Kwanini nawachukia wanaume?

Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!
Nenda kapime mdogo wangu, nenda kapime. Kwanza utajielewa uko katika hali gani na pili (hili siombi litokee) ikiwa umeathirika ni bora kujua mapema ili kuwahi kuikabili hali hiyo kitaalamu. Usisubiri mpaka iwe umechelewa. Ninakuombea matokeo yasiwe mabaya. Kila la heri.
 
Kwakua hukufanya zinaa kwa kukusudia na umeshatambua kuwa ni kosa MRUDIE MUNGU FUNGA NA UOMBE USIKU NA MCHANA MUNGU ATAKUSAIDIA UTAACHA KBS HY TABIA UTASOMA NA KUFAULU NA KUPATA KAZI NZURI, jiepushe na zinaa ukimwi uko na unaua
 
Nawashukuruni kwa michango yenu napenda niweke wazi tu kuwa
jambo linalonikosesha furaha zaidi kwa sasa ni kila ninapofikiria kwenda
kupima. Kweli Nakosa amani!

Pata ushauri nasaha then hutaogopa kupima HIV, na pindi utakapopima itasaidia sana kukurudisha ktk hali yako ya kawaida,... ila tena kwenye zizi atapungua kondoo mmoja !
 
pole kwa yaliyokukuta bibie! Rudi kwa muumba hope ni kwake pekee utapata nafuu, muombe akuondolee hilo balaa ifanye hiyo kuwa past na ondokana na fikra hizo Mwenyezi ni mkubwa atakusamehe na kukuongoza katika yaliyo mema na kukupatia mume atakae kuheshimu na kukupenda be strong girl! all the best
 
Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuamua nini hatima ya chuki uliyonayo dhidi ya wanaume,inawezekana kabisa kuwa nawe ulichangia hao wanaume kukufanyia walichokufanyia ila sikulaumu sana maana mazingira ya hali uliyokuwa nayo siyajui ila nina maswali haya yafuatayo;

1.Kati ya hao rafiki za baba yako kuna aliyekulazimisha kufanya nawe mapenzi?

2.Baba yako au mama yako hakuwa na ndugu ambao wangeweza kukusaidia?

3.Umekwishakwenda kuonana na daktari wa mambo ya saikolojia?

4.Unaweza kukaa muda gani bila kufanya ngono?Maana kwako na kwa uzoefu ulionao inaonekana ni kama mchezo fulani tu ambao unaweza cheza wakati wowote ili mradi cash inaingia.

Nakupa pole kwa yote uliyopitia na natumai utanijibu kwa ufasaha.
 
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?

....dahhh, nakupa pole kwakuwa kutoka rohoni mwangu unastahili pole...
usijilazimishe kupenda, la msingi jilinde/ujiepushe na maradhi pia na "mzigo" wa mimba/mtoto.

..jitahidi uyajenge maisha yako, iweke sawa imani yako mwenyezi mungu nae atakusaidia.
pole sana.
 
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?
dah pole sana mcharuko ujue wanawake kwa asilimia tumeumbwa kwa mateso pia sometimes tunaweka shida zetu mbele tunasahau thamani yetu
ni kosa kubwa sana wadada tunafanya kutumia miili yetu ili kupata kitu flani
mimi mwenyewe nilivokuja mjini nilikuwa na matatizo kibaaaaaaao hela,kazi nk na ni wanaume wengi tu walikuwa wananitaka ila namshukuru mungu niliweza kuyashinda majaribu.wanaume wanajua sisi ni weak so wanatumia matatizo yetu kutuchezea while hawawezi ata kuyatatua.jitambue sasa mcharuko na anza maisha yako upya utaona mafanikio yake.achana na mapromise feki wanaume wanakupa juu ya kifua hawana lolote ni watu tu kama wewe hata wao wana matatizo yao kibao .nenda hata mabenki utaona wanavodaiwa mamikopo hata kurudisha hawawezi sembuse kutatua matatizo yako? wake up my dia
 
Its one among the sad stories i ever heard. Very sorry for what happened to you. I really share your pain.but you have to do the following
1.you MUST go for counselling
2.you MUST be a god fearing girl. If you are a muslim, you should make sure that you pray 5 times a day and follow islamic way of life. If you are a christian,so should you.
3.you must hate ya illegal business that you are doing and you should value your body. You should find other sources of income which are not illegal.
I know how hard it is but ask god for his help.
 
