Kwanini TBC1 walikata matangazo ya LIVE, wakati mama Samia Suluhu akiongelea kilichotokea Foreign mpaka Naibu Waziri kutumbuliwa?

Hii story yako imekosa mashiko kabisa na unajaribu kuwavuruga watu wasijaribu hata kuuhisi ukweli wa tukio au unajaribu kuwavuruga watu wasipatwe na hisia hasi juu ya mkulu.

Hebu twende taratibu uone kama hata wewe haujaikataa story yako. Umesema aliyetumbuliwa ana bifu na makamu, okay, kama ametumbuliwa means katumbuliwa na rais hivyo makamu na mheshimiwa rais lao ni moja, ok? Sasa inakuwaje TBC waamue kusimama na yule jamaa dhidi ya rais na makamu wake? Ana nguvu kiasi gani huyu jamaa?

Hii story yako imekosa mashiko, imekosa miguu, imekosa hata makalio. Inadundadunda tu.
Sasa, lete yako yenye mashiko tuisadiki
 
Acha hzi na wewe!
Yaani hilo limtoe Naibu Waziri lisimtoe Waziri na balozi wa nchi atokako mgeni huyo? By the way, hivi huyu Naibu waziri aliyeingia, naye anaamini hayo aliyoagizwa yanaweza kufanya kazi? Ana Portifolio gani kufanya hayo maamuzi? Hata Wakurugenzi alioagizwa kuwashughulikia hana mamlaka ya kuwagusa.
Atatoa mapendekezo kwa mkulu,mkulu atawapangua
 
Nisipo ona cheche za hawa watu hua nakosa furaha kabisa, hasa kuhusu mambo kama haya mubashara na yanaohusu wananchi kuwekwa gizani.

Sky Eclat
lucas mobutu
Frank Wanjiru
GENTAMYCINE

Tunaambiwa channel za taifa lolote, hazitakiwi kua na upande "BIASSED" kwa chochote kinachotokea nchini, wala kusafisha machafu ya serekali, wala hazipo kwaajili ya kutaka faida kama vyombo vingine vya habari, (Non Profit Organizations).

State channels are there for a "NOBLE CAUSE". But are we (tanzania) diving in information, but lacking knowledge.???
 
cha msingi ni kujiuliza ni kwanini aliteuliwa kuwa naibu waziri?
anybody anaweza kupewa uwaziri, utajuaje kama ni mzuri au mbaya?

swali ni, kwa nini Mahiga anaachwa wakati Rais anasema hii wizara kila siku anailalamikia?

Mahiga is a lightweight douchebag
 
If that is the case, waziri anaponaje? Nani mkuu kati ya waziri na naibu wake??
Acha uongo wako kama hukusikia kaa kimya......

Alichosema Mama Samia ni kwamba kule Wizarani kulitokea uzembe mkubwa Kiongozi wa Kimataifa anakuja nchini Raisi hana Taarifa...badala yake Taarifa wanapeleka ngazi za chini.

Hivyo Rais anakosa taarifa muhimu kuhusu mgeni wa nchi.....

Inawezekana Ziara Ya Mwana Mfalme wa Uingereza ndio iliyomtoa Naibu Waziri na Katibu wake kwenye hiyo Wizara.
 
Sasa kwa nini waziri kapona?
 
TBC wambeya sana. Nasikia wanajua undani wa suala lenyewe kwa hiyo hawakujua Mama atasema kiasi gani. Wanadai Naibu aliyeondoka walipimana vifua na Mama Suluhu. Ilikuwa sakata la uchaguzi wa EALA.

Naibu aliwaagiza wabunge fulani wagome na kutoka bungeni kama Kiimbisa hatiruhusiwa kugombea uspika. Wabunge wakapiga simu kumwuliza Mama, naye akawaruhusu wapige kura hata kama Kiimbisa si mgombea. Bifu likaanzia hapo.

Nasikia Kiimbisa na Naibu aliyeondoka "wako vizuri".
Uwongo mtupu
 
Mwenye wizara ajitafakari.
Sema jamaa ndio anatutoa kimasomaso safari za ughaibun, ametuwakilisha hata juzi UN.
 
anybody anaweza kupewa uwaziri, utajuaje kama ni mzuri au mbaya?

swali ni, kwa nini Mahiga anaachwa wakati Rais anasema hii wizara kila siku anailalamikia?

Mahiga is a lightweight douchebag
Jamani Rais huwa hapati nafasi ya kukutana na mawaziri wake na kuwapa visemina elekezi vya ndani au kushauriana nao pale mambo yanapoonekana yanaenda isivyo kabla ya kufikia uamuzi wa kutumbua?
 
Jamani Rais huwa hapati nafasi ya kukutana na mawaziri wake na kuwapa visemina elekezi vya ndani au kushauriana nao pale mambo yanapoonekana yanaenda isivyo kabla ya kufikia uamuzi wa kutumbua?

ana tabia ya kuwapigia simu directly kuwapa ma amri

Lakini huyu Mahiga kwa nini ni untouchable?

Uozo wa Foreign Affairs uko chini ya Waziri Mahiga, kwa nini mbuzi wa kafara anakuwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu?
 
Back
Top Bottom