Mtoa mada kuna kitu hakijui kuhusu reli ya kati. Reli ya kati inaanzia Dar-es-salaam mpaka Tabora inagawanyika moja inaenda Mwanza kupitia Isaka(bandari ya nchi kavu), nyingine inaenda Kigoma na nyingine inaenda Kasanga. Kwa mujibu wa mradi hii ya kwenda Mwanza itachepuka ambacho moja itaenda Rwanda na Burundi kupitia Kahama-Geita-Kagera(upembuzi yakinifu ushafanyika miaka mingi iliyopita toka enzi za Kikwete). Ile ya Kigoma inaishia bandari ya Kigoma ambapo Kigoma inaunganisha Kongo(uvira) na Burundi(Bujumbura) kibiashara. Hii ya kwenda Mpanda Rukwa inaishia Bandari ya Kasanga ambayo inaunganisha Tanzania na Kongo(Lubumbashi) kibiashara. Kwa hiyo wazo la raisi ni zuri kwa sababu ujenzi wa reli utaimarisha soko la usafirishaji mizigo wa ndani (Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Dodoma, Shinyanga, Kahama, Mwanza, Geita, Kagera), Pia tutaimarisha soko la nje Uganda, Rwanda,Burundi na DRC. Mpango wa ujenzi wa reli hii kwa standard gauge sio mpya ulikuwepo toka enzi za JK. My Take tusiwe watu wa kupinga kila kitu, wakati mwingine tufanye research kwanza. By Sammy