Elections 2010 Kwanini ni vigumu kuiba kura katika Uchaguzi Wetu - Tusitafute visingizio

Mwanakijiji;

Mwaka 1995 kulingana na takwimu za mawakala wa CUF kule ZNZ ilionyesha kuwa Maalim Seif kashinda kwa asilimia kubwa dhidi ya incumbent Dr Salmin Amour lkn matangazo ya ZEC yalimpa ushindi Dr Salmi kwa aslimia 50.1 dhidi ya 49.9 za CUF!

CUF walienda hata kwenye jumuia za kimataifa kuomba warudie tena kujumlisha matokeo ya kura ya vituo vya uchaguzi lkn ZEC ikasisitiza tena na tena kuwa matokeo waliyotangaza ni halali na hawatarudia tena kujumlisha matokeo;machafuko yaliyotokea hapo baadae hamna asiyeyajua!

Wasi wasi wangu ni kuwa hata kama Dr Slaa atashinda,na hata kama mawakala wa CHADEMA watafanya kazi nzuri sana ya kuwa makini kwenye vituo vya kura,lkn je kama NEC ikatangaza matokeo jinsi wanavyotaka wao na kwa hiki kipengele kinachosema NEC haipingwi popote pale tutafanya nini?

Malafyale.. hilo tatizo halipo mwaka huu; matokeo yanatangazwa kila kituo na kila jimbo linatangaza rasmi.. hakuna haya ya takwimu za mawakala! Na as a matter of fact.. mawakala hawahesabu kura wao wanaangalia tu, sasa hawa mawakala wa Zanzibar walileta namba zao wote wakazijumlisha na zikapingana na zile za Tume ya Uchaguzi? How realiable was their tally?
 
mimi naungana na mwanakijiji, tusipige mavuvuzela kusubili kura ambazo hazipo, kipindi hiki cha lala salama, chadema inahitaji kuoresha mbinu za kimkakati, kwani ccm isipoangushwa mwaka huu, ndio basi tena itachukuwa miaka mingi ijayo kuipata ccm dhaifu kama hii ya leo. zanzibar ni ngome ya cuf, je kuna jitihada gani zinafanyika angalau chadema ipate robo ya kura za zanzibar? ukweli mwingine mchungu kuusema nimeuona, kwa ngazi za chini chadema ina wapenzi na mashabiki wengi ambao kwao uwanachama sio lazima ila wanaiunga mkono chadema kama mkombozi wao, lakini mtandao wa kiuongozi uko dhaifu kiasi fulani, pili rasilimali fedha ndio tatizo kubwa, chadema taifa inagharamia kampeni za mgombea urais, kuna wagombea udiwani ambao mpaka sasa wamefanya mkutano mmoja tu wa hadhala. lets do something.:A S thumbs_up:
 
Mwnaakijiji wizi wa kura upo wa namna nyingi.
Moja: zinaandaliwa karatasi nyingine za kupigia kura ambazo tayari zina tick kwa mgombea ambaye anatakiwa kushinda then wakati wa kuhesabu zinafanyiwa exchange na zile karatasi ambazo zina tick kwa mgombea mwingine 'wasiye mtaka'.


Hilo haliwezekani.. zinafanyiwa "exchange" wapi sasa? Chumba mnaingia toka asubuhi mpo humo, mtu hawezi kuingia hivi hivi tu kwenye kituo. Sasa makaratasi yanafichwa wapi kabla hayawa exchanged.. hivyo mnajua ukaguzi unaofanyika kabla ya kuingia ndani.. kwanza kabisa (na nilisahau) kabla hata ya kuangalia masanduku mnaruhusiwa kutembea kwenye kila chumbahadi darini mkitaka kuhakikisha the kituo is absolutely clean!

Namna nyingine ni kutumia ubabe kama uliotumika 1995 kule Zanzibar.
kashinda Seif lakini anatangazwa Salmin Amour na hakuna wa kuingilia kati.

Hili ni suala la NEC na siyo suala la kuiba kura!.. Wapinzani wameingia kwenye ucahguzi wakijua kabisa kuwa matokeo ya kura ya Urais yakitangazwa hayawezi kuhojiwa mahali popote. Ni sheria waliijua na walikubali kucheza nayo; wapinzani bara hawakuonesha wanataka tume huru kwani wameshiriki katika chaguzi mbalimbali zilizoendeshwa na tume hiyo hiyo na hiyo kuonesha kuikubali. So.. mkiniuliza mimi, hakuna kisingizio.. wao watumie mbinu twende tushinde hakuna kulilia kura zisizoibwa!
 
Da! Mwnakijiji nikikumbuka kipindi kile ulivyoitetea CCJ, nikijumlisha na hoja yako hii ya leo ya kusema hakuna wizi wa kura,
Nachoka kabisaa.
 
Malafyale.. hilo tatizo halipo mwaka huu; matokeo yanatangazwa kila kituo na kila jimbo linatangaza rasmi.. hakuna haya ya takwimu za mawakala! Na as a matter of fact.. mawakala hawahesabu kura wao wanaangalia tu, sasa hawa mawakala wa Zanzibar walileta namba zao wote wakazijumlisha na zikapingana na zile za Tume ya Uchaguzi? How realiable was their tally?

MKuu unakumbuka kilichotokea Kenya? Jamaa walivyoona matokeo kutoka vituoni sio mazuri wakamwita Kivuitu upesi upesi atangaze matokeo.....
 
Da! Mwnakijiji nikikumbuka kipindi kile ulivyoitetea CCJ, nikijumlisha na hoja yako hii ya leo ya kusema hakuna wizi wa kura,
Nachoka kabisaa.

mmh.. jamani mnataka wote tuanze kuimba "kuna wizi wa kura" wakati kiakili haikubaliki hata kivitendo? Hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kuonesha kura zinavyoibwa ambaye siwezi kuonesha ni kwa jinsi gani hilo atakalopendekeza haliwezekani. Nimeweka ushahidi wa kiakiil kuwa kama kuna maeneo CCM wangeweza kweli kuiba kura na walikuwa na sababu ya kufanya hivyo ni Moshi Mjini na Karatu.. kwanini hawakuiba?

Anayejua kura zinaweza kuibwa Tanzania kituoni aseme basi nimsikilize.. I'm open minded. Ila tusiwatafutie watu kisingizio.. Ushindi na kushindwa katika hili uko mikononi mwa Chadema na miye nawasupport kwa asilimia 100 kushinda lakini siyo kwa kulilia "tutaibiwa kura". Ushindi utakuja kwa kupata kura nyingi Period! Now.. go and get them! washawishi watu wapige kura, wasihi watu waichague Chadema n.k lakini hilo la wizi ... miye kwa kweli simo..
 
MKuu unakumbuka kilichotokea Kenya? Jamaa walivyoona matokeo kutoka vituoni sio mazuri wakamwita Kivuitu upesi upesi atangaze matokeo.....


mbona nimesema hilo.. kuwa kinachoweza kutokea ni NEC huko lakini siyo kuiba kura.. hayo ya NEC nimeshayazungumzia kwa upande mwingine.. Sitaki watu wahofie kupiga kura kuichagua Chadema kwa sababu ati kura zao zitaibwa na CCM watashinda tu.. inakuwa ni kama negative reinforcement..
 
Kuna namna kuu tatu zimeshajitokeza hapa Tanzania za uibaji wa kura:
1. Tume za Uchaguzi kulazimishwa kutangaza matokeo ambayo si halali.
2. Wapiga kura wasiojua kusoma na kuandika kubambikiwa kura.
3. Masanduku bandia ya kura kubadilishwa na masanduku halali
Mara hii idadi ya WATANZANIA wasiojua kusoma wala kuandika imeongezeka sana.
 
Pole sana Mzee Mwanakijiji. Wizi wa kura upo. Umesahau chaguzi zilizopita mgombea mmoja alienda kupiga kura kwenye kituo lakini matokeo yalipotangazwa ikaonekana hajapata hata kura moja. Ina maana yeye mwenyewe na familia yake, ndugu zake na marafiki zake hawakumpa kura! Mwanakijiji athari za umaskini zinajidhihirisha katika mambo mengi. Mojawapo ni kuwarubuni mawakala wenye "njaa" ili kubadili tarakimu.
 
Kuiba kura kupo, hata ukiwasikiliza ccm wanasema kabisa jimbo fulani hatushindi mpaka tuibe kura, Pia hata mawakala wenyewe wanasema wameshiriki kuchakachua. hii yote inategemea na wakala mwaminifu tu. kama wanaweza kuwahonga wapiga kura watashindwa nini kuwahonga wasimamizi ambao kwa idadi ni wachache! ndio maana kama yutakumbuka chaguzi za mwaka 1995 majimbo mengi yaliwekewa mapingamizi na uchaguzi uliporudiwa wenye haki walishinda. ile sheria baadaye ilipitishwa ya kulipa kiasi kikubwa cha pesa ndio ilichangia watu kutoweka pingamizi kwa chaguzi za hivi karibuni, sikumbuki sheria ilitungwa lini.
 
mbona nimesema hilo.. kuwa kinachoweza kutokea ni NEC huko lakini siyo kuiba kura.. hayo ya NEC nimeshayazungumzia kwa upande mwingine.. Sitaki watu wahofie kupiga kura kuichagua Chadema kwa sababu ati kura zao zitaibwa na CCM watashinda tu.. inakuwa ni kama negative reinforcement..
Pengine mwenzetu haujapiga kura au kuangalia mchakato mzima wa kupiga kura, kuzihesabu na matokeo kutangazwa kwa muda mrefu. Sisi wengine tumeyashuhudia haya tangu mwaka 1975. Tuna mengi tumeyaona. Itoshe tu kusema CCM haiko tayari kuondoka madarakani.
 
Ndugu yangu Mwanakijiji katika makala ambayo imekutoa kwenye chati ni hii. Maoni yako wala siyo ya kitaalamu hata chembe.

Hebu tuangalie baadhi ya hoja zako kwa kifupi tu...................Kwanza umejijibu mwenyewe kuwa wizi wa kura yawezekana sasa maandishi mengi ni ya nini?

Lakini, kura zaweza kuchezewa lakini ili zichezewe kunahitaji ushirika wa zaidi ya mtu mmoja. Yaani, msimamizi wa kituo, wawakilishi wa wagombea, waangalizi wa ndani na wa nje na vile vile wapiga kura wenyewe.
Kinachofanyika na ambacho huwa kinafanyika ni kuwanunua mawakala wa vyama vya upinzani jambo ambalo ndilo liliigharimu Chadema karibu viti vyote vya Tukuyu na vinginevyo wakati wa By-elections isipokuwa jimbo la Tarime. Kwa hiyo hoja yako hii hapa chini siyo ya kweli hata kidogo:-

Siyo hapo tu, kama kweli Kura zingekuwa zinaibwa kirahisi hivyo, kwanini wameshindwa kuiba kura Pemba ambapo CUF imeendelea kutesa kwa miaka 15 sasa tangu mfumo wa vyama vingi uende na kwanini kura za Jimbo la Darajani (ambalo nadhani sasa limegawanywa - niko tayari kusahihishwa) haziibwi na matokeo yake zinakuwa za karibu sana?

Kama CCM iliweza kuwarubuni wagombea wa vyama vya upinzani kuwapelekea fomu walizozichukua kugombea ubunge na udiwani kwa malipo yanayosadikiwa kati ya Tshs 20-50milioni kwa ubunge na Tshs 0.5 hadi 2 milioni kwa udiwani watashindwa kuwarubuni mawakala ambao wengi wao ni njaa tupu?

