Kwanini siri kubwa kwenye $300m ya Barrick?

Kitu ambacho hamjakijua ni mind your business!!
Sijui Kama nitaeleweka! Pambania maisha yako, pambania familia yako pambana upate fedha upunguze matatizo uliyonayo.

Lalamikia serikali yako kukupatia mambo ya msingi Hospitali na huduma nyengine ila wewe jiwekeze kujikimu hayo mengine utadata; hakuna atakae kupa taarifa ya uhakika hapa hiyo hela imekwenda kivipi.
Umenena kama msemaji wa serikali
 
Deni la taifa ni 56t, what is $300m? Mkuu unajua unachoongea au umelishwa ujinga na Kabudi na ww ukaumeza kama ulivyo?
Calm down mkuu, tunaweza kujadili kwa hoja bila kuita watu wajinga.
Kusema nimelishwa ujinga ni sawa na kusema mimi ni mjinga.

Nilichosema ni kwamba hao wanaotudai wakiona upenyo wa kukamata mali zetu tukaweza kupunguza deni wanalo tudai angalau 5% tu kibiashara kwao ina faida, utakubaliana na mimi ktk hili kama umewahi kujaribu biashara yoyote maishani mwako hata ya mgahawa au duka.
Au kama umewahi kufanya kazi sekta binfsi kampuni ya kibiashara.
 
Mkuu kwa sasa ndani ya hii nchi yetu hakuna popote kuna mijadala yenye mitazamo mbadala zaidi ya hoja za kusifia, humu mitandaoni pekee ndio kulikobaki kwenye hoja huru. Humu mitandaoni ndio pekee viongozi wanakopita na kupata mrejesho wa uongozi wao kwa kusoma mawazo mbadala. Kiongozi anapopita humu na kukuta ujinga wake ukipata watetezi, anazidi kupata nguvu ya kuendeleza huo ujinga.

Sasa ngoja twende pamoja uone kwanini nina haki ya kukuita mjinga, nimekuambia deni la taifa ni 56t, hiyo pesa ya Barick ambayo Kabudi alisema ikisemekana tumelipwa wanaotudai watakamata vitu vyetu ni $300m. Miezi miwili iliyopita serikali imetangazwa kwa mbwembwe zote kwamba mwezi nov tumekusanya 1.9t na mwezi dec 1.8t. kama kweli hofu yetu ni wale wanaotudai wakisikia tumelipwa $300 kama 700b+ watakamata mali zetu, je wakisikia tumekusanya 3t+ ndani ya miezi miwili si watakuja wakamate mpaka na wake zetu? Ni hivi, kama umeishiwa pumzi ya utetezi ni vyema ukakaa kimya kuliko kutumia sababu dhaifu kujenga utetezi wako.
 
Anaweza kukulipa na akafanya siri kwa public kutokana na makubaliano. sawa sawa tu na mikataba ya siri wanayo fanya kila siku.

Watajulishwa wanahisa kwa siri, itatoka public kwenye hesabu ya ukaguzi za kampuni husika iliyo lipa wakati tayari ishatumika.
Au watakapojulishwa wanahisa kwenye kikao hca wanahisa wakati zimeshatumika, sababu hapo kupitishwa malipo zimeshapitishwa.

Wana sahinishana ile Non Disclosure Agreement (NDA) tu.

..siyo rahisi kwa masuala ya fedha kwa makampuni yaliyoorodheshwa ktk masoko ya mitaji ya mabeberu.

..tena wanaweza kuingia ktk matatizo na mamlaka za udhibiti [ regulatory authorities] kwasababu mikataba ya namna hiyo inachukuliwa kuwa ni RUSHWA.
 
Mkuu kwa sasa ndani ya hii nchi yetu hakuna popote kuna mijadala yenye mitazamo mbadala zaidi ya hoja za kusifia, humu mitandaoni pekee ndio kulikobaki kwenye hoja huru. Humu mitandaoni ndio pekee viongozi wanakopita na kupata mrejesho wa uongozi wao kwa kusoma mawazo mbadala. Kiongozi anapopita humu na kukuta ujinga wake ukipata watetezi, anazidi kupata nguvu ya kuendeleza huo ujinga.

Sasa ngoja twende pamoja uone kwanini nina haki ya kukuita mjinga, nimekuambia deni la taifa ni 56t, hiyo pesa ya Barick ambayo Kabudi alisema ikisemekana tumelipwa wanaotudai watakamata vitu vyetu ni $300m. Miezi miwili iliyopita serikali imetangazwa kwa mbwembwe zote kwamba mwezi nov tumekusanya 1.9t na mwezi dec 1.8t. kama kweli hofu yetu ni wale wanaotudai wakisikia tumelipwa $300 kama 700b+ watakamata mali zetu, je wakisikia tumekusanya 3t+ ndani ya miezi miwili si watakuja wakamate mpaka na wake zetu? Ni hivi, kama umeishiwa pumzi ya utetezi ni vyema ukakaa kimya kuliko kutumia sababu dhaifu kujenga utetezi wako.
Ni hivi unaweza kumuonesha mtu udhaifu wake akajiona mjinga yeye mwenyewe bila kuitwa mjinga.
Sio busara kuita watu wajinga, kwa mfano na mimi nikija na maneno makali utaona tunaanza kuhamisha mjadala wenye hoja zenye afya kuhusu mada kuu tutabaki na matusi, na hapo uliowalenga watakosa hoja zako nzuri.

Wakati mwingi ni rahisi mtu kufuata ushauri wako kama haujajaribu kumtweza utu wake, au niite hauja 'mdharirisha', mtu akiumizwa nafsi anakuwa mgumu kupokea ushauri wako na mtaishia uadui na ushindani usio na faida.

Jambo jingine lazima utambue suala la udhaifu wa hoja ya mtu ni mtazamo, unachokiona wewe ktk nafasi uliyopo na taarifa ulizo nazo unaweza kuona hoja yako ni ndio sahihi, lakini ukiwa sehemu nyingine au katka nafasi nyingine ambayo unaona hoja yake dhaifu unaweza kuona yeye aliona au alijua kitu sahihi na wewe hoja yako ilikuwa dhaifu kwa muktadha huo mpya.

Its about perspective, we view things from different angles, different perspectives.
Tafadhari sana mkuu nakuomba uangalie hiyo video ya mdau toka Harvard utajifunza kitu kikubwa sana na kuanza kuheshimu mawazo ya kila mtu. Usisahu ku-switch on subtitles , captions.
 
..siyo rahisi kwa masuala ya fedha kwa makampuni yaliyoorodheshwa ktk masoko ya mitaji ya mabeberu.

..tena wanaweza kuingia ktk matatizo na mamlaka za udhibiti [ regulatory authorities] kwasababu mikataba ya namna hiyo inachukuliwa kuwa ni RUSHWA.
Inaweza kuwekwa wazi kwenye mamlaka husika za udhibiti, anyway tuendelee kujadili nami najifunza kitu toka kwenu.
 
Ni hivi unaweza kumuonesha mtu udhaifu wake akajiona mjinga yeye mwenyewe bila kuitwa mjinga.
Sio busara kuita watu wajinga, kwa mfano na mimi nikija na maneno makali utaona tunaanza kuhamisha mjadala wenye hoja zenye afya kuhusu mada kuu tutabaki na matusi, na hapo uliowalenga watakosa hoja zako nzuri.

Wakati mwingi ni rahisi mtu kufuata ushauri wako kama haujajaribu kumtweza utu wake, au niite hauja 'mdharirisha', mtu akiumizwa nafsi anakuwa mgumu kupokea ushauri wako na mtaishia uadui na ushindani usio na faida.

Jambo jingine lazima utambue suala la udhaifu wa hoja ya mtu ni mtazamo, unachokiona wewe ktk nafasi uliyopo na taarifa ulizo nazo unaweza kuona hoja yako ni ndio sahihi, lakini ukiwa sehemu nyingine au katka nafasi nyingine ambayo unaona hoja yake dhaifu unaweza kuona yeye aliona au alijua kitu sahihi na wewe hoja yako ilikuwa dhaifu kwa muktadha huo mpya.

Its about perspective, we view things from different angle, different perspectives.
Tafadhari sana mkuu nakuomba uangalie hiyo video ya mdau toka Harvard utajifunza kikubwa sana na kuanza kuheshimu mawazo ya kila mtu. Usisahu ku-switch on subtitles , captions.

Kwanza samahani kwa kukukwaza, ila uzuri najua sasa utakuwa umeelewa namna ya kujenga hoja zako ukiwa nje ya box. Narudia tena samahani kwa kukukwaza. Pia nashukuru kwa hiyo clip yako, lakini nitashindwa kuipitia kwani MB ni chache.
 
Wewe itunze link au jina siku ukiwa ktk nafasi nzuri ya kuingalia ni nzuri sana, sio kwako na kwangu tu bali mtu yeyote hasa viongozi wetu.
 
Sometime nawaza watanganyika nasema elimu bure na shule za kata ni mtaji mkubwa wa kutawala na sio kuongoza.

Nakumbuka hii ripoti ilitaka kumtoa mtu roho pale Dodoma na ilisemwa kuwa ni professional rubbish kuwa haina ukweli Wala uhalisia. Na zaidi tukaaminishwa kiwa tunaidai Barrick trillioni 425 na tukahaidiwa zitalipwa serikali hii sio ya mchezo mchezo maana tumeibiwa vya kutosha.

Wakaja mabeberu kukutana na majike ya hapa bongo zikapigwa danadana na acaccia tukaambiwa watalipa kishika uchumba yaani mahali itakuwa bilioni 700.

Nashangaa juzi nchi inaolewa bila kuambiwa fidia au mahari imelipwa ya bil 700 au nchi imeolewa bure.

Na makinikia yanaendelea kusafirishwa na Smelter hatujaambiwa inajengwa wapi.

Awamu hii ya kitapeli kuliko awamu zote, na ni awamu ya kifisadi kuliko inavyodhaniwa
 
Bwashee mbona tangu mkataba usainiwe umekuwa mtu wa kuhangaika hangaika kama kuku anayetaka kutaga?!

Mbona mwenzio Tundu Antipas Lisu ametulia!
 
Hiyo ni ratio ya kawaida kwenye uwekezaji bwashee!
Ccm mnaharaka ya nini miaka 59 mnashindwa kutoa elimu ya raia wenu wachimbe wenyewe mnauza madini kwa bei ya kutupwa na isiyo na faida. Kama sio ufisadi ni nini?

Thamani ya korosho inazidi ya madini hivi mnajiskiaje kiwa mapato ya korosho kuzidi mapato ya madini
 
Jamaa anasikitika Muhongo alifutwa kazi sababu alisema hiawezekani kujengwa smelter hapa bongo chakusikitisha mwaka wa 5 jiwe kashindwa na makinikia yanaendelea kusafirishwa ndio hapo anaona watawala wanaweka shule zakata bila elimu ili zitoke product poor kama wewe mnaoshangilia porojo maana ndio mtaji
Bwashee mbona tangu mkataba usainiwe umekuwa mtu wa kuhangaika hangaika kama kuku anayetaka kutaga?!

Mbona mwenzio Tundu Antipas Lisu ametulia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom