Kwanini ni rahisi kujua mke akichepuka?

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,794
2,000
KWA NINI NI RAHISI MWANAMKE KUGUNDULIKA ATOKAPO NJE YA NDOA?

Hakika mwanamke ni rahisi sana kugundulika endapo anatoka nje ya ndoa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamke aishi na mwanamme mmoja tu, na hakumpa kabisa uwezo wa kuonyesha mapenzi kwa watu wawili tofauti kwa kiwango sawa, hivyo mwanamke akiamuwa kutoka nje ya ndoa ni muda mchache mumewe hugundua na kama mume ni mjanja kidogo tu, basi anaweza kumgundua mke wake siku ya kwanza anayopata mwanamme mwengine nje ya ndoa. Inawezekana zipo sababu za ziada zinazowafanya wanawake kugundulika kiurahisi pindi atokapo nje ya ndoa yake, lakini mimi nitazionyesha sababu tatu pekee, ambazo kwangu mimi hizo ndizo kuu, na nyenginezo zilizopo nitawaachia ukumbi wengine na wao waziorodheshe kwa mujibu wa uzoefu wao.

Kwanza, ni ‘Jaala’ ya Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ameiumba nafsi ya mwanamke ipende mwanamme mmoja kwa wakati mmoja, halikadhalika ameuumba mwili wa mwanamke umridhishe na kumburudisha mwanamme mmoja. Kisheria, hakuna rukhsa ya kidini mwanamke aliyoamriwa kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, kwa sababu moyo wake hauwezi kugawika kupenda zaidi ya mmoja na akaonyesha uwiano sawa, ingawa hali hii pia hutokea kwa wanaume wenye wake zaidi ya mmoja. Lakini wanaume angalau wamepewa uwezo wa kuficha mapenzi yao, hivyo kitu hicho huwasaidia. Hivyo mwanamke akichepuka lazima adharau kumoja apende kwa dhati kwengine, sasa kwa kitendo hicho ndio maana huwa ni rahisi kugundulika, kadhalika endapo akiutumia mwili wake kuburudisha mchepuko wake basi maumbile yake hayatakaa kimya, yatamshitaki tu kwa mumewe ikiwa mume huyo si ‘mume bwege’.

Pili, mwanamke ni mtu wa fakhari ya mapenzi, maana yake nini? Hii ina maana mwanamke siku zote hutaka kuona yeye ndiye anaependa zaidi kuliko mwenza wake, iwe kwa kutamka, ishara na hata kwa vitendo, hivyo hata kama itakuwa wako mbali mbali na mchepuko wake, yeye hupenda wawe wanawasiliana kila wakati, hasa kwa zile siku za awali za mahusiano, sasa hapa ndipo mara jungu hulikoroga kwa kujisahau kwamba pale alipo amemilikiwa na kuanza huonyesha ishara kwa mchepuko wake bila kuzingatia kwamba labda mumewe atagundua, aidha humuacha mumewe chumbani yeye akabaki sebuleni kwa kisingizio cha kuangalia TV, huku akichati na huo mchepuko wake au hata kumpigia simu kuzungumza nae, na huu ni udhaifu maalum wa kimaumbile ambao Mwenyezi Mungu amewaumbia wanawake na maisha hawataweza kubadili hili.

Tatu, jambo jengine ambalo kwa Makala hii ni la mwisho, ni yale maumbile ya mwanamke kupenda sana vitu vipya, sina maana kwamba mwanamme hapendi, hapana, lakini kimaumbile hasaa, wanawake hupenda zaidi vitu vipya, pindi mwanamke anapo pata kitu kipya, basi anaweza hata kukisahau kile cha zamani, sasa kwa muktadha huu, pindi mwanamke anapoamua kuwa na mtu nje ya ndoa ambaye kwake ni mpya, hapo huweza hata kumdharau mume wake na kuwa tayari kwa lolote, alimuradi amridhishe yule mpya zaidi kuonyesha kwamba anampenda sana, ili na yeye arejeshewe mapenzi kama yale na mtu huyo, sasa hapo ndio mara mambo yaliyofichika hupata mwanya wa kufichuka.

