Kwanini tunampoteza Kabila Kwa sababu ya Kagame?

Kwanini tunampoteza Kabila Kwa sababu ya Kagame?

Hata mimi naingana kabisa na mtoa hoja,acheni kukosoa vitu vidogo vidogo kama takwimu za idadi ya watu,nenda kwenye hoja ya msingi.
Kwa maoni yangu mkulu hajakosea kuimarisha uhusiano mzuri la Rwanda ila jambo la kujiuliza je ana mkakati wowote wa kufanya hivyo kwa nchi zingine kama congo,zambia nk? Kama hana mpango wowote atakuwa amefanya terrible mistake
 
Safi tatizo ninaloliona ni watu kuleta ujuaji kwenye mambo ya msingi uvyama!!
 
Mleta mada wacha kukurupuka, nchi yetu inajenga SGR kwa ajili ya hizi nchi, Burundi, Rwanda, DR Congo....tatizo ni lipi? Jamani wabongo kwa nini wengi wetu wanakuwa na akili za mgando? Kagame kaleta msimamo Rwanda kwa kunyoosha nchi yake, as a matter of fact kila rais yabidi awe na msimamo kama huu. Mbabaishaji yeyote yule lazima atakuwa anapinga jitihada za Kagame na Magufuli katika nchi zao.
 
Ishu ya copper naielewa vizuri sana. Ila nawashangaa hao wadau wanaojaribu kuihusisha VAT na kushuka kwa mizigoo DAR wakati VAT imeanza July na kupubngua kwa mizigo kumeanza mapema zaidi na ukiwaambia hizo sababu za China na Zambia wengi wanabisha

Eti hii sheria ya VAT kwenye ancillary cargo handling services si ilipitishwa July, 2015? Halafu siyo mizigo ya DRC tu iliyopungua. Au siyo?
 
Eti hii sheria ya VAT kwenye ancillary cargo handling services si ilipitishwa July, 2015? Halafu siyo mizigo ya DRC tu iliyopungua. Au siyo?
Sijajua exactly wameanza kuitumia lini maana mwaka jana inaonekana kwamba haikuwa tatizo sasa inakuwaje ionekane ni tatizo hii leo? Maana kwa discussion zinavyoendelea inaonekana kana kwamba imeanza kuwa enforced hivi karibuni kwa hiyo ndo wanasema kwamba eti imesababisha kupungua kwa mizigo..
 
Hii analysis sijaielewa na kwanza kwa kuonyesha tu mtoa mada ni mtu asiye makini angalia hiyo population ya Rwanda. Ameshindwa hata kwenda Google kujiridhisha. Hapo tayari una question uwezo wake wa kujenga hoja vizuriii....
acha ujinga na wewe
 
Kwa mujibu wa mtandao wa TATOA, hii VAT ilianza kutumika July 2015.
 
View attachment 397504View attachment 397505

Kama ni kweli Rais wetu anamsikiliza Paul Kagame kama mshauri wa baadhi ya mambo hasa swala la kuifufua ATCL na Bandari naamini Kagame bado ni Tatizo na atakuwa na masilai binafsi na si vinginevyo!!

Kagame pamoja na kushinda kwenye Mijadala ya kimataifa akiongelea maswala ya uchumi kama " Global Economic Forum"
Lakini bado anashauri ushauri wa kizamani kabisa kujenga mfano swala la kujenga Reli (standard gauge) kwenda nchini kwake nchi ambayo ina watu kama 10milioni+

Baada tungefufua reli ya TAZARA ambayo ingeweza kuwafikia watu zaidi ya 150milion+ kutoka Zambia, Malawi, Zimbabwe na nchi zingine !!.

Hilo lingefanya bandari yetu iweze kuwa busy kuzihudumia nchi zaidi ya 10 Kusini mwa Jangwa la Sahara kuliko sasa!!

Ambapo hata Kongo imeanza kututilia shaka kutokana na Urafiki wetu na Kagame Kwa sababu wakongo wanajua kabisa huyu jamaa huwa anataka urafiki wa masilai kwa nchi yake !!

Sasa nikisema Kagame anaihujumu bandari yetu nitakuwa nakosea ? Kwani mkumbuke bandari yetu jamaa alishaitaka toka zamani Kwa kutoa maneno ya kejeli kwa Rais mstaafu?

Nikisema reli itakayojengwa itatumia garama kubwa kwa manufaa ya watu wachache nitakuwa nimekosea?

Nikisema uhusiano wetu na Congo umepungua baada ya kumkaribisha Kagame nitakuwa nimekosea?

Tuache unafiki Kagame anayajua haya yote na alikuwa na wivu sana enzi za Kikwete lakini sasa hivi atakuwa akijifungia anatuchekea sana!!

Na ukizingatia Rwanda imekuwa ikituhumiwa na USA na UN kufadhiri waasi walioko nchini Congo amabao wanapambana na Majeshi yetu pia je huu urafiki wetu na Rwanda amuoni kama unaongeza sintofahamu Kwa uhusiano wetu na Congo?

Na inaweza ikawa sababu moja wapo inayofanya mizigo ya kwenda Congo imepungua bandarini kipindi hiki?

Kwanini Rafiki yetu asiendelee kuwa Rais wa Kongo kuliko Kagame !!

Yaani unapoteza nchi yenye watu milioni 80+ na kuikumbatia nchi yenye 10milion+ alafu unategemea biashara?
ni kweli kagame sio mtu wa kuaminika lakini hili la reli lina maslahi makubwa kwa nchi yetu. hatujengi reli kwa ajili ya rwanda tu ila kwa ajili yetu zaidi. reli itapita kilometa karibu zote nchini kwetu kuelekea rwanda. kote ipitapo nchini petu inahitajika na itasisimua maendeleo. kuhusu reli ya tazara sio ya kufufua kwani haijafa. tatizo ni uongozi mbaya na sera mbaya ya usafiri wa reli. reli inaachwa kuuliwa na ushindani usiostahili wa usafiri wa barabara. jambo hili lisipoangaliwa ujenzi upya wa reli ya kati itakua pia 'tembo mweupe' tunapojidai tutajenga std gauge rail tunasau kama tazara ni std gauge.
 
Poa mkuu Kwa maelezo mazuri!!
 
kama ana mawazoo mazuri tumpokee, usilete chuki zako za ki kwele kwele hapa. magu kashachambua kipi kizuri, mwache bwanaaa
 
Hii analysis sijaielewa na kwanza kwa kuonyesha tu mtoa mada ni mtu asiye makini angalia hiyo population ya Rwanda. Ameshindwa hata kwenda Google kujiridhisha. Hapo tayari una question uwezo wake wa kujenga hoja vizuriii....
Unaweza fikiri unajua lakini hujijui kama hujui kagame si mjinga wewe Fuatilia ni nchi gani imeongoza kwa kiwango kikubwa kutopitisha mizigo Bandari ya DSM tu kwanza mengine utafikirishwa
 
Unaweza fikiri unajua lakini hujijui kama hujui kagame si mjinga wewe Fuatilia ni nchi gani imeongoza kwa kiwango kikubwa kutopitisha mizigo Bandari ya DSM tu kwanza mengine utafikirishwa
Akili ndogo at work. Based on your argument I can say you are not worth of my time. Ningetumia muda kuonyesha fallacy ipo wapi katika argument yako lakini wanasema mbuzi hawezi pigiwa gitaa kwa hiyo huo muda sina. Tafuta akili ndogo kama wewe ndo wa quote na uanze kubishana nao
 
kama ana mawazoo mazuri tumpokee, usilete chuki zako za ki kwele kwele hapa. magu kashachambua kipi kizuri, mwache bwanaaa
Hawezi kuwa na mawazo mazuri zaidi ya Yale yenye faida Kwa Rwanda full stop!!
 
Ishu ya copper naielewa vizuri sana. Ila nawashangaa hao wadau wanaojaribu kuihusisha VAT na kushuka kwa mizigoo DAR wakati VAT imeanza July na kupubngua kwa mizigo kumeanza mapema zaidi na ukiwaambia hizo sababu za China na Zambia wengi wanabisha

VAT ilianza toka 2015 lakini sasa hivi wameipitisha bungeni......haya matatizo ya DRC ilianza kabla hata Magu kuwa Rais.
Ni kweli sasa hivi Zambia na DRC wanatumia bandari za Beira na Durban na sasa hivi Angola wanamkakati wa kufufua reli kwa hiyo DRC wataitumia hiyo bandari.

Bila kumumunya serikali yetu inashindwa kutumia bandari ipasavyo kuna siasa nyingi...na ndio shamba la bibi la viongozi.
Bora wangewaachia wataaalam waiongoze bandari au kuikodisha.
 
Congo imefanywa masikini kwa sababu za ubinafsi wa wanasiasa. Bado kwenye miundo mbinu wapo nyuma sana. Wazungu wanapiga sana coltan yao na madini mengine.
Nadhani sio vibaya kulipoteza soko la Rwanda, na nijuavyo upo mkakati wa nchi hii yote kupitiwa na mfumo wa reli, ambazo zitaunganisha na kuifungua nchi hii ikawa na mawasiliano ya kibiashara na hao kina Zambia na Malawi.
 
Labda nikuulize tu swali dogo sana hivi kwa mfano kusingekuwepo hiyo nchi ya Congo inamaana Tanzania ingekuwa masikini na isinge songa mbele kimaendeleo? Yaani " Jitu " kabisa kama Wewe unakuja humu kulia lia kwa Rasilimali za nchi za Wenzako wakati Wewe hapa hata tu nusu ya Rasilimali zako ambazo pengine kama ungezitumia vyema na kuwa na usimamizi nazo mzuri leo hii Tanzania ingeshindana na South Africa, Egypt na hata nchi baadhi za huko Ulaya na Wewe kuondokana na kumpa lawama Rais wangu mpendwa Paul Kagame wa nchi yangu ya maziwa na asali ya Rwanda.

Hapa dharau kwa watu wa aina yenu warwanda ni kawaida sana..

Huwa sipendi kuwadharau baadhi yenu humu lakini kwa aina hii ya uwezo wenu mdogo sana wa kufikiri mliona hakika sitoacha kuwadharau na mtanisamehe kwa hili tafadhali. Najua argument yako juu ya hili ni too geographical than strategical.

Huu hapa chini [emoji116][emoji116] ni ukweli Tanzania tuna fursa zaidi congo kuliko Rwanda

Umeona kuwa pengine Tanzania ingefaidika sana na Congo ya Kabila kwakuwa tu nchi yenyewe ni kubwa na ina Watu wengi lakini ukasahau kwamba inawezekana hawa Rwanda wakawa wadogo Kijiografia na kiidadi ya Watu lakini kimkakati wakawa na faida kubwa sana Kibiashara na Tanzania hata kuliko hao Congo.

Hii inaonyesha wewe mrwanda halisi.
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Siku nyingine ukija humu na Mada zako jitahidi kwanza kufanya utafiti ili ueleweke vizuri na Watu ambao Mwenyezi Mungu alitubariki upeo mkubwa na akili nyingi tokea tukiwa hatujazaliwa.

Hapa unaonyesha mtia mada yuko sahihi maana majibu ya hoja zako ni ya wivu zaidi kuliko uhalisia [emoji116][emoji116]

Kwa kukusaidia tu na nakuomba nenda pale Bandarini au maeneo mengi ambapo kuna Wafanyabiashara wa kutoka Congo ndipo utajua kuwa hawa Watu ni " mikosi ". Wakongo naturally ni Matapeli na Wasanii sana na hupenda mno " kitonga " a.k.a dezo dezo katika mambo yao mengi na hili halina ubishi kwamba katika Wafanyabiashara ambao waliichafua Bandari yetu ya Dar ni hawa wa Congo kutokana na Utapeli na Ujanja Ujanja
Someni vizuri hapa na....... [emoji116][emoji116][emoji116]
waliokuwa wakiufanya hadi Mkombozi wetu Rais Dkt. Magufuli alipokuja na kuwadhibiti.

Rwanda inaweza kuwa ndogo na ukaidharau lakini kwa kukusadia tu na hili hata Watu wa TRA watakusaidia ni kwamba hakuna Wafanyabiashara ambao ni wakweli na wana nidhamu ya Kibiashara kama wa kutoka nchini kwetu Rwanda na labda badala ya kutudharau na kutudhihaki hivi kupitia ,
......na hapa nikilinganisha ni juu pale napata ukakasi sana I see..

Rais wetu Paul Kagame nadhani ungetuomba radhi na kutushukuru kwani Wanyarwanda hawajawahi kukwepa kulipa Kodi yoyote ile stahili katika Biashara zao wanazozifanya au kuzipitisha hapa Tanzania.
Dharau nyingine tena kwa Tanzania... [emoji116][emoji116][emoji116]

Hivi ni lini mtaishukuru Rwanda nyie? Rwanda tumewakosea nini? Mbona Mataifa mengine yanayowatieni Umasikini na bado mnayakumbatia tu hamuyasemi? Kuna chochote mnatudai Rwanda ili kama vipi tuwaombe Mkopo Wordl Bank na IFM ili tuwalipeni? Hivi ni kweli hakuna jema ambalo Rwanda tunalo na nyie Watanzania mnaweza kuliiga ili nanyi pia liwasaidieni? Rais Dkt. Magufuli kuonekana kumkubali Rais wetu Kagame ni dhambi? Nyie ni nani kumpangia Rais achague Marafiki? Mbona huyo " aliyestaafu " aliwakumbatia INTARAHAMWE na kuwa na ushikaji wa kupitiliza na Nkuruzinza lakini mlikuwa kimya hata pale tu nchi kubwa za Ulaya na Marekani zilipokuwa zinaishutumu Burundi na huyo Rais wake?

Please give us a break and mind your own business.
 
Back
Top Bottom