Kuhusu kuwa na mawakala vituo vyote wala siyo suluhisho kwa sababu kama mawakala siyo waaminifu watarubuniwa tu.

Baada ya mawakala kurubuniwa watasaini matokeo ambayo hayashahibiani na hesabu za kura na yule ambaye hastahili atakuwa amechaguliwa kuwa kiongozi haramu.

Kuhusu kutokuwepo hukumu kwenye mahakama zetu kuhusiana na matokeo ya kura kuchakachuliwa ulioiibua kwenye mada yako:-
Ipo imani ambayo imejengeka kuwa ni rahisi kwa kikundi cha watu au watu kuiba kura na kumuongezea mtu mwingine kura kinyume cha sheria. Watu wenye imani hii (naiita imani kwani hakuna ushahidi wowote kuwa kura zimewahi kuibwa, yaani ushahidi unaoweza kusimama Mahakamani!) huwa na wasiwasi kuwa uchaguzi unapofanyika basi kuna makundi ya watu ambayo yanakula njama kuiba kura na kubadilisha matokeo.


Tatizo la hii hoja yako ni kuwa si maeneo yote yenye kero za wizi wa kura mahakama ilikwisha kuyapokea na kuyayafanyia kazi na hivyo kumaanisha ya kuwa mahakama hapa haitusaidii sana kuelewa sakata hili. Mahakama hushughulikia hoja zilizopo machoni pake na kamwe haishughulikii hoja ambazo hazijalalamikiwa. Kwa lugha nyingine ili upate uhimili wa kimahakama katika hoja zako inabidi uthibitishe ya kuwa maeneo ambayo tunahofu ya kura kuibiwa yalikwisha kushughulikiwa na mahakama zetu kupitia malalamiko kadha wa kadha ambayo ungeliyataja.

Labda kuongeza ufahamu wetu kwenye hilo ningependa kutoa mfano wa jimbo la uchaguzi la Starehe nchini Kenya. Jimbo hilo aliyeshinda mwaka 2007 alikuwa ni Askofu Magreth Wanjiru wa ODM lakini mpinzani wake Bw. Kamana wa PNU alikwenda Mahakamani kubisha ya kuwa matokeo yaliyotangazwa hayakuheshimu kura zilizopigwa na akaomba uhesabuji wa kura urudiwe. Hili ombi mahakama zetu hazijawahi kulisikiliza na kwa hiyo huwezi ukasema ya kuwa hakuna uchakachuaji wa kura kwa vile mahakama hazijathibitisha. Mahakama haziwezi kuthibitisha mambo ambayo hayajalalamikiwa.

Mahakama kuu ya Kenya iliagiza "recount" na matoeko yake Kamana Maina akaonekana kumbe ndiye aliyepaswa kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa ni mshindi lakini asiyestahili ndiye aliyetangazwa mshindi yaani Askofu Magreth Wanjiru. Huyu Askofu alikwenda kuwa Naibu Waziri wakati ni kihiyo tu. Hii ndiyo hali halisi ya chaguzi zetu na ndiyo maana viongozi tulionao ni wabovu na wala siyo wananchi hawajui kuchagua viongozi wazuri ila mfumo uliopo unaruhusu uchakachuaji wa matakwa ya wananchi.

Wizi wa kura wa kutoheshimu matokeo ndiyo ulio mkubwa hapa nchini na hata hapa Arusha ninaamini ya kuwa Bw. Lema alimshinda wa CCM aitawaye Felix Mrema jimbo hili mwaka 2005 na endapo kura zingelirudiwa kuhesabiwa kingelikuwepo kilio na kusagaga meno kwa CCM. Lakini Bw. Lema hakwenda mahakamani kwa sababu ambazo zipo nje ya mada hii, hivyo sitazijadili.

Wizi wa pili ambao safari hii huenda ukatumika ni kumwongezea mgombea kura na hili wasiwasi umeongezeka kutokana na NEC kutuzuia wapigakura kulinda kura zetu tukiwa mita 200 kutoka kwenye vituo vyetu vya kupiga kura!!!!!! Wanasema twende nyumbani na tutajulishwa matokeo tu. Sasa tutajuaje ya kuwa baada ya sote kuondoka mawakala na wasimamizi wakashirikiana kubadilisha kura ndani ya maboksi ya kura ili kumbeba mgombea ambaye tayari ameshindwa uchaguzi? Hata ukienda mahakamani na maboksi yaliyochakachuliwa bado utajikuta umeshindwa tu.

Hili linawezekana kwa sababu NEC haina watumishi wa kudumu na inategemea watumishi wa umma kutoka serikali za mitaa. Tumeona jinsi wakurugenzi wanaotenda haki kama yule wa hapa Arusha Bw. Mbuya CCM imembughudhi kwa kutofanya yale ambayo wao wanataka. Sasa itakapokuja kuchakachua matokeo kwa kubadilisha kura ndani ya maboksi ya kura tuwategemee hawa makuhani wa CCM kutenda haki jamani? Let us be fair and reasonable on this...........

Mwisho kauli yako hii ya kutubeza wale wenye hofu na kuchakachuliwa matokeo kuwa hatujui utaratibu wa upigaji kura hapa nchini zinakera kwa sababu kwanza hutujui lakini umekuwa mwepesi sana kutuhukumu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kweli hili limenishangaza sana na kunisikitisha mno........ We are doing this for ourselves but for the benefi of our posterity and nothing less......Tungeweza kunyamaza na kusema watajijua kwani ugali mezani si upo lakini kama una kiona mbali lakini hukitumii kwa manufaa ya wenzio hata kama wewe hupati kitu machoni pa Mwenyezi Mungu wamchukiza.....Ndiyo maana tunajitolea kuelimisha umma ambao ndiyo ulitugharimia sana kuipata elimu hii.......................Kwa siku zijazo kauli kama hii uitafakari kabla ya kuitoa.....


Ukweli ni kuwa wenye hofu hii ya "wizi wa kura" ni kwamba hawajui upigaji kura wetu ulivyo na kwanini hatua zilizochukuliwa mwaka huu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitachangia sana kuondoa wasiwasi wa wizi wa kura. Bahati nzuri nina uzoefu wa kushiriki kama mwangalizi wa Uchaguzi Mkuu katika mojawapo ya chaguzi zetu nchini na kuweza kutembelea maeneo ya Shinyanga, Mwanza na Musoma wakati wa kampeni na wakati wa Uchaguzi kuweza kutembelea vituo vya uchaguzi zaidi ya hamsini vya Mwanza. Nimeshiriki toka kituo kinafunguliwa hadi kura zinamalizwa kuhesabiwa. Kwa hiyo, siandiki kinadharia bali kwa uhakika wa ushuhuda wangu mwenyewe ambao nina uhakika unaweza kurudiwa na mtu mwingine yoyote aliyepata nafasi kama yangu.
hayo maeneo machache ambaye vyama vya upinzani vimefanya vizuri ni kuwa vina mtandao mkubwa wa kulinda matokeo yao na wapiga kura walikuwa hawazuiwi kuwa mita 200 nje ya vituo vya kupiga kura kama itakavyokuwa safari hii.

Uchaguzi lazima uthibitiwe na wapiga kura siyo wasimamizi, mawakala au waangalizi ambao huwa na ajenda zao za siri. Nitakupa mfano mwingine chaguzi ya Zimbabwe haikuwa ya huru wala haki lakini SADC, EAC na AU walidai chaguzi ile ilikuwa ni huru na haki.....Waangalizi hawa walirudia upuuzi huu kule Kenya.......................
 
Mwanakijiji Heshima yako mkuu
Mimi naweza kutoa mfano wangu mwenyewe katika uchaguzi uliofanyika 2005. Nilipiga kura katika kituo kimoja hapa Arusha, kura yangu nilipeleka upinzani (Yaani Rais, Mbunge na Diwani). Cha ajabu kesho yake kwenye kituo kile Upinzani uliambulia sifuri. lakini si mimi tu niliyestaajabu niliyoyaona bali kuna watu wengine pia. siwezi kuwasemea hao maana kura ni siri ya mtu. Lakini mimi nathibitisha pasi shaka kwamba kura yangu ilienda upinzani na ilichakachuliwa.

Mzee MMJ, Mbinu inayotumika ni kucheza na mawakala, hii ndiyo mbinu kubwa sana inayotumika kuchakachua (si kuiba) matokeo. na ndiyo maana wengi humu tunajaribu kuviasa vyama vya upinzani kuhakikisha vinapata mawakala wazalendo ambao hawako tayari kununuliwa. maana wakala akisha kusaini ile fomu ya matokeo hakuna ujanja tena.

Vyama vya upinzani (Hasa Chadema na CUF) lazima vihakikishe vinapata mawakala waaminifu kabisa ili kuepusha kubadilisha matokeo kwenye vituo.
 
mbona nimesema hilo.. kuwa kinachoweza kutokea ni NEC huko lakini siyo kuiba kura.. hayo ya NEC nimeshayazungumzia kwa upande mwingine.. Sitaki watu wahofie kupiga kura kuichagua Chadema kwa sababu ati kura zao zitaibwa na CCM watashinda tu.. inakuwa ni kama negative reinforcement..

Uko sawa mkuu kwamba watu wasiwe na hofu ya kupiga kura, lakini mwisho wa siku wizi ni wizi tu whether ni kupitia vituoni au NEC....
 
Kaka nashukuru sana kwa maelezo yako mazuri na mapana kuhusu topic husika, kwangu mimi ningependa tuu niungane na wenzangu kwamba suala la wizi wa kura lipo na limelipotiwa mara nyingi katika chaguzi za nyuma na "PRECEDENT" ya hayo yapo mfano katika shauri la maombi ya uchanguzi katika ya Dr. Fortunatus Lwanyatika Masha Vs Dr. William Ferdinard Shija suala wizi wa kura lilikuwa ni moja ya masuala yaliyoletwa mbele ya Mahakama na ikadhibitika kweli wizi ulikuwepo. Ni imani yangu ya kuwa unaweza kubaliana na mie kuhusu hayo iwapo tu utakuwa tayari fanya mapitio ya baadhi ya kesi za uchaguzi.

Asante.
 
CCM sio lazima waibe kura munaweza kuhisabu kama kawaida lakini mshindi akatangazwa Kikwete La pili siku ya kupiga kura majina yote ya wapiga kura wa upinzani yanaondolewa kwenye list na kama jina lako halimo kwenye list ndio hata kukaribia huruhusiwi kwenye kituwo la tatu teknolijia ya KICHINA unatia tick kwenye picha ya Lipumba lakini kwandani zote ni picha za kikwete.
 
MMKJJ anatuchanganya tu hapa, na I doint know why. Unless hatumuelewi ana maana gani na neno "kuiba". Mimi nadhani njia yoyote itimikayo na mamlaka husika (kwa kusaidiana na wadau wengine) katika kumnyima mgombea ushindi ni 'kuiba' kura.

Hujuma katika process hii haianzii siku ya kupiga kura tu -- inaanzia nyuma zaidi -- hususan katika zoezi la uandikishaji n.k.

Pili MMKJJ atueleze kule jimbo la Florida katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2000 kulitokea nini? Mamlaka husika (ya jimbo hilo) haikumwibia kura Al Gore? Kila wakirudia kuhesabu, difference ya ushindi wa Bush katika jimbo hilo ilikuwa inazidi kupungua -- kuanzia zaidi ya kura 10,000 mwanzoni mwa zoezi la kurudia kuhesabu hadi kufikia kura 537 wakati Supreme Court ilipositisha zoezi na hivyo kumpa ushindi Bush. Kumbuka Decision ya Supreme Court ilikuwa ni 5-4 in favour of Bush.
 
Back
Top Bottom