Steven Joel Ntamusano
JF-Expert Member
- Jun 17, 2023
- 2,951
- 1,993
Ipo video inatembea Youtube inayoonyesha namna serikali ya Rwanda ilivyofungua bandari kavu tayari kwa ajili ya mzigo wa DP World. Tayari kwa ajili ya biashara ya kuweka mzigo unaokuja bandari ya Dar na kwenda Dubai.
Mwarabu alijipanga siku nyingi sana. Hii ni biashara iliyoanza tangu miaka 2010 katikati. Ujenzi wa Reli yetu kwa kiwango cha SGR ni sehemu ya serikali ya JPM kujiweka tayari kwa ajili ya kupitisha mzigo unaotoka DRC na Rwanda na unaoelekea katika nchi hizo ukitokea katika bandari ya Dar.
Zipo tuhuma nyingi sana zinazopandikizwa na wanasiasa wenye kuvizia urais wa 2025 na 2030, wao wanachukulia giza ya ubaguzi dhidi ya wazanzibari kuwa ni nyepesi tu hawajiulizi juu ya madhara ya kudumu ya ubaguzi huo!.
Hawajiulizi juu ya chuki wanayoitengeneza dhidi ya watanzania wenzao kwa kigezo tu cha biashara hii ya DP World.
Iwapo wanasema kuwa Samia ameuza nchi kwa waarabu, vipi kuhusu Paul Kagame wa Rwanda aliyemaliza kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji wao, na yeye kauiza Rwanda kwa waarabu?.
Kagame aliyeipigania Rwanda huko msituni akipoteza maelfu ya wanajeshi vitani, anaweza kweli kuja kuiuza nchi yake kwa pesa ya mwarabu?.
Watanzania wenzangu tusikubali kushikiwa akili, na kuchezewa vichwani kama watoto wa miaka mitano. Hakuna mwenye nia wala lengo la kuiuza nchi. Na hao waarabu waache kununua nchi kama Somalia, Sudan na Eritrea zenye utajiri mwingi wa mafuta na madini eti aje kuinunua Tanzania!.
Tupunguze uoga huu ni muda wa kukubali kupokea changamoto mpya za utendaji kazi pale bandarini. Ni muda wa kuondokana na matumizi mengi ya kazi za karatasi zinazochanika na kupotea na kukubaliana na utendaji wa kidigitali wenye tija nyingi ndani ya muda mfupi wa kazi.
Ikiwa Samia anatuuza kwa waarabu ambao ni wajomba zake, vipi kuhusu Kagame na yeye anaiuza Rwanda kwa mwarabu huyo huyo?.
Ni huyu huyu Kagame aliyeisaini mkataba na Arsenal wa mapesa mengi na leo hii dunia nzima inakaribishwa Rwanda kwa maneno tu yanayokuwa mgongoni mwa jezi ya Lionel Messi na Neymar. Kila wanapovaa jezi ya PSG, dunia nzima inakaribishwa Rwanda kupitia matangazo ya umeme yanayokatiza kwenye kioo cha runinga kila mechi ya Arsenal inapochezwa pale Emirates.
Tunahitaji sana marais wenye maono na wanaosimamia kile wanachokiamini mfano wa Paul Kagame, ambaye hatakuwa na muda wa kusikiliza kelele za wajuaji na wajinga wenye kushikiwa akili zao na wanasiasa wenye malengo yao ya kibinafsi.