Kwanini Nyerere hakumkubali Lowassa?


Haya ndiyo matatizo ya wacheza kolokolo. Wapi hapo Nyerere amesemwa vibaya? Wapi hapo nyere amekashifiwa? Je kusema alikuwa na chuki ni kosa? Kusema alitumia propaganda ni kosa? Naona umepita mithiri ya tractor lenye jembe butu, unafyeka na kuacha magugu nyuma. Tengeneza maelezo yako yakae vyema.
 
kwa nn nyerere amuonee lowassa! Mbona kituko? Lowasa anakoelea ni kubaya, sijui anautaka urais hata kwa gharama gani!
 

Maneno yako ni mazuri pia, lakini yafaa utamke na uweke wazi. Ameiba nini na nini? Ameiba ibaje? Alivyoviiba viko wapi ili wananchi wajue, mwizi hukamatwa na kushitakiwa. Amekamatwa na nani na kithibiti kiko wapi. Njoo na vielelezo vyenye ushahidi hapa wala si maneno ya kufikirika.
 
Ahsante sana mkuu.
Nyie wana Lowasa tafadhali tafakarini maneno haya kwa busara sana mtayaelewa, lakini mkileta ulevi wenu na kukurupuka mtaishia pabaya. Waulizeni CDM, wanajua technique nzuri za kuwakamata Watanzania na ndo mana kila siku wanazidi kuwapiga bao. Wanaepuka sana kumponda Baba yetu wa Taifa.
Fanyeni mzaha na jina la kilaza wenu toka Msoga lakini siyo jina la Mwalimu Nyerere, MTAPOTEA!.
 

Anayetakiwa kuthibitisha vyanzo vyake haramu ni wewe unayemtuhumu. Vinginevyo kama huna ushahidi unakaa kimya tu.
 
Hongera sana mkuu kwa kusema ukweli! Tusubiri wafuasi wa NAPE.

El.na kundi lako muogopeni mungu si siri watanzania ombeni mungu usiku kucha ili hili kundi lisifanikiwe kuingia ikulu
 

Akili ni nywele kila mtu ana zake. Soma vizuri maelezo hayo na usitake kukuza mambo. Ni wapi nimemsema vibaya mwalimu hapo?
 
Bora muongelee humuhumu mana mkiongea hadharani,mi ntakuwa wa kwanza kuwapiga mawe,wasemeni wengine lakini siyo Nyerere,huu ni usenge,Nyerere alipigania hii nchi,huwezi kumtukana kwa sababu ya maslahi yako,Lowassa ni mwizi kuliko wezi wote Tz hata yeye mwenyewe analitambua hilo,acha kumtukana Nyerere,unatuudhi sana tena wengine huwa hatuchangii humu kazi yetu ni kusoma tu ila hakika wewe mwehu umenikera hadi nmekuandika,usijaribu tena kumsema Nyerere mana tutakuassassinate wewe na huyo mwizi wetu.
 
Kweli hapa Lowasa unapoteza pesa zako, mtu huyu uliyemtuma anahoja za kutukumbusha maovu yako na pale anaposema mwalimu alikuwa na chuki binafsi na nyie na JK kwa hali hii ya swahiba wako hupati kitu hapa hata utoe chapaa!
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake. Soma vizuri maelezo hayo na usitake kukuza mambo. Ni wapi nimemsema vibaya mwalimu hapo?

Tuseme sawa hujamsema vibaya.
Uliposema kwamba mwalimu alikua na chuki binafsi na EL hapo hukumsema vibaya. Hata uliposema alimtengenezea EL zengwe pia hukumsema vibaya na hata uliporopoka kwamba mwalimu alisema uongo napo ulimsema mwalimu vizuri tu.
Tumia akili yako vizuri mkuu siyo useme maneno kama mtu asiyeshirikisha ubongo.
EL nae atakua anapoteza hela zake kama ataajiri kilaza kama wewe usiyeweza kumtetea na kuishia kumkashifu Mwalimu Nyerere.
 
Lowassa asipochaguliwa sasa hivi,haitakuwa kwa ajili ya Nyerere. Na kama ukisema Nyerere,ambaye yuko ndani ya jeneza ndie anayemzuia Lowassa kuwa Rais,I swear this Lowassa fellow will not become Presiident.
 
natumai umekuja kuandika huu upupu baada ya kuhongwa nyamachoma na whisky pale mwika
endelea kujitahidi lakini lowassa kwa urais 2015 ni ndoto za alinacha
 

Mi naona mtoa mada yupo sawa. Kawaida wtz huwa hampendi kuambiwa ukweli. Wote tunakumbuka ilivyokuwa. Ni kweli hayo yalitokea kika mtu anajua. Ingekua sio zengwe iwapo nyerere angekaa kimya na kuacha demokrasia ifanye kazi yake. Ingekuwa fair pia kama asengeweka msimamo juu ya mali za Lowasa. Alikuwa kiongozi mzuri lakinh alikuwa na mapungufu pia. Kwani mtoa mada amemsingizia?
 
Kweli hapa Lowasa unapoteza pesa zako, mtu huyu uliyemtuma anahoja za kutukumbusha maovu yako na pale anaposema mwalimu alikuwa na chuki binafsi na nyie na JK kwa hali hii ya swahiba wako hupati kitu hapa hata utoe chapaa!

Lowasa = Mkaa. I mean yaani hata uuoshe vipi hauwezi kuwa mweupe!!
 
Hongera sana mkuu kwa kusema ukweli! Tusubiri wafuasi wa NAPE.
Majungu matupu na kutumwagia upupu humu barazani. Mbona wakati ule Nyerere alipomsema Lowasa na wapambe wake walikaa kimya?Si Lowasa wala wapambe wake kina Pasco et al waliomtaka Nyerere athibitishe kauli yake dhidi ya Lowasa,miaka 12 baada ya kifo cha Nyerere na kwa kuuchungulia urais,mnakuja na upupu wenu
kumtetea bwana wenu bila haya ya uso!
Mtawadanganya vijana ambao walikuwa watoto wadogo enzi hizo.
 
NA zile ranchi za alizojigawia nao ni uonevu wa Nyerere.

Umenikumbusha mkuu. Kuna siku ng'ombe wa Lowasa alikufa pale ranchi ya Mkata, Lowasa wakati huo akiwa Waziri Mkuu alikwenda na msafara wa Kiserikali na Maaskari wa kumlinda kutoka Dar hadi Mkata! Fikiria thamani ya ng'ombe mmoja wa Lowasa na gharama za Serikali; magari ya Serikali na Walinzi! Matumizi mabaya ya mali za umma, halafu wapambe wanamwaga upupu kuwapotosha watu kwa manufaa ya bwana wao.
 
Huyo Ndugu Lowasa anafahamika kwa tabia yake ya ukora! na ni mtu hatari sana hapa Tanzania! usione hivi yeye na kundi lake amesababisha nchi kuwa katika hali ya umaskini.Anajaribu makanisani! hata juzi alikuwa huko mskiltini wakati wa maulid! Jamani tuchunge sana mtu hyu! Akiwa Rais atakuwa kama wale wa Misri wenye kutaka ten percent kwa kila biashara inayofanyika hapa nchini
 

Matusi na vitisho vyako havizuii maoni huru. Ubabe wako katika kuandika sentensi haupindishi ukweli. Hasira zako hadhiathiri chochote katika ninayoamini. Busara zako zilizotuama makalioni ndizo zilizokuelekeza undike matusi badala ya kupinga hoja kwa hoja zenye akili. Hujui, wala sikulazimishi uamini. Mimi ni mtu ninayeyakubali sana mazuri ya mwalimu, yake mengi kuliko mabaya. Lakini ni mtu wa pande mbili. Kama kuna ambacho alikuwa wrong kidogo hatuwezi kukaa kimya.
 

Kwa hiyo ulitaka waziri mkuu atembelee baiskeli na sungusungu ndiyo wawe walinzi wake?
 
Strange as it is, when people aspire for the big post, they first have to deal with Nyerere in one way or another. That is what we call a legacy...whether good or bad legacy, is upon the indivual who choose to look at the matter. But for me, Nyerere was the man. He mastered the game and played it very well, not matter how much we try to deny or refuse that fact!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…