Naibu Waziri Kapinga asema Rais Samia ameidhinisha Bilioni 20 kuboresha mabwawa ya umeme

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Naibu waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameidhinisha Tsh. bilioni 20 kwa ajili ya kufanya maboresho makubwa katika mabwawa ya umeme ya Kidatu, Kihansi na Mtera ili kuongeza ufanisi wa mitambo na kuwezesha mabwawa hayo kuzalisha umeme wa uhakika.

Kapinga amesema hayo leo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilipotembelea Mkoani Iringa katika bwawa la Kihansi “Mipango ya Serikali ni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa Nchi nzima na wa ziada hivyo ukarabati huu ukifanyika wa uboreshwaji wa mitambo ya uzalishaji umeme utaongeza nguvu katika ufanyaji wa kazi“

Kapinga amewataka Wananchi waondoe hofu kuhusu suala la umeme kwani ifikapo February mwakani majaribio ya uzalishaji umeme yataanza katika bwawa la Mwalimu Nyerere na June mwakani uzalishaji umeme utaanza na hivyo kuwa na umeme wa uhakika.

F5mOCr8WsAAYQ7r.jpg
 
Back
Top Bottom