jamani.. Zinaibwaje? Zamani ilikuwa rahisi kwa sababu sanduku linapakizwa kwenye baskeli kwenda kuhesabiwa sehemu nyingine.. Siyo mnasema "wizi upo" kinadharia inawezekana lakini mtu aniambie unawezekana vipi? Wildcard anasema kuwa zanzibar waliiba ah wapi!, kuna suala la tume ya uchaguzi kuingiliwa hilo limetokea kenya na ninaamini ndilo lenye uwezekano mkubwa wa kutokea tanzania mwaka huu..
Uwizi upo kwenye kuwarubuni mawakili! kuna jamaa aliniambia ilivyotekea jimbo la Arusha mjini nilitamani nimpige ila basi ndo ilitokea, Anasema kuwa yeye alikuwa ni WAKALA wa chadema, Walipewa laki 3 kwa ajili ya kubadilisha matokeo ya ubunge, na anasema walipokea na matokeo yakabadilishwa. NDO MAANA CHADEMA INATAKIWA WATAFUTE MAWAKALA WAAMINIFU SANA! wasiweke Bora liende!Jamani siku moja Profesa Lipumba alisema alipopiga kura kwenye kituo fulani alipigia CUF(URAIS,UBUNGE NA UDIWANI)lakini matokeo yalipotoka Mbunge na Diwani hawakupata hata kura moja,sasa tuite hiyo ni nini kama sio wizi?Au mimi sielewi nini maana ya neno WIZI?
Taarifa kutoka Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia mkoani Mbeya zinasema kuwa lori la kampuni ya Azam linalomilikiwa na mfanyabiasha maarufu Bakhresa leo hii tarehe 18 Oktoba, 2010, limekamatwa likiwa na shehena kubwa la karatasi za kupigia kura zitakazotumika uchaguzi mkuu Oktoba 31.
Maafisa wa TRA tunduma walishtuka baada ya kukuta karatasi hizo za kupigia kura zimefichwa kwenye shehena ya vipodozi. Inasemekana kuwa mzigo huo wa karatasi za kupiga kura ulitokea Afrika Kusini na ulipakiwa kwenye gari la Azam kutoka kwenye gari lililotoka na mzigo kutoka Afrika Kusini.
Taarifa zinasema kuwa lori hilo la Azam linashikiliwa na TRA na mzigo huo umekuwa sealed. Kuna hofu kuwa vigogo wenye njama za kuiba kura wanaweza kujaribu kufuta ushahidi kuhusu kukamatwa kwa karatasi hizi za kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, karatasi hizo za kupiga kura tayari zimewekewa tiki kumchagua Jakaya Kikwete wa CCM na lengo ni kuwa zisambazwe kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini na zihesabiwe kama kura halali.
Tafadhali mwenye taarifa zaidi kutoka mpakani Tunduma atupatie ukweli wa jambo hili
" ........ Wadau huu ni ukweli mtupu magari mawili ya A.A.Bahresa(named Azam on board)T 501AEM na T 263 AJN yako hapa kituo kikuu cha polisi mkoa Mbeya,binafsi nimeona hizo karatasi za kura ambazo JK kapigiwa kura ya ndio na ziko kama karatasi milioni tano kwa haraka haraka hope police watatoa taarifa kamili,wametutoa nje sijui wanazichakachua "
I know the perception.. wanaibaje kura? Mawakala hawahesabu kura!
MKJJ
Siku zote mamuluki hutumia njia nyigi za kuingia madarakani, mojawapo ni kuiba kura.
Uchaguzi wa serikali za mitaa pale Mbagala masanduku ya kura yaliibwa na kufichwa na baada ya wiki mbili yakaonekana yamechimbiwa chini na yalikuwa na kura. Na CCM walishinda hiyo mitaa.
Hivyo basi wizi wa kura upo. Wakijua kuwa eneo hilo uwezekano wa kushindwa ni mkubwa wako tayari kuiba masanduku ya kura. Hivyo basi kulinda kura ni mhimu. Kama wao wenyewe kwenye kura za maoni wameibiana sembuse kwenye uchaguzi huu
kaka yale matokeo huwa yanageuzwa wakati wa kutangaza yaani wana swap zile namba tu basi. na wale mawakala wanakuwa wameshapewa chochote. Umaskini ndilo jambo ambalo linatutesa.
Uwizi upo kwenye kuwarubuni mawakili! kuna jamaa aliniambia ilivyotekea jimbo la Arusha mjini nilitamani nimpige ila basi ndo ilitokea, Anasema kuwa yeye alikuwa ni WAKALA wa chadema, Walipewa laki 3 kwa ajili ya kubadilisha matokeo ya ubunge, na anasema walipokea na matokeo yakabadilishwa. NDO MAANA CHADEMA INATAKIWA WATAFUTE MAWAKALA WAAMINIFU SANA! wasiweke Bora liende!
wizi unatokea pale mtu mwenye authority kama aliyokuwa nayo mwalimu nyerere mwaka 1995 kumshurutisha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya zanzibara kutangaza kitu tofauti na hali halisi; kama ambavyo dtv walikuwa wajumlisha matokeo kutoka vito vyote na cuf kuibuka kidedea.
Hata mwaka huu dalili zinajionyesha kuwa wenye authority watatumia mamlaka waliyo nayo kuishurutisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo according to their wishes. je huu sio wizi wa kura? Kama sio puatie msamiaati wake mpya.
M.M Mwanakijiji,
Nataka kujua yale masanduku yaliyopo kwenye vituo vya kupigia kura nani anahusika kuyalinda na kuhakikisha hayana karatasi ambazo zimeshapigwa TICK?(Nimeyaona kwenye vituo)-Je,ni walewale watumishi wa serekali ambao wananjaa ndio wanapewa jukumu la kulinda?Hapo kuna nini mwanakijiji?
......Endapo hesabu ya idadi ya kura za mgombea zinakosewa kwa malaki halafu taarifa inatoka nani wa kutujulisha kuwa kuna kasoro?nani wa kufuatilia irekebishwe?
......Watu wote tunafika vituoni kupiga kura pamoja na wasimamizi wanaotoka katika vyama vyote,je kuna nafasi ya kukagua masanduku yote ambayo yatatumika kupigia kura ili kujihakiki wenyewe .
......Kama kuna masanduku ambayo yanatoka sehemu nyingine na tukaambiwa yametoka vituo vingine vya kupigia kura nani atakaye hakikisha kuwa ni kura halali?
......Kuhesabu kura siku zote inafanyika usiku na sio mchana kutokana na ukweli kazi huisha jioni sana,sasa kama wanataka kufanya umafya wa wizi wa kura usiku ni mtanzania gani ambaye atakuwa tayari kulinda magari yote yatakayokuwa yanaingia na kutoka vituoni?au ni haohao polisi?
......Hata hivyo njia naziona ni nyingi sana za kupindisha matokeo kirahisi sana.
......Mwanakijiji,nadhani unajaribu kuangalia kwahesabu za haraka haraka ni njia gani ambazo walikuwa wanatumia kupindua matokeo pamoja na njia rahisi ya mtangazaji wa matokeo ambaye hapingwi na kifungu chochote cha sheria endapo anamtangaza mtu hata kama hajashinda lakini anahesabika kashinda.
....Kwa mtazamo wako nina uhakika kwa kipindi hiki watanzania wameungana na watajaribu kwa njia zote hizi kuainisha njia za panya hili serekali iundwe kwa uhalali.
Thanks Mwanakijiji.
Kuna habari zinazunguka hapa mjini Arusha kwamba kuna gari limekamatwa sehemu za Kisongo zenye kura bandia na Wananchi wamelivamia kwa mawe.
Mwenye taarifa zaidi atupe habari!
aah wapi! hata picha moja hamna na wote mnajua matokeo yasiyohojiwa ni yale ya Rais tu, ya wabunge wote na madiwani yanautaratibu maalum. Inanitisha sana kuona watu wanaamini kweli kuwa ni rahisi sana kuiba kura kiasi kwamba sitoshangaa watu wengine wamekata tamaa hata ya kupiga kura kwa sababu wameshajiambia kuwa kura zitaibwa au kutakuwa na uwezekano wa kuiba ili wawatangaze CCM kuwa ni washindi. Hiki ni kisingizio cha kutotaka kushinda.
Tuwahamasishe watu waende kupiga kura kwa wingi kuchagua mgombea tunayemtaka na mabadiliko tunayoyataka. Kama watu wengi wataenda kupiga kura uwezekano wa jambo lolote la kijinga kutokea utakuwa ni mdogo sana. Lakini watu wakiamini kuwa kura zao zitaibwa no matter what.. why vote?