Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Kwanini si muumini wa Serikali Tatu...

Mchambuzi; Sasa ndugu yangu Mchambuzi; serikali tatu inatokana na ukweli kuwa tunataka kurudisha nchi ya Tanganyika. Sasa sina tatizo na kurudishwa kwa Tanganyika lakini ukiirudisha Tanganyika kama nchi NI LAZIMA uwaulize wananchi waka kama Wanataka Muungano na Zanzibar! Huwezi kurudisha nchi ya Tanganyika halafu uwasukumize kwenye Muungano na nchi nyingine ... Zanzibar.

Sasa ili tuzungumzie 'serikali tatu' ni lazima tuamuze kama Zanzibar itaendelea kuwa nchi baada ya shirikisho au la; kama watakuwa tayari kufuta hiyo ibara waliyoibadilisha 2010 ili wasema kuwa wao ni "sehemu" ya Jamhuri ya Muungano. Unafikiri Wazanzibari watakubali? Au Watanganyika tukubali kusema sisi ni "sehemu" ya Jamhuri ya Muungano bila kujitaja kuwa na "sisi" ni nchi?
Mkuu MMM, nimesoma bandiko lako na umejenga hoja nzito.
Niseme kuwa kurejea kwa Tanganyika si kwasababu Zanzibar ipo, la hasha!
Ni miongo takribani minne tangu Tanzania izaliwe rasmi na Tanganyika kutoweka.
Hadi hivi sasa wazanzibar wanaamini kuwa Watanganyika hawashughulishwi na suala la muungano kama wao.Kinachowasukumu kusema hivyo si kwasababu ya ukweli bali ukweli kuwa Tanganyika imeridhika kutoa ili kujenga muungano wa nchi moja yenye kanchi ndani yake kama ilivyo sasa

Matokeo ya ridhaa ya Watanganyika yanapokelewa na wazanzibar ambao basically wanaserikali yao kwa mitazamo mbali mbali.

1. Tanganyika kupitia Tanzania inawanyonya bila chembe ya ukweli na pengine ni kinyume chake
2. Matatizo ya kiuchumi na kijamii ya Zanzibar kutwishwa Mtanganyika
3. Kuitumia Tanganyika katika kupunguza gharama za shughuli zao kwa hisa za 'Tanzania''
4. Kuleta ubaguzi kwa Watanganyika wakati wakuitumia Tanzania kuzuia backfire ya ubaguzi.
5. Kujitambua kama Zanzibar na kuiacha Tanzania isipokuwa katika mafao na fursa

Kwa msingi huo Watanganyika bado wanaamini katika spirit ya muungano ambayo imevunjwa nguvu na Wazanzibar. Ili kuondokana na mambo 5 hapo juu Watanganyika wanajiuliza, katika Tanzania tuliyo nayo wapi mshirika wenzetu?

Kwamba neno Tanzania linatumika katika hisa tu bila kuwa na mafao ya aina yoyote.
Ndipo wanasema ni vema kukawa na mipaka ya mambo ili kila mmoja aangalie ustawi wake bila kumtwisha, kumlaumu au kumsimanga mwingine.Kwamba Tanganyika imetoa lakini 'dividend' ni matusi, kejeli, lawama na dharau. Kuna sababu za kuendelea na hali hiyo?
Hoja ya kurudi Tanganyika inapata nguvu kwa sababu hizo.

Ama hapo chini umeeleza vema sana ya kuwa kama tunahitaji shirikisho basi lazima washiriki wawepo. Kwa bahati mbaya Tanganyika haijarudi rasmi ili kusimamia masilahi yake.
Tumeiuliza tume ya Warioba, hiyo serikali ya muungano imepatikanaje?
Haiwezekana SMZ ikawakilishwa na Tanganyika ikawa ''ghost'' lakini ikatupiwa sheria zinazoihusu.

Leo serikali ya Tanganyika na nchi yake ikirudi itakuta sheria zilizoandikwa na akina Warioba tena wakiwemo Wazanzibar. Wazanzibar wakiandika sheria zao hakuna Mtanganyika aliyeshiriki.
Kwanini basi asirejee Mtanganyika ili naye aamue kama kuna umuhimu wa kushirikiana na znz kwa jambo lolote lile?
Hapa ndipo hoja yetu ya kurudi Tanganyika inapokuwa na nguvu sana.

Tunasikia wazanzibar wakisema wanataka abcd katika rasimu na wala si kura ya maoni. Hii maana yake ni kuwa katika mchakato wa sasa wao wana 'dictate terms za shirikisho''. Sababu za ku-dictate ni kuwa wanafanya debate against 'vacuum'.

Wzn wantaka ulinzi na usalama, sasa nani anyejua kuwa hilo ni hiytaji la Tanganyika?
Je, kama Tanganyika ikirejea ikasema haihitaji hilo hatuoni kama ni kuleta utata siku za usoni?
Hoja ya kurudi Tanganyika inabaki na nguvu zake

Kuhusu Zanzibar kukubali kuwa sehemu ya shirikisho, kwa vile hawakukubali kuwa sehemu ya Tanzania hilo ni wazi hawatakubali kuwa sehemu ya shirikisho. Si wajibu wetu kuwaambia au kuwashawishi, ni wajibu wetu kuwapa 'terms of reference' za hilo shirikisho.

1. Wakubali kuwa wao kama Tanganyika watapoteza 'utaifa' na kuupata kupitia shrikikisho.
2. Kwamba, hakuna kujadili nini kiwemo ndani ya rasimu kwanza bila kujua shirikisho ni la namna gani
3. Waamue kwa kufuata kura ya maoni kama wanapenda shirikisho au hapana.
Hata Nyerere alishawahi kusema kama hawataki hatawapiga mabomu.

Ili mambo yote yaende samba mba kura ya maoni iziangatie mambo haya
1. Kuwauliza Watanganyika kama kuna umuhimu wa muungano na baada ya Tanganyika kurudi
2. Kuwauliza wazanzibar kama wapo tayari kuwa sehemu ya muungano na kupoteza huo unaoitwa 'utaifa''

Matokeo ya hapana kwa yoyote maana yake ni kuwa tuvunje jahazi kila mtu kivyake.

Kwa msingi huo kurudi kwa Tanganyika ni kutoa nafasi ya kujitathmini kama kuna umuhimu wa muungano baada ya kupanga taratibu zake. Ni kutoa fursa kwa zanzibar kujitathmini utayari wa muungano

Tusiogope kurudi kwa Tanganyika kwa hofu ya kuvunjika muungano. Tanganyika haiwezi kubeba muungano yenyewe. Kama uwepo wake utamaanisha kifo cha muungano hilo ni jema zaidi kuliko kuishi kwa matumaini ya seikali moja taifa moja ambayo ni ndoto, serikali mbili ambazo zimeshindwa.

In other words, plan A na B zimeshindikana, ipo moja tu ambayo ni C (serikali 3). Plan C itawezekana baada ya Tanganyika kurudi. Hiyo ikishindikana tunayo plan D ambayo italeta suluhu na amani ya kudumu, vunja muungano kila mtu kivyake.
 
nadhan tungeanza na kura ya maoni kama kweli muungano unahitajika au la.... maana chuki za wazanzibari dhidi ya watanganyika and vice-versa ni kubwa sana sasa kuna haja gani ya kulazimishana.... kibaya zaid kila upande unaona unawafaidisha upande wa pili isivyo halali!!!
 
Kama kuna mtu anaamini MWANAKIjiji anaamini anachoandika anajidanganya kumjadili MWANAKIjiji haamini anachoandika ila tuu huamini watu wanachokielewa. Na kuhusu muungano sidhani kama kuwa na serikali tatu ni suluhu, Ukisikia viongozi wengi na wapiga chepuo la serikali tatu wana ajenda moja moyoni nayo ni devide and rule mfano. Nanukuu Yaani wazanzibar tunakubali kufanya nchi kuwa kama halmashauri! By mwanasheria Mkuu znz, hofu kuu ni kupoteza mamulaka wala si muungano,
Na style hiyo inapigiwa debe na wapinzani kwa bidii coz zanzibar upinzani una nguvu kuliko ccm bila kuongeza jitihada za ccm bara pia bara upinzani mkuu unauzika zaidi bila kuhusisha znz japokuwa haiathiri chochote kutokana na population ya bara. Sasa Hii hoja ina manufaa gani kwa wananchi wa Zanzibar? Nanukuu tena kuhusu tff kuwakilisha Tanzania ni nongwa Zanzibar ni mwakilishi halali caf je kimefanyika nini tofauti ya maendeleo ya mpira ikilinganishwa na kabla hawajawa wawakilishi? Na hoja hiyo inaumuhimu gani kwa wazanzibar?. Ndio maana wengi wa znz wanautamani muungano ila kwa viongozi kwa nia yao ya kuhodhi madaraka hawataki serikali mbili wala moja wanalazimisha tatu uvivu wa kufikiri na kuamua ni huu. Tunazungukia kuibuka kwa hoja hii ya serikali 3 kwa Mara ya pili sasa Hivi wale wenye mitizamo ya g55 wamekufa wote Tanzania ama kwavile nyerere ndo kafariki na hoja zake kuhusu muungano zote tunazizika naye? Huo ni ufisadi mwingine wa mawazo mazuri ya historia ya viongozi Tanzania. Kama kuna mawazo mazuri ya kuboresha muungano ni kuwa na serikali moja imara inayosimamia misingi ya uongozi na viongozi wanaowajibika kwa wananchi na kuwepo majimbo nchi nzima.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi ,

Umetoa changamoto kubwa lakini nashangazwa jinsi (tena si mara moja) unavyosisitiza kuwa "tusichanganye baina ya dhana ya ‘nchi’ na dhana ya ‘serikali’ tunapojadili mfumo wa utawala ndani ya muungano wa nchini mbili."

Kweli hizi ni dhana mbili tofauti lakini nchi (kwa maana ya jamhuri ya muungano) haiwezi kujadiliwa bila kuangalia mfumo wa serikali utaofanya nchi kuwa moja kama kusudio la awali la muungano.

Kwanini unakwepa ukweli wa muundo wa serikali una nafasi kubwa ya kuamua hatma ya muungano? Msome vizuri Mzee Mwanakijiji anasema, "Sasa kinachorudishwa katika "serikali tatu" ni nchi ya pili! Hairudishwi serikali! Inarudishwa nchi inaitwa Tanganyika halafu hiyo nchi itakuwa na serikali yake "kama" ilivyo Zanzibar! HIvyo, kutakuwa na nchi mbili zinaunda shirikisho! NI kwa sababu hiyo shirikisho siyo nchi moja tena bali ni nchi mbili zenye serikali tatu! Serikali ya Nchi ya Zanzibar (ambayo bado ipo) na serikali ya nchi ya Tanganyika (ambayo itarudishwa) na serikali ya ushirikiano (Shirikisho) ambayo kwa kweli itakuwa na madaraka lakini haitokuwa na eneo au nchi - haijalishi Katiba inasema nini."

Last edited by a moderator:
Napata shida sana ninapoutafakari muungano huu! Kiwepesi kabisa bila kujikita kwenye hoja nzito zilizotolewa hapo juu naamini kabisa nia ya kuuanzisha muungano huu ilikuwa ni kuleta NGUVU na si UDHAIFU!
Umoja ni nguvu utengani ni udhaifu ( ....Muungano ni nguvu utengano ni udhaifu!??....)
Maswali rahisi tu...Muungano huu umetuletea faida zipi (hasa sisi wa huku bara)? Tunaung'ang'ania kwa sababu zipi hasa? Au kuna ajenda za siri ambazo sisi wa kawaida hatuzijui? Wenzetu wanataka kwenda zao sisi tunawang'ang'ania hatimaye pamoja na mengine tunaambulia matusi ya nguoni kutoka kwao.

Nimezaliwa ndani ya Muungano (na "kwa bahati mbaya" sikuikuta Tanganyika...nasikia alikuwa usingizini!), nimesoma mawazo ya wengi hapa na nimejielimisha sana kutoka kwao. Mtazamo wangu wa awali juu ya huu muungano ulikuwa ni serikali moja nchi moja!! Lakini wenzetu hiyo kitu kwao wala sio m'badala! wao wanataka muundo wa serikali tatu na ukifuatilia sababu za kina zilizojadiliwa na wakongwe hapa utaona mwisho wa siku ni sawa na kurefusha njia ya kufikia "kikomo cha muungano"..tumia hata sababu za "pasu kwa pasu" baina ya Tanganyika na Zanzibar kwenye maeneo yote ya serikali ya tatu! Na kwa kutumia maeneo hayo pia utajua ni kwa kiasi gani hawa wenzetu wamekuwa "KUPE" kwa Tanganyika aliyelala na hajaamka since 1964.

Mwl. Nyerere hakusema sisi Tanganyika (...kwanza hata hatupo...) tuung'ang'anie muungano pindi wenzetu watakapokuwa wanataka kwenda zao! Wenzetu wanataka kwenda, na hata leo hii ukiitisha kura ya maoni kule kwao utapata jibu hilo, basi tuwaachie waende zao. Hata mke/mme mliyezaa naye watoto akitaka kwenda zake na wewe ukaendelea kumng'ang'ania kwa hisia tu kwamba anaweza kuja kubadilika unajua madhara yake hapo mbeleni.
Kama nilimuelewa vizuri Mwl. Nyerere, ni kwa sisi Watanganyika "watarajiwa" kuwa wamoja! Kumbuka kwa sasa sisi ni Watanzania wao ni Wanzanzibar Watanzania!!?

Serikali tatu ni "kurefusha tu njia ya kupeana talaka", Serikali mbili ni kuendeleza dhana ya "UMOJA NI UDHAIFU UTENGANO NI NGUVU" uliopo hivi sasa, Serikali moja ingekuwa suluhisho japo ndio hivyo kwa wenzetu shubiri na katu hawawezi kukubali bila mabavu. Sasa ya nini kuzitaka serikali tatu na tunajua mwisho wa siku tunarudi kwenye hii "kila "mtu na chake?

Gharama zoote za sherehe zilizowahi kufanywa za muungano, zoote tulizoingia kuuendesha huu muungano, zote zote kabisa! na hizi tunazotaka tena kuziingia za serikali ya tatu, Mzee Mwanakijiji, hatungeweza kusaidia angalau elimu yetu ikainuka? Sasa ya nini tunasita kumuamsha Tanganyika? Aje atutetee! Kwa nini tunataka kuahirisha tena kwa kupitia kwa serikali tatu? Tumuamshe Tanganyika ajikute yuko mwenyewe na sio amkute yule aliyempa sindano ya usingizi..japo nia ilikuwa ya kujenga.

Naungana na mmoja humu aliyesema kuwa KURA YA MAONI ingefanywa, tena mapemaa! na najua hata Watanzania wa Tanzania watakuwa wamechoka na hawa Watanzania wa Zanzibar na kuwaachia waende zao.

Au Mzee Mwanakijiji pengine sisi kizazi kipya kuna mambo mnayotuficha hatuyajui juu ya huu Muungano!?Tuelimisheni tafadhali. Kuna la ziada la "Muungano" kiuchumi? au ni hizi faida za kisiasa na kijamii tu? Hakuna haja ya kuahirisha mpaka miaka 20 ijayo, watakuja kutulaumu sisi kama tunavyowalaumu ninyi kutumia gharama na hazina zetu kuendesha kitu kisichokuwa na tija kwa Watanzania wa Tanzania!!

Tuamue leo kwani hatuna akili za kutosha kufanya maamuzi sahihi kuliko kusubiri labda atatokea Mwokozi? Haya haya ya kutojiamini na kusubiri subiri mpaka kesho ndio yametapakaa mpaka kwenye sectors nyingine na hakuna big results za kujivunia kwenye karibu kila eneo...hata ile amani yetu tuliyojivunia inaanza kuharibika na chimbuko bila shaka ni kutokea kwa wenzetu huko!!

Natamani kuiona Tanganyika!
 
Mzee Mwanakijiji, Kobello, MTAZAMO

Tutajadili sana juu ya structure nzuri ya muungano lakini haitakuwa na maana iwapo tutasahau kwamba - kitovu cha kero za muungano ni ukosefu wa demokrasia, na moja ya kanuni za msingi kabisa za demokrasia ni – ‘the right of people to self determination’. Haki hii imekosekana kwa pande zote mbili za muungano, kufuatia uchakachuaji wa mkataba wa muungano kama nilivyokwisha jadili elsewhere:

· Ujio wa katiba ya muda (1965-1977).
· Kufutwa kwa utambulisho wa Tanganyika kama nchi kupitia sheria namba 22 ya mwaka 1967, na badala yake kuanzishwa kwa utambulisho wa ‘Tanzania bara’ kama nchi.
· Kufutwa kwa utambulisho wa Zanzibar kama nchi kupitia katiba ya JMT (1977) na badala yake kuanzishwa kwa utambulisho wa ‘Tanzania Visiwani’ kama nchi.

Mwanzoni, problems of democracy (hence call for right of people to self determination) found their concentrated expression in Zanzibar, na wazanzibari wakafanya bidii na kujipatia katiba yao ya kwanza mwaka 1979, ambayo ilifanyiwa marekebisho muhimu kama vile ‘bill of rights’ nk, 1984. Pia wazanzibari walifanikiwa kurudisha utambulisho wa nchi yao ya Zanzibar, kwani mapinduzi ya kumng’oa sultani yalifanikishwa na Zanzibar, sio Tanzania visiwani. Na ni majuzi tu wamejipatia katiba yao ya kuwapeleka towards ‘self determination’, huku watanganyika wakiwa bado wanahaha kufanikisha hilo kwa upande wao. Ndio maana awali nilijadili kwamba tunapojadili suala la muungano, ‘tusifanye mzaha na cultural and historical national identities’.

Kumbukeni kwamba yote haya yanaungwa mkono na maneno yafuatayo ya Mwalimu Nyerere (1964) kwamba:

“Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo.”

Mwalimu Nyerere alikuwa ni mtu wa kujichanganya kidogo kuhusiana na mfumo wa muungano, na niliwahi jadili hili elsewhere sababu zilifanya awe hivyo.

Vinginevyo, muungano wowote ule hauwezi kufanikiwa iwapo hautatoa kwa pande zote za muungano ‘the right of people to self determination’. That’s the bottom line.

Issa Shivji katika moja ya makala zake anajadili kwamba:

No kind of union, whatever its form, between states can function unless the following conditions are satisfied:

1. That there is a clear demarcation of jurisdiction or powers of the constituent parts.
2. That all sides try their best to respect this demarcation without trying to usurp each other’s powers or encroach on each other’s sphere of control.
3. That there is a standing machinery in the form of courts (either regular or special) to resolve difference of opinion and or allegations of encroachment; And
4. That the governments and individuals of the constituent parts are willing, and as a matter of practice, try to resolve their jurisdictional disputes through the courts.

Nadhani mtakubaliana nami kwamba kwa miaka karibia hamsini ya muungano, none of the above has been satisfied. Narudia tena swali kwenu wakuu:

· Iwapo hali imekuwa hivyo kwa miaka karibia hamsini chini ya serikali mbili, je serikali moja itatatua vipi kero zilizopo?

Bado hamjaja na jibu kwa swali langu.
Mzee Mwanakijiji, kuhusu suala la Tanganyika, kwanza niseme tu kwamba jina “TANGANYIKA” ni haki kwa wananchi, haki waliyonyang’anywa na bunge la TANU miaka sita tu baada ya uhuru wa Tanganyika. Je, ungependa tuanze kujadili Tanganyika kama nchi au kama serikali?

· Iwapo utaamua tuanze kuijadili kama nchi, Tanganyika kama ‘nchi’ ilikufa rasmi kupitia sheria namba 22 ya mwaka 1967 na badala yake nchi ya ‘Tanzania Bara’ ikazaliwa rasmi. Hata iwe kwa dhamira ipi, bunge halikuwa na nguvu ya kisheria kubadilisha jina la nchi ‘Tanganyika’ kuwa nchi ‘Tanzania bara’. Nchi ya Tanganyika ilikombolewa na Umma kupitia Tanganyika African National Union (TANU), 1961. Sasa chama hiki kilipata wapi madaraka ya kubadilisha jina na utambulisho wa Tanganyika? Je chama kiliwahi kuwauliza wananchi au wanachama wake iwapo wanataka utambulisho wao uondolewe? Kwanini ghafla iwe muhimu wananchi waulizwe iwapo wanataka haki hiyo irudishwe?

· Iwapo utaamua tuanze kwa kujadili Tanganyika kama serikali, tofauti na nchi ‘tanganyika’, serikali ‘Tanganyika’ imekuwepo kwa kipindi chote cha muungano lakini imekuwa ikifichwa na kofia ya rais wa muungano. Sidhani kama kuna haja ya kujadili kwa kina suala hili kwani nimeshalijadili kwa kina. Vinginevyo, suala la mamlaka ya rais wa JMT kwa serikali ya Tanganyika lilikubaliwa liwe ni suala (kupitia mkataba wa muungano1964) lakini cha ajabu ni kwamba, badala ya serikali hii kupewa mamlaka yake kama mkataba ulivyodhamiria, sambamba na Zanzibar, upande wa Tanganyika ukachakachuliwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba mfumo wa shirikisho umekuwa ukionekana ndio mfumo bora katika post – conflict environments – kwa mfano Bosnia, DRC, Iraq, Sudan, South Africa, na mfumo huu upo under consideration katika nchi zenye machafuko za Sri Lanka, Nepal n.k. Conflict za muungano wetu ni suala la kujtakia tu, na ni suala ‘imminent’; Sasa iwapo solution kwa wenzetu hao juu imekuwa ni kufuata mfumo wa shirikisho, kwanini na sisi tusiepuke machafuko mapema kwa kukataa serikali mbili au moja (zote hizi ni unitary), mfumo ambao umezaa migogoro kuliko mafanikio kwa miaka 50? Muungano unaofuata Unitary system ni muungano unstable, undemocratic and inefficient kiuchumi fotauti na muungano unaofuata mfumo wa shirikisho, na nimejadili sana hili elsewhere.

Unitary system katika muktadha wetu inajadilika nje ya muungano tu, sio ndani ya muungano. Lakini kusema ‘inajadilika’ haina maana kwamba ‘inakubalika’ kwani kwa ‘size’ ya nchi yetu in terms of land mass and population (plus its distribution), federation in Tanganyika (hata nje ya muungano), utakuwa ni ni mfumo efficient kisiasa, kiuchumi na kijamii – na hapa, sina maana kwamba serikali zaidi ya moja is synonymous to rais zaidi ya mmoja. Ni kwa dhana hii, nimekuwa nikiunga mkono hoja ya Samuel Sitta kwamba shirikisho ni suluhisho lakini shirikisho lenye Rais mmoja;

If we aim to sustain a working democracy in our union, federalism is the best way forward!

Cc Nguruvi3, joka kuu, Jasusi, JingalaFalsafa
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi, tunajuaje kama Watanganyika au Wazanzibari wanataka Muungano? lakini tunajuaje pia kuwa wapo watu wanataka nchi ya Tanganyika irudi?
 
Mkuu MMM, nimesoma bandiko lako na umejenga hoja nzito.
Niseme kuwa kurejea kwa Tanganyika si kwasababu Zanzibar ipo, la hasha!
Ni miongo takribani minne tangu Tanzania izaliwe rasmi na Tanganyika kutoweka.
Hadi hivi sasa wazanzibar wanaamini kuwa Watanganyika hawashughulishwi na suala la muungano kama wao.Kinachowasukumu kusema hivyo si kwasababu ya ukweli bali ukweli kuwa Tanganyika imeridhika kutoa ili kujenga muungano wa nchi moja yenye kanchi ndani yake kama ilivyo sasa

Matokeo ya ridhaa ya Watanganyika yanapokelewa na wazanzibar ambao basically wanaserikali yao kwa mitazamo mbali mbali.

1. Tanganyika kupitia Tanzania inawanyonya bila chembe ya ukweli na pengine ni kinyume chake
2. Matatizo ya kiuchumi na kijamii ya Zanzibar kutwishwa Mtanganyika
3. Kuitumia Tanganyika katika kupunguza gharama za shughuli zao kwa hisa za 'Tanzania''
4. Kuleta ubaguzi kwa Watanganyika wakati wakuitumia Tanzania kuzuia backfire ya ubaguzi.
5. Kujitambua kama Zanzibar na kuiacha Tanzania isipokuwa katika mafao na fursa

Kwa msingi huo Watanganyika bado wanaamini katika spirit ya muungano ambayo imevunjwa nguvu na Wazanzibar. Ili kuondokana na mambo 5 hapo juu Watanganyika wanajiuliza, katika Tanzania tuliyo nayo wapi mshirika wenzetu?

Kwamba neno Tanzania linatumika katika hisa tu bila kuwa na mafao ya aina yoyote.
Ndipo wanasema ni vema kukawa na mipaka ya mambo ili kila mmoja aangalie ustawi wake bila kumtwisha, kumlaumu au kumsimanga mwingine.Kwamba Tanganyika imetoa lakini 'dividend' ni matusi, kejeli, lawama na dharau. Kuna sababu za kuendelea na hali hiyo?
Hoja ya kurudi Tanganyika inapata nguvu kwa sababu hizo.

Ama hapo chini umeeleza vema sana ya kuwa kama tunahitaji shirikisho basi lazima washiriki wawepo. Kwa bahati mbaya Tanganyika haijarudi rasmi ili kusimamia masilahi yake.
Tumeiuliza tume ya Warioba, hiyo serikali ya muungano imepatikanaje?
Haiwezekana SMZ ikawakilishwa na Tanganyika ikawa ''ghost'' lakini ikatupiwa sheria zinazoihusu.

Leo serikali ya Tanganyika na nchi yake ikirudi itakuta sheria zilizoandikwa na akina Warioba tena wakiwemo Wazanzibar. Wazanzibar wakiandika sheria zao hakuna Mtanganyika aliyeshiriki.
Kwanini basi asirejee Mtanganyika ili naye aamue kama kuna umuhimu wa kushirikiana na znz kwa jambo lolote lile?
Hapa ndipo hoja yetu ya kurudi Tanganyika inapokuwa na nguvu sana.

Tunasikia wazanzibar wakisema wanataka abcd katika rasimu na wala si kura ya maoni. Hii maana yake ni kuwa katika mchakato wa sasa wao wana 'dictate terms za shirikisho''. Sababu za ku-dictate ni kuwa wanafanya debate against 'vacuum'.

Wzn wantaka ulinzi na usalama, sasa nani anyejua kuwa hilo ni hiytaji la Tanganyika?
Je, kama Tanganyika ikirejea ikasema haihitaji hilo hatuoni kama ni kuleta utata siku za usoni?
Hoja ya kurudi Tanganyika inabaki na nguvu zake

Kuhusu Zanzibar kukubali kuwa sehemu ya shirikisho, kwa vile hawakukubali kuwa sehemu ya Tanzania hilo ni wazi hawatakubali kuwa sehemu ya shirikisho. Si wajibu wetu kuwaambia au kuwashawishi, ni wajibu wetu kuwapa 'terms of reference' za hilo shirikisho.

1. Wakubali kuwa wao kama Tanganyika watapoteza 'utaifa' na kuupata kupitia shrikikisho.
2. Kwamba, hakuna kujadili nini kiwemo ndani ya rasimu kwanza bila kujua shirikisho ni la namna gani
3. Waamue kwa kufuata kura ya maoni kama wanapenda shirikisho au hapana.
Hata Nyerere alishawahi kusema kama hawataki hatawapiga mabomu.

Ili mambo yote yaende samba mba kura ya maoni iziangatie mambo haya
1. Kuwauliza Watanganyika kama kuna umuhimu wa muungano na baada ya Tanganyika kurudi
2. Kuwauliza wazanzibar kama wapo tayari kuwa sehemu ya muungano na kupoteza huo unaoitwa 'utaifa''

Matokeo ya hapana kwa yoyote maana yake ni kuwa tuvunje jahazi kila mtu kivyake.

Kwa msingi huo kurudi kwa Tanganyika ni kutoa nafasi ya kujitathmini kama kuna umuhimu wa muungano baada ya kupanga taratibu zake. Ni kutoa fursa kwa zanzibar kujitathmini utayari wa muungano

Tusiogope kurudi kwa Tanganyika kwa hofu ya kuvunjika muungano. Tanganyika haiwezi kubeba muungano yenyewe. Kama uwepo wake utamaanisha kifo cha muungano hilo ni jema zaidi kuliko kuishi kwa matumaini ya seikali moja taifa moja ambayo ni ndoto, serikali mbili ambazo zimeshindwa.

In other words, plan A na B zimeshindikana, ipo moja tu ambayo ni C (serikali 3). Plan C itawezekana baada ya Tanganyika kurudi. Hiyo ikishindikana tunayo plan D ambayo italeta suluhu na amani ya kudumu, vunja muungano kila mtu kivyake.
Mkurugenzi wa haki za binadamu,habari uenezi na mawasiliano ya umma CUF Mh,Salim Bimani wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara.
Akizungumzia kuhusu suala la kuyadai mamlaka kamili ya Zanzibar Bwana Bimani ameleza kuwa kwa wakati huu wazanzibar wenye mshikamano mkubwa wa kudai nchi yao wapo tayari kwa lolote lile na watahakikisha kuwa watapambana kwa njia ya amani na yoyote yule ambae haitakii mema Zanzibar mpaka pale watakapoyapata mamlaka kamili ya nchi yao
 
Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu. Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu - hili ni jambo dogo zaidi lakini tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!

Mimi napinga serikali tatu - naamini kama kweli watu wanataka tuimarishe Muungano basi ni kuunda nchi moja, serikali moja mifumo mbalimbali au utengano! Kwani nani kasema ni lazima tuungane? Hatutakuwa nchi ya kwanza duniani kuvunjika na watu kuendelea kuishi pamoja na ujirani mwema.
Pamoja na nia njema ya kuuenzi muungano , naona argument ya MMKJJ falls short of the actual facts on the ground.
Watetezi wakuu wa muungano wanatakiwa kuwa CCM.
Sasa Wazanzibari walipokuwa wanavuruga muungano kwa kujiimarisha kiutawala "ndani ya muungano" maana yake nini haswa katika kuuenzi muungano.
Pili, wazanzibari, hadi Rais wa wakati huo, Amani Karume, walijionyesha wazi wazi kutoukubali muungano, hisia zilizoeleweka vema na Watanganyika.
Sasa Watanganyika wameamka, na wanataka serikali yao, na kuonyesha kuchoka kuwabeba beba hawa ndugu zetu, kosa ni la nani?

Na katika muda huo, watetezi wa muungano walikuwa wapi?
 
Sasa Watanganyika wameamka, na wanataka serikali yao, na kuonyesha kuchoka kuwabeba beba hawa ndugu zetu, kosa ni la nani?

Na katika muda huo, watetezi wa muungano walikuwa wapi?

una uhakika wanataka serikali yao? au wanataka nchi yao? kwenye nchi sasa na serikali ya sasa wao wamekosa nini hasa ambacho watakipata ikija Tanganyika?
 
Mchambuzi, tunajuaje kama Watanganyika au Wazanzibari wanataka Muungano? lakini tunajuaje pia kuwa wapo watu wanataka nchi ya Tanganyika irudi?
una uhakika wanataka serikali yao? au wanataka nchi yao? kwenye nchi sasa na serikali ya sasa wao wamekosa nini hasa ambacho watakipata ikija Tanganyika?
MMM, hakika hakuna mwenye kujua ndio maana tunasema waulizwe kama muungano bado una umuhimu kwao. Waulizwe kwa kura ya maoni kwasababu ndio utaratibu unaotumika sehemu nyingi duniani. Timor, South Sudan, Eritrea n.k. waliulizwa wakasema hapana. Lakini pia Puerto Rico japo hakukuwa na muungano nao walipewa fursa ya kuamua kama wanapenda kuwa sehemu ya taifa kubwa, waksema ndiyo. Kura ya maoni ndiyo itatupa ukweli.

Tunajuaje kama wapo Watanganyika wanataka nchi yao irudi hilo ni suala linaloonekana kwa mantiki.
Hakuna anayeweza kuomba DNA test ya mama yake. Tanganyika ilikuwepo na ipo lakini ikiwa imefunikwa na jina Tanzania. Leo zanzibar wanaodai mamlaka a.k.a kuvunja muungano kama wangekaza buti wakondoka definite itabaki Tanzania bara ambayo ni Tanganyika. Kutaka kuomba maoni ya Watanganyika ili nchi yao irudi ni sawa na kuomba ''maternal test''.

Tanganyika haijakosa kitu ambacho wanaweza kukipata ikirudi. Muhimu wanapoteza sana kwa kutokuwepo kwake. Leo tunaongelea muungano, rasimu ikiwa na maoni ya wazanzibar juu ya shirikisho, nani anasimama kwa masilahi ya Tanganyika? Leo Tanganyika inabeba muungano kwa gharama kubwa zenye ujira wa matusi, kashfa na kejeli, je ni kwa kitu gani ambacho itapoteza kama ikirudi na kujiepusha na matatizo ?
Na ni uyatima unaohusu nini hadi Zanzibar wawe na upper hand katika ku-dictate terms za muungano zinazowahusu Watanganyika? Kwa hali iliyopo sasa Tanzania bara a.k.a Tanganyika inatetewa na nani kiasi cha kuamini kuwa ni muhimu kuendelea kubeba muungano yenyewe? Ni kwa masilahi gani hasa ambayo yanaisukuma Tanganyika ichukue gharama ili hali inahitaji resources zake kwa watu wake?
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, in reference to post #107:

Mchambuzi, tunajuaje kama Watanganyika au Wazanzibari wanataka Muungano?

Sote hatujui, lakini njia pekee ya kupata jibu ni ‘a referendum'. Lakini kabla ya referendum kuitishwa, ni lazima serikali za washiriki wa muungano – Tanganyika na Zanzibar zitambulike kwanza kwa mujibu wa Katiba zao. Ndio maana tumekuwa tunajenga hoja kwamba mchakato wa katiba mpya upo ‘flawed' kwani ulitakiwa kwanza utanguliwe na mchakato wa katiba ya Tanganyika. Vinginevyo ni dhahiri kwamba wananchi wengi hawana tatizo na uwepo wa muungano, kinachoendelea ni manung'uniko ambayo kiini chake ni mfumo mbovu wa muungano. In this light, naweza argue kwamba – iwapo kura ya maoni itaitishwa baada ya kurejeshwa kwa Tanganyika, ni dhahiri kwamba majority (no matter how small) watapendelea muungano uendelee. Kitachofuata ni mjadala mkali juu ya aina ya muungano.

lakini tunajuaje pia kuwa wapo watu wanataka nchi ya Tanganyika irudi?

Hili ni swali zuri na la msingi sana. Madai haya yamegawanyika katika makundi makuu matatu: Kwanza, wapo watu wanaodai kwanza irudi ‘Serikali ya Tanganyika", na masuala mengine yafuate baadae. Pili, wapo wanaodai kwanza irudi "Nchi ya Tanganyika", na masuala mengine yafuate baadae. Na tatu, wapo wanaodai vyote viwilikwa pamoja – kujerea kwa ‘Tanganyika kama nchi' na ‘Tanganyika kama serikali'. Lakini tatizo lililopo ni kwamba makundi yote haya yanasahau kwamba TANU ilikuwa ‘very clever' mwaka 1967 kwani baada ya kutafakari kwa miaka mitatu (1964-1967) ikabaini kwamba ili kufanikisha azma ya kuizika Tanganyika kama nchi na Tanganyika kama serikali, njia rahisi ikawa ni kwa kuifuta ‘Tanganyika kama nchi' kwanza, kwa kupitia sheria namba 22 ya bunge la TANU, na TANU ikaamini kwamba kazi iliyobakia ya kuipoteza ‘Tanganyika kama Serikali', itakuwa ni kazi rahisi kupitia mfukoni mwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Huko nyuma umehoji kwanini tume ya nyalali ilichukua maoni ya wachache na kupendekeza mfumo wa serikali tatu; nadhani unafahamu kwamba sio tume ya jaji nyalali tu, bali hata tume ya jaji kisanga nayo ilipendekeza mfumo wa serikali tatu; Je ni kwanini? Hii ni kwa sababu, kama anavyojadili mdau mwenzetu JingalaFalsafa, yapo masuala ambayo yanahitaji nguvu ya kura (kwa maana ya kura nyingi) lakini yapo masuala mengine ambayo yahahitaji nguvu ya hoja; Kama nilivyojadili awali, ‘Tanganyika' kama nchi ilifutwa kimakosa, na Tanganyika kama serikali inanyonywa kimakosa kupitia kiini macho cha muungano. Hii ndio sababu kwanini katika suala hili, ‘uzito wa hoja' ni muhimu kuliko ‘uzito wa sanduku la kura ya maoni'.

Ingawa Mwalimu alipinga wazo la serikali moja, lakini baadae alikuwa na mwelekeo huo, hasa kupitia muungano wa vyama vya TANU & ASP (1977), muungano ambao ulizaa CCM, huku chama hiki kikijinyakulia rasmi mamlaka ya juu kabisa ya nchi na kuwa superior hata kwa vyombo vingine kama bunge na mahakama. CCM pia ilijichukulia mamlaka juu ya masuala ya muungano lakini pia masuala yasiyo ya muungano (rejea kuongezeka kwa idai ya masuala ya muungano kila kukicha). Kufuatia hali hii, Katiba ya JMT (1977) ikafanya jaribio la kuifuta Zanzibar kama nchi, ambapo mshirika huyu wa muungano akabatizwa jina jipya la ‘TANZANIA VISIWANI'. Lakini jaribio hii halikufanikiwa kwani miaka miwili tu baadae, Zanzibar ikajipatia katiba yake ya kwanza since revolution (1964), na kujirudishia utambulisho wake wa ‘Zanzibar', na kufutilia mbali utambulisho batili wa TANZANIA VISIWANI, kwani mapinduzi hayakutokea Tanzania visiwani bali Zanzibar. Mkuu Mzee Mwanakijiji: · Kwanini iwe halali kumrudishia mshirika mmoja wa muungano (Zanzibar) utambulisho wake (1979) baada ya kubainika kwamba utambulisho wa TANZANIA VISIWANI ulikuwa ni batili, na isiwe halali kufanya hivyo kwa mshirika mwingine wa muungano (Tanganyika- ukipenda mwite Tanzania bara?

[FONT=&quot [USER=118]Mzee Mwanakijiji[/USER], nadhani unatambua kwamba baina ya Tanganyika na Zanzibar, kufikia tarehe ya muungano, ni Tanganyika pekee ndio ilikuwa na katiba yake iliyopatikana mwaka 1962. Zanzibar haikuwa na katiba yake, kwahiyo busara ikawa kwamba (kwa mujibu wa makubaliano ya muungano,1964), Katiba ya Tanganyika (1962) iazimwe na kufanyiwa marekebisho ili iwe Katiba ya muda ya JMT, huku zanzibar nao wakiendelea kuendesha serikali yao kwa kutumia sheria zilizopo Zanzibar huku mchakato wao wa kujipatia katiba ukiendelea. Cha kushangaza ni kwamba, miaka kumi na nne baada ya muungano (1979), tunaona Zanzibar ikiwa na Katiba yake mpya, huku Tanganyika ikipokonywa haki hii ya msingi, uporaji ambao unaendelea hadi hivi tunavyozungumza. [/FONT]
[FONT=&quot [USER=118]Mzee Mwanakijiji[/USER], ebu tafakari hili kwa kumrudia tena shivji kwamba:

[/FONT]
No kind of union, whatever its form, between states can function unless the following conditions are satisfied:
1. That there is a clear demarcation of jurisdiction or powers of the constituent parts.
2. That all sides try their best to respect this demarcation without trying to usurp each other's powers or encroach on each other's sphere of control.
3. That there is a standing machinery in the form of courts (either regular or special) to resolve difference of opinion and or allegations of encroachment; And 4. That the governments and individuals of the constituent parts are willing, and as a matter of practice, try to resolve their jurisdictional disputes through the courts.

Pia tafakari kwa kumrudia Mwalimu kwamba:

"Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo."

Mkuu Mzee Mwanakijiji,

· Kwanini katiba ya JMT (1977) hiyo hiyo iwe ndio katiba inayosimamia masuala ya Tanganyika (ukipenda Tanzania bara) wakati mshiriki mwingine wa muungano ana katiba inayosimamia masuala yake yasiyo ya muungano?
Ni muhimu tuelewe kwamba kama ilivyo kwa Katiba ya Zanzibar ambayo it owes its legal validity and political legitimacy to the internal historical processes of Zanzibar (to the people of Zanzibar), not to the union constitution, hivyo pia inatakiwa iwe kwa Tanganyika (ukipenda Tanzania bara).
 
Last edited by a moderator:
Serikali iwe moja. Anayetaka kuungana kwa serikali mbili hana nia ya muungano au tatu hautaki Muungano ila analazimika kuungana nje ya utashi wake. Matokeo yake utafika wakati atauvunja tu muungano. Ya nini kusubiri uvunjike baadaye badala ya kuivunja sasa na kuanza kusahihisha athari zake mapema? Serikali 3 ni kufunika kichwa kwa majani huku ------ yakiwa wazi. MMK you are absolutely right. Serikali moja au la! Tuanze mapema.
 
kwanza malechela ndie alikua waziri mkuu wakati wa G55 na akiwa kiongozi wa bunge alikubali hoja ya kurejea kwa Tanganyika.
hii ili mgharimu nafasi yake kama waziri mkuuu..hivo anapo pinga serikali tatu ni kama kigeu kigeu

hoja ya wanao taka serikali mbili iendelee mimi naikubali kwa sharti moja....tanganyika ifufuke..zanzibar ife na badala yake kuwe na serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano.

makao makuu ya muungano yawe zanzibar
kuwe na rais wa Tanganyika na rais wa tanzania ambae siku zote lazima awe mzanzibari

serikali ya Mungano iendeshwe zanzibar ,
wizara zile za serikali ya zanzibar ziwe za Muungano
BANKI KUU YA MUUNGANO IHAMIE ZNZ
MABALOZI WOTE WAHAMIE ZNZ
tANGANYIKA IWE NA WIZARA ZILE ZA AMABZO HAZI HUSU MUUNGANO NA MWISHO WAO NI TANGANYIKA TU
RAIS WA TANGANYIKA ATAKUA HANA MAMLAKA YA KIMATAIFA
KODI ZOTE ZITABAKI KUWA ZA MUUNGANO ISIPO KUWA PAYEEE TU
TANGANYIKA HAWATAKUWEMO EAC WALA UN WALA FIFA..
TANGANYIKA ISWE NA UWEZO WA KUINGIA MIKATABA BILA YA RUHUSA YA SERIKALI YA MUUNGANO KUTOKA ZNZ
YAANI KWA UFUPI TUBADILISHANE UENDESHAJI ZNZ IWE NDIO MUUNGANO NA NYIE MUBAKI NA TANGANYIAK
 
nadhan tungeanza na kura ya maoni kama kweli muungano unahitajika au la.... maana chuki za wazanzibari dhidi ya watanganyika and vice-versa ni kubwa sana sasa kuna haja gani ya kulazimishana.... kibaya zaid kila upande unaona unawafaidisha upande wa pili isivyo halali!!!

you can't force the nature but nature will force ,and place where is no revolution there is evolution .tafuta tokeo la uzao baina ya black africans and arab,uzao baini ya black africans na asians na baina africans na euroepeans .just google jibu utakalo pata utakaa ,uwashawishi afro arabs to join as one nation of blacks africans ,and thats is a foremost problem between that cast in zanz and other blacks of zanz and thats of Tanganyika .anyway napita tuu .
 
Katika mambo yote wadau wamechangia mm nimona kila upande wa muungano unajambo unaona au kuhisi hautendewi sawa. Mfano ZNZ wanalalama sana kwny masuala ya kimataifa na Watanganyika ni kwny 'changu chetu chako chako'

Hivyo basi suluhisho la uhakika kabisa ni kuwa na serikali moja ishuhulikie mambo yote kitaifa pamoja na mambo mengine madogo madogo yafanywe na serikali za majimbo.

Laa kama ZNZ au Watanganyika hawataki tujitenge na kila mtu awe huru kujiamulia mambo yake Full stop
 
Mchambuzi;7176074]Sote hatujui, lakini njia pekee ya kupata jibu ni ‘a referendum'. Lakini kabla ya referendum kuitishwa, ni lazima serikali za washiriki wa muungano – Tanganyika na Zanzibar zitambulike kwanza kwa mujibu wa Katiba zao. Ndio maana tumekuwa tunajenga hoja kwamba mchakato wa katiba mpya upo ‘flawed' kwani ulitakiwa kwanza utanguliwe na mchakato wa katiba ya Tanganyika. Vinginevyo ni dhahiri kwamba wananchi wengi hawana tatizo na uwepo wa muungano, kinachoendelea ni manung'uniko ambayo kiini chake ni mfumo mbovu wa muungano. In this light, naweza argue kwamba – iwapo kura ya maoni itaitishwa baada ya kurejeshwa kwa Tanganyika, ni dhahiri kwamba majority (no matter how small) watapendelea muungano uendelee. Kitachofuata ni mjadala mkali juu ya aina ya muungano
Referendum ndiyo itakayotoa jibu halisi la kujua kama wananchi wanataka muungano/hawataki tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya viongozi wamejivika joho la kuwa wananchi kwa kusema muungano uwepo huku wengine wakisema hawataki na wengine wakitaka mamlaka nusu wanayoita kamili(huwezi kuwa na mamlaka kamili ukiwa na ulinzi wa kuazima)

Hilo linawezekana tu kama serikali na nchi ya Tanganyika vitaondolewa katika muungano.
Na wala sidhani kama kutakuwa na mjadala mkali kwasababu watu wakiamua muungano uendelee basi watakuwa wameridhia makando kando yanayokuja na huo muungano.
Endapo watasema hapana basi mjadala unafungwa hapo hapo tunabaki na ujirani mwema.

Mfano, baada ya rasimu kutoka, zanziabar wamebadili msimamo na kusema iwepo passport ya Tanzania-Tanganyika na Tanzania-Zanzibar. Hii ni baada ya kubaini Tanganyika inarudi na uwezekano wa Tanganyika kusema yaishe unazidi kuongezeka. Katika hali hiyo Zanzibar wamekubali kwa mara ya kwanza kuwa na neno Tanzania ambalo kwao ni najisi hata kulitamka. Kukubali kwao ni ishara kuwa uwepo wa Tanganyika kama mshiriki unabadilisha equation kwa namna yoyote, iwe kuvunja au kuungana.

Mjadala uliopo unaonekana mkali kwasababu tu znz ndio inajiona inahitajika na hivyo ku-dictate terms za muungano.
Kama tukiwaendekeza sisi tutakuwa losers kama ambavyo tumekuwa kwa miaka 50 ya kubeba muungano wenyewe. Tutajifanya Watanzania lakini haiondoi ukweli kuwa ni Watanganyika.
Sasa basi kwanini tusipiganie masilahi yetu bali tukae tunaendekeza masilahi ya watu wengine?

Je tunahitaji muungano kuliko znz wanavyohitaji kiasi cha kuamini kuwa tunaweza ku-sacrifice Tanganyika kwa ajili ya znz? Ni sababu zipi za maana hasa
 
Mkuu Nguruvi3, naomba nitoke nje kidogo ya mada; Kuna mtu mmoja wa idara ya takwimu alikuwa ananieleza juzi kwamba Tanzania inafaidika zaidi na uhusiano wa kiuchumi na visiwa vya comoro kupitia biashara ya mbuzi na n'gombe pekee kuliko uhusiano wa kibiashara na visiwa vya zanzibar; sikupenda kuamini taarifa hii, wewe unaionaje? Kama ni kweli, basi Kwa kweli ndugu wetu wanzanzibari kazi wanayo;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

..Watanganyika tutapata serikali yetu.

..Hiyo itatupa nafasi ya kuwa na chombo kinachotusemea kuhusu masuala ya muungano.

..Wazanzibari wakidai wapewe 21% ya ajira za muungano, basi atakuwepo Mtanganyika atakayeuliza kwanini iwe hivyo.

..sasa hivi Makamu wa Raisi ni Mzanzibari. Ofisi yake ndiyo inashughulika na kero za muungano. Waziri wa nchi mwenye portfolio ya muungano naye anatokea Zanzibar. Sasa unategemea wa-Tanganyika tutatendewa haki hapo??

cc Mzee Mwanakijiji, Mchambuzi
 
Back
Top Bottom