Mkuu Tilatila,
Tlaatlaah , with due respect, nakuomba usitake kutupeleka huko, tukaishia kuhitlafiana kwa mambo ya kiimani. TEC ndie msimamizi wa Wakristo Wakatoliki Tanzania, ni taasisi iliyosimama wima iko very straight, haitaki ujinga, wala usiingize kwenye mambo ya kijinga!, hawawezi kushiriki ujinga!.
Kitendo cha TEC Kukataa wito wa tume ya uchunguzi wa matukio ya oct.2025, kuna dhihirisha ukweli kuwa TEC wako straight, hawawezi kushiriki ujinga!.
Kwa vile baada ya tumme ya Uchunguzi, inaundwa tume jinai, kama una ushahidi wa TEC kuchochea vurugu na ghasia hizo za oct.2025 na wewe ni shuhuda wa namna viongozi wa TEC walivyohubiri chuki na walivyotamani fujo, vurugu, maafa na uharibifu kutokea katika wakati uchaguzi mkuu wa oct upeleke kwenye Tume jinai!.
Kwa kawaida, TEC, hawatakagi ujinga kabisa!. Hata Baba wa Taifa, angekuwa hai, asingeshiriki ujinga kama huo, yule Mzee ni Mkatoliki, hatutakagi kabisa ujinga!.
P