Kwanini tuko hapa? Nini kimetokea baada ya Waafrika kuchukua mamlaka?

OnTheEarth

Member
Jan 1, 2023
75
63
Maisha ya mwafrika kama ambavyo yalivyo maisha ya jamii nyingine duniani yamepitia zama mbalimbali muhimu. Kuanzia zama za chini kabisa za maendeleo mpaka hii ya leo aliyomo, hizo zote ni muhimu kwa mtu kujifunza na kukua.

Jambo lililowazi na muhimu, katika zama zote hizi, ni 'Kukua'. Hii inamaansha uwepo wa mageuzo yenye maendeleo katika mifumo yote ya maisha ya mtu.

Kwa jinsi zama hizi zilivyo, kuanzia ya chini kabisa mpaka hii tuliyopo sasa, utaona historia inachukuwa nafasi muhimu katika kujifunza namna bora ya kuendelea kukua, ili kuwa bora zaidi.

Kabla ya Utawala wa wageni, Wafrika waliishi katika tawala za Koo. Na hii si tu kwa Wafrika ni, pia jamii zingine. Kwa kadiri ya ujuzi au taaluma, na uchumi wake, ukoo uliweza kujitanua na kuwa eneo kubwa la utawala. Kwa kweli tunaweza kusema, kwamba hata tawala za jamii nyingine, katika historia ya ulimwengu, msingi wake ni koo.

Kwa kuangalia pekee ukweli huo, na kwa kuzingatia hali kwamba baadae Wafrika walitawaliwa na jamii nyingine, tunajifunza kwamba koo zetu Wafrika hazikuwa bora.

Kwa sababu hiyo, pamoja na vitu vingi tunavyoweza kuviangalia juu ya koo au jamii; au taifa fulani kuwa lenye nguvu na kutawala koo au jamii au mataifa mengine ni, kiwango chake cha juu cha maadili.

Historia ya Wafrika kama zilivyo jamii nyingine zisizo bado starabika, imepitia nyakati mbili huku nyakiti moja ikijirudia: ya kwanza, kijitawala na, ya pili kutawaliwa. Hii ya kwanza ya kujitawa ilianza zama za mwanzo kabisa za maendeleo ya binadamu: tawala za koo na, kisha baadae baada ya utawala wa wageni - wakoloni wazungu na waarabu kwa nyakati tofauti tofauti.

Katika zama za mwanzo za maendeleo ya binadamu ni, dhahiri kwamba baadhi ya koo za kiafrika zilifanikiwa kukua na kujitanua kiutawala na hivyo kudhibiti koo zingine. Hii inaweza kumanisha vilevile kiwango cha ustawi wa watu wa koo hizo na, au maslahi pekee ya watawala wa koo hizo.

Maisha na ustawi wa watu katika zama hizi za tawala ndogondogo, kwa kweli si kama huu tunaouona hii leo. Kuanzia maendeleo katika matibabu mpaka ufahamu wa baadhi ya mambo kama tulivyo nayo hivi leo.

Kama ambavyo tunaona hali ya maisha ya Wafrika pote Afrika na vile vile mwenendo wa viongozi wake, kwa kuzingatia hilo tunaweza kusema, tofauti pekee ya hali ya maisha na ustawi wa watu kwa nyakati hizi mbili ni, idadi ya watu. Idadi ya watu katika ustawi na, maendeleo ya watu na, uchumi ni jambo nyeti na msingi. Ukweli mwingine katika nyakati hizi ni, nyakazi zenyewe.

Wakati wa ukoloni hasa Wazungu hali ya huduma za jamii ilikuwa nzuri; kwa maana kwamba mahitaji yaliyohitajika kwa jamii yalipatikana kwa kiwango kinachotakiwa. Hatuwezi kusema wakati huu haikuwa na changamoto, kwa kweli zilikuwepo na nyingi ya hizo zilitokana na ukweli wenyewe kwamba teknolojia ilikuwa bado haijakuwa kama ilivyo hizi leo.

Kando na hilo, wakoloni hawakujenga miundombonu na huduma kwa baadhi ya maeneo kwa sababu mbalimbali za kiuchumi na utawala.
Kwa ujumla, hali ya huduma- upatikanaji wake; wakati wa ukoloni ilikuwa bora ukilinganisha na baada ya ukoloni.

Huduma kama shule na hospitali, ukiacha kwamba zilikuwa mbali - watu walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu na elimu, lakini miundombinu na vifaa vilivyohitajika kwa ajili ya elimu na matibabu, vilipatikana kwa kiwango cha juu na bora.

Tunaweza kuona hilo hivi leo, kwa kuwa hata leo Afrika nzima tunayo majengo mengi yaliojengwa na wakoloni; kwa kulinganisha na yale yaliojengwa na Wafrika baada ya kuchukua mamlaka.

Kama mtu mmoja au ye yote ataamua angalau kuwa makini juu ya Mapambano Ya Uhuru Afrika, utaweza kuona kwamba mambo si kama tunavyoyasikia, na kusoma kwenye taasisi zetu za elimu. Kwa nini? Kwa sababu: inawezekanaje mtu mdhoofu kimwili na kiakili apigane na mtu mwenye afya njema kimwili na kiakili?

Dunia yetu, kwa namna isio wazi sana, iko katika utaratibu wa mageuzo mbalimbali yenye maendeleo ya mifumo ya uchumi na utawala. Mageuzo haya yanatokea kwa nyakati maalum na yanapokuja yanashughulika na kubadilika kwa mifumo ya uendeshaji wa uchumi na utawala.

Changamoto tuliyonayo yanapotokea mageuzo haya ni, kuwa baadhi ya watu, kwa kujua hayo, huamua kutengeneza propaganda: nyeupe na, au nyeusi.

Wengi wa wapigania Uhuru wa Afrika na, ambayo ndio hao au wasaidizi wao walikuja kuwa viongozi wa nchi zao, waliwadanganya wenzao wanaotaka kuwatawala.

Pia katika hao wapigania Uhuru, wapo baadhi yao waliowafanyia wenzao vitendo ovu kwa ajili ya kupata madaraka. Hali hii kwa kweli ina mzizi wake kwenye tawala za koo.

Kwa hiyo, tendo lenyewe lililoitwa 'Kupigania Uhuru', na pia uchukiaji wa mamlaka wenyewe, ulikuwa wa makosa na karoso kubwa.

Hali hii ndio tuliyonayo hadi leo. Angalia, viongozi hapa kwetu Afrika na mataifa mengine ambayo bado hayajastarabika wanaingiaje mamlakani?

Watu wanaodanganya, ili wawe au wachaguliwe kuwa viongozi wanashindwaje kufanya udanganyifu kwenye mambo ya maendeleo na huduma za jamii?

Watu walipata kusema The cause Justify the End.

Ndio kusema kwamba, Afrika iko hapa ilipo; na au hayo tunayoyaona na kuyasikia pote barani ni, kwa sababu watu waliopewa mamlaka, HAWANA SIFA ZA KUWA VIONGOZI.

Watu hawa kwa sababu hawana sifa hizo, na kwa kuwa, hawawezi kutekeleza na kusimamia maendeleo na huduma za jamii na; kushughulikia matatizo na usalama wa watu wao, badala yake wanatafuta vitu vya kujificha na kuficha kushindwa kwao.

Watu hawawi masikini kwa sababu ya ushoga. Kukosekana kwa huduma na mahitaji muhimu ya jamii si kwa sababu ya ushoga. Matumizi mabaya ya fedha za umma hayasababishwi na ushoga: kwa sababu watu walio katika Hali hii ni, wagonjwa wa akili.

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba, mtu ambaye ni mgonjwa na, ambaye Serikali ina wajibu wa kumpatia usalama, anawekewa sheria ya kuondoa usalama wake au hata uhai wake!

Kama kila mtu angejaribu kuwa makini, na pengine kwa sababu hatuko makini ndio sababu kila kitu kimeharibika! Hivi inawezekanaje mtu ambaye hana matatizo ya akili, akili yake ni njema, akashiriki au kufanya matendo haya ya kuumiza na chukizo hivi?

Ajabu hapa Afrika ni, kwamba Serikali, ambayo imeapa kulinda raia wake; ndio iko mstari wa mbele kuua raia wake!

Aidha, raia ambao nao wana wajibu wa kulinda uhai; ama kwa kujua au kutojua, wanashiriki kuwaangamiza ndugu zao, ambao hao ndugu zao ni wagonjwa wanaotakiwa kupata msaada wa matibabu.

Masuala ya maendeleo na matatizo mbalimbali katika jamii au taifa yanataka daima utafiti wa kutosha na zaidi watu makini na wenye sifa, ili kuyafikia au kuyaelewa.

Hatuwezi, kama jamii au taifa kupata maendeleo na kulinda uhai; ikiwa tunafikiri hawa tuliowaweka kuwa viongozi wetu; kuyachukuwa mawazo yao moja kwa moja bila kufanya utafiti wa kutosha; hata kama kwa namna moja au nyingine tunanufaika kimwili kutoka kwao. Kufanya hivi ni, kudhoofisha maendeleo na ni kinyume na uumbaji.

