Wakuu, naombeni tusilipoliticise suala la Prof. Beregu, kama kastaafu na anaendeleaa kwa mkataba, its just a favour, don't turn a favour into right. Mwajiri ana haki ya kusema asante imetosha, kama suala la Dr. Rashid wa Tanesco, mwajiri serikali imekubali inatosha, ikaitangaza nafasi yake.
Msitake kuisingizia Chadema, mbona Dr. Mvungi ni NCCR na aligombea urais, kakosa, karudi chuo na bado ni NCCR?.
Mbona wako wahadhiri ni mwiba mkali kwa serikali na wanavumiliwa?. I think its high time, Beregu akubali yaishe, aondoke kama kina Shivji, heshima yake itabaki kuwa juu, kuliko kutaka kuendelea kuvuta shuka ilhali kumekucha na muda wake ni tayari kumekuchwa.
Ila pia lazima tukubali Prof. Mukandala kaukwaa uVC kama asante kwa kazi nzuri ya Redet inavyowafanyia CCM. Kama umepata post kwa favour, lazima umaintain status quo. Msimlaumu Mkandala, "Ukiaminiwa, jiaminishe".
Wako wanaokumbuka Daruso ikiwa mwiba kwa Serikali, ni kina Mwikabe walioi ccmmsha Daruso na kuifanya kama tawi la CCM japo leo wako upinzani, hizi njaa zitatuuwa bure!.