Kwanini nawachukia wanaume?

Mcharuko

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
209
172
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka 2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukiakutoka moyoni. Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?
 
Of course ulikuwa unatumia mwili wako kama kitega uchumi na si kitega mapenzi.

Tulia, itafika wakati utapenda, na ukibahatika kupata anayejua kupenda, utajua raha ya kuwa na mwanaume, wako tena wako peke yako kudaaadeki.
 
unahitaji msaada wa kisaikolojia.

Back to the topic baadhi ya wanaume ni kama wanyama hawana utu. Ila bora ungeomba msaada kwa marafiki wa mama yako,
 
Samahani kwa hili swali wazazi awakuacha mali yoyote ambayo ingeweza kukusahidia kama ingeuzwa na apakuwepo na ndugu wa kuweza kukufadhili upande wa baba au mama yako.wanaume ni watu wazuri sana kama he has a GOD fear.n
 
Pole sana kwa maisha magumu/machungu uliyopitia
1.futa hasira na chuki uliyonayo moyoni kuhusu hao wanaume
2.jaribu kusahau mambo uliyoyafanya zamani
3.umefanikiwa kwenda chuo tafuta kazi nyingine achana na hiyo unayofanya (uchangudoa)
4.mshirikishe muumba wako akusaidi uweze kujitambua na kuishi maisha uliyokuwa unayatamani

Naanimi ukijiamini/kuachana na yote utafanikiwa na mwisho wa yote hao wanaume unaowachukia utampata mmojawapo atakayekupenda/kukuoendolea upukwe na machungu yanayokupelekea kufanya yote unayofanya.



 
unahitaji msaada wa kisaikolojia.

Back to the topic baadhi ya wanaume ni kama wanyama hawana utu. Ila bora ungeomba msaada kwa marafiki wa mama yako,

Hata kama ni marafiki wa mama yako, kuna baadhi ya wanaume bado hawana utu ni wanyama tu!
 
Mie labda nipo tofauti na wewe kimtizamo bi mcharuko, wanaume ni wazuri tu, inategemeana na wewe ulikuwa na msimamo gani ulipowafuata na kutakwa kimwili, pili hukua na ndugu wa pande zote mbili kuweza kukusaidi?
 
Mcharuko pole saana Mpenzi na hii story ulotoa hapa.... INASIKITISHA kwa kweli. Pole saana. However Men are funny creatures... Mwanaume yeyote yule haaminiki dear.. wapo exceptions ambao waweza kua waaminifu but majority wako hivo.. in other words ina maana it is better woote uwachukulie wako hivo ili ujue jinsi ya kuwa-handle. Wanaume awe babako, awe Mjombako, awe babuyo, awe kakako, awe binamu.. woote hao wana possibility kubwa ya kukulala wewe.... it is a sad fact but true.

Back to you.... Wee ni more of a psychological problem. inaonesha you enjoy sex, ila tu kuwaamini ndo kero kwako, kumuamini mmoja wao akawa your shoulder ndio inakua shida... However you should know kua as much as they are funny creatures wana umuhimu saana katika maisha yetu in one way or another... Na the good thing ni kua you and only you have the power ya kuamua ni jinsi gani wakutreat... you want them to treat you like shit; they will treat you like shit! You want them to treat you like a hooker: they will treat you like a hooker! You want them to treat you like a queen; they will treat you like a queen! In short you just have to study em' know the type of guy you like... And stick to him.

Note that sio kazi ndogo kujitune uweze wapenda... But jaribu dear for ni muhim. Best of Luck.

Pamoja Saana
ADI.
 
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza
kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu
nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini
ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa
kivuli.

Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto
wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili
baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu
ulizidi.

Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba
Wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba
yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia
hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina
jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.

Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka
2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi
ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume
maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi
nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.

Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa
kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukia
kutoka moyoni.

Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi
kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?


Pole mwaya, nakuonea huruma sana ila ni mapito tu hayo. Unahitaji counseling maana utakuwa umeathirika kisaokolojia na ndio maana unawaona wanyama. Jaribu kutafuta counselling ingawa sijui vituo vyao.
 
tatizo watu wengi mkishikwa na matatizo mnakimbilia binadamu wenzenu kuwaomba....

ungeanza na kumuomba mungu kwanza uone .......

no one can make you feel inferior without your consent..........
 