Kuhusu Afrika kuwa chini kimaendeleo, hili ni jambo ambalo chanzo chake ni Wafrika wenyewe kukataa kukabiliana na jinsi walivyo- tabia zetu. Wafrika hatutaki na tunapinga imani na elimu. Ukitaka kuthibitisha hili na lilivyo chanzo cha uharibifu wa maisha na uhai, angalia ndoa zilivyo Afrika.
 
Mwafrika amekua duni zaidi kabla ya ukoloni na baada ya ukoloni.

Sheria zilizotungwa baada ya mkoloni mweupe kuondoka zimekua kandamizi mara 100 zaidi ya mkoloni.

Enzi ya mkoloni system ya administration ilikua effective and efficient leo ni majanga matupu.

Kuna ukweli mchungu na unauma sana ambao hatupendi kuukubali lakini ndiyo ukweli kwamba; MWAFRIKA BADO HAJAWEZA KUJITAWALA!
 
Hoja kama hizi then useme waz bora mtawala mweupe, unakuja kushambuliwa humu eti una mawazo ya kijinga ya kutetemekea mabeberu!! Ukwel ni kwamba pamoja na mateso yao ya kikoloni Taifa lingekua mbali san kiuchumi na kimaendeleo. Uzuri tunazo references nying tu baada ya uhuru kweny Nchi za kiafrika.
 
Mtu anaenda Uchina anakutana na Mao anarudi katuvalia chun lai na kutuburuzia kwenye Ujamaa bila kuturuhusu tuihoji siasa yake hiyo mpya.

Ghafla anatangaza Azimio la Arusha na kuanza kutaifisha mali halali za wananchi.
 
Wapigania UHURU waliwadanganya waafrika wawasapoti kuwafurusha wakoloni baada ya wakoloni kuondoka watawala wakageuka kuwa madikteta wakawageukia waafrika wakaanza kuwatesa waafrika.Unapigania UHURU kuwaondoa wazungu kisha unaunda makundi ya kigaidi na kihalifu ( vikosi vya kumlinda rais ) vikulinde dhidi ya wanaotaka kukuondoa kisa utendi haki kwa kwenda kinyume na matarajio ya wananchi,kwa kuviamuru vikosi vyao vya kigaidi kuteka,kutesa na kuua watu kwa mtindo wasiojulikana Ili kulinda tumbo,SAsa nini tofauti yako na wakoloni, angalau wakoloni walifanya hayo huku wakiletea watu maendeleo.

Thus huwa nasema wapigania UHURU walipigania maslai yao binafsi kwa kuwatumia waafrika na sio kupigania maslai ya waafrika wote ilikuwa ni kiini macho tu, thus baada ya UHURU wao ndio walionufaisha matumbo yao hadi SAsa vizazi vyao huku mamilioni ya waafrika wakitopea kwenye lindi la ufukara. Ukifanya study utagundua angalau mwafrika alikuwa ana nafuu kabla ya UHURU ajira zilikuwapo tele, chakula tele, elimu na afya zilikuwapo tele.

Walipigania UHURU ndio walipotosha waafrika walikuwa na ajenda binafsi za maslai yao wao thus baada ya UHURU wakageuka kuwa wakoloni weusi kwa kuwatendea mabaya waafrika.
 
Nchi hii bora wakoloni wangebaki tu mpaka 1995 angalau tungekuwa tushapata akili za kuongoza nchi.
 
Wewe acha kulinganisha mtu wa miaka 400+ na 60+
Marekani na nchi nyingine zilizo endelea walipitia haya haya tuna yo yapitia leo!
Please try to think outside the box
That’s all!
 
Wewe acha kulinganisha mtu wa miaka 400+ na 60+
Marekani na nchi nyingine zilizo endelea walipitia haya haya tuna yo yapitia leo!
Please try to think
emoji3166.png
outside the box
emoji403.png

That’s all!
Hilo linafahamika, liko wazi. Miaka sitini kama ilivyo miaka mia nne haimanishi kuanza kwa uhai au maisha ya mtu.

Ukiangalia miaka mia nne ya mataifa yalioendelea na miaka sitini ya mataifa yanaoendelea, utaona nini yanaaksi: nyuma kabla na mbele baada ya miaka 400. Hivyo hivyo kwa mataifa ya miaka 60.

Siyo kwamba hakuna kilichofanyika au kinachofanyika, lakini kilifanyikaje au kinafanyikaje na kwa kufanyika hivyo, kunaaksi nini.

Duniani wote ni, kwa ajili ya kuwa bora na bora zaidi. Lakini tunakuwaje bora? Hili halitegemei pekee muda au umri. Ndio sababu leo kuna mataifa wakati fulani tulikuwa sawa kiuchumi na umri wetu ni sawa hata; lakini leo wako bora kuliko sisi.
 
Back
Top Bottom