Salam kwa wanaume wa mmu ambao mna tabia za kupita mitaa ya corner bar sinza,buguruni rozanna,ohio city centre,tunisia rd kinondoni,takadiri oysterbay,jolly's pub,masai pub na kwingineko kwa aina hiyo.Kuanzia leo wakati unamchukua changu remind yourself of this sad story,wakati unafungua kioo cha gari na kufanya pssssiiii kumbuka unayemwita ni Bi Mcharuko,yuko hapo barabarani,anaumwa mbu,anakimbizana na polisi,vibaka ni wa kwake,baridi ni ya kwake,mvua ni ya kwake,sio kwamba kataka bali ni kwa sababu alizozitoa Mcharuko.Mhurumie mtoto wa mwenzio,kaa naye mbali,ukimkimbia akakosa mteja then kichwa kitachanganya atatafuta namna nyingine ya kuishi.Kama ni uchangu sisi wanaume ndo machangu kwa sababu tusingekubali kuwa wateja wao soko wangepata wapi?
kwako Mcharuko,hongera kwa kufunguka,huo ni ushindi 50 percent,vita iliyobakia kupata ushindi wake wasikilize waliokushauri humu ndani(wengi sio wote).As of HIV usiogope hata kama itakuwa positive ukifuata masharti utaishi vizuri na watoto HIV -ve utapata.
Salam aleikum.
 
kweli bishanga namini kwa hili ata wewe umejifunza
 
we subiri,nakutafutia siku.
siku ndo leo ? yaani mcharuko kanisikitisha kweli leo bwana ujue watu wakiwa juu ya kifua wanatoa mapromis kumbe wallet ipo ziro balance
mcharuko usitoe tena mwili wako shosti tena anza kuvaa kininja kabisa utatoka tu mbona?
 
Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuamua nini hatima ya chuki uliyonayo dhidi ya wanaume,inawezekana kabisa kuwa nawe ulichangia hao wanaume kukufanyia walichokufanyia ila sikulaumu sana maana mazingira ya hali uliyokuwa nayo siyajui ila nina maswali haya yafuatayo;

1.Kati ya hao rafiki za baba yako kuna aliyekulazimisha kufanya nawe mapenzi?

2.Baba yako au mama yako hakuwa na ndugu ambao wangeweza kukusaidia?

3.Umekwishakwenda kuonana na daktari wa mambo ya saikolojia?

4.Unaweza kukaa muda gani bila kufanya ngono?Maana kwako na kwa uzoefu ulionao inaonekana ni kama mchezo fulani tu ambao unaweza cheza wakati wowote ili mradi cash inaingia.

Nakupa pole kwa yote uliyopitia na natumai utanijibu kwa ufasaha.
1.Yupo

2.Ndugu yangu kama wewe ni mtoto basi sahau habari za ndugu baada ya kifo cha
wazazi wako/ Kama ni mzazi sahau vilevile kama baada ya kifo chako ndugu watachukua
jukumu la kuwalea wanao. Vinginevyo uwe umeacha kitu ambacho hata wao itakuwa ni
rahisi kunufaika kwao. Mmoja katika ndugu wa baba yangu kikwazo kilikuwa ni mkewe
ambaye alikuwa anaonyesha waziwazi chuki dhidi yangu kila nilipokuwa nawatembelea, sina
uhakika ila nahisi huyu mkewe alikuwa ni kikwazo kwangu kupata msaada kwa baba mdogo.

3.Sijawahi onana na daktari wa hayo mambo

4. Napenda ufahamu kuwa kwenye kazi ya kujiuza kuna wakati husikii starehe yoyote zaidi
ya karaha ndio maana inakuwa ni faraja kwetu unapopata watu wenye matatizo ya kimwili
na kuna wengine (sina uhakika kama walikuwa wanafanikiwa) Huenda kwa waganga wa asili
ambao huwasaidia anapoenda na mwanaume basi mwanaume hujikuta anashindwa kufanya lolote
hadi kujihisi kuwa ana matatizo. Sina uhakika na hili kwani sijawahi kufanya.
 
siku ndo leo ? yaani mcharuko kanisikitisha kweli leo bwana ujue watu wakiwa juu ya kifua wanatoa mapromis kumbe wallet ipo ziro balance
mcharuko usitoe tena mwili wako shosti tena anza kuvaa kininja kabisa utatoka tu mbona?
siku ndo leo ya kufanya nini?
 
