Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,048
49,731
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia.

Screenshot_20230928-082105_1.jpg

Screenshot_20230928-081812_2.jpg

BADO KM 51.1 KUUNGANISHA TABORA-KIGOMA KWA LAMI

IMEELEZWA kuwa bado kilomita 51.1 ili kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa barabara ya lami na hivyo kuandika historia ya aina yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Kigoma sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 na Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1.

“Kwa kweli nimeridhika na kasi ya ujenzi sehemu ya Kazilambwa-Chagu yenye urefu wa KM 36 ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 99”, amesema Eng. Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amemtaka mkandarasi STECOL Cooperation Ltd anayejenga sehemu ya Malagarasi-Ilunde-Uvinza KM 51.1 kufanya kazi usiku na mchana ili kuandika historia ya kuunganisha mikoa ya Tabora na Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi huo umefikia asilimia 45 na watamsimamia kikamilifu mkandarasi ili maeneo yanayoweza kuathiriwa na mvua yakamilishwe mapema ili kuepuka visingizio na kuwawezesha wasafiri na wasafirishaji wa mikoa hiyo kunufaika na barabara ya kisasa.

Zaidi ya shilingi bilioni 62.7 zinatumika katika ujenzi huo ambazo ni matapo ya ndani na mkopo nafuu kutoka mifuko ya OPEC na Abu Dhabi.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya amemtaka Mbunge wa Urambo Mhe. Margareth Sitta kuhamasisha wananchi wa jimbo hilo kulinda miundombinu inayojengwa katika jimbo hilo ikiwemo taa na alama za barabarani ili kuepusha ajali na kuendana na kasi ya Serikali ya kupendezesha barabara nchini.

“Tunawajengea barabara na mzunguko wa kisasa round about ili kupunguza ajali eneo lililokuwa na kona kali na kutengeneza taswira nzuri ya Urambo hivyo hakikisheni miundombinu hii inalindwa na kuendelezwa kwani inatumia fedha nyingi za Serikali “, amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Kwa upande wake Mhe. Margareth Sitta ameishukuru Serikali kwa uwekezaji mkubwa wa miundombinu ya kisasa katika wilaya ya Urambo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi kuthamini uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

View: https://youtu.be/wmpjkZkgfR4?si=PuPssK4vU2XqJbXx

Nawakumbusha tuu mradi ulianza tarehe 7/10/2021 baada ya Rais Samia kuingia madarakani,hakuna Cha Mwendazake kuanzisha na blaa blaa kama hizo,huku section ya kwanza Kigoma-Malagarasi alijenga JK

View: https://youtu.be/MfRWwiENKz8?si=S4TOiH1TvwP7NTKs
 
Aiseee sijawahi kufikiri kuwa mpaka Sasa kuna barabara ya mkoa wowote Tanzania haina lami.
CCM ilaaniwe kwa uovu na wizi
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morogoro via Ifakara.
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morohoro
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Toa hiyo Kigoma -Kagera.Hiyo ina lami kuanzia Kakonko ambako ni upande wa Kigoma.
 
Toa hiyo Kigoma -Kagera.Hiyo ina lami kuanzia Kakonko ambako ni upande wa Kigoma.
Nitoe Ili iwaje,kwani Barabara nzima Hadi Kigoma Ina lami? Hata hizo zingine hapo Kuna vipande havina lami.

Wewe si ulitaka kujua kwamba kumbe unaweza safiri Mkoa hadi.mkoa na ukala vumbi some sections? Ndio hizo Sasa nimekuwekea.
 
Tukiwaambia kwamba hakuna alichofanya Cha maana Mwendazake kwenye Barabara za lami wakati wa Uongozi wake muwe mnaelewa.

Imagine Hadi Leo hii huwezi fika Kigoma bila kutembea kwenye mavumbi na hali Iko hivyo kwenye Mikoa Mingi sana.

Sasa kipele kimepata mkunaji ambao km 51 zilizosalia zinaenda kukamilika kabla ya desemba 2024 hivyo Kigoma-Dar itakuwa lami.Kazi hii ya kutukuka anaifanya Rais Samia

View: https://www.instagram.com/p/Cxr9S90sNAh/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==

Wewe unaona hicho ndicho cha maana sana! Kwa ujinga huu ndio unatufanya tutawaliwe na koo kumi miaka nenda miaka rudi, wenzetu wanaendelea sisi tumebaki kuhesabu kilomita za lami!
 
Wewe unaona hicho ndicho cha maana sana! Kwa ujinga huu ndio unatufanya tutawaliwe na koo kumi miaka nenda miaka rudi, wenzetu wanaendelea sisi tumebaki kuhesabu kilomita za lami!
Wewe ulitaka tutawaliwe na Koo zipi Kwa majina na idadi? Ukomo wako ndio wa maana au? Kama kujenga Barabara sio jambo la maana Sasa wewe kwako la maana ni lipi?
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morohoro
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Njombe-Morohoro?
Au unamaanisha Njombe-Morogoro mimi naishi Dar es Salaam nasafiri hadi Makete ni lami tu.
 
Utakuwa unaishi Canada.Nyie mlikuwa mnaishi Kwa propaganda za Mwendazake.

Sasa Kwa taarifa Yako Barabara zifuatazo ni vumbi tupu.

Kigoma-Tabora
Mpanda-Sumbawanga
Kigoma-Mpanda
Morogoro -Songea
Mbeya-Tabora
Mbeya-Singida
Arusha-Musoma
Arusha-Simiyu
Njombe-Morohoro
Mtwara-Masasi via Tandahimba
Morogoro -Lindi
Kigoma-Kagera

Hiyo ni Baadhi tuu ya Barabara kuu za Mikoa kwa Mikoa ambazo zimejaa mavumbi au Baadhi ya vipande Bado ni mavumbi.
Rami za Kigoma zilianza kujengwa wakati wa Magufuri. Nyakanazi Kigoma chini ya African Development Bank na Tabora Kigoma aliacha wakandarasi wanaendelea, hivyo jiwe ndo alipigania. Samia labda vipande vipya atavyoanza navyo 2025.
 
Rami za kigoma zilianza kujengwa wakati wa magufuri. nyakanazi kigoma chin ya African dvpt bank na Tabora kigoma aliacha wakandarasi wanaendelea,,hivyo jiwe ndo alipigania.Samia labda vipande vipya atavyoanza navy 2025
Miaka 5 Anapigania si ndio? 🤣🤣🤣

Aliyekwambia lami za Kigoma zilianza na Magufuli ni nani? JK ndio alikuwa wa kwanza kujenga lami Kigoma na madaraja ,ilitazamiwa baada ya Mwendazake kuwa Rais amalizie lakini hakuna alichofanya Cha maana huko Kigoma.

Aliishia kulamba lamba na akafa akacha Mkoa una mavumbi vile vile alivyoukuta.Samia anafuta hizo vumbi zote kabla ya 2025.
 
Back
Top Bottom