Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Niliwahi kuitumia iPhone kipindi fulani....ni upuuzi mtupu...limitations na complications ni nyingi..,yaani sina hamu nayo kabisa..ukilinganisha na simu za android....ukiwa nayo inakufanya ujisikie tofauti lakini hakuna lolote .....mara ya mwisho nilimwachia mke wangu sababu anapenda kujisikia
 
Unajua hap a bado nashindwa kuelewa, mi nimeleta video za fornite tu kama sikosei, na sikumbuki na sina uhakika kama niliiweka ya EverythingApplepro, ila nimeona wewe ndio ulileta video yak moja. kama nimeweka naomba uniekee post number ili nitizame na point yak nielewe vizuri

Were die uliekariri milioni moda inanunua mini, mano wewe ulisema kuwa simu ya milioni unategemea kit flan na kitu flani kiwepo.


Hakuna mahali nimesema kuwa kuna kampuni inayomzidi samsung kwa rams na memory.

Ila wewe unasema kuwa sam hakuweka 8GB rams kwenye s9 kea sababu kuna possibility kuwa haikuwezekana, ukanambia ram hazipachikwi tu. Ni kwanini Note 9 inakuja na 8GB rams na version nyengine ina 6GB rams? more is better mkuu au sio? kwanini sam amefanya ivo? kwanini asiweke tu 8GB rams kwenye model zone na tech annoy na zone ni high end phones?

Mkuu Intel sio kampuni ndogo, wala intel hawatengezi vitu vya low quality. Kama apple ameona chip ya intel a well known company ipo cheaper kwanini asihamie uko tu? Apple haters ndio wanasema kuwa ah apple anasource low quality items. LOW QUALITY unajua what it means?


Mkuu, unanisikitisha mtu wa tech anashangaa Software can cause a glitch on hardware. Software na hardware zinafanya kazi kwa pamoja, ndio maana ukiingia settings ukiweka Airplane mode, unashindwa kupata huduma yoyote ya mawasiliano hali yakuwa antenna bado ipo na simu hujaichomoa. Na usiwadanganye wenzako, wewe ni hater wa apple na unaongea kile wanachoongea apple haters, ni asilimia 1.7 ya simu zote zilizouzwa ndio zilizoripotiwa kuwa na tatizo la antennagate, mimi nimetumia iphone 4 na hakuna icho kitu nilicho experience. Ilikuwa inafanya kazi vizuri tu. Pia Steve amesema kuwa walifanya error kwenye software, ambapo ilikuwa inafanya makosa ya calculation kwenye kudisplay signal bars, ilikuwa inaonesha 2 more signal bars instead of the correct one.


Mkuu mimi sio wa kunifundisha ramani inatengezwa vipi. labda nkwambie wewe inavotengezwa, kwa sababu wewe umesema kuwa Apple ni watu wa low quality na cheap choices. Nikakwambia kuwa google maps inatolewa bure, sasa kwanini unadai kuwa apple is going cheap? Apple hater as usual misinforming the public. Google maps ni free na kutengeza Apple maps was adding up costs in the financial reports tu. Kama Apple watu wa cheap kwanini watumie mabilioni kutengeza maps zao basi?

Google wapo so advance kwenye suala la ramani na wamepiga hatu sana, kwenye huu uwanja Apple atulize kipira tu na aendelee kuship iphones with gmaps.

Chief kuna vitu nikwambie wewe sio wewe unambie mimi. Ikiwa Nokia phones were profitable and were about to keep on leading the market, je hio sio pesa? Hapo Board haipati pesa? Wewe kama investor, na unajua kabisa kampuni yako itakuingizia hela miaka 20 au 50 ijayo, tena hela ndefu, na hapo ulipo huna shida yoyote, utakubali mtu aje akwambie nakupa bilioni 100 unipe kampuni hio wakati wewe kwa mwaka unaweza kutengeza zaidi ya hio?


unapokuja kubrag kuhusu nokia sales, waambie wasomaji Nokia alikuwa na model ngapi za simu na bei zake na Apple alikuwa na model ngapi za simu na bei yake. Pia waambie kuwa simu za nokia zilikuwa zikisambaa worlwide, wakati Apple alikuwa ka base na At&T wake tu.

Na pia Nokia alikuwa na os ya meego kwa ajili ya highend,Nokia N9 ilikuwa discontinued kabla haijatoka, japo ilikuwa discontinued iliuza simu zaidi ya milioni 5 hebu. Kati ya s2 na iphone 4 ipi inamzidi Nokia N9?
Unazungumzia kimauzo ama kivipi yaani? mana kimauzo Apple kauza nyingi tu kuliko N9.


Sifa zote hizo ulizozitaja, lakini imeshindwa ku compete na Apple na Samsung 😀

Yaani ili ufikie asilimie 40 tu ya mauza ya Sam au Apple utengeze simu milioni 200 😀 na wewe ndio unaona sifa hio. Yaani wewe unatengeza simu nyingiiiiiii halafu mwisho wa siku jamaa anatengeza simu zake tano, anakuita kwa asilimia 60? wewe hii umeona ni sifa ya kujisifia? 😀 pole mkuu.

Ata ivi vitecno viduchu havitaki matangazo vinajiuza tu wenyewe pia utafananisha na Samsung? Hivi Samsung au Apple anapotoa tangazo huwa wanashindana na Nokia ya tochi au? 😀 Wanatafuta market ya nokia torch users waanze kutumia iphone x na note 9?

Kwao una maanisha kuwa Apple hana invention wala technology ama?

Chief kumbe unatumia uwezo wako kuwa misinform public. Usitumie sifa ulokuwa nayo ukawa unawadanganya watu hapa.

Apple ame invent vitu vingi tu, na alivokuwa haja invent yeye basi ameviboresha au amebadilisha market.

Sisahau kauli yako ulivodai kuwa Nokia akikohoa Apple matrilioni yatamtoka, ivi kweli kabisa asikohoe basi Nokia? Huu uwanja wa technology huwezi kila kitu ukawa wewe una manufacture kila kitu. Hata Nokia hakuwa akitengeza kila kitu mkuu.

Kuwa muwazi na mkweli utakuwa huru. Mapenzi yako kwa nokia yasikufanye ukawa kipofu kwenye ukweli. Simu za nokia na symbian wake wamekufa na killer wao ni android na ios sio Elop kama unavojidai. Tayari board imeona kuwa imeachwa mbali na OS mpya na ikajitambua kuwa haiwezi ku compete, ikawalazimu waio symbian tu waje na nyengine ndo hao akina meego, nao pia wamekufa hawakusucceed kwenye market ambayo tayari ios na android zimeanza mapinduzi. Nokia na Blackberry wamekufa kifo cha mende! kampuni mbili izo zilikuwa zinatapatapa kuokoa Jahazi, Nokia wakaingia mkenge kwa MS na BB kaingi mkenge kwenye android, upande ambao Samsung kaucheza kama maradona.

Pole Chief Mkawa, kubaliana na matokeo, Symbian hata irudi saiv itabuma tena, kwa interface ile na ya meego? hawana pakupapatua. Yaani izo nokia za android saiv zinauzika kwa sababu ya jina tu la Nokia, lakini hamna kitu na still hazionekani kwenye soko.
 
Kiukweli wapo wanaotumia iphone kwa ulimbukeni kuwa wataonekana wako class flani hivi,but pia wanaoztumia kwakuzipenda kiuhalisia
 
Upande wa Bluetooth sio kwa ajili ya kurushiana videos tu mkuu. Kuna kustream music na hometheatre system via bluetooth, pia magari kibao infotainment system zake ni more bluetooth compatible than other connections
Apple wanachofanya ni kutengeza their own eco system, ili kuhakikisha devce zao zina run kwenye perfomance wanayotaka wao.

Hata ivo, ukijailbreak iphone hizi mambo ulikuwa unapata fresh tu. SI kwamba iOS haiwezi kufanya hilo jambo kama ma haters wanavotaka watu waamini, ila wameirestrict tu lakini ukijailbreak unapata features nyingi tu.

Mfano 3gs ulikuwa huwezi kushare hotspot, ila ukijailbreak inashare fresh. Wanachofanya Apple saiv, ni kama imewalazimu kukubali matokeo, wakaanza kuimplement features ambazo zlikuwa unapata kwa kujailbreak sasa wakafanya haina haja ya kujailbreak.
 
Umechanganya mambo mawili kwa wakati mmoja.
Video ya everythingApple pro ni proof kwamba iphone hazina lead tena kwenye optimisation na speed ya simu kwa ujumla nimekupa huyo ni fan wa apple asie na bias ila nyie huku endeleeni tu kutetea.

Na fortinite nakujibu sijui mara ya ngapi hiii, lete video inayoonyesha setting usiniletee video za kitoto zinaonesha huku na huku basi,unajua naweza kukutengenezea hapa video kama hio nokia ya tochi inarun hilo game smooth kuliko simu yoyote duniani, ni easy kufake hizo video. Tafuta video moja ya pc gaming review ya vlogger mkubwa kama linus hivi then utaona gaming review inafanywaje.


Were die uliekariri milioni moda inanunua mini, mano wewe ulisema kuwa simu ya milioni unategemea kit flan na kitu flani kiwepo.
Ndio nategemea kwa wakati fulani simu ya milioni iwe na kitu fulani kutokana na technology ilipofikia, huwezi ukatoa hela nyingi na kuuziwa kitu kisicho na thamani ya hela.



Ndio maana nikakuambia hapo juu, unapoipinga kampuni kubwa zaidi ya ram duniani unatakiwa uwe na hoja zenye mashiko,huleti hoja nikuamini wewe ama samsung? Na kuna utofauti baina ya s9 na note 9 wa miezi 6.


Officially umequalify kuwa isheep mkuu, nimekupa website kibao tena za fans wa Apple na website kubwa kubwa hata google mwenyewe sasa hivi intel kapitwa vibaya vibaya na qualcomm kwenye modems sehemu nyengine mara mbili zaidi bado unabisha.

Ba intel ni mtaalamu wa cpu, haimaanishi ni mtaalamu wa kila kitu.



hivi mkuu asilimia 1.7 ya mamia ya mamilioni wanayouza Apple ni ndogo?japo hizo data hujazithibitisha ila still ni namba kubwa,ni zaidi ya mkoa wa kawaida wa Tanzania.

Na wewe ni fan wa Apple utaona? Dunia nzima imeona ila wewe hutaona,BBc CNn watareport ila kwako itakuwa ni uzushi tu.

Na hilo ni tatizo la hardware halina uhusiano wowote na software,tatizo linatokea pale unapoziba mkono wako kwenye Antenna,tumia akili angalau kidogo nakuomba. Futa neno Apple kichwani mwako ufikiri angalau sekunde.



Hapana unapo preload ramani kwenye simu unataka watu watumie hio, wangapi wana fikra ya kwenda store na kuchagua nyengine?uthibitisho angalia malalamiko waliyoyapata Apple na kesi za polisi zilivyokuwa nyingi.

Sasa jiulize umetoa milioni 2 umenunua simu,unapanda gari lako unaiambia simu ikupeleke morogoro,simu inakupeleka unashuka upo lindi,is this your definition of high quality? Walijua Apple ila they dont care sababu wanajua kuna watu wanaabudu tunda watanunua tu. Wangapi walipelekwa kwenye misitu?wangapi walipata ajali?

Google wapo so advance kwenye suala la ramani na wamepiga hatu sana, kwenye huu uwanja Apple atulize kipira tu na aendelee kuship iphones with gmaps.
Ushauri mzuri.


Kwani sasa hivi hawaingizi? Wao ndio wafanya biashara wanaojua. Baada ya kuuza department ya device Nokia kwa dola bilioni 16 ameinunua Alcatel lucent na kutanua kampuni kwa upande mwengine, wamebeti hela zao kwenye 5g,subiri hadi 2020 tutajua kama wapo sahihi ama la.

Na nokia ina miaka 150 hizi ni baadhi ya specialist zao
-matairi ya magari
-kiwanda cha makaratasi
-radio call za kizamani
-watengenezaji computer
-simu
-network etc

Wameweza kusurvive muda wote huu kwa ku adapt na mazingira, ukiangalia mapato ya Nokia sasa hivi na department ya simu yoyote ukitoa samsung na Apple, Nokia wapo juu. Si lg,sony,Htc,xiaomi, etc ambaye anaingiza hela kwenye simu na hata Huawei am not sure.



Mkuu kwani simu inayoongoza kwa mauzo duniani ni ipi? I mean single device sio mauzo ya jumla.
-simu ya kawaida kitochi cha 1100 iliuza 250m
-smartphone nokia 5230 iliuza 150m

So overall simu pamoja na smartphone nokia ndio ana record, mauzo yake hayakuwa yakitegemea wingi wa aina bali hata device moja moja.

Na sijakutajia N9 kubrag mauzo,just nakwambia simu iliokuwa discontinued, unaelewa maana yake? Hakuna tangazo popote pale iwe barabarani ama kwenye tv,no software updates,no support etc dead phone kabla haijazinduliwa ila still watu wakainunua hivyo,sijui unapata my point?


Unazungumzia kimauzo ama kivipi yaani? mana kimauzo Apple kauza nyingi tu kuliko N9.



Sifa zote hizo ulizozitaja, lakini imeshindwa ku compete na Apple na Samsung 😀
So umehamia kwenye mauzo na umeshindwa ku compare features? Hata dagaa wanauza sana kushinda nyama ya kuku ama samaki wakubwa it doesnt make dagaa better. Unaweza list ya features ambazo simu yako pendwa ilikuwa inafanya zaidi?


Model za biashara hazifanani na Nokia alikuwa true deicated kwa watu wote duniani? Hakuwa bepari. Kampuni pekee iliokuwa inafanya research za simu za shilingi 30,000.

Na hata mapato yao at that time yalikuwa makubwa.

[/quote]Ata ivi vitecno viduchu havitaki matangazo vinajiuza tu wenyewe pia utafananisha na Samsung? Hivi Samsung au Apple anapotoa tangazo huwa wanashindana na Nokia ya tochi au? 😀 Wanatafuta market ya nokia torch users waanze kutumia iphone x na note 9? [/quote]
Hapana mkuu kaangalie Aggrey na msimbazi matangazo ya Tecno na itel kama uchafu vile yalivyo mengi.

Inategemea na aina ya tangazo, yapo yanayotafuta wateja wa tochi pia. Na sijaelewa mantiki yako hapa. Unataka kukataa hayo makampuni hayaspend 10b usd kwenye matangazo?


Kwao una maanisha kuwa Apple hana invention wala technology ama?

Chief kumbe unatumia uwezo wako kuwa misinform public. Usitumie sifa ulokuwa nayo ukawa unawadanganya watu hapa.
Hii ni public forum badala ya kunituhumu kwa heshma na taadhima naomba useme uongo wangu.

Apple ame invent vitu vingi tu, na alivokuwa haja invent yeye basi ameviboresha au amebadilisha market.
Taja inventions zake.

Sisahau kauli yako ulivodai kuwa Nokia akikohoa Apple matrilioni yatamtoka, ivi kweli kabisa asikohoe basi Nokia? Huu uwanja wa technology huwezi kila kitu ukawa wewe una manufacture kila kitu. Hata Nokia hakuwa akitengeza kila kitu mkuu.
Kuna utofauti baina ya manufacturing na inventions ni vitu viwili tofauti na kuhusu Nokia na apple unafahamu kila iphone inayouzwa Nokia anapata hela kwa amri ya mahakama?na mwaka jana tu Apple kamlipa nokia 2B (trilioni zaidi ya 2) baada ya figisu za mahakamani tena.

Mkuu nimekupa ushahidi kipindi elop anaiua symbian Nokia alikuwa anauza simu kuliko samsung na Apple combined, na symbian ilikuwa ni top operating system at that time,kama una data tofauti naomba uzilete hapa na sio maneno matupu.

Symbian haiwezi kurudi,ila nimekupa mifano kama ingekuwepo still ingedanikiwa sababu mahitaji ya smart feature phone ni makubwa.

Kuna mambo mawili makubwa yametokea duniani mwaka jana.
-Hmd amerudi na simu za nokia
-kutoka kwa jio phone india.

Mambo hayo yamepelekea.
-kwa mara ya kwanza duniani mauzo ya smartphone yameshuka
-mauzo ya feature phone yamepanda.

Huo ni ushahidi tosha mkuu si kila mtu anahitaji smartphone lenye kioo kikubwa,kuna mtu anataka tu simu ndogo ya whatsapp,apige simu simu na fb basi,simu ambayo hata akiidondosha mara 100 kuharibika ni ngumu.
 
Umechanganya mambo mawili kwa wakati mmoja.
Video ya everythingApple pro ni proof kwamba iphone hazina lead tena kwenye optimisation na speed ya simu kwa ujumla nimekupa huyo ni fan wa apple asie na bias ila nyie huku endeleeni tu kutetea.
Are you sure EverythingApple Pro hayupo Bias? inaonekana unajicontradict mwenyewe sasa, ni wewe ndie ulisema kuwa Apple ndio mwenye processor zenye speed kuliko wote, leo hii unasema kuwa hana tena Lead? mhhh

Lete wewe basi yenye kuonesha settings unazozungumzia. Tujaalie zote mbili zilikuwa zinarun under minimum settings, huoni kuwa iPhone ina perform better na 4GB rams zake over Samsung's 6GB ram? Why?

Ndio nategemea kwa wakati fulani simu ya milioni iwe na kitu fulani kutokana na technology ilipofikia, huwezi ukatoa hela nyingi na kuuziwa kitu kisicho na thamani ya hela.
Sasa kwanini unanambia kuwa mimi ndie niliekariri pesa fulani inanunua nini? wakati ni wewe mwenyewe ndio uliekariri.

Ndio maana nikakuambia hapo juu, unapoipinga kampuni kubwa zaidi ya ram duniani unatakiwa uwe na hoja zenye mashiko,huleti hoja nikuamini wewe ama samsung? Na kuna utofauti baina ya s9 na note 9 wa miezi 6.
Bado mkuu hujatetea unachotetea. nazungumzia Note 9 na sio s9. Note 9 inakuja na version yenye 6Gb of Rams na nyengine inakuja na version ya 8Gb of rams. Sasa kama wewe unasingizia kuwa Samsung hakuweza kuweka 8GB of rams kwenye S9 kwa sababu ramu hazipachikwi tu na huenda akawa hakuwa na hio tech miezi sita iliopita, tena vipi anatoa simu same model, made during same period lakini with different Ram memory? Kwanini asiweke tu 8Gb of rams kwenye note 9 zake zote?

Nikuulize, what is the reason behind to call me an isheep? 😀

Kwakuwa Apple kaona bora atumie intel instead of Qualcomm ndio amekuwa ana opt for low quality products? Kwaio basi kampuni nyingi wanatumia Low quality products, kwa sababu almost all PCs zinatumia intel chips, that means they are of low quality!!!



1.7% out of 100% umeiona ni kubwa sana kuliko 98.3% working phone with similar design... Ata kipofu mkuu hawezi kukubaliana na wewe.

Apple akipiga mayowe tu, media zote na haters kama wewe mnaamka mkiombea liwe baya mpate la kuandika. Kuripotiwa na cnn au bbc ndio ujue kama Apple is a Big company. All eyes on Apple. ukitaka usitake, najua hili linakuuma sana unapoona Apple yupo juu ya Nokia, unapoona iphone ni simu ya juzi tu lakini Nokia ipo zamani kifo cha mende.

Hivi watu wangapi wametekwa Tanzania na Cnn na BBc hawana habari lakini katekwa Mo tu habari imefika kote uko? ndio ujue kuwa Apple ina influence kubwa sana. Habari za nokia sizipati, ni juzi tu hapa naona na wao wameamua kuingia kwenye Notch city, wakati wenzao walipofanya waliwacheka na kuwazomea 😀

Hakuna mahali nimekataa kuwepo kwa tatizo la antenna, au ipo sehemu? kama ipo onesha basi. Mimi nashangazwa na mahaters, mnavolifanya kuwa simu zote mbovu, mapaka ukadai kuwa niende nkanunue simu Aggrey nitaikuta na hilo tatizo. Umemaanisha kuwa every iphone 4 ilikuwa na hili tatizo, na huo ni uongo! kwa sababu binafsi nilikuwa natumia iphone 4 na sijawahi kuexperience hilo tatizo la kwamba eti network bar zinapungua.

Na hilo tatizo linaweza kuwa hardware ONLY na linaweza kuwa Hardware with SOftware issue, hata apple wenyewe walipoletewa hili tatizo katika statement walisema ni software Glitch na watajaribu kutoa update.

Juzi hapa, kulikua na charge gate, mbona tatizo limekuwa solved kwa kutumia software basi wakati port ni harwdare na cable yako ni hardware? lakini Apple wamefix kwa software tatizo lua kucharge. Au njoo uwaambie wasomaji kuwa nalo ni jambo jipya kuwa tatizo la kuchaji simu linasolviwa na software wakati ni hardware.



Sikiliza mkuu, Tatizo huwajui watumiaji wa Apple products. The only reason, watu walitumia Apple products kwa sababu wanapenda kutumia Apple products, hivo basi wakaona kuwa finally sasa wanayo Map app from the manufacturer, hawa ni watu ambao wanapenda kubaki kwenye eco system ya Apple. Walivotoa Apple maps, kama utaamini, sijawahi kuifungua hio app mpaka ale nilipoona malalamiko ya watu na kusema ngoja nione watu wanacomplain nini, nikafungua maeneo nnapokaa wala sikutaka kwenda kwenye miji nisioijua, nilichokuta nilicheka, kwa sababu wanadata za tangu yaani mji au haukuwa, ni very old data information. I have always been a google map user kwa sababu najua kwanza ipo zamani na wako well experienced na wanajua ku collect data, kama sikosei, its not even apple collecting data for their map app, sijui kuna kampuni walinunua ambayo inahusu maps. Yaani its not something from scratech bali wali acquire from reay made company.

How can a software problem classify a device as low Quality or makes a company low quality? Mbona husemi Nokia kuwa wao ndo one of those with low Quality standards? Unatumia symbian os ambayo iko super vulnarable to virus. No wonder Symbian became a failure!

So umehamia kwenye mauzo na umeshindwa ku compare features? Hata dagaa wanauza sana kushinda nyama ya kuku ama samaki wakubwa it doesnt make dagaa better. Unaweza list ya features ambazo simu yako pendwa ilikuwa inafanya zaidi?
Anae brag Nokia kauza simu milion 500 nani kwani? mie au wewe?

Sina haja ya kulist features ambazo Apple made them better, you can see for yourself. Nokia n9 had no home button, au sio? who cared? iPhone made it better. Nokia n9 ndio ilikuwa na hizo gestures za kunavigate, Apple made them better, multi touch screen were there, Apple made them better, the notch was there au sio? Basi Apple made it better, now even the Android maker ame optimize OS yake for the Notch 😀 the list keeps on Going.

Halafu huo mfano wako wa dagaa, ndugu yangu huoni unakurudia. Wewe unasifia kuwa Nokia kauza simu 300 milioni only one model, hii nokia hapa ndio dagaa lenyewe, hawa kina iphone na samsung ndio nyama na kuku na samaki wakubwa, kwaio vidagaa nokia doesnt mean they are better. Naomba ukae ufikirie tena huu mfano wako ndugu yangu. Unakurudia.

Model za biashara hazifanani na Nokia alikuwa true deicated kwa watu wote duniani? Hakuwa bepari. Kampuni pekee iliokuwa inafanya research za simu za shilingi 30,000.

Na hata mapato yao at that time yalikuwa makubwa.
Kwani Apple hafanyi research au? Mbona apple ina sifa nzuri ya customer care kwanza japo kuwa wanapenda kuwagonga watu kwenye kurepair. Kukiwa hakuna tech ya kutengeza kitu fulani, utafanya research tu hata kama ni cha buku 1, as long as unajua kitakuletea faida. Kwaio wakati Nokia wana wazo la kutengeza nokia tochi, itabidi wafanye research and development kwanza.

Sio Apple tu, kila kampuni inafanya reasearch kwenye product ambayo wanataka kutengeza.

Tecno Spark 8, haina lengo la kumwambia mtumiaji wa nokia tochi ahame atumie tecno k8. ni 2 different market. Tecno, itel na wengine, wanaotumia android, wanawaambia watumiaji wa izi samsung kuwa na sisi tupo tena bei rahisi na unapata all service.

Huwezi kukuta s2 eti inalinganishwa na nokia torch, wakati target market ni tofauti.

Hii ni public forum badala ya kunituhumu kwa heshma na taadhima naomba useme uongo wangu.
Umedai kuwa Apple ditched 3d touch, while ipo kwenye simu zake inaendelea kutumika. Unasema kuwa Nokia akikohoa tu Apple anatoa matrilioni. Mbona haendelei kukohoa basi. Unawaambia watu kuwa iphone 4 (na ulimaanisha in general) kuwa zinatatizo la antenna gate na ukafikia kusema mtu aende aggrey akanunue iphone 4 basi atakuta hilo tatizo. haya uloyasema yana ukweli? 3d touch bado inatumika, Nokia kakohoa mara moja tu na hakohoi tena, iphone 4 sio zote zilizoathirika na unaweza kwenda agrrey ukapata ilokuwa haijaathirika. Ukaenda to the Extreme, eti unaweza kutengeza fortnite ikarun kwenye Nokia torch!

Taja inventions zake.
Go through Apple patents.

Sio Nokia tu, Apple analipa na wengine, ndio ujue kuwa katika uwanja wa technology kuna kutegemeana. Kama zilivo simu zako za Nokia zenye android, wananunua snapdragon kwa Qualcomm, wangetengeza zao basi.

Mkuu nimekupa ushahidi kipindi elop anaiua symbian Nokia alikuwa anauza simu kuliko samsung na Apple combined, na symbian ilikuwa ni top operating system at that time,kama una data tofauti naomba uzilete hapa na sio maneno matupu.
How old was symbian? and how old was iOs na Android by that time. Hata saivi kama shabiki wa liverpool anakwambia Liverpool ilikuwa ikiongoza, tulia, watu wameanza kuingia sokoni ndani ya muda mfupi tu wamempiga na chini Symbian na nokia wake wakitapatapa taabani, mnamsingizia Elop LOL!

Kama symbian au Meego ilikuwa na uwezo wa kuendelea kudominate manake ingekuwa profit kwa Nokia investors, kwanin hawajaendelea nayo? Izo pesa walizozipata wameenda kuekeza Alcatel. Nlifikiri zimetiwa mfuno kumbe zimerudi tena kwenye uwekezaji. Wamejua kuwa HAWAWEZI KU COMPETE WITH THE RISE OF IOS na ANDROID DEVICES!
Kuna mambo mawili makubwa yametokea duniani mwaka jana.
-Hmd amerudi na simu za nokia
-kutoka kwa jio phone india.

Nokia android kama kawaida, haina ishu.

Mambo hayo yamepelekea.
-kwa mara ya kwanza duniani mauzo ya smartphone yameshuka
-mauzo ya feature phone yamepanda.
Kushukua kwa mauzo ya smartphone haimaanishi kuwa eti features phone (especially Nokia) ndio anatereresha market, tatizo la smartphone ni ghali sio wengi wenye ku affroc na hasa hivi sasa. Hivi unasahau kuwa a phone is more than just a calling an texting device saiv? Facebook kwa sms pia unaweza kwenye nokia torch.
 
Are you sure EverythingApple Pro hayupo Bias? inaonekana unajicontradict mwenyewe sasa, ni wewe ndie ulisema kuwa Apple ndio mwenye processor zenye speed kuliko wote, leo hii unasema kuwa hana tena Lead? mhhh
Kama site za fans wa apple zimekuwa bias against apple wenyewe tutumie site gani sasa.

Tumia hata 1% ya akili yako

simu yenye processor yenye nguvu zaidi duniani impitwa speed na isio na na nguvu je ipi imekuwa optimised zaidi?

Na jamaa anaonesha kabisa hadi mfano wa kurender 4k ameeka jinsi exynos ilivyokuwa blazing fast,


Lete wewe basi yenye kuonesha settings unazozungumzia. Tujaalie zote mbili zilikuwa zinarun under minimum settings, huoni kuwa iPhone ina perform better na 4GB rams zake over Samsung's 6GB ram? Why?
Umekazania tu gb za ram, as if ndio most specs inayotumika kurun games vitu muhimu wala huna haja navyo.

Na videos kadhaa nilizoziona youtube zote ni newbie au wapiga hela ndio wamezieka mtu anafungua tu game na ku compare. Huwezi ukachukua simu ya QHD na kucompare na FHD it will never works until utweak games zote mbili zirun at same setting. Nimekuambia hapo juu na nakwambia hapa tena. Unless mtu aoneshe hiki kitu kwenye setting hakuna comparison.


Sasa kwanini unanambia kuwa mimi ndie niliekariri pesa fulani inanunua nini? wakati ni wewe mwenyewe ndio uliekariri.
Kuwa na expectation na kutegemea tech fulani iwe kwenye flagship si kukariri bali ni kujielewa.


Serious mkuu? Kwanini iphone asitumie tu kioo kimoja simu zote? Kwanini kaeka ukubwa tofauti? Kama unataka simu ya 8gb nunua ya 8gb kama 6gb inakutosha nunua 6GB, kuna watu wanatumia tu whatsapp simu zao,


Nikuulize, what is the reason behind to call me an isheep? 😀
Hio ni brandname ya fans wote wa apple ambao wao wanasifia everything from Apple na kukandia everything kinachoenda against Apple bila logic yoyote.


Kwakuwa Apple kaona bora atumie intel instead of Qualcomm ndio amekuwa ana opt for low quality products? Kwaio basi kampuni nyingi wanatumia Low quality products, kwa sababu almost all PCs zinatumia intel chips, that means they are of low quality!!!
Hapa naendelea kukuelezea maana ya isheep.

Fikiria mkuu mwenyewe, unatumia modem ya gigabit lte inakupa speed ya maana unatoka sababu ya utofauti wa few dollar unaipa tenda kampuni isio na experience ya modem inakutengenezea modems kimeo. Simu zako zinatoka zinakuwa na speed kidogo kushinda flagship za kampuni zote.

Halafu fans zako wanaanza kushangilia ujinga wao uliofanya. Kondoo pekee ndio wana ujinga huu kila wanaposwagwa wanaenda. Jina la isheep wamepewa fans wa Apple sababu hii.

Kukazania kwenye modems nakupa tena source nyengine.

Qualcomm: Snapdragon 845 phones destroy Intel modem rivals in speed tests

Hapo sd845 ni hadi 53% faster zaidi ya intel.

Na mkuu usifananishe biashara ya modem na processor ni vitu viwili tofauti. Tunanunua laptop zenye processor za intel na sio laptop zenye modem za intel. Ukikuta laptop ina line ile modem sio ya intel itakuwa ni Qualcomm,Ericson,broadcom etc.

Sababu kampuni fulani ni bora kutengeneza bidhaa A haimaanishi ni bora pia kutengeneza Bidhaa B.


Serious mkuu? Unajua ni simu ngapi za note 7 zililipuka? Marekani walikuwa na incident kama 92 tu na worldwide hazifiki hata 1000 compare na mamilioni ya simu zilizouzwa hio haifiki hata asilimia 1, ila still simu zote zilirudishwa.

Asilimia 1.7 ni kubwa sana. Na job alikuwa akidanganya mwanzo mwisho kwenye hio issue.

Na pia mkuu Aplle hakufix hio antenna mwisho wa siku walitoa tu macover ya bure ili watu wasishike lile eneo la antenna. Hakukuwa na sofware wala firmware iliosolve. Na mpaka leo iphone ni moja kati ya simu mbovu zaidi linapokuja suala la kushika network. Mjini tu unaweza usipate full bar ya network. Namaanisha hadi hizi mpya.

Kuna uzi mzuri huu wa forbes unaelezea mambo yote ya antenna
Apple Didn't Learn From The iPhone Antennagate Scandal




Does it matter wameitoa wapi? Kama bidhaa haipo tayari ilitakiwa isiletwe sokoni simple and clear. Ninunue simu ya milioni kisha ikanitupe msituni?unaanza vipi kutetea hapa?


Problem moja haijustify ila kukiwa na multiple problems inajustify.

Na tena na tena narudia symbian ilikuwa discontinued ikiwa na marketshare kubwa kushinda ios na android. It was never a failure. Symbian haikushindwa sokoni ilishindwa kwenye vichwa vya kina Elop.


lmao you mean copying them?

So kucopy innovations za watu na kuzimodify ni ufahari nao?

So akiuza Nokia ni dagaa ila mukiuza nyie ni kuku? Mbona sasa munakimbilia kwa dagaa kila siku ku licence technology?


Sababu zoote za apple kufanya research uliyotoa ni customare care?kweli wewe fans wa Apple.
Hivi kuajiri mtu akatoa support nzuri na kuwahudumia vizuri wateja kuna mahusiano gani na mtu kuingia maabara na kuvumbua mambo mapya?


Simu za lowend smartphone lengo lake mojawapo ni kutransform user wa feature phone wanunue smartphone, ili baadae waje wanunue model kubwa.

Mfano mtu anaenda dukani kuna tecno ya button ya 70,000 na anakuta tecno ya touch ya smartphone ya 80,000 anakuwa tempted na kununua touch. Akianza kuingia ulimwengu wa fb na insta simu inakuwa slow, jinsi matumizi yanavyoongezeka na yeye anajichanga kutafuta simu nzuri zaidi.

Hata google mwenyewe ametengeneza android mpya inaitwa android go kwa ajili ya kazi hii tu.



Sijaelewa your point hapa

Go through Apple patents.
Patents hazimaanishi uvumbuzi tu,patents zinaweza kuwa hata designs. Ungetaja uvumbuzi wao ingekuwa la maana sana. Kampuni moja inaweza ikawa na patents hata laki 1.


Sio Nokia tu, Apple analipa na wengine, ndio ujue kuwa katika uwanja wa technology kuna kutegemeana. Kama zilivo simu zako za Nokia zenye android, wananunua snapdragon kwa Qualcomm, wangetengeza zao basi.
Ndio kuna kutegemeana ila wengine ni wategemezi zaidi. Na usifananishe kununua kifaa kama soc kwa kampuni nyengine na kudakwa wizi na kulazimishwa umlipe uliemuibia.

Apple alidakwa anaiba technologya nyingi za Nokia ikiwemo touch screen user interface na related technologies ndio maana Nokia analipwa kwa kila iphone inayotengenezwa.

Na Apple hajamlipa Nokia matrilioni mara moja,do your homework.


Unapokandia operating systems ambazo kila siku unaendelea kuzicopy its so fun. Kama ni ourdated, hazifai, etc kwanini kila siku mpo busy kucopy feature zake na kuweka kwenye version mpya za os zenu?


Nokia android kama kawaida, haina ishu.
Just to be clear Nokia hatengenezi simu za android bali HMD ndio anatengeneza simu za nokia za android na sidhani kama anahusika hapa.



Miaka yote hiyo wakati mauzo yanaongezeka hazikuwa ghali? Sasa hivi yamepungua zimekuwa ghali? Na kwanini miaka yote mauzo ua feature phone yasiongezeke? Mpaka hizo factor mbili zilipotokea?
 
Nyie hamkuiga top notch? Unaongea as if iphone x ndio simu ya kwanza kuwa na notch

Jiulize Simu gani ilikuwa na notch before Iphone ? Na hiyo notch ilifanya kazi gani

Then jiulize ni simu ngapi zina notch baada ya iPhone [emoji23]. Watu wameiga lakini bado hawajaweza kuweka features kama zilivyo kwenye notch ya iPhone. Same applies to fingerprints Apple wakitoa soko zima lina respond na watu wana copy

Tukisema Apple wako serious muwe mnatuelewa.
 

Mkuu nikujibu Kwa screenshot hapo chini .. Umewaelewa Apple sasa , kampuni ya tech yenye customers care kuliko kampuni yoyote duniani
 
Notch zinatengenezwa na kampuni za display, zamani ilikuwa haiwezekani kuwa na notch sababu ilikuwa technology hairuhusu ila baada ya technology kuwa kubwa zaidi sasa hivi inawezekana.

Kampuni ya kwanza kutengeneza notch ni sharp, kwenye simu zao za series za aquos. Wote tunaijua sharp ni kampuni kubwa ya display.

Aquos za mwanzo walitoa kabisa camera pale juu zikawa na bezel chini tu, na camera pia wakaieka chini hii design watu hawakuipenda.


Then kutokea hio design wakaja na water drop notch na notch za kawaida pia.




Baada ya sharp wa pili kutoa notch ni essential Simu iliyokuwa designed na Andy Rubin mwanzilishi wa Android.

Iphone ikawa simu ya tatu kuwa na notch.

Watu wanaicopy iphone kwenye notch? Ndio wanacopy hilo sikatai ila vile vile na yeye sio muanzilishi amecopy kwa waliomtangulia.
 

Vizuri sana , umeleta Simu mbili tu zilizokuwa na notch na notch zao hazikuwa na kazi za uhakika, Apple kaiweka notch kai revolutionize kaifanya notch kuwa na maana then simu kibao ndo tunaona zinatoka na notch na bado hazijawa na features kama IPhone X .. Kwa hapa tukubali tukatae hamna notch bora na yenye maana kama notch ya IPhone kwa maana ya functionality.
 
Hivi ukiambiwa utaje simu tano zenye camera nzuri duniani hata Hao Apple(iphone) wanaingia?

Nani unamuamini kwenye rating za camera za simu tukaangalie rank zikoje!

Nakuhakikishia IPhone haikosi top three kama siyo kuwa wa kwanza . Upande wa HDR hauna mashaka ndo wa kwanza hamna mtu wa kukohoa..
 
Nani unamuamini kwenye rating za camera za simu tukaangalie rank zikoje!

Nakuhakikishia IPhone haikosi top three kama siyo kuwa wa kwanza . Upande wa HDR hauna mashaka ndo wa kwanza hamna mtu wa kukohoa..
Una camera ya kuipita
-Huawei p10 pro
-mate 20 pro ?

I wonder even kama unaipita pixel 3.

Na rank ni utoto huo, halafu fans wa Apple mnapenda kweli kurank vitu kwa maksi.

Ukicompare camera inabidi uangalie aspect zote kuanzia stabilization, sensor iliotumika, low light perfomance, aperture, software,HDR, raw, etc kuna mambo mengi sana.

Kabla ya kuingia Deep una camera ya kuzipita hizo simu mbili? Kama hauna tuanze kutafuta best of the rest.
 
So tunaongelea ubora au nani kaanza? Excuse zenu ni hizo hizo,kwamba anaboresha,

Yaani mtu aanzishe kitu uige halafu unasema changu ni bora? Kuiga na kuimprove kitu kunaondoa fact kwamba umeiga?
 

Mkuu sasa nana unaleta utoto kwenye issue serious , unasema ranking ni utoto? Kwa mtu wa tech anasema ranking ni utoto? Unajua ranking maana yake na inafanyikaje?

Anyway Mimi sikutaka ranking , we ndo ulitaka ranking baada ya Apple ku solve issue ya beautygate na chargegate ambayo mlikuja hapa na kelele kibao na nikawaambia Apple wanajua wanapoenda na sasa wamei solve mnatafuta pa kukimbilia

Again hata hao wanaofanya ranking wanaangalia vitu Vyote hivyo then wanatoa score Kwa kujumlisha kila feature ya camera. Sasa wewe ranking unadhani inafanyikaje...pitia pitia jisomee uone ranking inakujaje, ranking haiji tu kisa mtu kasema au kapenda , camera zinafanyiwa testing ya kila kitu

Attachment nimekupa tumalize ubishi kama unaendelea kubisha basi endelea



Na hapa jisomee jinsi score zinavyopatikana siyo unakuja kudanganya watu eti wasiamini ranking za marks, marks zinakuja Kwa vigezo haziandikwi andikwi zile.

View attachment 909840
 
Huwa sikubaliani na dxomark kwenye simu wapo biased na kibiashara zaidi, ili wakurank kwenye database zao inabidi ufanye optimisation ya software yao kitu ambacho ni ujinga. Camera output yake kila mtu anaweza kuona kwa macho yake sio kitu ambacho unahitaji eti namba fulani kuonyesha hii ni nzuri kushinda hii.

Nikuulize wewe unaewatetea hizo score zinawakilisha nini? Low light perfomance? Ois? Zoom?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…