Kwanini nawachukia wanaume?

Ushauri wa dharura, kabla sijagusia tatizo la msingi...

Usithubutu hata kwa kulazimishwa, kwenda kupima HIV kwa sasa... Narudia tena usithubutu kwenda kupima kwa sasa. Nina uzoefu na madhara ya kupima HIV kwa watu kama wewe, na nakuhakikshia, ukipima leo na bahati mbaya ukakutwa umeathirika, hautamaliza mwaka kabla hujafa kifo cha aibu.

Kwa sasa jichukulie kuna uwezekano kuwa hujaathirika, na jitahidi kadiri ya uwezo wako kutumia mbinu zote za kujikinga. Siku ukiwa tayari (nitakuelewesha baadae nini maana ya 'kuwa tayari'), then, nenda kapime.

Ila kwa sasa narudia tena, usithubutu kwenda kupima... kuna uwezekano wa 75% hujaathirika...
 
Pole sana kwa matatizo yote... Mtangulize sana mungu nae atakuonyesha njia... Ukiweza onana na wataalam wa saikolojia watakusaidia zaidi... Pole tena!
 
Usitegemee mwanaume akuthamini kama we mwenyewe hujithamini. Wanaume tunapotongoza huwa tunaangalia, kama wewe ni slope, wanaume watakutumia na kukuacha nenda rudi. So, solution ya kwanza ni kubadilika we mwenyewe. JITHAMINI, USIJIONE RAHISI.
 
Usithubutu hata kwa kulazimishwa, kwenda kupima HIV kwa sasa... Narudia tena usithubutu kwenda kupima kwa sasa. Nina uzoefu na madhara ya kupima HIV kwa watu kama wewe, na nakuhakikshia, ukipima leo na bahati mbaya ukakutwa umeathirika, hautamaliza mwaka kabla hujafa kifo cha aibu.
Hapa sikubaliani na wewe, nadhani kuishi kwa wasiwasi japo hutakufa (kama unavyosema) but afya yako itazorota kwa wasi wasi wa kuwa anao au hana! Kumbuka Mcharuko tayari ana mixed psychological disoders, kwanza alipata Trauma kwa kufiwa na wazazi, second ananyanyasika kijinsia na kihisia , third moyo wake umejaa chuki, nne maisha yake hayajawa na mwelekeo mzuri, so ukimwambia asipime Ukimwi unamwongezea tatizo la tano la kuishi kwa wasiwasi! Ushauri wangu, nadhani post yake ililenga kuonyesha anavyojisikia ili tumpe ushauri mzuri na ni vema tumwone kama binadamu anayetaka kubadili Maisha yake. Hatua ya Kwanza ni yeye Kuamua kuachana na Uchangu Doa, ya pili ni kuchukua hatua ya kuacha, ya tatu ni kuchunguza iwapo uchangudoa umemletea madhara yatakayo haribu future yake kama vile Ukimwi na hii inahitaji awaone wataalamu wa afya, ya nne mwongozo na ushauri wa muda mrefu wa kisaikolojia ili kumsaidia kubadili mind yake isifikirie mabaya yaliyojitokeza bali ifikirie jinsi anavyoweza ishi vizuri sasa, ya tano anahitaji kujishirikisha katika masuala ya kijamii yatakayo badili maisha yake-kujipatia kipato, biashara au kazi yenye heshima ili ajitegemee, dini, n.k. Kupima Ukimwi yaweza kuwa hatua ya kwanza kabisa

Meanwhile Mcharuko naomba uzingatie kujilinda..Condom Muhimu hasa katika Muda huu ambao naamini unatransition kuachana na Uchangudoa
 
kati ya mambo yaliyopata kunigusa ni hadi ndani ya moyo wangu ni swala lako.Lakini najipa moyo kuwa liko njiani kutoweka kwa hatua uliyo anza kuchukua.jambo muhimu sana kujua ni kwamba inaakupasa USAMEHE na kusahau kabisa ulivyo tendwa na hao majamaa.kusamehe ni hatua pekee itakayoweza kukuokoa kwenye hili.Pili ujue watu wametofautiana (wanaume).so,do not generalize them by the conclusion you drawn from those who used your problems as their opportunity.that is who men are..................Also the fate of your business is not promissing.samehe mama na usahau na ukapime kama ni mzima uokoke na Mungu wangu atakurudishia utu wako ulioibwa na shetani.sema AMEN......
 
Pole sana Mcharuko,hayo yote ni mzunguko wa maisha,heri wewe umeshajikwamua na kufikia elimu hiyo,nadhani unajua wangapi rafiki zako ktk biashara iyo walio ktk shida kubwa kuliko yako.Jifunze kusamehe na kusahau Muombe sana Mungu atakuonesha njia na utampata mme mwema atakayekusahaulisha shida zako ulizopitia zamani.
 
Dah! Pole bibie, jenga hofu ya mungu. Karibu kanisani kwetu ufanyiwe maombi.
 
Salam kwa wanaume wa mmu ambao mna tabia za kupita mitaa ya corner bar sinza,buguruni rozanna,ohio city centre,tunisia rd kinondoni,takadiri oysterbay,jolly's pub,masai pub na kwingineko kwa aina hiyo.Kuanzia leo wakati unamchukua changu remind yourself of this sad story,
salamu na kwa wakaka/wababa/wababu wanaotafuta wachumba humu.
 
Mungu mkuu uketie mahali pema palipojuu! Naomba shusha uwepo wako wa roho mtakatifu ndan ya mcharuko!,navunja tabia na pepo wachafu ktk jina la yesu. Nakataa matatizo hayo yanayopata katika jina lililojuu, Mungu ba....... Amen
 
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?
\
Hi story haiendani na posti zako za nyuma. Inaelekea wewe ni mtunzi mzuri unayeweza kukoga nyoyo za hadhira zako. Sori hii Haina ukweli wowote. Unapoteza muda wa watu tu.
 
\
Hi story haiendani na posti zako za nyuma. Inaelekea wewe ni mtunzi mzuri unayeweza kukoga nyoyo za hadhira zako. Sori hii Haina ukweli wowote. Unapoteza muda wa watu tu.

inawezekana haimuhusu yeye ila kuna mtu inamuhusu au pengine kuna mtu yatamkuta.
Acha watu wapate mafundisho.
 
inawezekana haimuhusu yeye ila kuna mtu inamuhusu au pengine kuna mtu yatamkuta.
Acha watu wapate mafundisho.


>> ** Sawa, Husninyo nimekuewa ila asijaribu kusingizia kukosa wazazi. Suala la wazazi kutangulia mbele ya haki ikichukuliwa kirahisi hivi basi kila mtoto wa kike atakuwa malaya au wa kiume atakuwa nini................. Kwa wanaofanya hivyo basi wanasingizia ila ni nafsi au dhamira zao ndizo zimewafanya kutenda uovu.
 
umalaya kazi!heshimu kazi yako...mi sioni haja ya kukupa pole kwani ndio maisha tunayoishi kila siku cha msingi tu kuwa imara!chuki haisaidii itakubomoa wewe kwani unao wachukia hawakujali,cha msingi angalia usawa wa bahari ukiona kumejaa ww ogelea.
 
"Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?"
unalalamika lakini inaonekana unaipenda kazi yako!wanasema kila MALAYA huwa anastory ya kutokea!
 
\
Hi story haiendani na posti zako za nyuma. Inaelekea wewe ni mtunzi mzuri unayeweza kukoga nyoyo za hadhira zako. Sori hii Haina ukweli wowote. Unapoteza muda wa watu tu.
Ahsante kwa mtazamo wako, nimefundishwa mengi huko juu nazidi kusikia uchungu ninaposoma
Comment mbalimbali. Nipo hapa Jf kwa siku nyingi kiasi nimeingia kwa ID hii ili niweze kutoa ukweli
hata hivyo imenichukua muda toka kujiunga mpaka kufanya kile nilichodhamiria mwisho wa yote
nimefundishwa kusamehe. NIMEKUSAMEHE!
 
Back
Top Bottom