Kwanini ndege huyu ameitwa ndege mwaarabu?

Si alikuepo kabla waarabu hawajaingia East africa?
kabla ya hapo alikuwa akiitwa jina gani?
 
Simfaham kiundani ndio maana nikauliza humu ili anaemjua atujuze mi huwa namuona tu.
Sawa mkuu, Ndege huyu anapenda sana mazingira ambayo ni ya upatikanaji wa chakula(mizoga) mara kwa mara na pia huwa anapenda pembezoni mwa bahari au ziwa ambapo watu hujishughulisha na shughuli za uzalishaji wa samaki. Kule kwetu ndege huyu tunamuita TAI, Tunamuita hivyo kwa sababu akimeza chakula kabla ya kushuka sehemu ya shingo lake hutuna na kuning'inia mithili ya tai.
 
Mazingira yake kimaisha yukoje kuanzia mahitaji hadi hali ya hewa aipendayo?
Hao asili yao ni aquatic yaani wanapatikana sehemu zenye maji mengi kama bahari nk ingawaje wanaweza kaa sehemu yoyote hasa anapokuwa mzee kwasababu ya kufuata chakula baadaya uwezo wake wa kutafuta chakula kupungua,ndege wengi wenye midomo mirefu na miguu makazi yao ni sehemu zenye maji mengi
 
Basi kwa makabila ya tanzania 124, baadhi yao wana jina naye mfano sisi tunamwiita "DYOVU"
 
Kwa hiyo kwa kiswahili anaitwaje? Hiyo hiyo marabou stork?
Marabou Stork Related Keywords _ Suggestions - Marabou Stork Long Tail ___.jpg
Marabou-Stork.jpg
 
Bwana afya au alibharwe (Kwa Kihacha, Kisimbiti na Kisweta); acheni kuwadanganya watu kwamba ana asili ya Urabuni**
 
Sawa mkuu, Ndege huyu anapenda sana mazingira ambayo ni ya upatikanaji wa chakula(mizoga) mara kwa mara na pia huwa anapenda pembezoni mwa bahari au ziwa ambapo watu hujishughulisha na shughuli za uzalishaji wa samaki. Kule kwetu ndege huyu tunamuita TAI, Tunamuita hivyo kwa sababu akimeza chakula kabla ya kushuka sehemu ya shingo lake hutuna na kuning'inia mithili ya tai.
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi ni wapi huko ndege huyu huitwa tai?
 
Hao asili yao ni aquatic yaani wanapatikana sehemu zenye maji mengi kama bahari nk ingawaje wanaweza kaa sehemu yoyote hasa anapokuwa mzee kwasababu ya kufuata chakula baadaya uwezo wake wa kutafuta chakula kupungua,ndege wengi wenye midomo mirefu na miguu makazi yao ni sehemu zenye maji mengi
Lakini mkoa wa shinyanga ni mkame na hao ndege ni wengi sana
 
Back
Top Bottom