HITIMISHO;

Kama nilivyoeleza katika ufunguzi wa makala hii kwamba si lengo lagu kuonyesha ujabari wa mwanamme kwa mkewe au udhaifu wa mwanammke kwa mumewe, lengo ni kufikisha mawazo yangu kwa wenzangu ili tuokoe maisha yetu ya ndoa, ndoa ambayo huzaa watoto, watoto ambao kutegemea malezi, malezi yanayoaminika kuwa ni bora ni yale ya pande mbili, yaani Baba na Mama, ambapo tafiti zinaonyesha watoto wengi wananyanyasika na kuathirika kisaikolojia pale wazazi wao wanapoachana na kuambulia malezi ya upande mmoja.

Na nirudie tena kusema, licha ya sababu nyenginezo zinazotajwa za ndoa kukatika ambazo hizi mimi sizikubali, lakini sababu kuu na ya msingi ninayoiamini na kuikubali kuwa ni ya kweli ni pale wanandoa mmoja wapo anapoiacha ndoa yake na kuanzisha mahusiano na mtu mwengine.

Nitoe nasaha tudumu kwa uaminifu katika ndoa zetu, tuwe waaminifu, kila mmoja atekeleze wajibu wake wa msingi na wajibu mwengine ili kunusuru hii hali, ambayo kwa sasa imekuwa mtango unaotambaa, kila kona unayopita habari ndio hio mambo yamekuwa ‘shaghala baghala’.
 
Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,219
2,000
Wanawake wanazini sana tu na hawagunduliki. Mwanamke ana kinai, anatamaa, anahamu ya kubadili ladha kama mwanaume.

Wanaume sisi ni waoga sana kusikia mwanamke katamani nje, ni waoga sana wa kuchapiwa, tunaona kama kuchapiwa ni udhaifu kwetu ndo maana tuna hizi theories za mwanamke kaumbiwa mwanaume mmoja, hawezi tamani nje n.k lakini wanazini wanawake tena wengine for fun wala si kwamba hampendi mumewe.

kuna ambao wanazini na mtu huko jioni anarudi kwa mumewe na wala hamkumbuki huyo aliyezini naye.

Hofu ya MUNGU na utii wa kiapo cha ndoa ndio kigezo kutakachomfanya mwanamke azini au la, na hii inatuhusu hata ss wanaume. Ukiwa na hofu ya MUNGU na mtii kwenye kiapo chako cha ndoa utaiogopa na kuikimbia zinaa.

Kinyume na hapo bila kujali jinsia, sisi wote ni binadamu wenye tamaa ya mwili.
 
Hplp2275H

JF-Expert Member
Jan 21, 2021
393
1,000
Mkuu bujibuji Mambo Sasa Hivi yamechange...
Wanacheat vizuri Na wapo ndoani Wala hatung'amui Hilo .. na yote hayo tumeyasababisha sisi ... Tumewafanya kuwa na moyo yabisi ,Sura zisizo na haya na mioyo isiyo na hofu.
Ngoja watakuja kutoa shuhuda zao hapa.
 
simon2016

Senior Member
Oct 19, 2020
148
500
Mbona sasa hujasema mwanamke akipigwa mzigo akirudi baada ya uchakataji uchi unakuaje ? Km unazidi kubana au vipi?

Kwa tuliosoma masomo ya sanaa hio inaitwa udhaifu wa mwandishi katika falsafa yake au imani yake.

Mwsho wote tunaotembea(kuwachakata) nao walikua mabikra hata hao malaya(kama hujamkuta bikra), wapi tunakosea wote tunajua na muda huohuo wote hatujui?

Sasa imani na hofu yake mbele ya Mungu ndio pona pona yako , dunia imeribika unaaweza tulia ukakutana na mzigo ukabaki unajuta kwa nini ulitulia kikubwa jali nafsi yako ifike mbinguni hata kama ukipata ambacho hukutalajia.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,377
2,000
Wanawake wanazini sana tu na hawagunduliki. Mwanamke ana kinai, anatamaa, anahamu ya kubadili ladha kama mwanaume.

Wanaume sisi ni waoga sana kusikia mwanamke katamani nje, ni waoga sana wa kuchapiwa, tunaona kama kuchapiwa ni udhaifu kwetu ndo maana tuna hizi theories za mwanamke kaumbiwa mwanaume mmoja, hawezi tamani nje n.k lakini wanazini wanawake tena wengine for fun wala si kwamba hampendi mumewe.

kuna ambao wanazini na mtu huko jioni anarudi kwa mumewe na wala hamkumbuki huyo aliyezini naye.

Hofu ya MUNGU na utii wa kiapo cha ndoa ndio kigezo kutakachomfanya mwanamke azini au la, na hii inatuhusu hata ss wanaume. Ukiwa na hofu ya MUNGU na mtii kwenye kiapo chako cha ndoa utaiogopa na kuikimbia zinaa.

Kinyume na hapo bila kujali jinsia, sisi wote ni binadamu wenye tamaa ya mwili.
Umenena haswaaaa.....
 
mwandende

JF-Expert Member
Feb 16, 2017
5,940
2,000
Mkuu nje ya zama za sasa za technology,,

Mwanamke kumgunduwa ni ngumu sana.

Mfano zamani hakukuwa na Simu mke utajuwaje kama kagegedwa?na wewe upo kazini?.

Hizi Simu ndy zimetufumbuwa macho wanaume..

Hakuna cha zaidi.
 
Flashfifty

Member
Feb 10, 2021
63
150
Nadhan ni rahisi kwa mwanaume kugundulika akichepuka kuliko mwanamke unless mwanamke awe ameamua kukamatwa apart from that women always play very smart tena mwanamke ana uwezo wa kuwa na wanaume watatu kila mmoja akaitwa baby na ilihali anapendwa mmoja tu...period
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,718
2,000
Nipo nachat na mke wa mtu hapa, kwa maswali yangu ya mitego na udadisi... maelezo ninayochukua hapa ni taa nyekundu kwa anayedhaniwa kuwa ni mumewe.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,794
2,000
Wanawake wanazini sana tu na hawagunduliki. Mwanamke ana kinai, anatamaa, anahamu ya kubadili ladha kama mwanaume.

Wanaume sisi ni waoga sana kusikia mwanamke katamani nje, ni waoga sana wa kuchapiwa, tunaona kama kuchapiwa ni udhaifu kwetu ndo maana tuna hizi theories za mwanamke kaumbiwa mwanaume mmoja, hawezi tamani nje n.k lakini wanazini wanawake tena wengine for fun wala si kwamba hampendi mumewe.

kuna ambao wanazini na mtu huko jioni anarudi kwa mumewe na wala hamkumbuki huyo aliyezini naye.

Hofu ya MUNGU na utii wa kiapo cha ndoa ndio kigezo kutakachomfanya mwanamke azini au la, na hii inatuhusu hata ss wanaume. Ukiwa na hofu ya MUNGU na mtii kwenye kiapo chako cha ndoa utaiogopa na kuikimbia zinaa.

Kinyume na hapo bila kujali jinsia, sisi wote ni binadamu wenye tamaa ya mwili.
Wacha tuendee kujifariji kuwa hawazini ili TUWE NA AMANI
 
ndandambuli

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
653
500
KWA NINI NI RAHISI MWANAMKE KUGUNDULIKA ATOKAPO NJE YA NDOA?

Hakika mwanamke ni rahisi sana kugundulika endapo anatoka nje ya ndoa, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemuumba mwanamke aishi na mwanamme mmoja tu, na hakumpa kabisa uwezo wa kuonyesha mapenzi kwa watu wawili tofauti kwa kiwango sawa, hivyo mwanamke akiamuwa kutoka nje ya ndoa ni muda mchache mumewe hugundua na kama mume ni mjanja kidogo tu, basi anaweza kumgundua mke wake siku ya kwanza anayopata mwanamme mwengine nje ya ndoa. Inawezekana zipo sababu za ziada zinazowafanya wanawake kugundulika kiurahisi pindi atokapo nje ya ndoa yake, lakini mimi nitazionyesha sababu tatu pekee, ambazo kwangu mimi hizo ndizo kuu, na nyenginezo zilizopo nitawaachia ukumbi wengine na wao waziorodheshe kwa mujibu wa uzoefu wao.

Kwanza, ni ‘Jaala’ ya Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ameiumba nafsi ya mwanamke ipende mwanamme mmoja kwa wakati mmoja, halikadhalika ameuumba mwili wa mwanamke umridhishe na kumburudisha mwanamme mmoja. Kisheria, hakuna rukhsa ya kidini mwanamke aliyoamriwa kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja, kwa sababu moyo wake hauwezi kugawika kupenda zaidi ya mmoja na akaonyesha uwiano sawa, ingawa hali hii pia hutokea kwa wanaume wenye wake zaidi ya mmoja. Lakini wanaume angalau wamepewa uwezo wa kuficha mapenzi yao, hivyo kitu hicho huwasaidia. Hivyo mwanamke akichepuka lazima adharau kumoja apende kwa dhati kwengine, sasa kwa kitendo hicho ndio maana huwa ni rahisi kugundulika, kadhalika endapo akiutumia mwili wake kuburudisha mchepuko wake basi maumbile yake hayatakaa kimya, yatamshitaki tu kwa mumewe ikiwa mume huyo si ‘mume bwege’.

Pili, mwanamke ni mtu wa fakhari ya mapenzi, maana yake nini? Hii ina maana mwanamke siku zote hutaka kuona yeye ndiye anaependa zaidi kuliko mwenza wake, iwe kwa kutamka, ishara na hata kwa vitendo, hivyo hata kama itakuwa wako mbali mbali na mchepuko wake, yeye hupenda wawe wanawasiliana kila wakati, hasa kwa zile siku za awali za mahusiano, sasa hapa ndipo mara jungu hulikoroga kwa kujisahau kwamba pale alipo amemilikiwa na kuanza huonyesha ishara kwa mchepuko wake bila kuzingatia kwamba labda mumewe atagundua, aidha humuacha mumewe chumbani yeye akabaki sebuleni kwa kisingizio cha kuangalia TV, huku akichati na huo mchepuko wake au hata kumpigia simu kuzungumza nae, na huu ni udhaifu maalum wa kimaumbile ambao Mwenyezi Mungu amewaumbia wanawake na maisha hawataweza kubadili hili.

Tatu, jambo jengine ambalo kwa Makala hii ni la mwisho, ni yale maumbile ya mwanamke kupenda sana vitu vipya, sina maana kwamba mwanamme hapendi, hapana, lakini kimaumbile hasaa, wanawake hupenda zaidi vitu vipya, pindi mwanamke anapo pata kitu kipya, basi anaweza hata kukisahau kile cha zamani, sasa kwa muktadha huu, pindi mwanamke anapoamua kuwa na mtu nje ya ndoa ambaye kwake ni mpya, hapo huweza hata kumdharau mume wake na kuwa tayari kwa lolote, alimuradi amridhishe yule mpya zaidi kuonyesha kwamba anampenda sana, ili na yeye arejeshewe mapenzi kama yale na mtu huyo, sasa hapo ndio mara mambo yaliyofichika hupata mwanya wa kufichuka.

HITIMISHO;

Kama nilivyoeleza katika ufunguzi wa makala hii kwamba si lengo lagu kuonyesha ujabari wa mwanamme kwa mkewe au udhaifu wa mwanammke kwa mumewe, lengo ni kufikisha mawazo yangu kwa wenzangu ili tuokoe maisha yetu ya ndoa, ndoa ambayo huzaa watoto, watoto ambao kutegemea malezi, malezi yanayoaminika kuwa ni bora ni yale ya pande mbili, yaani Baba na Mama, ambapo tafiti zinaonyesha watoto wengi wananyanyasika na kuathirika kisaikolojia pale wazazi wao wanapoachana na kuambulia malezi ya upande mmoja.

Na nirudie tena kusema, licha ya sababu nyenginezo zinazotajwa za ndoa kukatika ambazo hizi mimi sizikubali, lakini sababu kuu na ya msingi ninayoiamini na kuikubali kuwa ni ya kweli ni pale wanandoa mmoja wapo anapoiacha ndoa yake na kuanzisha mahusiano na mtu mwengine.

Nitoe nasaha tudumu kwa uaminifu katika ndoa zetu, tuwe waaminifu, kila mmoja atekeleze wajibu wake wa msingi na wajibu mwengine ili kunusuru hii hali, ambayo kwa sasa imekuwa mtango unaotambaa, kila kona unayopita habari ndio hio mambo yamekuwa ‘shaghala baghala’.
Sahihi kabisa,mimi mwenyewe shuhuda
 
Flashfifty

Member
Feb 10, 2021
63
150
Alifanya maksudi nijue nikajua nikambwaga mwaka wa pili huu analialia tu,je unamzungumziaje huyu?

Sasa huyu alijimaliza mwenyewe tuite “mbwa kala mbwa” alikua hana uhakia na maamuzi yake au hisia zake which ni ujinga ukitaka kufanya hizi vitu unatakiwa uwe na uhakika na maamuzi yako kwamba hayotokugarimu kwa namna yoyote ile apart from that bora kutulia tu...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom