Elections 2010 Kwanini ni vigumu kuiba kura katika Uchaguzi Wetu - Tusitafute visingizio

jamani.. Zinaibwaje? Zamani ilikuwa rahisi kwa sababu sanduku linapakizwa kwenye baskeli kwenda kuhesabiwa sehemu nyingine.. Siyo mnasema "wizi upo" kinadharia inawezekana lakini mtu aniambie unawezekana vipi? Wildcard anasema kuwa zanzibar waliiba ah wapi!, kuna suala la tume ya uchaguzi kuingiliwa hilo limetokea kenya na ninaamini ndilo lenye uwezekano mkubwa wa kutokea tanzania mwaka huu..

wizi unatokea pale mtu mwenye authority kama aliyokuwa nayo mwalimu nyerere mwaka 1995 kumshurutisha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya zanzibara kutangaza kitu tofauti na hali halisi; kama ambavyo dtv walikuwa wajumlisha matokeo kutoka vito vyote na cuf kuibuka kidedea.

Hata mwaka huu dalili zinajionyesha kuwa wenye authority watatumia mamlaka waliyo nayo kuishurutisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo according to their wishes.
je huu sio wizi wa kura? Kama sio puatie msamiaati wake mpya.
 
Jamani siku moja Profesa Lipumba alisema alipopiga kura kwenye kituo fulani alipigia CUF(URAIS,UBUNGE NA UDIWANI)lakini matokeo yalipotoka Mbunge na Diwani hawakupata hata kura moja,sasa tuite hiyo ni nini kama sio wizi?Au mimi sielewi nini maana ya neno WIZI?
Uwizi upo kwenye kuwarubuni mawakili! kuna jamaa aliniambia ilivyotekea jimbo la Arusha mjini nilitamani nimpige ila basi ndo ilitokea, Anasema kuwa yeye alikuwa ni WAKALA wa chadema, Walipewa laki 3 kwa ajili ya kubadilisha matokeo ya ubunge, na anasema walipokea na matokeo yakabadilishwa. NDO MAANA CHADEMA INATAKIWA WATAFUTE MAWAKALA WAAMINIFU SANA! wasiweke Bora liende!
 
habari ndo hiyo:
Taarifa kutoka Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia mkoani Mbeya zinasema kuwa lori la kampuni ya Azam linalomilikiwa na mfanyabiasha maarufu Bakhresa leo hii tarehe 18 Oktoba, 2010, limekamatwa likiwa na shehena kubwa la karatasi za kupigia kura zitakazotumika uchaguzi mkuu Oktoba 31.

Maafisa wa TRA tunduma walishtuka baada ya kukuta karatasi hizo za kupigia kura zimefichwa kwenye shehena ya vipodozi. Inasemekana kuwa mzigo huo wa karatasi za kupiga kura ulitokea Afrika Kusini na ulipakiwa kwenye gari la Azam kutoka kwenye gari lililotoka na mzigo kutoka Afrika Kusini.

Taarifa zinasema kuwa lori hilo la Azam linashikiliwa na TRA na mzigo huo umekuwa sealed. Kuna hofu kuwa vigogo wenye njama za kuiba kura wanaweza kujaribu kufuta ushahidi kuhusu kukamatwa kwa karatasi hizi za kupiga kura.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, karatasi hizo za kupiga kura tayari zimewekewa tiki kumchagua Jakaya Kikwete wa CCM na lengo ni kuwa zisambazwe kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini na zihesabiwe kama kura halali.

Tafadhali mwenye taarifa zaidi kutoka mpakani Tunduma atupatie ukweli wa jambo hili
" ........ Wadau huu ni ukweli mtupu magari mawili ya A.A.Bahresa(named Azam on board)T 501AEM na T 263 AJN yako hapa kituo kikuu cha polisi mkoa Mbeya,binafsi nimeona hizo karatasi za kura ambazo JK kapigiwa kura ya ndio na ziko kama karatasi milioni tano kwa haraka haraka hope police watatoa taarifa kamili,wametutoa nje sijui wanazichakachua "
 
Mzee Mwanakijiji umetoa mchango wako tunashkuru sana
Ila hapa usitarajie (baadhi) ya watu kukuelewa, kwasababu akili zao kwa kipindi hiki ziko likizo, kinachofanya kazi ni UPENZI na sio UBONGO

Natamani ningezisogeza hizo siku iwe kesho tutoke kwenye hii situation
 
I know the perception.. wanaibaje kura? Mawakala hawahesabu kura!

kaka yale matokeo huwa yanageuzwa wakati wa kutangaza yaani wana swap zile namba tu basi. na wale mawakala wanakuwa wameshapewa chochote. Umaskini ndilo jambo ambalo linatutesa.
 
Kama hakuna wizi wa kura mbona hata wao tume ya uchaguzi wa wanalijua na kuwatahadharisha wapiga kura wasiuze shahada zao za kupigia kura! Hao wanaopita mitaani na kunakili shahada za wapiga kura wanafanya hivyo kwa manufaa gani? Kwa hili sitaki kuamini!
 

MKJJ
Siku zote mamuluki hutumia njia nyigi za kuingia madarakani, mojawapo ni kuiba kura.
Uchaguzi wa serikali za mitaa pale Mbagala masanduku ya kura yaliibwa na kufichwa na baada ya wiki mbili yakaonekana yamechimbiwa chini na yalikuwa na kura. Na CCM walishinda hiyo mitaa.

Hivyo basi wizi wa kura upo. Wakijua kuwa eneo hilo uwezekano wa kushindwa ni mkubwa wako tayari kuiba masanduku ya kura. Hivyo basi kulinda kura ni mhimu. Kama wao wenyewe kwenye kura za maoni wameibiana sembuse kwenye uchaguzi huu


aah wapi! hata picha moja hamna na wote mnajua matokeo yasiyohojiwa ni yale ya Rais tu, ya wabunge wote na madiwani yanautaratibu maalum. Inanitisha sana kuona watu wanaamini kweli kuwa ni rahisi sana kuiba kura kiasi kwamba sitoshangaa watu wengine wamekata tamaa hata ya kupiga kura kwa sababu wameshajiambia kuwa kura zitaibwa au kutakuwa na uwezekano wa kuiba ili wawatangaze CCM kuwa ni washindi. Hiki ni kisingizio cha kutotaka kushinda.

Tuwahamasishe watu waende kupiga kura kwa wingi kuchagua mgombea tunayemtaka na mabadiliko tunayoyataka. Kama watu wengi wataenda kupiga kura uwezekano wa jambo lolote la kijinga kutokea utakuwa ni mdogo sana. Lakini watu wakiamini kuwa kura zao zitaibwa no matter what.. why vote?
 
kaka yale matokeo huwa yanageuzwa wakati wa kutangaza yaani wana swap zile namba tu basi. na wale mawakala wanakuwa wameshapewa chochote. Umaskini ndilo jambo ambalo linatutesa.

jamani, matokeo ya kura yakibadilishwa mtu anaweza kwenda kufungua kesi kwani masanduku yale hayatupwi. Kwamba kuna uwezekano wa kuwa na ukiukwaji wa taratibu hilo lawezekana lakini massive rigging sasa hivi nimesema ni "ngumu mno"... Tusiwatishe watu kuwa kura zao zitaibwa. Kura wakapige kwa wingi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya kuzuia uwezekano wa wahalifu kuchakachua upigaji kura.
 
Uwizi upo kwenye kuwarubuni mawakili! kuna jamaa aliniambia ilivyotekea jimbo la Arusha mjini nilitamani nimpige ila basi ndo ilitokea, Anasema kuwa yeye alikuwa ni WAKALA wa chadema, Walipewa laki 3 kwa ajili ya kubadilisha matokeo ya ubunge, na anasema walipokea na matokeo yakabadilishwa. NDO MAANA CHADEMA INATAKIWA WATAFUTE MAWAKALA WAAMINIFU SANA! wasiweke Bora liende!

Kama matokeo yalibadilishwa kwanini Chadema hawakwenda mahakamani ili matokeo yaangaliwe upya? Tena mwaka huu na sheria imebadilishwa ili kuharakisha kesi za uchaguzi. Kuiba kura siyo rahisi hivyo kama kumchomolea mtu stendi!
 
wizi unatokea pale mtu mwenye authority kama aliyokuwa nayo mwalimu nyerere mwaka 1995 kumshurutisha mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya zanzibara kutangaza kitu tofauti na hali halisi; kama ambavyo dtv walikuwa wajumlisha matokeo kutoka vito vyote na cuf kuibuka kidedea.

Hata mwaka huu dalili zinajionyesha kuwa wenye authority watatumia mamlaka waliyo nayo kuishurutisha tume ya uchaguzi kutangaza matokeo according to their wishes.
je huu sio wizi wa kura? Kama sio puatie msamiaati wake mpya.


Kama "wenye authority" watafanya hivyo mnachosema watafanya kwanini watu waende kupiga kura? Kama mawakala wanaweza kuhongwa kirahisi hivyo na kubadilisha matokeo wakati ni kosa la jinai kwanini watu waende kupiga kura. Maana kila ninapowasoma ninaona kuwa ni hopeless case kwenda kupiga kura:

a. NEC watamtangaza wanayemtaka
b. Kura zitaongezwa kwa wagombea wa CCM vituoni
c. Mawakal wa vyama watakatiwa kitu kidogo ili wachakachue kura
d. Kura hazitolindwa vizuri.


Kama yote a - d yana ukweli (hasa ukisoma sentiments za watu hapa), ni wazi kuwa mpiga kura wa Tanzania hana sababu ya kwenda kupiga kura. Hiki ni kisingizio cha kuwapatia ushindi CCM kirahisi, na miye nina hofu wanaokieneza wana lengo hilo kabisa.. KUWAKATISHA TAMAA WAPIGA KURA WA UPINZANI WASIPIGE KURA KWANI KURA ZAO ZITAIBWA! CCM wanajua hili. Ni lazima tukatake.. KURA HAZIIBWI NA KILA MTU AKAPIGE KURA YAKE!!!! LETS CHANGE THE MESSAGE!
 
M.M Mwanakijiji,
Nataka kujua yale masanduku yaliyopo kwenye vituo vya kupigia kura nani anahusika kuyalinda na kuhakikisha hayana karatasi ambazo zimeshapigwa TICK?(Nimeyaona kwenye vituo)-Je,ni walewale watumishi wa serekali ambao wananjaa ndio wanapewa jukumu la kulinda?Hapo kuna nini mwanakijiji?

Nimeshalijibu hilo soma article hapo juu
......Endapo hesabu ya idadi ya kura za mgombea zinakosewa kwa malaki halafu taarifa inatoka nani wa kutujulisha kuwa kuna kasoro?nani wa kufuatilia irekebishwe?

Utaratibu upo.. soma article.. au sheria... wale wasimamizi hawajifanyii mambo kutoka katika mawazo yao.

......Watu wote tunafika vituoni kupiga kura pamoja na wasimamizi wanaotoka katika vyama vyote,je kuna nafasi ya kukagua masanduku yote ambayo yatatumika kupigia kura ili kujihakiki wenyewe .

soma article nimejibu hilo mweh!

......Kama kuna masanduku ambayo yanatoka sehemu nyingine na tukaambiwa yametoka vituo vingine vya kupigia kura nani atakaye hakikisha kuwa ni kura halali?

Hakuna masanduku yanayohama kituo cha kura au kuingia kituo cha kura, na kama kuna haja ya nyongeza kuna utaratibu ulio wazi kabisa wa kusimamia hilo. Soma article.
......Kuhesabu kura siku zote inafanyika usiku na sio mchana kutokana na ukweli kazi huisha jioni sana,sasa kama wanataka kufanya umafya wa wizi wa kura usiku ni mtanzania gani ambaye atakuwa tayari kulinda magari yote yatakayokuwa yanaingia na kutoka vituoni?au ni haohao polisi?
......Hata hivyo njia naziona ni nyingi sana za kupindisha matokeo kirahisi sana.

Hii yote ni shuku, kama hujui ni kuwa kura zikianza kuhesabiwa hatoki au kuingia mtu kituoni hadi matokeo yatangazwe!
......Mwanakijiji,nadhani unajaribu kuangalia kwahesabu za haraka haraka ni njia gani ambazo walikuwa wanatumia kupindua matokeo pamoja na njia rahisi ya mtangazaji wa matokeo ambaye hapingwi na kifungu chochote cha sheria endapo anamtangaza mtu hata kama hajashinda lakini anahesabika kashinda.

Basi hakuna haja ya kupiga kura!

....Kwa mtazamo wako nina uhakika kwa kipindi hiki watanzania wameungana na watajaribu kwa njia zote hizi kuainisha njia za panya hili serekali iundwe kwa uhalali.
Thanks Mwanakijiji.

ur welcome
 
Kuna habari zinazunguka hapa mjini Arusha kwamba kuna gari limekamatwa sehemu za Kisongo zenye kura bandia na Wananchi wamelivamia kwa mawe.

Mwenye taarifa zaidi atupe habari!
 
Kuna habari zinazunguka hapa mjini Arusha kwamba kuna gari limekamatwa sehemu za Kisongo zenye kura bandia na Wananchi wamelivamia kwa mawe.

Mwenye taarifa zaidi atupe habari!

Your signature is a symbol of hatred.
 
MMM,

Nakubaliana na wewe kwamba kwenye kelele zote za kuibwa kura sijawahi kusikia unatia timu huko! Binafsi sijawahi kufikiri kura zinaibwa kumbe siko mwenyewe.
Lakini nakubaliana nawe kwamba uchaguzi ukivurugwa yes. ndio maana siungani na watu wanazungumzia sana vyombo vya ulinzi maana ukivizungumzia sana... ndio vitakuwa deployed and that will be even worse.
 
Mwanakijiji tupo pamoja. hili la kuiba kura ni kutafuta visingizio tu, lakini cha msingi hapa wagombea watafute mbinu mbalimbali za kuomba kura na pia kuwashawishi watu wafike vituoni na kupiga kura period. mtu akipata kura nyingi haziwezi kuibwa/kubadilishwa
Tatizo tulilonalo sasahivi ni ku judge matokeo kwa kuangalia watu wanaohudhuria mikutano sasa hivi lakini lazima tujue kuwa katika hao wapo wasiojiandikisha, wapo ambao hawatapiga kura, wapo na mashabiki wa vyama vingine (hawabadiliki), nk nk.
 
aah wapi! hata picha moja hamna na wote mnajua matokeo yasiyohojiwa ni yale ya Rais tu, ya wabunge wote na madiwani yanautaratibu maalum. Inanitisha sana kuona watu wanaamini kweli kuwa ni rahisi sana kuiba kura kiasi kwamba sitoshangaa watu wengine wamekata tamaa hata ya kupiga kura kwa sababu wameshajiambia kuwa kura zitaibwa au kutakuwa na uwezekano wa kuiba ili wawatangaze CCM kuwa ni washindi. Hiki ni kisingizio cha kutotaka kushinda.

Tuwahamasishe watu waende kupiga kura kwa wingi kuchagua mgombea tunayemtaka na mabadiliko tunayoyataka. Kama watu wengi wataenda kupiga kura uwezekano wa jambo lolote la kijinga kutokea utakuwa ni mdogo sana. Lakini watu wakiamini kuwa kura zao zitaibwa no matter what.. why vote?

MMJ, Hapo kwenye red ni ukweli kabisa watu baadhi naskia wakisema hawatapiga kura kwa ajili hiyo au wengine wanatamani kupigia upinzani lkn wanahofia kupoteza kura kwa kile wanachokiamini CCM kuiba kura! imani inaathiri maamuzi ya walio wengi!
 
MMM,

Naomba u-evaluate response za watu kwenye hii post yako... ndio utajua kwamba Tanzania elimu ya uraia (au elimu ya kupiga kura iko chini sana)... Cha kusikitisha sana tena sana... Mgombea Urais mmoja kuji-involve kwenye upuuzi kama huu....

We have a long way to go kaka:mmph:
 
Mkuu Mwanakijiji, kwa utaratibu uliouleza katika makala yako, kinadharia nakubaliana na wewe kwamba hakutakuwa na wizi wa kura.

Hata hivyo, uzoefu unaonyesha kwamba wizi haufanyiki kabisa maeneo ambayo yana upinzani wa kutosha, bali hufanyika kule ambako hakuna upinzania kabisa kwa kuhakikisha chama tawala wanapata 100% ya kura kutoka maeneo hayo. Maeneo yenye upinzani haki itatendeka na mtagawana hizo kura lakini kule ambapo upinzani ni dhaifu sana, wenzenu wana-maximize kura za huko na majumuisho yanakuja chama tawala wakiwa mbele.

Hebu fikiria; nini kitatokea katika yale majimbo 21 na kata karibia 500 ambayo wagombea wa chama tawala wamepita bila kupingwa? hii in maana kura zote a uraisi zitaishia kwao vilevile. Nakumbuka mwaka 2005; tena hii ilikuwa Dar es Salaam, baadhi ya vituo mawakala wa vyama vya upinzani hawakupewa kitu zaidi ya 'lunch box' na mawakala wa chama tawala na wakaishia kusaini fomu za matokeo bila hata kuhakiki hizo kura.

Matokeo ya mwaka huu yawazindue viongozi wote wa mageuzi ili walipe umuhimu suala la kujenga matandao wa matawi mikoanai na vijijini. Sidhani kama tungekuwa na wasiwasi huu kama upinzani ungekuwa na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa kutosha.
Kama mageuzi yatashindwa, tutakuwa tunalipa dhambi ya kutomsikiliza Chacha Wangwe (RIP)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom