Trust None
JF-Expert Member
- Feb 12, 2018
- 1,260
- 4,415
Kumekuwa na tabia ya kuhoji uraia wa Watanzania wenye majina yanayofanana na ya nchi za Rwanda na Burundi, kwanini hatuhoji uraia wa watu wenye majina yanayofanana na Wajaluo wa Kenya au Wamakonde wa Msumbiji, au Wamalawi, Zambia au majina ya Kiarabu na Kizungu?
Hapa napata uelewa kwanini hayati alipendekeza kufundishwa somo la Historia ya Tanzania. Wengi hawaelewi historia yetu kabla na wakati wa ukoloni.
Tukizingatia kigezo cha majina, basi wengi wetu si Watanzania. Mnakumbuka 'Ngoni Migration?' 'Migaration of Bantu Speaking Prople?' Someni mambo yanayohusiana na Nilotes, Hamites, Cushites, Pygmies, Bantu, Khoisan
Tukiendelea ku-judge uraia kwa kigezo cha majina, nani atabaki Tanzania?
Majina mengi ya Burundi na Rwanda yanafanana na majina ya Kigoma na ya wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera. Pia lugha ya asili ni moja, inatofautiana kwenye matamshi tu. Watu hawa wanaelewana kwa kuwa lugha ni moja. Majina mengi yanafanana kwa mfano: Nkurunzinza, Miburo, Ntibazonkiza, Majambele, Misago, Nyawenda, Minani, Mapfalakola, Tuishime, Yamungu, Nahimana, Nduru, Machumi, Myandagaro, Munezero, nk.