Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,104
- 2,349
NB: JF Moderators, naomba hii thread ijitegemee. Najua imeshajadiliwa lakini naona huyu wakili kaja kivingine. Tuwape watu nafasi wajadili hoja yake..
Back to the topic;
✍️Ni kweli Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kuunda ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na kumteua Dr Salim A. Salimu kushika wadhifa huo..
✍️Vivyo hivyo Rais ally Hassan Mwinyi aliwahi kufanya kosa la namna hii na nafasi hiyo kushikwa na Hayati Augustine L. Mrema wakati kikatiba PM akiwa John Malecela..
✍️Sasa Rais Samia Suluhu Hassan naye kafanya makosa hayahaya.
Je, makosa ya mwingine yanaweza kuhalalisha jambo?
✍️Msikilize Wakili Msomi Boniface Mwambukusi akitolea ufafanuzi wa kisheria na kikatiba wa makosa haya..👇👇👇👇
Aliyoyasema kwa ufupi (quotes):
".....Ni kweli Rais kikatiba ana mamlaka na haki (right) ya ku - constitute na ku - abolish any office at anytime. Lakini haki na wajibu huu hau - extend kwenye office ambazo zimeanzishwa na katiba....."
".....Kwa mfano; ofisi ya PM, DPP, AG, Bunge au CAG ni ofisi za umma zilizoundwa na kuwekewa utaratibu na masharti maalumu kikatiba kuanzia katika uteuzi, utendaji na uwajibikaji wa watu wanaoteuliwa na kushika ofisi hizi..."
"....Mfano, Waziri Mkuu anapoteuliwa ni lazima athibitishwe na wananchi kupitia Bunge lao. Kwa maana hiyo, ni makosa na kwa kweli haiwezekani Rais atafute mtu mwingine kwa mlango wa nyuma (au wa uani) na amkasimishe majukumu ya kikatiba ya Waziri Mkuu. Hizo zitakuwa vurugu na ni kukiuka katiba.."
Ndugu Petro E. Mselewa, Pascal Mayalla JokaKuu denooJ Mag3 na wengine mna maoni yoyote?