Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Kilchofanyika Tarime tunakijua; watu wa kule ni jasiri sana kiasi kwamba hawaogopi hayo maji ya upupu na hata wakiamua risasi hawaiogopi pia. Tunajua watu walivyoumizana na walivyokuwa tayari kuumia ili mradi wapate haki yao - damu ilimwagika kule!. Wadanganyika wengi hatuko hivyo ndiyo maana mtu akisema tulinde kura zetu hata kama ikibidi 'kumwaga damu', anaonekana mtu wa ajabu. Kweli hatutaki damu imwagike, kwa hiyo hatutaki kilichotokea Tarime kitokee Tanzania nzima. Kwa zitto nako watu ni ngangari sana ila sikumbuki wao walifanyaje.naomba tuchukue muda kumwelewa mwanakijiji, anauliza mbona kila mara moshi mjini cc, wanashindwa kuiba kura? Mbona kwa zitto walishindwa? Mbona tarime walishindwa. Kilichofanyika huko mwaka 2005 na katika uchaguzi mdogo ndicho kinachotakiwa kufanyika mwaka 2010 na hoja ya kura kuibiwa itashindwa kufanya kazi. Hebu tujiulize ni nini kilfanyika katika majimbo hayo ambayo chadema ilipata ushindi?
Ninachojua, hasa kwa kura za ubunge, tofauti ikiwa ndogo ni rahisi kuiba lakini tofauti ikiwa kubwa sana inakuwa vigumu kuiba kwani inabidi wabadilishe masanduku mengi sana. Kwa upande wa Moshi, uelewa wa kule ni mkubwa kuliko sehemu nyingi Tanzania; wanajitokeza wengi kupiga kura na kule umaskini si mkubwa sana hivyo hawanunuliki kirahisi. Kwa mfano huwezi kununua shahada kule kwa shs 1000 kama inavyofanyika karagwe!
Sehemu nyingine CCM wanakuwa hawajui kama watashindwa na hivyo wanaacha 'kujiandaa', matokeo yanakuja kama surprise kama ilivyotokea kwa Kaunda. Kwa mfano katika uchaguzi wa 2005 ilionekana kuwa Chadema ingepata viti zaidi ya 40, lakini haikuwezekana kwani mbinu za kuiba kura, kuwanunua wapiga kura, nk zilifanyika katika maeneo yote waliyotabiriwa kushindwa na unajua Chadema waliambulia viti vingapi! Kwa ujumla ni mkusanyiko wa mambo mengi mpaka uone CCM imekubali kushindwa. Kuna nguvu ya Dola pia - kumbuka ya Bukoba mjini, ya Biharamulo (uchaguzi mdogo) nk