Marafiki wa mama wengi ni kina mama wa nyumbani
hakuwa na marafiki ambao wanajimudu sana kiuchumi
kama hao wawili ambao walikuwa ni wakubwa zaidi mmoja
huwa anachoma vitumbua na mwingine huwa anakopesha
sabuni!

ok nimekuelewa. . .
Pole sana,
mtangulize Mungu
 
Pole sana mtoto mzuri wa CBE, naamini ulichosema ni ukweli mtupu maana pale CBE ni kama wanachuo wote wa kike ni CDs ingawa baadhi bado ni safi. Baada ya baba yako kufariki dunia ulifanya kosa kubwa sana la kiufundi kujilegeza kwa hao rafiki zake na baba yako, walipojaribu kuomba 'k' nawe ukalegea, ukweli ni kwamba wewe ndiye dhaifu zaidi kuliko hata hao wanaume unaowazungumza hapa. Hebu jiulize ni watoto wangapi yatima leo hawana wazazi, hawafanyi u-CD lakini bado wanaishi vizuri? Mungu ni mwema sana siku zote, pamoja na shida ulizokuwa nazo angeweza kukupatia mbinu mbadala za kujipatia kipato, kwa nini hukufikiria kufanya kazi nyingine halali ukakimbilia ngono? Haya, umeenda chuo umeendelea na biashara hiyo hiyo, nani alaumiwe, wanaokutongoza au wewe unayegawa bila mpaka?

Maandiko yanasema: 'Mungu hamjaribu mtu yeyote, lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe. Tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi, nayo dhambi ikikomaa huzaa mauti'. Take care madam!
 
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?

Story yako inaweza kuwa ya kusikitisha kwa upande mwingine na ya kulaumiwa kwa upande mwingine. Kwa ridhaa yako nirususu kusema yafuatayo:
1: Ni kweli kwamba watu huchagua majina mara nyingi kuendana na tabia, lifestyle na maisha yao kwa ujumla, yeyote atakayepinga hili hana uelewa wa kutosha kwa hapa tunakubaliana.
2: Kwa upande mwingine, Your Life style is Your Own Doing!
Nikiongelea zaidi hapa niseme, Matatizo yote mtu anayokumbana nayo ndiyo yanayomfanya awe mtu katili au mtu mwema, awe jasiri awe akate tamaa. Na jambo zuri ni kwamba, mtu anapokabiliwa na matatizo anakuwa na WIDE WINDOW OF CHOICES. Ukipata nafasi usoma kitabuu Cha Mtanzania mmoja kiko amazon, 'Anaother Story..Not! na Siri Za Maisha, mwandishi, Dr. Isangula anasema ' Ni lazima kila binadamu autane na matatizo ili aweze kubapata 'Wisdom'' . Kwamba 'Problems if met in the right ways,they can be stepping stones to success'' Kina mambo mengi sana hasa akiongelea falsafa ya Vinctor Frankyl na Pavlov, kwa kunukuu tena kwama ,Pavlov alisema ukiwa na stimuli au kichochea una respond na wewe huna uamuzi kwa response zako' mfano umefiwa na mzani unasikitika na lazima utafute msaada,unatongozwa na hao jamaa na unasema huna jinsi. Lakini Victor Frankyl anasema Kila mtu anapokubana na matatizo kuna dirisha pana la kufanya maamuzi ,kwamba kuna 1) Imagination- Uwezo wa kujenga picha ya jinsi maisha yako yatakavyokuwa kulingana na maamuzi yako, 2)Independent will kwamba hakuna anayekulazimisha kuamua unachoamua,yaani ni wewe mwenyewe na matatizo yalikusukuma tu lakini hayakukulazimisha 2) Self awareness- Uwezo wa kutambua madhara yatakayojitokeza kutokana na maamuzi yako mfano ni lazima ulifikiria kuhusu Ukimwi,Mimba maginjwa ya zinaa kabla ya kuamua kutoa uloda 4) Conscience -ulitambua kuwa unacho/utakachofanya ni kinyume cha maadili,tamaduni na misingi ya dini. Ukifikiria yote hayo, naendelea kunukuu ' Then you have a Freedom and Power to choose... and though you Have the Freedom to Choose, there is always the Counter force to your Freedom, If the FORCES inside you are so STRONG than your FREEDOM then you'll make the WRONG DECISION''

Hapo unaona kuna Counter force ambayo kwako ilisukumwa sana na matatizo yako lakini mwisho wa siku ulikuwa na UHURU wa kuchagua na labda unegekuwa hauko katika biashara hiyo na ungekuwa mtu mwema kabisa. Simaanishi wewe si mwema, lakini kwa kuwa una chuki dhidi ya wanaume na unawaona makatili hapo umepoteza wema. Mwanaume kukutongoza si kosa, kosa ni wewe kukubali! Si vema kusema 'Hukuwa na jinsi' hapo juu tumeona ulikuwa na Freedom ya kuchagua. Kama unegesema walikubaka hapo inekuwa story nyingine lakini, 'Uliamua kukubali' Hapa neno muhimu ni kuwa Uliamua kukubali! Ukaamuza kuwa na Maisha yako uliyo nayo sasa! Ukaamua kuziba hisia za utu wako! Ukaamua Shida zikuongoze kufanya maamuzi mabaya! Ukaamua kuondoka nyumbani na kumfuata mwanaume kama ni gesti au wapi! Ukaamua kuvua nguo mwenyewe ukika gesti!At least uliamua kutafuta shule lakini ulipofika hapo shuleni CBE ukaamua kuwa changudoa. Sehemu nyingi ya Maelezo yako ULIAMUA mwenyewe! Ukweli ni kwamba hapa si Wanaume bali ni maamuzi yako mwenyewe
FAHAMU KUWA HAPA SIKUHUKUMU bali najenga hoja yako kwa kuwa JF ni sehemu ya Kusaidiana

NINI CHA KUFANYA
Awali nilinukuu kuwa kila mtu lazima apitie matatizo ili apate wisdom na mwishowe awe mtu mwema au mbaya. Kwa kuwa inaonekana una Uwezo wa KUAMUA, kumbe sasa wawezo kuyatumia matatizo yako kama STEPPING stone kupata wisdom na SUCCESS. Waweza sasa KUAMUA kuacha maisha yako. Nakushauri utafute kitabu cha huyu jamaa kina Busara nyingi ambazo siwezi kuzieleza hapa. Acha ninukuu kwa mara ya mwisho, 'Maisha au matatizo uliyonayo sasa yametokana na Maamuzi yako ya siku za nyuma, ndiyo maana una maisha mazuri au mabaya kabisa kupindukia, kwa kuwa maisha ya siku za mbele FUTURE ni muhimu zaidi na kwa kuwa huwezi kuibadili PAST yako, Unayo nafasi ya kuishi maisha mazuri sasa ili FUTURE yako iwe nzuri. Maisha unayoishi sasa yatakuwa PAST katika FUTURE yako na kama ukiishi kwa UBAYA sasa basi Hukumu yake utaipata katika FUTURE yako kama maisha ya PAST yako yanavyokuhukumu sasa, sasa ambapo ni FUTURE ya iliyokuwa PAST yako'' Japo hata mimi nilipata shida kuelewa jamaa anamaaisha nini kwa PAST na FUTURE ila ukisoma kwa utulivu utajua anamaanisha nini.

Wewe si Mcharuko, unayo POWER within You! Una nafasi ya kubadili maisha yako hasa kama hujawa addicted na UCHANGUDOA. Kaza msuli katika Shule, Soma mama, Ukombozi wa Masikini ni elimu. Taratibu jiondoe katika Uchangudoa. Wanaume japo wapo wakatili wapo wenye utu wanaojua kupenda, wapo vijana wa saizi yako. Nimeambatanisha link za vitabu vya huyu Dr Isangula ambavyo vitakusaidia katika hii transition ya Kujenga Maisha yako Mapya, kujenga Future yako! Maisha ni zaidi ya kuwa na fedha Mfukoni! Maisha ni kuishi kwa Weama na WISDOM

All the best sasa UNAPOMUA kujenga FUTURE yako
Nisamehe kama nimetumia maneno makali ya kukukwaza na pia sikufanya spell check kwa kuwa nimebanwa kidogo na majukumu na nilitaka upate ujumbe

http://www.amazon.com/Siri-Za-Maish...=sr_1_1?s=books&ie=UTF8&qid=1319814431&sr=1-1
http://www.amazon.com/Another-Story...r_1_12?s=books&ie=UTF8&qid=1319814454&sr=1-12
 
pole dadangu lakn unaweza kuacha hiyo kitui ukiamua na muombe sana mungu maana hiyo roho itakuwaa inakufuatilia roho ya kisasi na mwisho wewe ndo unaumia Mungu ni mwema atakupa mtu ambaye atakufaa
 
Kwanza pole!Pili,una matatizo ya kisaikolojia ambayo yanatibika,tatu,haujipendi,hili linahitaji maelezo ya kina ili ujue ni jinsi gani hujipendi,hali uliyonayo ni kawaida kuwatokea watu wenye matatizo kama yako,niliwahi kuwachukia wanawake kutokana na waliyonifanyia lakini nilikuja badilika coz wanadamu tuko tofauti japokuwa sijaamua kujihusisha na mahusino ya kimapenzi,usijali utabadilika ukitaka!
 
Back
Top Bottom