Kibukuasili
JF-Expert Member
- May 15, 2010
- 1,050
- 604
Mimi ni mshabiki mzuri wa ngumi. Hivi karibuni kumekua na mwamko mkubwa wa ngumu za kulipwa nchini. Shida kubwa inakuja pale panapokua na pambano zuri lakini muda unakua sio rafiki kabisa.
Tukiangalia ngumi za Marekani ambazo nyingi wanapigana Las Vegas huwa zinakua masaa ya alfajiri kwetu. Kwa kuwa kuna tofauti ya karibu masaa 10 ina maana kwa Las Vegas inakua bado ni mapema tu. Haya ya kwetu main card inaanza saa saba usiku au zaidi. Mimi binafsi siwezi kwenda ukumbini kwa sababu muda sio rafiki. Japo nina usafiri lakini sioni kwa nini niendeshe gari saa 9 usiku mwenyewe eti nimetoka kwenye ngumi. Nafikiri siko peke yangu ambaye nashindwa kwenda kwa sababu hiyo. Mtu asiye na usafiri wa kujitegemea ndio ngumu zaidi. Utapta wapi daladala saa hizo, na bajaji/bodaboda sio salama sana wakati wa usiku mkubwa.
Ningeshauri waandaaji wa ngumi wabadilishe utaratibu. Michezo ya awali ianze mapema ili pambano kubwa lianze kwenye saa 2 hivi ili liishe mapema watu waende majumbani kwao ikiwa bado ni mapema. Wanakosa watazamaiji wengi kwa ratiba yao ngumu.
Hata kuangalia kwenye TV nyumbani nako ni mtihani. Kukaa mwenyewe kwenye TV saa saba usiku unaweza kujikuta umelala na ngumu zenyewe usizione, hasa inapotokea mapambano ya utangulizi hayana msisimko.