Kwanini tunahoji uraia wa Watanzania wenye majina ya asili ya Burundi/Rwanda na si nchi nyingine?

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Kumekuwa na tabia ya kuhoji uraia wa Watanzania wenye majina yanayofanana na ya nchi za Rwanda na Burundi, kwanini hatuhoji uraia wa watu wenye majina yanayofanana na Wajaluo wa Kenya au Wamakonde wa Msumbiji, au Wamalawi, Zambia au majina ya Kiarabu na Kizungu?

Hapa napata uelewa kwanini hayati alipendekeza kufundishwa somo la Historia ya Tanzania. Wengi hawaelewi historia yetu kabla na wakati wa ukoloni.

Tukizingatia kigezo cha majina, basi wengi wetu si Watanzania. Mnakumbuka 'Ngoni Migration?' 'Migaration of Bantu Speaking Prople?' Someni mambo yanayohusiana na Nilotes, Hamites, Cushites, Pygmies, Bantu, Khoisan

Tukiendelea ku-judge uraia kwa kigezo cha majina, nani atabaki Tanzania?
Majina mengi ya Burundi na Rwanda yanafanana na majina ya Kigoma na ya wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera. Pia lugha ya asili ni moja, inatofautiana kwenye matamshi tu. Watu hawa wanaelewana kwa kuwa lugha ni moja. Majina mengi yanafanana kwa mfano: Nkurunzinza, Miburo, Ntibazonkiza, Majambele, Misago, Nyawenda, Minani, Mapfalakola, Tuishime, Yamungu, Nahimana, Nduru, Machumi, Myandagaro, Munezero, nk.

EAF-German-East-Africa-Map.jpg

dbf80cd8129a0cad0fd99852972e20ee.png
 
Kuna watu kama Dotto Mashaka Biteko, waziri wa madini na mbunge wa bukombe ni Mtusi 100%, wazazi wake wote Watusi (mwenyezi mungu awarehrmu) na kaoa familia ya Watusi.

Pacha wake Kulwa Masunga Biteko, ni afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje, kituo cha kazi ni ubarozi wa msumbiji. Huyu ni afisa usalama na ni mtusi.

Kwenye misiba ya wazazi wao yote nilihudhuria, kulikuwa na magari kibao yenye plate za Rwanda, na wanao ndugu kibao huko kwao.

Hawa ni wajumbe wa vikao nyeti nchini Tanzania.
 
Kumekuwa na tabia ya kuhoji uraia wa Watanzania wenye majina yanayofanana na ya nchi za Rwanda na Burundi, kwanini hatuhoji uraia wa watu wenye majina yanayofanana na Wajaluo wa Kenya au Wamakonde wa Msumbiji, au Wamalawi, Zambia au majina ya Kiarabu na Kizungu?..
Unaijua Bahima Empire wewe??? Watu wa izo sehemu wana movement ya siri ya kutawala nchi zote duniani kwa maslahi yao.
Ndo mana kiusalama ni jambo nyeti sana.
 
ila hii imekaaa sawa kweli

Mjaluo wa Tanzania awe na mahusiano ya kindugu zaidi na Mngoni wa Songea kuliko mjaluo wa Kenya !!!!....
 
Tatizo la watu wa hizo nchi wakiingia bongo hawapendi kujichanganya na wabongo na wanaoana wao kwa wao. wakenya, Wazambia na Wamalawi wakiingia Tz wanajichanganya na kuoana na Watz hivyo kuonekana ni wenzetu tu. Mmalawi aliyezamia Tz 2000 ni mwenzetu zaidi kuliko mnyarwanda aliyeingia 1980s
 
Ni mtazamo tu
 
Kuna watu kama Dotto Mashaka Biteko, waziri wa madini na mbunge wa bukombe ni Mtusi 100%, wazazi wake wote Watusi (mwenyezi mungu awarehrmu) na kaoa familia ya Watusi....
Si tuliambiwa ni mtoto wa Dada, Dada wa wapi huyo
 
Kumekuwa na tabia ya kuhoji uraia wa Watanzania wenye majina yanayofanana na ya nchi za Rwanda na Burundi, kwanini hatuhoji uraia wa watu wenye majina yanayofanana na Wajaluo wa Kenya au Wamakonde wa Msumbiji, au Wamalawi, Zambia au majina ya Kiarabu na Kizungu?..
Point nzuri. Wamasai kwa mfano wenyewe wanaita eneo wanaloishi kuwa ni umasai na si Tanzania au Kenya maana hilo eneo ndipo lilipo. Na Wajaluo halikadhalika
 
Mipaka imewekwa kwenye ardhi na haitenganishi watu moja kwa moja.

Raia wanaoishi maeneo ya mipakani ni kawaida kuwa na uhusiano wa kindugu upande wa pili. Hiyo siyo dhambi, ni hali halisi ya maisha ya jamii zetu.

Hata hivyo, hali hiyo ikionekana kutishia usalama wa nchi, tahadhari na hatua stahiki huchukuliwa kwa umakini mkubwa.
 
Hayati Idd Simba mlisema hivi hivi mwisho wa siku ni mdengereko wa rufiji.
 
Kuna watu kama Dotto Mashaka Biteko, waziri wa madini na mbunge wa bukombe ni Mtusi 100%, wazazi wake wote Watusi (mwenyezi mungu awarehrmu) na kaoa familia ya Watusi.

Pacha wake Kulwa Masunga Biteko, ni afisa mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje, kituo cha kazi ni ubarozi wa msumbiji. Huyu ni afisa usalama na ni mtusi.

Kwenye misiba ya wazazi wao yote nilihudhuria, kulikuwa na magari kibao yenye plate za Rwanda, na wanao ndugu kibao huko kwao.

Hawa ni wajumbe wa vikao nyeti nchini Tanzania.
Ukiniambia pia kuwa ana asili ya Kigoma maeneo ya Bitale kule juu Mkongoro nitakuelewa unachotaka kutuambia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom