BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 5,172
- 11,532
Kati ya sekta huria ambazo kila kinyangarika yumo basi ni NDOA.
Hii "sekta" ya ndoa huwezi kujua mtaalamu ni yupi wala majnuni ni yupi. Kila mtu kawaka moto anajitia mjuvi, hapoi wala haboi.
Ukiingia mitandaoni na penginepo, kila Tom na Jeri anafundisha kuhusu ndoa. Hata wachungaji nao ati ni walimu wa ndoa.
Kila aliye kwenye ndoa naye anajifanya mwalimu wa ndoa. Hata kama ndoa imemshinda lakini bado anang'ang'ana kuwa kungwi wa ndoa na kujifanya anagawa nasaha uchwara za ndoa.
Nashauri sasa serikali iunde VETA MAALUMU ambamo watapikwa makungwi wa ndoa na wapewe vyeti kabisa vya kitaaluma ili kwamba tunapohitaji ushauri wa KITAALAMU kuhusu ndoa tuwafuate hao.
Hatutaki huu utaratibu wa kila kanjanja anayejiita padri au pasta au mtu aliye kwenye ndoa kujifanya anatoa mawaidha ya ndoa wakati sote tunajua hana huo ujuzi wala maarifa. Ni kujitutumua tu.
Huwezi kukuta kila mtu akijifanya wakili au injinia. Huko kuna utaalamu hapataki Toms and jerries.
Lakini kwenye ndoa kila mtu ni fundi na rabi. Alaaah!
MY TAKE: Hili nalo mkalitazame.