Najiskia vibaya sana. pole sana mpendwa kwa matatizo ya maisha. Naamini huipendi kazi yako ya kuuza mwili na nina imani kua ukitaka kujitoa katika mtego huo utatoka tu.
Wanaume (kama wanawake) like to take advantage of the needy ones.
  1. Muhimu kabisa ni kupunguza mahitaji yako. Usitaki kabisa kuhishi maisha yalio juu ya uwezo wako (mimi siku hizi nahishi bila simu ya mkononi, ni mfano tu)
  2. upende mwili wako sababu nafsi yako inahishi katika mwili wako, na nafsi yako imeumbwa ikifanana na Mungu. You are devine and your body is the temple. sasa ukisha utoa udhu mwili wako, huoni kama unafukuza the devine part in you?
  3. Jipe heshima mwenyewe. Kabla ya kukosewa hivo na hao wanaume ulikua na mtazamo wa maisha HIyo experience ya hao wanaume ni moja ya matatizo ya maisha ila kuna mengi ya kabla ya hapo, na mengi zaidi kisha hapo. Ukijilazimisha kuhishi katika hali hiyo unaziwia baraka zingine kujitokeza maishani mwamko.
  4. Mwisho, kumbuka Mungu ana mpango wa ajabu kwa kila mwanadamu (a wonderful plan). Unaamini mpango wako wa ajabu ni kuuza mwili wako? Nimefurahi kusikia unasoma, endelea na masomo mpendwa na anza kufikiria kazi zingine. labda hazilipi kama hiyo ila zinalipa upande wa heshima. Unakua na amani moyoni, unajipa heshima na watu wanakuheshimu pia.
Kuna wanawake wengi sana wamejitoa katika mtego huo wa kupata pesa kirahisi na leo wanakua na maisha mazuri. Nakutakia kila la heri...
but please don't do that to yourself...
 
Mhhhh!!! Pole sana.
Unamhitaji Mungu akuponye nafsi yako ambayo imejeruhiwa sana, then Mungu aweza kukupa mume mwaminifu ambaye utampenda, naye atakupenda. Usikate tamaa, yupo Mungu aweza kukusaidia.
 
Nasikitika mno,maisha yako hayatofautiani na ya rafiki yangu niliyejuana nae juzi.Babake na mamaye walifariki 2000/04, maprofesa, kwakuwa ni mtoto wa mke mdogo hawakuthaminiwa,alijitahidi ila kidato cha 5 yalimshinda akafungua goli, alifukunzwa na shangazie na kuja kuzalia Dar,alijua umuhimu wa xul na kurudi kumalizia kidato cha 6,Yupo Dodoma chuo,hana mkopo japo kachaguliwa, kitega uchumi pekee ni mwili wake coz ndugu hawamtaki na mwanaume aliyemzalisha hanamsaada kwani nae mwanafunzi.Mimi naumia saana,sipendi ajiuze, ila afanyaje na hela hana?Ni mzuri sana wa sura na mdogo kiumri,hakustahili,kaomba nimtafutie kazi ila mie mwenyewe cna ndo najiandaa kujiajiri. Nimsaidieje?
 
wanaume tupo poa sana.mwanamke ukikosa upendo wa mwanaume ni sawa na maua yasiyo mwagiliwa maji.pole sana.mia
 
Pole sana.....
Story yako inasikitisha sana.
nakushauri mrudie Mungu ataponya nafsi yako ilipoumia,pia tafuta concellor awe anakushauri.
 
Pole sana mrembo, kwakweli wanaume wengi wanatabia mbaya na hawana ubinadamu kwa watoto wawenzao,mshukuru Mungu mpaka hapo ulipofikia, na achana na hayo mambo ya uchangu kwani hatima yake sio nzuri unaweza kupoteza ndoto zako zote ulizozipanga...nibora uombe saada hata kupitia magazetini au vituo vya dili kuliko kazi unayoifanya,Muombe mungu na niamini atakuitikia dua yako kwani wewe ni yatima na anakuona kiumbe wake unavyotabika,pole sana mungu atakusaidia na atakuondolea kila misukosuko.
 
Back
Top Bottom