Mfano kama Tanzania wakidhamilia kabisa tukapata umeme wa uhakika, tukajenga bandari ya kisawasawa mtwara, DAR na Tanga.
Harafu tukaweka ma-treni ya umeme:
-kutoka Tanga mpaka mpakani mwa kenya,
-kutoka Mtwara mpaka mpakani mwa nchi zote za kusini
-Kutoka Dar mpaka DRC, Rwanda na Burundi
-Uwanja Wa ndege charge ikapungua kwa namna yake.
Naamini Kenya watagoma kuungana na kufanya soko la pamoja.
MkamaP,
..sasa kwanini hatujaribu hata project kati ya ulizotaja??
..project ya bandari na reli ya kenya inakuwa financed na China.
..lakini sisi ndiyo marafiki wa China wa muda mrefu, nini kimeshindikana??
..mimi nadhani huu uongozi tulionao ni incompetent.
Alikusudia kuonyesha Ego maniac...wakuu page ya 14.....sijaelewa william alikusudia nini kuandika hii thread???
sishangai maana hata na wewe uliwahi kuja na vihoja vyako mfu ukala kona......Willy,
Mafanikio mema mkuu. Usikatishwe na kelele za haters wa hapa JF.
Muhimu ni conviction yako katika hiyo kazi unayoomba. Ninaamini ukifanikiwa utasaidia kuingiza mtazamo mpya na mawazo mapya huko EA.
Kikubwa tu mkuu ukifanikiwa usituangushe. Watanzania ni mabingwa sana wa maneno lakini vitendo sifuri. Jikite kwenye kutatua matatizo na bahati mbaya kwenye EA yapo mengi sana.
Nimepitia majina ya wagombea na una qualifications zote za kutuwakilisha vizuri kuliko wengi wa hao waliopitishwa maana uzoefu ni mwalimu mzuri kuliko elimu ya madarasa. Inahitaji uwezo kuingia huko kwenye mameli na mpaka ukafika sehemu na kufanya mambo yako bila kubebwa na mtu. Hiyo ndio shule ya maana na ya kweli na sio kuwa na uwezo mkubwa wa kukariri ili kufaulu mitihani.
Wengine tungependa kuona watu wengi ambao wamepikika hapa JF wanachukua nafasi za uongozi kwa faida ya nchi yetu.
Mafanikio mema mkuu,
Mtanzania aka Mwakalinga.
My profile:
1. Born in Tukuyu.
2. Jamhuri Primary School, Mnazi Mmoja; DSM.
3. Kwiro Secondary School, Mahenge; Morogoro.
4. Kidatu Sugar Instituon, Kilombero; Morogoro.
5. DSM Marine Engineering School (DMTU), DSM.
6. Field Kagera Sugar Factory, Kyaka; Bukoba.
7. Field Mv. Bukoba, Mwanza; Mv. Mwongozo & Liemba; Kigoma.
8. JKT Oljoro/Makuyuni, Camps; Arusha.
9. CMB Marine Engineering Insistute; Antwerpen, Belgium.
10. Field CMB-Belgian Shipping Line ( as Assistant Engineer)
11. Worked Tanzania/Chinese Shipping Company; DSM/Hongkong.
12. Associate Degree in Criminology & Police Science; Westchester College in New York, USA.
13. BA in Political science, Lehman University at New York City, USA.
14. One year Internship at Dominican Republic Permanent Representative to the UN, General Assembly; New York; USA.
15. Worked at Sterycircle Inc, as Class A Haz Mat & Poison at Disposal Facilities. Dealing with (Transportation + Financial Covering the Incinerator)
16. Started CCM branch in New York City, USA.
- Now aspiring to represent our Nation, to the EAC Assembly.
William.
Mkuu kusema kweli nami niltegemea hoja mujarabu toka kwa mkuu kutuonyesha anaenda kutufanyia nini sisi Watanzania kwenye hilo Bunge. Nilitegemea aje na vipaumbele japo vitatu vya haja ambavyo ingekuwa ndio agenda yake kila akiingia kwenye ukumbi wa Bunge hilo.Wana JF tujaribu kuwa wakweli hata kwa mara moja tuachane na unafiki ambao unatutafuna kama taifa na kujikuta hapa tulipo. Hii hoja imeletwa na William Malecela mwenyewe tena kwa mbwembwe tosha eti, kwa nini ninagombea Ubumge wa EAC - My case! Nilitegemea kweli angekuja na hoja ya kitu gani kinampa msukumo huo na sisi kama taifa tutafaidika vipi na kuwepo kwake huko. Lakini ukiyatafakari yote aliyoyatamka unapata picha halisi kuwa kigezo pekee anachokitegemea katika kuukwaa ni jina Malecela, period. Elimu (ya kuungaunga), sifa, uwezo, uzoefu (wa kiujanjaujanja) na lugha (ya kuokotezaokoteza)... zote haziko upande wake na ukimvua ubini anabaki mtupu kabisaa asiye na sifa ya kugombea hata udiwani, huo ndio ukweli ingawa mchungu kwake na kwa mashabiki wake. Hii ni JF and I rest my case.
.
Unajua watu walisema mengi kuhusu huyu jamaa kuwa hafai wengine wakasema ni Looming Disaster to our Nation kila mtu alisema chake.
Sasa baada ya huyu jamaa kuleta hapa my case zake za kugombea nikaona duh! Ndiyo haya?! bora angenyamaza kimya maana baada tu ya kuanza kujieleza ndipo wasiwasi uliponiingia na ndipo nimefahamu kuwa huyu hafai kuliwakilisha Taifa letu Afrika Mashariki!
My friend William, all I can say is ... tafuta kazi nyingine ya kufanya!
Better to remain silent and be thought a fool than to speak out and remove all doubt." -- Abraham Lincoln
.
Mkuu,
Siamini kama kweli viongozi ni incompetent lakini yawezekana wanafanya hayo kwa sababu wanaambiwa na mataifa ya magharibi nini cha kufanya na nini cha kutofanya, ili ufanye project kama hizo unatakiwa usipige kelele kwenye vyombo vya habari na wala usiende kukopa kwa ajili ya project hizo.
Ukipiga kelele wataku GBAGBO ama ku-GADAFFI, fanya taratibu kwa ukimya wakija kungutuka umeshamaliza kazi-inakuwa imekula kwao tayari.
Mfano, lakini unaweza usiwe mfano wenye tija nao ni hivi, hakuna haja ya kuwatoza kodi ama kuwauzia hawa wachimba madini yetu ingekuwa nzuri kama wangefanya butter trade nayo ni hivi:
-Wewe chukua mgodi wa buzwangi nijengee chanzo cha uhakika cha umeme life span miaka 60
-Wewe chukua mgodi wa mwadui nijengee bandari ya Mtwara na Tanga life span miaka 60
-Wewe chukua mgodi wa Nzega resolute nijengee Reli za umeme kuunganisha miji hiyo life span miaka 60
-Wewe chukua mgondi wa chamongo lakini unizalishie chakula tani kadhaa kwa mwaka kwa mda wa miaka 60.
-nk
Kwa hiyo kama hawana utalaam wakujenga ktk maeneo husika, ni wao watarudi kwao wakodi makampuni ya ujenzi na waje wajenge, wewe wakukabidhi tu kitu tayari, nafikiri hiyo itapunguza rushwa na tutakuwa tunaona sababu ya madini kuchimbwa.
Umesoma mambo mengi so what is ur profession.
Sijaona A level sehemu ulo somea!!
Umesoma mambo mengi so what is ur profession.
William,
..mimi sikubaliani na suala la kuruhusu watu waingie Tanzania bila passport.
..nasema hivyo kwasababu bado Tanzania haina national IDs wala ssn system.
..pia utalinda vipi ARDHI katika mazingira kama hayo ya kuruhusu Wanyarwanda,Wakenya,Waganda,na Warundi waingie Tanzania?
..pia tutalinda vipi soko letu la AJIRA ambapo unemployment ni kubwa mno?
..zaidi, with one visa to east africa kuna formula gani ya kugawana mapato.
..check this: Kenya has 9% of lake victoria, Uganda has 42%, and Tanzania has 49%. naomba unieleweshe faida tutakazozipata ktk matumizi ya rasilimali za lake victoria ikiwa tutafungua mipaka yake.
..pia Kenyatta Airport inapokea ndege nyingi kuliko KIA na Dar. Kenya imekuwa ikilaghai watalii kwamba vivutio vya Tanzania viko Kenya. Katika mazingira hayo kuna faida gani kuruhusu watalii toka Kenya waingie Tanzania bila malipo yoyote? Pia Tanzania sera yake ni kuwa na watalii wachache wakubwa, wakati Kenya ni mass tourism. Katika mazingira hayo how do we deal with Kenya wanapotu-pressure tufungue mpaka wa Golongoja[mbugani serengeti]??
..unadhani Tanzania itajikwamua namna gani toka kuwa wazalishaji wa malighafi ktk east africa, kwenda kuwa wazalishaji wakubwa wa bidhaa za viwandani?
NB:
..nakushauri uje kwenye International Forum ya JF huko ndiko mijadala ya East African Community imepamba moto.
Umesoma mambo mengi so what is ur profession.