Kwanini TBC1 walikata matangazo ya LIVE, wakati mama Samia Suluhu akiongelea kilichotokea Foreign mpaka Naibu Waziri kutumbuliwa?

Van persie

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,099
719
Nimesikitishwa na kufedheheshwa na kitendo cha Televisheni ya Taifa[TBC 1] kukatisha matangazo ya mubashara wakati mama Samia Suluhu, Makamu wa Rais, alipokuwa akielezea mkanganyiko na kilichotokea Foreign siku za hivi karibuni na kupelekea Naibu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashiriki kufutwa kazi.

Ghafla wakati Mama Samia anazungumzia kiini cha nini kimetokea, TBC 1 wakakata matangazo ya mubashara bila kueleza tatizo. Inaonesha ni makusudi tu. Baada ya hapo wakarudisha haraka mkulu alipoenda kwenye podium.

Hii censoring imenishangaza na kuniuzunisha. Kweli tumerudi kwenye nyakati za giza aisee!
 
TBC wambeya sana. Nasikia wanajua undani wa suala lenyewe kwa hiyo hawakujua Mama atasema kiasi gani. Wanadai Naibu aliyeondoka walipimana vifua na Mama Suluhu. Ilikuwa sakata la uchaguzi wa EALA.

Naibu aliwaagiza wabunge fulani wagome na kutoka bungeni kama Kiimbisa hatiruhusiwa kugombea uspika. Wabunge wakapiga simu kumwuliza Mama, naye akawaruhusu wapige kura hata kama Kiimbisa si mgombea. Bifu likaanzia hapo.

Nasikia Kiimbisa na Naibu aliyeondoka "wako vizuri".
 
Hii story yako imekosa mashiko kabisa na unajaribu kuwavuruga watu wasijaribu hata kuuhisi ukweli wa tukio au unajaribu kuwavuruga watu wasipatwe na hisia hasi juu ya mkulu.

Hebu twende taratibu uone kama hata wewe haujaikataa story yako. Umesema aliyetumbuliwa ana bifu na makamu, okay, kama ametumbuliwa means katumbuliwa na rais hivyo makamu na mheshimiwa rais lao ni moja, ok? Sasa inakuwaje TBC waamue kusimama na yule jamaa dhidi ya rais na makamu wake? Ana nguvu kiasi gani huyu jamaa?

Hii story yako imekosa mashiko, imekosa miguu, imekosa hata makalio. Inadundadunda tu.
 
Hata wakati mama anaongea alikua kama kifua "kimejaa" hivi hakua kawaida..nashangaa wakamuondoa hewani then wakarudisha wakati muheshimiwa rais anaongea..anyway BTW Jana nilipenda muheshimwa Rais alivyokua mtaratibu safi sana.
 
Hakuna sababu ya kupoteza muda kujadili sababu za waziri kumwagwa,cha msingi ni kujiuliza ni kwanini aliteuliwa kuwa naibu waziri?pia ni kwanini alipomwagwa tu akateuliwa mwingine kwa kasi ya mwanga?Hapa jibu ni kwamba,kilichosababisha awe naibu waziri ndicho hichohicho kilichosababisha kumwagwa Mara baada ya kuwa opposite.
 
TBC wambeya sana. Nasikia wanajua undani wa suala lenyewe kwa hiyo hawakujua Mama atasema kiasi gani. Wanadai Naibu aliyeondoka walipimana vifua na Mama Suluhu. Ilikuwa sakata la uchaguzi wa EALA.

Naibu aliwaagiza wabunge fulani wagome na kutoka bungeni kama Kiimbisa hatiruhusiwa kugombea uspika. Wabunge wakapiga simu kumwuliza Mama, naye akawaruhusu wapige kura hata kama Kiimbisa si mgombea. Bifu likaanzia hapo.

Nasikia Kiimbisa na Naibu aliyeondoka "wako vizuri".
Acha uongo wako kama hukusikia kaa kimya......

Alichosema Mama Samia ni kwamba kule Wizarani kulitokea uzembe mkubwa Kiongozi wa Kimataifa anakuja nchini Raisi hana Taarifa...badala yake Taarifa wanapeleka ngazi za chini.

Hivyo Rais anakosa taarifa muhimu kuhusu mgeni wa nchi.....

Inawezekana Ziara Ya Mwana Mfalme wa Uingereza ndio iliyomtoa Naibu Waziri na Katibu wake kwenye hiyo Wizara.
 
Sawa,
Kwanin asianze na Mkuu wa ile Wizara mpaka amtumbue naibu wake?
 
Acha uongo wako kama hukusikia kaa kimya......

Alichosema Mama Samia ni kwamba kule Wizarani kulitokea uzembe mkubwa Kiongozi wa Kimataifa anakuja nchini Raisi hana Taarifa...badala yake Taarifa wanapeleka ngazi za chini.

Hivyo Rais anakosa taarifa muhimu kuhusu mgeni wa nchi.....

Inawezekana Ziara Ya Mwana Mfalme wa Uingereza ndio iliyomtoa Naibu Waziri na Katibu wake kwenye hiyo Wizara.
:D:D:Dalitaka kukwepa kuonana na mwana mfalme nn? tungesikia yupo mapumziko huko anakoendaga
 
Hii story yako imekosa mashiko kabisa na unajaribu kuwavuruga watu wasijaribu hata kuuhisi ukweki wa tukio au unajaribu kwavuruga watu wasipatwe na hisia hasi juu ya mkulu.
Hebu twende taratibu uone kama hata wewe haujaikataa story yako. Umesema aliyetumbuliwa ana bifu na makamu, okay, kama ametumbuliwa means katumbuliwa na rais hivyo makamu na mheshimiwa rais lao ni moja, ok? Sasa inakuwaje TBC waamue kudimama na yule kamaa dhidi ya rais na makamu wake? Ana nguvu kiasi gani huyu jamaa? Hii story yako imekosa mashiko, imekosa miguu, imekosa hata makalio. Inadundadunda tu.

logical thinking ya watetezi wa mkulu wengi ni negative.
 
TBC hii sasa mnaionea na sio inawaonea. mnajua hii ni kwa ajiri ya kusave interest za watu fulani na nyie bado mnaifuatilia ilihali hamuendani na watu hao?
 
Acha uongo wako kama hukusikia kaa kimya......

Alichosema Mama Samia ni kwamba kule Wizarani kulitokea uzembe mkubwa Kiongozi wa Kimataifa anakuja nchini Raisi hana Taarifa...badala yake Taarifa wanapeleka ngazi za chini.

Hivyo Rais anakosa taarifa muhimu kuhusu mgeni wa nchi.....

Inawezekana Ziara Ya Mwana Mfalme wa Uingereza ndio iliyomtoa Naibu Waziri na Katibu wake kwenye hiyo Wizara.

Acha hzi na wewe!
Yaani hilo limtoe Naibu Waziri lisimtoe Waziri na balozi wa nchi atokako mgeni huyo? By the way, hivi huyu Naibu waziri aliyeingia, naye anaamini hayo aliyoagizwa yanaweza kufanya kazi? Ana Portifolio gani kufanya hayo maamuzi? Hata Wakurugenzi alioagizwa kuwashughulikia hana mamlaka ya kuwagusa.
 
Hoja ilikuwa nini aliongea Samia jana wakati matangazo yamekatwa, hicho nilichokiandika ndio alichokiongea....

Sasa kuhusu ubunge EAC hayo ni mastori ya Town sikusikia.

Back
Top Bottom