa watu ambao wanatumia simu badala ya benki ambazo zina gharama nafuu.

Hypothesis: Watu hawatumii benki kwa kuwa benki zinaonekana kama ni za watu fulani wenye hadhi na fedha nyingi (It can be tested)

Au ni kuwa watu huwa hawana muda wa kujua kuhusu gharama za masuala ya kifedha.

Signed

Oedipus
You are asking the obvious.

Wilaya inaweza kuwa na ATM machines kumi tena zikiwa makao makuu ya wilaya. Vibanda vya kutolea/kutuma pesa vipo hata kwenye ngazi ya kitongoji kijijini.

Gharama ya kuweka ATM machine moja kama miundombinu stahili linganisha na kibanda cha Mpesa/Tigooesa/AirtelMoney.
 
MIMI NINA SWALI MOJA.
KWA NINI HAWAPRINT GHARAMA ZA KUWEKA,KUTOA,KUTUMA NA KUHAMISHA IWEPO KARATASI NTU UKIFIKA TU KWENYE ATM UNAIONA NCHANA KWEUPEE.....
??
Hiyo ndio ugomvi wao na sisi wateja. Ndio maana mtu akiwa na heka mbuzi zinapotea bila habari
 
Aliyesema kufungua akaunti bank ni 20,000 namwambia hivi kesho kutwa aende NMB au CRDB akawaambie Hu kasema kufungua akaunti ni bure, hakuna cha barua ya serikali ya mtaa wala nini! ni NIDA tu.
Mimi binafsi nilifungua akaunti hizo bure kabisa ila huwa napokelea mshahara kisha nakwangua wote nahamishia BANCABC.
Huko hakuna makato yoyote, ukiweka 10000 utaikuta 10000 yako mwezi ujao. Sio hizo njemba hapo juu uki-request statement hadi unajiuliza haya makato nimekatwa mimi kama nani?! kwa BANCABC kutoa hadi milioni makato hayazidi 2000 ukitolea kwenye ATM zao, ukitumia VISA makato ni 3000.
Huko EQUITY BANK nasikia nako kumenoga, hawana makato ya mwezi na pia hata kuangalia salio ni bure kabisa.
Bank za nje zipo vema sana. Sababu zimekaa kiushindani so wanampatia mteja anachotaka.

Ila za hapa bongo zimekalia dharau tukizitema wanakuja kutubembeleza bembeleza na upuuzi wao mbwa kabisa.......

Wakiona wanashindwa ushindani wanakwenda kushitaki ccm ili kuwawekea ukiritimba bank za nje ambazo zinaperform vizuri katika soko......

Ujinga mtupu... Wanafanya biashara kipuuzi sana benki zote za tanzania.....
 
Unachoongea ni sawa na kusema kwanini watu wanapanda ndege let say Dar to Dom kwa gharama ya juu wakati kuna mabasi yanayokwenda huko kwa gharama nafuu...
 
Kiongozi, Chukulia mazingira ya Dar, Jinsi ambavyo ATM ziko maeneo mengi tofauti tofauti, plus unaweza kutoa hela kwa mawakala wa huduma za kifedha kama fahari Huduma na Nmb wakala
Unajua gharama za kutoa pesa kwenye fahari huduma?
 
Hili la kusema watu wengi hudhani kuwa benki ni kwa ajili ya watu fulani ni sahihi kabisa. Ndio maana watu wengi hawana account za bank. Lakini watu hao wengi wasio na bank accounts wana miliki simu na wanapokea na kutuma fedha kupitia accounts za simu.

Iko hivi, watu wengi hawana taarifa sahihi juu ya matumizi ya accounts za bank. Kuna rafiki zangu siku moja walikua wanang'ang'ania kuwa wataendelea kutumia CRDB kwa sababu ipo kila mahali...mimi nikawaambia sitaitumia sababu muda mwingi naishi Dar es Salaam. Je, ukienda mkoani? Nikawajibu, ni mara ngapi kwa mwaka naenda mikoani? Na nikienda hata robo mwaka haifiki narudi hapa hapa. Zaidi ntakaa week 2 tena za likizo. Kuna bank kuhamisha pesa toka bank kupeleka Tigo/voda ni bure ila kila mwisho wa mwezi unakatwa sh 250/- hata kama wamepandisha siku hizi, basi tuseme 500/- bado ni nafuu sana.

Lakini kwa nini utumie simu? Wakati kuna visa?
Kuna bank kutoa kwa visa unakatwa sh 3,000 bila kujali kiasi unachotoa. Wakati tigo kutoa laki 2 ni elfu 5. Kuna kipindi mzee alikua anaumwa kalazwa hospitali, na mimi ndio nilikua caretaker. Kuna gharama kule hospitali haziko kwenye bima, sasa ndugu na jamaa wakawa wanataka wanitumie pesa kwa simu, haki nakwambia niliwapa account yangu ya bank. Mtu akihoji niende kwa bank muda huu sijui bla bla namwambia nenda kwa wakala niwekee juat like unavyoenda kuweka tigopesa.
Ilisave sana gharama za kutolea pesa. Maana nikienda ATM navuta laki 2 mpaka 4 kwa buku wakati tigopesa ningetakiwa niwaachie elfu 10 hapo.

Cha msingi ni taarifa.
Mkuu upo sahihi nafikiri watu hatuna taarifa za kutosha ngoja Mimi nikifanyie kazi
 
Kutuma pesa toka NMB kwenda m-pesa nk ni gharama kubwa Sana ukilinganisha na m-pesa kwenda m-pesa au mitandao mingine.Huyo mleta mada hajafanya ulinganishi.
huwa nataman weweke hata rate kwamba sasa kabla hujafanya muamamla utakatwa kiasi kadhaa.yan nilifanya gizan.najirushia buku app kwenda hlopesa.nimekatwa buku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili nalo linahitaji research aisee, nikiwa hko kijijini interior mpka nitafte bank? Nikiwa na shida ya haraka nafanyaje? Umempa fundi kazi kamaliza sa 1 usiku unaenda bank gani kumtumia hela? Mwisho wa siku bank ina umuhimu wake na mashirika ya simu yana umuhim kwa transaction za haraka
 
Kiongozi, Chukulia mazingira ya Dar, Jinsi ambavyo ATM ziko maeneo mengi tofauti tofauti, plus unaweza kutoa hela kwa mawakala wa huduma za kifedha kama fahari Huduma na Nmb wakala
Sawa, lakini ushawahi jua makato ya kutoa hela kwenye ATM isyo yako? Yaani kwa VISA etc..? Kwa mfano Baclays wapo maeneo machache sana kwa hapo Dar. Unataka mtu wa Baclays afanyeje? AU mtu wa NMB.. Ikifika mwisho wa mwezi, foleni yake kwenye ATM zao kisa walimu almost wote wapo huko unaijua?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom