Idadi ya wanaaotaka Tanganyika haina maana, kilicho muhimu ni hoja za wanaotaka Tanganyika kama zina mashiko ukilinganisha na serikali 1 au serikali 2.hawa watu wanaoitaka Tanganika kwa sababu zao binafsi inabidi tujue idadi yao, kwani tayari tushajua watu karibi ishirini elfu walipendekeza serikali tatu kwenye tume ya katiba.vingenevyo watu watakuja na hoja zao wakitumia "watu" "watanzania" kupotosha kama inavyotokea
mringi ahsante.Tata mchango mzuri lakin.. Kwanza mimi ni mwamini wa Serikali moja ua mbili kamailivyo sasa au kuvunjika kwa muungano.
Kwa nini sitaki kusikia kitu kinaitwa serikali tatu?? Sababu kubwa siwezi shabikia kitu ambacho is bond to collapse in NO TIME. Kuwa na serikari tatu sio suluhu ya matatzo ya muungano hata kidogo mimi na fikiri ni kuongeza matatzo. Kwanza kutakua na dhana ya serikal ya Muungano ambayo kwa ilivyo itakua omba omba ikisubiria michango kutoka kwa nchi shirikishi pili itakua haina nguvu yoyote katika maamuzi ya dhidi ya wananchi wake hata ukiangalia vizuri utagundua kuwa rais wa tanzania ukiwa unaomba kura utatoa sera gani?? Rasilimali,Elimu,Miundo mbinu au nini?? Kwa vile mambo ya muungano ni 7 tu..ambayo yote hayana mashiko kwa uendeshaj wa nchi.ie katiba,jeshi,fedha,mambo ya nje,tume ya uchaguz,... Hivyo ni dhairi kwamba hichi chombo kinachotengenezwa ni chombo dhaifu sana ambacho akisusa tu hata kiongoz wa nchi moja shirikish linakufa.na viongozi wa tanzania watakua wakiwa kwa vile hawana chochote zaidi ya jina. Sasa ndugu zangu kwanin tukubaliana kwenye kitu ambacho hakina nguvu ya kutusaidia au kuvunjika kwake ni raisi sana. Itakua mali ya viongozi ugomvi wao inakula kwa tanzania wakati inatakiwa kuwa other way round.inatakiwa kuwe na tanzania ambayo inaweza take control of its destiny sio kuongozwa na nchi shirikishia.
Kwa ilivyo sasa serikali tatu za Jaji Warioba is a time bomb. Sasa ni kheri tukae chin tutengeneze kitu ambacho kitadumu for ages sio kusolve immediate problems,hivyo its either we move towards kuungana vizuri zaidi kwa serikali moja au tubakie na huu mfumo wa sasa tuuboreshe kwenda kwende serikal mmoja au worse case scenario tuuvunje tuunde nchi zetu vizuri. Hizi solution tatu atleast zinaweza dumu hata kwa decade mbili.
Na mwisho naungana na MKK na nguruvi kwamba kabla ya wote lazma wananchi wapige kura. Yote ni maamuzi magumu ambayo yanaitajika kufanywa ili we cut the cost na we move on sio kutuhairishia matatizo kwa serikali tatu.
Haswaaa!Hizi sintofahamu zote zinakuja kwa sababu tulichagua njia isiyo sahihi katika safari yetu ya kuutafuta utaifa na mshikamano ambazo ndiyo nguzo za Muungano.
Kwa sasa tuko katikati ya safari tunashindwa kuamua kama tuendelee na safari au turudi mwanzo.
Ni vigumu sana kurekebisha jambo la kisiasa ambalo mwanzo wake ulifanyika kimakosa. Hiki ndiyo tunachokiona kwa sasa.
Kama Tume ya Jaji Warioba isingekuwa imefungwa na hadidu za rejea kuhusiana na Muungano, basi ninatumaini tungekuwa kwa sasa tunafahamu nini wananchi wanataka kuhusu hili 'dudu' muungano kwa ustawi wa 'mataifa' yao. Kitu cha kushangaza kwa sasa tunasema tunataka serikali tatu wakati hata hiyo serikali ya pili haijulikani muundo wake na hata wananchi wake sijui wanaishi wapi.
Kura ya maoni ndiyo mzizi wa fitina na kuwepo kwanza kwa nchi ya pili ndiyo mwanzo wa usawa katika kutafuta political legitimacy kwenye negotiation table.
Serikali tatu kwenye political environment hii iliyopo ni hukumu ya kuvunja muungano lakini katika gharama kubwa ambayo ingekuwa offset na kura ya maoni.
Nilichojifunza ni kuwa wengi wa wanaopiga kelele kuhusu serikali 1,2 & 3,hawaelewi wanachoongea.Ukiwauliza economic,political na social impacts ya mfumo wa serikali wanaoutaka na mapungufu ya mfumo uliopo,wengi wao wanatoa majibu ya juu juu tena ambayo waliyasikia kwa mtu fulani,wanafuata mkumbo tu.UMAKINI WA HALI YA JUU unahitajika ktk haya masuala.Tusibipu majanga,tukumbuke kuwa 'in ignorance a farmer breaks an egg to prove if an embryo is alive'
Tiba ni moja tuwe serikari moja tu inatosha Mfano kule USA kuna Nchi 52 lakini serikari ni moja tu na haina kero za Muungano wala Wizara za muungano Cha Msingi ni ZNZ atawale Gavana au Waziri Mkuu na Tz bara atawale Gavana kisha Rais awe Mmoja tu na makamu wake wahamie Dodoma hapo kero na gharama kubwa ya kuendesha muungano ghari Duniani itakwisha .kwani Lengo la Nyerere ilikuwa kuanzisha muungano unaokuwa na kujibadilisha kwendana na wakati yaani kutoka Muungano Analogia wa 1964 na Kuwa Muungano Digtal Kama miungano ya kule UK kwa mama Marikia . Serikari tatu ni njia rahisi ya kuvunja Muungano Ndio Maana wale wasiotaka muungano wanataka serikari tatu ili yaje Kama ya kule URUSI chini Yeltsin au hapo sudan tu kuna vioja lukuki .serikari moja Ndio jawabu la kila jema juu ya muungano Ghari kama huu wetu kinyume na hapo ni Zenji wajiandae Kuwa Raia wa Nchi jirani na watalipia Viza na vibali vya kuishi bara huku Umeme na chakula toka Bara vikilipiwa kwa Dola na Uchumi wa Bara kukua kwa kasi ya ajabu kwani pesa toka hazina haina mgao kwenda Zenji itabakia Bara huku viongozi wakichapa kazi bila stress za kero za muungano .kwa kweli ili Haya yasitokee tunahitaji serikari moja tuMkuu wangu Nguruvi3 nimependa sana uliposema hapo juu kuwa, ndani ya serikali 3, mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama! Tafsiri ya wazi hapa ni kuwa ni lazima tufanyiane undava undava tu, na huo ndio ukweli na hakuna namna ya kuukwepa ndani ya serikali 3. Sioni nafasi ya Tanzania endelevu chini ya serikali 3. Sioni namna yoyote ya Usisi na Uwao kutufikisha kokote zaidi kwenye shimo la giza!
Kwa Mazingira na Nyakati(FIKRA) kama zetu, basi hakuna namna ya kuupuuza UMOJA na tukabaki salama! Bado naheshimu mawazo ya nchi moja, serikali moja, taifa moja. Siku zote mtu nguvu ya mtu mweusi ni Umoja!
Kila tunachoota leo chema chini ya serikali 3 au 2, hakiwezi kufikiwa kama hatutakuwa wamoja, na hakuna namna yoyote ya kujihakikishia Umoja chini ya Serikali 3 au 2.
Hii ni Afrika, tusijifananishe na wengine. Kuna namna zetu sahihi na mahususi kwetu za kuendesha mambo yetu!
Mungu wetu anaita sasa!
Tiba ni moja tuwe serikari moja tu inatosha Mfano kule USA kuna Nchi 52 lakini serikari ni moja tu na haina kero za Muungano wala Wizara za muungano Cha Msingi ni ZNZ atawale Gavana au Waziri Mkuu na Tz bara atawale Gavana kisha Rais awe Mmoja tu na makamu wake wahamie Dodoma hapo kero na gharama kubwa ya kuendesha muungano ghari Duniani itakwisha .kwani Lengo la Nyerere ilikuwa kuanzisha muungano unaokuwa na kujibadilisha kwendana na wakati yaani kutoka Muungano Analogia wa 1964 na Kuwa Muungano Digtal Kama miungano ya kule UK kwa mama Marikia . Serikari tatu ni njia rahisi ya kuvunja Muungano Ndio Maana wale wasiotaka muungano wanataka serikari tatu ili yaje Kama ya kule URUSI chini Yeltsin au hapo sudan tu kuna vioja lukuki .serikari moja Ndio jawabu la kila jema juu ya muungano Ghari kama huu wetu kinyume na hapo ni Zenji wajiandae Kuwa Raia wa Nchi jirani na watalipia Viza na vibali vya kuishi bara huku Umeme na chakula toka Bara vikilipiwa kwa Dola na Uchumi wa Bara kukua kwa kasi ya ajabu kwani pesa toka hazina haina mgao kwenda Zenji itabakia Bara huku viongozi wakichapa kazi bila stress za kero za muungano .kwa kweli ili Haya yasitokee tunahitaji serikari moja tu
Una uhakika na unachosema kuhusu kuifuta?Serekali moja ipi?mkuu wazanzbr kuufuta uzanzbr eti tu kisa muungano hatupo tayari kwa hilo tena sahau,huku zanzbr ni mamlaka kamili tu,kama mlishindwa kuifuta zbr kwa miaka 50 msitarajie kuifuta kwa kipindi hiki,zanzbr kwanza.
Una uhakika na unachosema kuhusu kuifuta?
mkjj hizo siasa za kumfanya kama nyerere mungu wetu achana nazo hazitusaidii,
kwanza nyerere alikua akidanganya na kutisha watu, si kweli kabisa kama serikali tatu ati tanganyika itakua na gharama ya kushugulikia watu wake na wa muungano plus watu wake. upuuzi tu serikali tatu maana yake mbili zitashughulikia maslahi ya nchi zao na muungano itasimamia yale mambo waliokubali kuyasalimisha kwa wote.
muundo huu tulionao, wa serikali ya TANganyika kujifanya ruhani na big brothers umeleta manunguniko mengi, umejenga chuki na hasama kubwa baina ya wazanzibari na watanganyika. na nnaamini kwa kua tu zanzibar ni ndogo lakini kama zanzibar ingekua kama kenya pangekua peshanuka. unazani kenya wangekubali kudhalilishwa rais wao na kufukuzwa kazi na rais wa nchi nyengine?
niwe muwazi hutowakuta wazanzibari walio wengi wenye kuunga mkono uamuzi wa nyerere kwa kutumia chama kumfukuza kazi rais jumbe. na nenda kafatilie zanzibar utagundua wazanzibari wanampenda sana na sana jumbe kuliko nyerere na wanaamini wazi kua nyerere alipinda hati za muungano kwa maslahi yake binafsi.
muungano wa serikali mbili uko bayana kua ni kuisokota zanzibar na kuichukulia ni subdivision ya tanganyika. muungano wa serikali tatu utatoa fursa sawa kwa nchi mbili zilizounda muungano. nnasikitika kusema ww mkjj si mpenda haki, na wala hupendi haki itendeke. unapenda kuona zanzibar inaangamia au kua sehemu ya tanganyika.
tuje kwenye muundo ulio sawa, tuwe na serikali ndogo ya muungano na iwe inachangiwa kwa usawa, wazanzibari hawajakataa kuchangia muungano, na vikao vimefanyika na wazanzibar wamekubali tuuunde mfuko wa pamoja wa matumizi na mapato ya muungano, mbona watanganyika mmekataa kwa nn ? sababu ni ile ile kuisokota zanzibar.
kua na serikali tatu na nchi mbili ni suluhisho zuri sana, maana lile la ubig brother litakufa, pili kila nchi itakua na nguvu ya kusimamia rasilimali zake na kupanga sera zake zauchumi kwa uhuru.
Serekali moja ipi?mkuu wazanzbr kuufuta uzanzbr eti tu kisa muungano hatupo tayari kwa hilo tena sahau,huku zanzbr ni mamlaka kamili tu,kama mlishindwa kuifuta zbr kwa miaka 50 msitarajie kuifuta kwa kipindi hiki,zanzbr kwanza.
Unauhakika unajua unachoongelea? Huu uzi ni mkubwa nakusihi uache kuuchafua, utendee haki yake.Yap ni kuifuta,zanzbr kutoka empire mpaka sasa mkoa,inatosha kwa sasa tuachiwe tupumue,zanzibr kwanza.
Dhana hii ya Mwalimu juu ya mkataba wa muungano wa shirikisho pia inathibitishwa na makala moja ya gazeti la Observer la Uingereza toleo ya Aprili 20, 1964 ambapo Nyerere alinukuliwa akisema:"Bara lenye ukubwa wake kamili, moja na lisilogawika, ndilo nataka liwepo; Hii haina maana huku ni kuwa na serikali moja kwa bara lote, katika hali ya kuwa na serikali kuu yenye mamlaka yote; Kinachotakiwa ni kuwa na serikali moja inayounganisha nyingi na kuwa na mamlaka katika maeneo Fulani Fulani; Zaidi ya hapo kunaweza kuwepo na serikali nyenginezo, hizi zikiwa na mamlaka yaliyo hafifu kidogo, na mamlaka hayo yakiwa yanatokana zaidi na katiba za ndani sio kutoka serikali kuu; Hii ni sawa na kusema kuwa afrika mpya inaweza kuwa ni dola ya shirikisho, ambayo nguvu zake zinagawiwa baina ya serikali kuu na serikali za mataifa washiriki kwa mujibu wa matakwa ya waanzilishi na vizazi vijavyo."
.Iwapo umma wa Zanzibar bila ya ushawishi kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona kuwa muungano una hasara kwa uhai wao, sitowapiga mabomu kuwalazimisha. Muungano utakuwa hauna tena sababu ya kuendelea iwapo washiriki wake wataamua kuukana
·"The Acts of the union were the first union constitution"
MKATABA WA MUUNGANO Baina ya JAMHURI YA TANGANYIKA
·Na JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR
KWA KUWA serikali ya Jamhuri ya Tanganyika na Serikali ya jamhuri ya watu wa Zanzibar zinafahamu uhusiano wa muda mrefu wa watu wake na mshikamano wao wa kidugu na kirafiki, na kwa hamu ya kutaka kukuza uhusiano huo na kuimarisha mshikamano na kukuza umoja wa watu wa Africa, zimekutana na kutafakari muungano wa jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar.
…tunapinga kwa sababu ya mantiki nzima ya kuwa na serikali tatu na nchi mbili! lakini wenzetu wanataka tuwe na nchi mbili na serikali tatu!
NA KWA KUWA Serikali za jamhuri ya muungano wa Tanzania na Jamhuri ya watu wa Zanzibar zinapendelea ya kwamba jamhuri hizi mbili ziungane kuwa jamhuri moja huru kwa masharti yafuatayo:
Kwa hivyo IMEKUBALIWA baina ya serikali ya jamhuri ya ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar kama ifuatavyo: i) Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitaungana na kuwa jamhuri huru moja. ii) Katika kipindi cha kuanza kwa muungano mpaka baraza la kutunga Katiba lililotajwa katika ibara ya (vii) litakapokutana na kupitisha katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania (kuanzia hapa kitaitwa kuwa ni kipindi cha mpito), jamhuri ya Muungano itaongozwa kwa masharti ya ibara ya (iii) mpaka (vi). iii) Katika Kipindi cha mpito Katiba ya jamhuri ya muungano itakuwa Katiba ya Tanganyika itakayorekebishwa ili kuweka….
· [FONT=" [B]Mzee Mwanakijiji[/B] hauoni tatizo hapa? Kiini cha mgogoro kinaendelea kuwa ni Katiba ya JMT (1977), tofauti na wanasiasa wanavyopenda tuamini kwamba mgogoro ni matokeo ya chuki ya watanganyika kwa wanzazibari au chuki ya wazanzibari kwa watanganyikai. Chuki zilizopo ni matokeo ya mapungufu yaliyojitokeza kwa miaka karibia 50. Ni kwa mantiki hii, rasimu ya katiba ikaja na pendekezo la mfumo wa shirikisho la serikali tatu. [/FONT] Kama nilivyojadili awali, Rasimu ya katiba haijaja na kitu kipya, badala yake imerejea mkataba wa (1964) ambapo Rasimu inasema hivi:Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. 2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA SEHEMU YA KWANZA MIPAKA, ALAMA, LUGHA, UTAMADUNI NA TUNU ZA TAIFA 1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi huru.
"The Acts of the union were the first union constitution"
Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalinbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. Muundo wa Serikali mbili unakubaliwa na wananchi, lakini unatokana na sera ya TANU na ASP, na kwa sasa CCM. Chama Cha Mapinduzi kikipenda kinaweza kubadili sera hiyo ya muundo wa Serikali mbili bila kuuliza wananchi kwanza. Kinaweza kufunya hivyo kwa kuhisi kuwa hivyo ndivyo wananchi wengi watakavyo; lakini pia kinaweza kufanya hivyo kwa sababu kinaamini kuwa inafaa kufanya hivyo, hata kama wananchi wengi hawakudai au hawapendi mabadiliko.
Na maneno haya ya Nyerere yasikike kwenye masikio yaliyoziba ya watawala wetu walioshindwa!
Hizi zote ni mbinu za viongozi wetu waheshimiwa kutaka kukiingiza Chama katika njia moja tu nyembamba, na kutuburura kama vipofu tuitumbukize nchi yetu shimoni. Ni jitihada za kukifanya chama na sisi wengine wote tukubali msimamo wao wa kutaka kuigawa nchi yetu.
· Sisi tumejadili kwa kina juu ya kero zilizopo na kwanini serikali tatu itazitatua kero husika; Kwanini nyinyi hamji na hoja kujadili matatizo yaliyopo kwa miaka karibia 50 sasa, yatatatuliwa vipi na mfumo wa serikali moja? Vinginevyo kuna mjadala nilianzisha siku kadhaa zilizopita ambapo nilijadili kwa kina kwanini shirikisho la serikali tatu litaleta ufanisi zaidi kisiasa, kiuchumi na kijamii kuliko unitary system mnayoipendelea. Unazidi kusema kwamba:Serikali tatu haitotatua matatizo ya Muungano itayaongeza tu.
Nafarijika kuona unakubali kwamba suala la gharama ni jambo dogo zaidi. Naomba nisisitize kwamba lets focus on efficiency ya mfumo - politically, socially and economically kuliko kuweka focus kwenye gharama kwani as long as kuna efficiency, costs will always be justified. Mataifa makubwa kama marekani na mengineyo yanafanya mambo mengi sana ndani na nje ya mataifa yao kwa gharama kubwa lakini mwisho wa siku, as long as kuna ufanisi kisiasa, kiuchumi na kijamii, walipa kodi always wanakuwa tayari kubeba gharama husika. Nina uhakika kwamba hata kwa Tanganyika na Zanzibar, this argument prevails.Tunaopinga serikali tatu hatupingi kwa sababu ya gharama tu, hili ni jambo dogo zaidi…
wale wote waliofaidi na wanaofaidiki muundo wa serkali 2 hawatapinga kamwe serkali 2. mi nawashangaa eti serkali tatu muungano utavunjika mara ni gharama najiuliza kwanini serkali 2 hazijafanya? hamuoni sasa kuwa na serkali 2 ni sawa na kutokuwa na kiranja na hivo kifo kiko wazi? sewrkali tatu itaimarisha muungano na kuleta nidhamu kwa serkali ya muungano ambaye ndiye MSIMAMIZI MKUU AWA SERKALI 2 ZILIZOPO. KWANI KWA SASA SERKALI 1 IKO JUU YA NYINGINE AU? NI HILI NDO LINALOLETA SHIDA KUWA ZANZIBAR WANASIMAMIWA NA TANGANYIKA KAMA HAJAJUA KWAHIVYO SULUHU NI KUWA NA SERKALI TATU MOJA IKIWA JUU ZILE 2 ZIKIWA CHINI YAKE. HAMUELEWI NINI CCM. SASA MJADALA WA KATIBU ULIKUWA WA NINI? ACHENI UKIGEUGEU MLIFIKIRI RAHISI NYOMkuu wangu Nguruvi3 nimependa sana uliposema hapo juu kuwa, ndani ya serikali 3, mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama! Tafsiri ya wazi hapa ni kuwa ni lazima tufanyiane undava undava tu, na huo ndio ukweli na hakuna namna ya kuukwepa ndani ya serikali 3. Sioni nafasi ya Tanzania endelevu chini ya serikali 3. Sioni namna yoyote ya Usisi na Uwao kutufikisha kokote zaidi kwenye shimo la giza! Kwa Mazingira na Nyakati(FIKRA) kama zetu, basi hakuna namna ya kuupuuza UMOJA na tukabaki salama! Bado naheshimu mawazo ya nchi moja, serikali moja, taifa moja. Siku zote mtu nguvu ya mtu mweusi ni Umoja! Kila tunachoota leo chema chini ya serikali 3 au 2, hakiwezi kufikiwa kama hatutakuwa wamoja, na hakuna namna yoyote ya kujihakikishia Umoja chini ya Serikali 3 au 2. Hii ni Afrika, tusijifananishe na wengine. Kuna namna zetu sahihi na mahususi kwetu za kuendesha mambo yetu! Mungu wetu anaita sasa!
wale wote waliofaidi na wanaofaidiki muundo wa serkali 2 hawatapinga kamwe serkali 2. mi nawashangaa eti serkali tatu muungano utavunjika mara ni gharama najiuliza kwanini serkali 2 hazijafanya? hamuoni sasa kuwa na serkali 2 ni sawa na kutokuwa na kiranja na hivo kifo kiko wazi? sewrkali tatu itaimarisha muungano na kuleta nidhamu kwa serkali ya muungano ambaye ndiye MSIMAMIZI MKUU AWA SERKALI 2 ZILIZOPO. KWANI KWA SASA SERKALI 1 IKO JUU YA NYINGINE AU? NI HILI NDO LINALOLETA SHIDA KUWA ZANZIBAR WANASIMAMIWA NA TANGANYIKA KAMA HAJAJUA KWAHIVYO SULUHU NI KUWA NA SERKALI TATU MOJA IKIWA JUU ZILE 2 ZIKIWA CHINI YAKE. HAMUELEWI NINI CCM. SASA MJADALA WA KATIBU ULIKUWA WA NINI? ACHENI UKIGEUGEU MLIFIKIRI RAHISI?Mkuu wangu Nguruvi3 nimependa sana uliposema hapo juu kuwa, ndani ya serikali 3, mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama! Tafsiri ya wazi hapa ni kuwa ni lazima tufanyiane undava undava tu, na huo ndio ukweli na hakuna namna ya kuukwepa ndani ya serikali 3. Sioni nafasi ya Tanzania endelevu chini ya serikali 3. Sioni namna yoyote ya Usisi na Uwao kutufikisha kokote zaidi kwenye shimo la giza! Kwa Mazingira na Nyakati(FIKRA) kama zetu, basi hakuna namna ya kuupuuza UMOJA na tukabaki salama! Bado naheshimu mawazo ya nchi moja, serikali moja, taifa moja. Siku zote mtu nguvu ya mtu mweusi ni Umoja! Kila tunachoota leo chema chini ya serikali 3 au 2, hakiwezi kufikiwa kama hatutakuwa wamoja, na hakuna namna yoyote ya kujihakikishia Umoja chini ya Serikali 3 au 2. Hii ni Afrika, tusijifananishe na wengine. Kuna namna zetu sahihi na mahususi kwetu za kuendesha mambo yetu! Mungu wetu anaita sasa!
Mzee Mwanakijiji, Kobello, na wengine wote mnaopendelea serikali moja:Kwanza niseme kwamba kwa kweli tupo wengi sana tunaopendelea Tanzania ifuate mfumo wa serikali moja lakini nadhani tofauti yetu na yenu zipo katika maeneo makuu mawili: ·
Kwanza, kwa upande wetu, tunaangalia zaidi practice kuliko theory, na katika hili, tunaona wale wote wenye kupendelea mfumo wa serikali moja katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wishful thinkers. ·
Tofauti ya pili baina yetu na nyie ni kwamba, mnapendelea Zanzibar to sacrifice na kukubali serikali moja, bila ya kujalisha kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza kero zaidi muungano zilizopo sasa.
Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.
Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.