SoC02 Kwanini naogopa ujauzito?

Stories of Change - 2022 Competition

Mahma

New Member
Jul 23, 2022
1
1
Ujauzito ni hatua muhimu katika maisha ya kila mwanamke.

Kuna wamama wanao furahia kipindi chote wanachobeba ujauzito na wengine huanza kuwa na khofu pindi tu anapojigundua kuwa ana ujauzito.

Licha ya kuwa asilimia kubwa wanawake huwa na khofu na wasiwasi, hali hiyo hupungua pindi wanapopata msaada na mashirikiano mazuri kutoka kwa ndugu zao marafiki na ushauri mzuri kutoka kwa wataalamu wa afya.

Muda mwengine hii khofu inaongezeka hadi kupelekea kufanya kila njia ya kuzuia wasishike kabisa ujauzito, au wasiendelee nayo au kuamua kutafuta mtoto wa kupanga.

Hofu hii inapoongezeka inakua sio hali ya kawaida na inahitaji kuwekwa sawa.

Khofu hii hutokea kwa watu wa Aina mbili, Wale ambao wameshawahi kujifungua na ambao hawajawahi kujifungua.

Kwa ambao hawajawahi kushika ujauzito khofu yao kubwa huwa inatokana na sababu zifuatazo:-

- Muhanga wa unyanyasaji wa kijinsia.

-Kusikia habari na matukio ya kuskitisha yanayotokea wakati wa kujifungua hasa kwa wasichana wadogo wasiofika umri wa miaka 18.

- kuangalia clips ( video) za mama anapojifungua wakiwa katika umri mdogo.

Ama kwa wale ambao wameshawahi kujifungua, khofu hii inakuja kwa sababu tu labda walipata hali isiyo ya kawaida katika mimba zingine zilizopita mfano maumivu makali wakati wa uchungu, kuharibika kwa ujauzito ( abortion), au mtoto kufia tumboni.

Kuna ambao walikua katika hali ya kawaida mimba zilizopita lakini bado huwa na khofu ya ujauzito hii inatokana na kuwa walipitia maumivu makali ya uchungu au kukosa huduma nzuri kutoka kwa wauguzi wakunga ama ndugu wa karibu na marafiki.

Sababu zingine zinazosababisha kuwa na khofu ya ujauzito ni:-

-Kukhofia ile hali ya kuchunguzwa maumbile yao ya siri na watu ambao hawajiskii huru ( comfortable) kwao, kuonekana zile sehem za maumbile yao ya siri hasa hasa kwa wahanga ambao walipitia udhalilishaji wa kijinsia, hii huwafanya wakumbuke matukio mabaya waliyoyaliyopitia na kuwaathiri kiakili na kisaikolojia.

-Kuwa na matatizo ya kiakili ikiwemo msongo wa mawazo na wasiwasi ( depression & anxiety) kabla ya kuwa na ujauzito

- Kujihisi kuwa wana uwezo mdogo wa kuvumilia maumivu kwahiyo huhisi kwamba watashindwa kuhimili maumivu makali ya uchungu na kujifungua.

- Kukhofia kuwa maumbile yao hayatarudi kama mwanzo baada ya kujifungua na kujihisi kuwa watashindwa kufurahia tena tendo la ndoa na kuhisi watakua na mipasuko ambayo huweza kuwasababishia kushindwa kudhibiti utokaji wa haja ndogo ama kubwa ( fistula)

- Kutokujithamini ama kukosa support ya mwenza wake, ndugu na marafiki.

- Kuwa na umri mkubwa sana ama mkubwa sana ( kwa mfano kumlazimisha mtoto mdogo kubeba ujauzito hata ikiwa italeta shida kwake ili tu apate adabu kwa vile ameshiriki vitendo vya ngono akiwa katika umri mdogo sana, hii itamharibia maisha na ndoto zake zote.

- Kuwa single mama, au mama asiye kuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake, ama alilea mimba za nyuma na mtoto peke yake bila kupata mashirikiano kutoka kwa mwenza wake.

Watu wengi wenye khofu ya ujauzito huchagua njia ya upasuaji kujifungua pasipo na sababu za kitaalam za kufanyiwa upasuaji wakiona ndio njia ya salama.

Vipi utaweza kuishinda hii khofu na kufurahia ujauzito wako

- Jiunge na pregnancy support groups ( vikundi vyenye kutoa support na elimu juu ya swala Zima la ujauizito ikiwemo umuhimu wa afya ya mama na mtoto, mlo mzuri na virutubisho vyote anavohitaji mama na mtoto aliyepo tumboni hadi atakapozaliwa

- Jaribu ku share mawazo na watu wengine ambao watakusaidia kukujenga kisaikologia na kukupa nguvu na sio wenye kukubomoa na kukukatisha tamaa, zingatia sana wawe ni watu wajuzi juu ya maswala ya ujauzito na wazoefu pia sio wapotoshaji.

- Tafuta daktari mzuri wa maswala ya akina mama Na uzazi ( Obs & Gyn) awe ndio daktari wako na unamuona yuko tayari kukusaidia wakati wowote utapohitaji msaada.

- Hudhuria kituo cha afya kufanya clinic kwa mpangilio na uwe na tahadhari unapoona Dalili yoyote ya hatari kwa mama mjamzito ikiwemo, kutoka damu ukeni, kuharisha sana, kuvimba mwili na nyenginezo.

Ukiweza kufuata huu muongozo, Ujauzito haitakua jambo la huzuni kwako bali itakua ni kipindi cha kufurahia na kuwa na matumaini mazuri kwa kile kilichopo tumboni mwako👏
 
Back
Top Bottom